Ritz,
Asalaam Alaykum Al Akhiy.
Hawa jamaa wameshindwa kabisa kujibu hoja kali na zenye minyambulisho na zilzala za nguvu. Labda yale mawe yamekua mazito mno sasa wanaona kimulimuli,kwa hiyo tusiwalaumu sana wanaposema ati hoja za Zali la Mentali a.k.a Mchimba Chumvi hawazioni!?ahaha!!
Mimi awali nilipoingia sikujua hawa jamaa kumbe wamo hapa jamvini kwa ajili ya Crusade kama ndugunyao George Bush na wale virongwe ma-Neo Cons. Lakini kila siku zinapokwenda nabainisha mengi hapa.
Kuna wakti walikua haweshi kututajia mambo ya Tanga na Wazee wetu wa Tanga,sisi tukawa kimya tunawacheka tu...nilipowafuata kuwavuruga kila mmoja kaanza kutaja makwao na yule mwingine akaacha kabisa kumtisha Sheikh Mohammed na yale mambo ya Makorora,sasa kakimbilia kwao Kicheba na Magila.
Kwa wale wa Mara na Tarime,nanyi pia nakuja hukohuko na nitaanza kwa kukuonyesheni ya kuwa huyo Nyerere wenu kaanza kula fadhila za Wazee wetu toke pale Musoma kwa Mzee Makongoro na Masheikh wengine wengi tu huko mabara. Nina tambara chafu saana la Nyerere alowafanyia kina Issa Makongoro na Sheikh Abdallah Mwita. Kwa hakika yule mtu alikua hakumbuki kabisa fadhila. Kila nikisoma hiyo hotuba ya upuuzi aloiweka huyo Yericko hapo juu,basi Wallahi nakumbuka jinsi gani Nyerere alishindwa hata kwenda mazikoni/msibani kwa Sheikh mohammed Yahya Ramia pale Bagamoyo. Alipopashwa habari na AbdilRahman Ramia,akadai ati yuko very busy kwenye simu na yule "changumemenya" Samora Machel!? Sijawahi kusikia maongezi ya simu ya siku nzima!? Na kuwasahau walokuweka na kukufadhili kwenye hayo madaraka!?
Leo hao jamaa ati wanamzoma Rais Al Jamuhuriya Al Maaruf Mrisho Bin Khalfan Kikwete,ati anasafiri sana. Embu wajaribu kupiga hesabu ya trip za huyo "Mwalim wao"!? Kuna trip nyingine alikua analazimisha huku anaambiwa kuwa ndege bado iko Government Hanger ina khitilaf. Chief Engineer wa Serikali yake takriban miaka 20 Mohammed "Babu" Mwita(mnywa kahawa,mtoto wa Kariakoo,mtu wa akili za Madrassa),alikua analalamika kuwa huyu Mzee Nyerere,iko siku atatufanya tufie angani maana anaingilia sana mambo asoyajua na mkaidi wa kusikiliza Wataalamu. Kwa issue hii,wale wajuba na mpendao kujipunja kamuulizeni Mkristo mwenzenu mtiifu Mzee Newa maana ndiye aliekua Pale Civil Aviation miaka mingi .
Jamaa naona kila habari tukiwapa hawazikubali,ati kwa sababu tu kuwa wao walikua hawazijui na wanajaribu kuzitia tashtit. Ndo maana Sheikh Mohammed huwauliza ,haya mambo mtayajuaje kwani nyinyi ni wageni na pia Wazee wenu ni wageni?
Nipo hapa leo, napitia ule utumbo wao wa W'end. Naona hamna lolote la maana zaidi ya matusi ya yule Kiroboto wao. Najua wale Manyangumi wa hoja wametahayari,pale The Big Show a.k.a The King Of Kings alipowaambia kuwa wanashinda hapa na kulala hapa hapa jamvini!ahaha!!
Naona yule kunguni wa hoja a.k.a Abu Jahal,ati anahangika kuingia kwenye "google search" na kupata fadhaa mbona hizi details hazipatikani!?ahaha!!...hawa jamaa kweli hamna kitu!
Tuendelee na mnakasha.
Cc; Ami
Sitie shaka nakuwekea vitu vipya na vya ndani every time...I never break my promises.