Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mohamed Said,

Nimemsoma Zitto Kabwe hakihotubia bunge kaongea maneno mazito sana utadhani naye anafyonza Ilm kwenye huu Mnakasha.

Humu jamvini watu wanataka kuwapangia Waislam waongozwe na Bakwata ambayo ni chombo cha serikali.

Ajabu...!
Mbona wao jumuiya zao haziongozwi na kupangiwa mambo yao na serikali??
Imekuwa bakwata kazi yao ni kutangaza mwezi tuh unapoandama na siku za watu za kufunga na kufungua kama matahira,ukionekana Kenya hawataki kutangaza,wanasubiri mwezi wa Tanzania kwanza kisha wawatangazie kufunga na kufungua,vihiyo wakubwa,
Nyerere katika hili la bakwata mzimu wake utamuandama hadi huko kaburini,iweje mambo yetu sisi yeye aamue kuunda chombo bila ridhaa yetu??huku wengine akiwaacha waunde vyombo vyao kwa ridhaa zao??
Hongera Zitto kwa ujasiri wako wa kusema ukweli...
 
Nguruvi3,

Umemsikia Kadinal Pengo na sakata la bomu Arusha.

Wewe ulisema Mohamed Said anahusika na matukio ya Zanzibar na Arusha.

Busara yako ipo wapi?
Sijasema amehusika! hilo la kwanza. Pili kama unataka kuiona busara ya kile nilichomaanisha hilo halina wahka nitaweka hapa
 
Nilijua tu Nguruvi3 lazima utakuja kuichukua hoja ya huyu bwana Rweye1,,
usipate shida na sisi nguruvi3,na wala usiumie sana kutaka kutusemea,mufti simba na bakwata yake isikughulishe sana,we kama unaona ana ilm kisa alikua katika barza la maulamaa na mufti hemed ibn jumaaa sawa,ila kama mtu ana ilm ya dini kisha anaitumia kwa maslahi ya tumbo lake basi haina maana ya ilm yake,

hakuna ataepoteza uislam wake eti kwa kmpinga Moh Said,ila tunaona ni busara aje apinge kwa hoja kama unakuja ww ili tuchambue na tupimie uzito wa hoja zenyew na sio kupinga tuh kutokana na hisia binafsi,sawa?
Hiyo sentensi niliyoikizia hakika umenigusa. Ni muhimu sana

Kwa maana nyingine hakuna undugu kama ndugu ni mchumia tumbo na unakubaliana nami kuwa tafsiri ya kuunusuru Uislam ya Mohamed ina walakini mkubwa sana.

Pili, alaaa! kumbe kuchumia tumbo kwa kufanya kinyume na dini ni makosa! Ok! sasa kupotosha, kudanganya na kusema uongo au kusengenya si yote yapo kundi hilo. Nashukuru ujumbe wako utakuwa umewafikia wengi.
Kwahili nakupongeza kwa ujasiri maana inataka moyo kusema maneno hayo mazito. Naomba walengwa wayazingatie.
 
Nguruvi3
Mimi katika list yangu hadi sasa wapo wawili,unataka nikuongeze uwe wa tatu??
la hasha sintofanza hivyo kwa kuwa najua hapo umejitoa ufaham kwa makusudi,mtu anaefaham mafuhum ya dini kisha akashindwa kuyatumia kwa maslahi ya dini kwa makusudi kabisa huyo anakua ameasi na kwa kias kikubwa mtu huyo huwa na sifa za kinafiki,,

Pia anachofaya Moh Said na sisi walamba buti zake kama mnavosema si kupigana jihadi,la hasha,ni kusimamia ktika ukweli ambao umefutwa kwa makusudi na kupotoshwa,sasa kwa kuwa wengi wetu tunaonekana kama ni watu wa imani hii basi ninyi mmekuja kutuhukum hivyo moja kwa moja,sisi hatuna tatizo na hilo,

Tutaendelea kusimamia kile tunachokiamini,ila bakwata yenu tunawaachia nyinyi na nyerere wenu,,,
 
Last edited by a moderator:
Ukristo duniani ni dini muflis kabisa wa hoja.Wako tayari hata kuuwa ilimradi wapate huruma ya Serikali.Kutokana na kufilisika kwao kihoja wanaogopa kila kitu cha waislamu.Wanatumika na mabeberu wanaotaka kuitawala dunia.
Tukio zima la Arusha ni la kupangwa siku moja kabla kikao cha maaskofu wa kikristo na wa kiislamu.
Don't even go there. Nimemsikia Mohamed akiwatahadharisha kuwa kuna uwezekano wa kukashifiana kidini. Don't go there. Otherwise ukifyatua makombora upande mwingine unaweza kabisa kujibu.
 
Naomba niweke rekodi vema. Kwanza kabisa Mohamed hayo maneno niliyokazia kuna ushahidi wa kutosha kabisa kuwa wewe hufanyi kama unavyomweleza RWEYE1. Nina ushahidi wa kutosha kuhusu wewe kupayuka jambo bila kupima(kumbuka lini tumeanza mnakasha na mara ngapi tumekuwa hapa JF). Kuna ushahidi wa kutosha kuwa unaongea usicho na ujuzi nacho. Sasa hapo jipime mwenyewe kuwa maneno hayo uliyosema yamekulenga au kumlenga Rweye1.

Nikirudi kwa Rweye1, naona ameingia kwa ghadhabu kidogo kama ilivyo kwa mtu mwingine.
Anayedhani kuwa yupo mtimilifu basi na atuambie! Lakini katika aliyoongelea ukiacha yale aliyoghadhabika kuna mambo muhimu kayasema ambayo nilitaraji yatajibiwa kwa hekima zile zile zitokanazo na hoja zake.

Kinyume chake ameshambuliwa, eti kwa kusema yeye ni Mwislam. Mohamed hakuna mtu anayeweza kujinasibu katika imani. Imani ipo kwa mtu na wala si chama cha siasa, mpira au mdumange.
Yeye akisema ni mwislam basi hilo ni baina yake na Mola wake.
Unaposema anajinasibu hapo unahalifu na kupoteza busara.

Kwani wewe ni nani hadi uweze kujua mwislam au mwingine awaye?
Kwani cheti cha uislam kinatolewa wapi na kwa rekodi gani kiasi cha kusema huyo anajinasibu!
Jamani imani ni kitu rahisi ukikielewa na ni kigumu sana ukiimba tu.

Nasema ni kiugumu sana ukiimba kwasababu maoni ya Mohamed ni kuwa Rweye1 alitakiwa amuunge mkono ili akamilike na awe ndugu. Mohamed anasahau kuwa tofauti ya mitazamo ni shemu ya Uislam.
Kama isingekuwa hivyo leo tusingekuwa na Sunni, Shia, Kadiani,Bohora, Ismailia n.k.

Hata katika wale waliotangulia bado kuna mahalifa na masheikh wakubwa waliotofautiana sana kimitazamo.
Ndiyo maana tumekuwa tunasikia kuwa jambo lina utata kutokana na tafsiri na mitazamo.

Mohamed alikataa kutoa kauli juu ya DVD ya Ilunga na kulipeleka suala hilo ''kwa maulamaa''.
Hapa ni wazi kuwa alikuwa na mtizamo tofauti na waislam wengine waliodhani kuwa Ilunga hakufanya jambo zuri.

Juu ya yote na mitizamo yote tofauti bado kila mmoja amebaki kuwa mwislam.
Leo kwanini Rweye1 aonekana kituko eti kwasababu amepingana na Mohamed.

Kinachotisha sana ni Mohamed kutumia maneno ya Mwenyezi kwa namna atakayo.
Hili la Mwislam kumnusuru mwenzake nalo linahitaji kuangaliwa.

Labda naomba msaada kwa Mohamed na vijana wake wanieleze, hivi akitokea Mwislam anamnajisi mwanamke kwa nguvu(kubaka) na mwanake huyo si Mwislam, je huyu mwislam aliyeona hilo anatakiwa amnusuru nani?

Nadhani tatizo la kutaka kumeza tu ni kubwa kuliko linavyoonekana.
Lazima kuwe na mawazo tofauti ili kuleta akhili na fikra zaidi.

Nadhani ndio maana kuna watu wanaamua tu Ijumaa maandamano na bila kufikiri watu wanaunga tela kwasababu kutofautiana na wenye Uislam ni kuukana Uislam.!
Jamani hili nalo linahitaji elimu yoyote zaidi ya akili za kawaida za mwanadamu?

Na mwisho, nawashangaa sana wale wanaosema Mufti Simba hana elimu ya dini. Nakumbuka na nasimama kusahihishwa kuwa wakati wa sheikh Hemed, huyu alikuwa katika kamati ya maulamaa.
Sasa sijui watu wanataka kusema au kuuambia nini ulimwengu kuhusu hili.

Kitu kimoja nilichosoma magazetini ni kuwa mufti Simba alisimamama na kusema Ponda hana elimu ya dini hata kidogo.
Hakuna aiyesimama kuhoji elimu yake wala ku-challenge maneno yake.

Sasa kama Ponda ni kiongozi kwanini mufti anayesemwa hana elimu ya dini awe dhalili licha ya yeye kuthibitisha kuwa Ponda ni mweupe.

Hebu angalieni mnasema nini kwanza, kupayuka au kusema mtu asicho na ujuzi nacho imekatazwa kama alivyosema Mohamed. Naona watu mnasema kila jambo hadi mengi yasiyofaa.
Msioongee hata yale ya chumbani kwenu.

Busara ipo wapi?

NGURUVI:

Hivi ni kwanini Askofu Method Kilaini alihamishiwa Bukoba kuwa Askofu msaidizi toka Dar?
 
Wilcard, huyu jamaa nishawahi kusema huko nyuma kuwa ni mjanja sana. Mambo yakinuka anaruka kama hakimu kiruka.
Leo amesahau Mkoba wa Ibadan! tena alikoalikwa na tambo kibao.

Maandamano yanaratibiwa na watu nyuma ya pazia na mengine tunayoyaona tu.
Waislam wa Ponda wapo Segerea wengine wanaandika na kuuza vitabu!!
Matukio kama ya Zanzibar na Arusha watu wanaandaa paper n.k. Huwezi kuwaona front line, they operate behind the curtain. Leo watu wanaruka sina ujuzi nalo. Huna ujuzi wakati 15 yrs umekuwa unachagiza uhalifu wa namna hiyo!
Kesha waruka wenzake anasubiri mwaliko kwenda kuthibitisha aliyoandika kama kwamba ni mtabiri wakati anajua fika kuwa 15yrs amehubiri uhalifu.

Nguruvi3,

Ndugu yangu hayo maneno yako ulikuwa unamlenga nani kama siyo Mohamed Said.

Hakuna tatizo kama unayakana maneno yako.

Tuendelee na mnakasha tusemezane...
 
Last edited by a moderator:
Moh Said,
Ndug Zitto kamaliza kila kitu,ametumia lugha yenye kueleweka sana,
Huo ndio ukweli tunaousema...
Muongo mkubwa, wewe na hilo zee lako hamsemi hivyo! Nyie mnasema adui wa waislam ni Nyerere, mfumo kristo na kanisa katoliki. Ulivyokosa akili na busara unathubutu kudandia hoja ya Zito! Soma utumbo wa ndugu yako Ami hapa;
Ukristo duniani ni dini muflis kabisa wa hoja.Wako tayari hata kuuwa ilimradi wapate huruma ya Serikali.Kutokana na kufilisika kwao kihoja wanaogopa kila kitu cha waislamu.Wanatumika na mabeberu wanaotaka kuitawala dunia.
Tukio zima la Arusha ni la kupangwa siku moja kabla kikao cha maaskofu wa kikristo na wa kiislamu.
 
Ajabu...!
Mbona wao jumuiya zao haziongozwi na kupangiwa mambo yao na serikali??
Imekuwa bakwata kazi yao ni kutangaza mwezi tuh unapoandama na siku za watu za kufunga na kufungua kama matahira,ukionekana Kenya hawataki kutangaza,wanasubiri mwezi wa Tanzania kwanza kisha wawatangazie kufunga na kufungua,vihiyo wakubwa,
Nyerere katika hili la bakwata mzimu wake utamuandama hadi huko kaburini,iweje mambo yetu sisi yeye aamue kuunda chombo bila ridhaa yetu??huku wengine akiwaacha waunde vyombo vyao kwa ridhaa zao??
Hongera Zitto kwa ujasiri wako wa kusema ukweli...

Potelea mbali hata kama Chadema watamfukuza Zito au kumzuia asigombee Urais mwaka 2015! Wananchi wanaimani nae!
 
Potelea mbali hata kama Chadema watamfukuza Zito au kumzuia asigombee Urais mwaka 2015! Wananchi wanaimani nae!
Wajameni,
Samahani kama nadandia treni kwa mbele. Sijaiona kauli ya Zitto. Kwani Zitto kasemaje?
 
Ritz,
Msome Zitto Kabwe hapo chini:
TAIFA LINA NYUFA

NDUGU KABWE Z. ZITTO, MB  BUNGENI TAREHE 6 MEI, 2013

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia leo katika mjadala huu muhimu sana.

Hapa Afrika kulikuwa kuna nchi, na bado ipo, inaitwa Ivory Coast. Ilikuwa ni nchi ambayo inasifika sana kwa amani na utulivu; na ilikuwa ni nchi ya kupigiwa mfano. Leo hii Ivory Coast imegawanyika vipande vipande. Ukienda leo Ivory Coast unakuta wanaoitwa Ivorite na wanaoitwa wageni ambao wazazi wao walienda Ivory Coast kufanya kazi miaka mingi sana. Lakini pili katika mgawanyiko huo kuna mgawanyiko mkubwa sana wa kidini kati ya watu wa Ivory Coast wanaotokea Kaskazini na watu wa Ivory Coast wanaotokea Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa tuna Sierra Leone nchi ambayo wageni walikuwa wanakirimiwa katika hali ambayo haijawahi kutokea hapa duniani. Lakini leo Sierra Leone ina rekodi kubwa sana ya watu wenye ulemavu kwa sababu ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Naomba nichukue nafasi hii kufuatia matukio ambayo yametokea hivi karibuni na hasa jana na siku zilizopita ninanukuu hotuba ambayo Rais wa Awamu ya Tatu Mheshimiwa Benjamin Mkapa aliitoa katika Bunge hili tarehe 4 Novemba, 1998. Alisema:

Mr. Speaker, after three years of my presidency, I can dare to modify the words of famous Zanzibar maestro Siti Binti Saada by saying, Tanzania is a good country, let one who wishes to come do so. God has showered blessings on our country. It is a country of unity, peace, love, rejoicing and exciding generosity. It is a country of people who love equality and justice. Our national unity brings from our firm believe in equality of human beings before God and before the Law. A Unity reinforced by correct policies of national building. Policies based on the principles of social justice, peace, harmony and development for all. A unity which is extra sensitive to policies, statements behavour and actions which may sore seeds discard hatred and suspicious among Tanzanias

Mheshimiwa Mwenyekiti sitatafsiri. Lakini naomba kila Mbunge ajiulize leo iwapo Rais Mkapa tukimpa fursa ya kuja kuhutubia Bunge hili anaweza akayatumia maneno haya tena? Hakuna mtanzania yoyote anayeweza kuthubutu leo kutumia maneno haya tena kwa sababu nchi yetu ina nyufa. Ina nyufa ambazo kwa kujua au kwa kutokujua sisi kama watu ambao tumepewa wajibi na wananchi wa kuitunza nchi hii na kuipeleka pamoja tumejikuta tukiingia katika kutoa kauli, maneno na vitendo ambavyo ni irresponsible vinavyopelekea kugawanya nchi; na yanayotokea sasa ni matumizi ya nyufa hizo.

NDUGU KABWE Z. ZITTO

Asubuhi hapa Mheshimiwa Lissu amesema, ametoa rekodi ya namna ambavyo wanasiasa wa chama kinachoongoza (CCM) wamekuwa wakitoa kauli dhidi ya vyama vya upinzani kuhusiana na masuala haya ya kidini. Wametoa mfano kuhusu chama cha CUF kilipoitwa chama cha waislam, wamekitolea mfano kuhusu CHADEMA kinavyoitwa mpaka sasa chama cha wakristo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inawezekana ikawa ni rahisi sana tuka-point fingers kwa wenzetu nyie, ni rahisi sana; lakini CUF wakati wanaitwa ni chama cha waislam ambao walikuwa hawaitwi ni chama cha waislam hawakunyoosha mkono kupinga. Wakati CHADEMA kinaitwa cha cha Kikristo ambao hawaitwi hivyo hawakunyoosha mkono. Matokeo yakeni nini? Tumejenga hofu kubwa sana katika Taifa na hii ni lawama kwa wote. Wote kama nchi ili tuseme kwamba hapa tumekosea na tuanze upya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, adui anapokuja kwenye nyumba anaangalia ni wapi ambapo ni rahisi kamba kukatika. Tumeji-expose, tumejiweka wazi. Leo mtu anayetaka kuishughulikia Tanzania ata-deal na udini tu. Kwa sababu anajua watanzania hivi sasa wamegawanyika katika misingi hiyo. Jana limetokea tukio Arusha, angalia kwenye mitandao ya kijamii mara moja watanzania wenyewe kwa wenyewe na ukiangalia majina ya watu wanaojadiliana wanaanza kusemana kwa dini zao. Ndiyo hatari ambayo tumeifikia; na ndio anachokitaka adui. Ni hicho. Atakuja, wanaitwa Agent Provacateur, watapiga, mtabaki mnagombana ninyi. Tukiruhusu NYUFA hizi ziendelee hatutakuwa taifa. Ni lazima sote kwa pamoja tusimame imara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, waislam na wakristo nchi hii hawana chuki kwa sababu wanaishi pamoja, ni marafiki, ni ndugu na kama ingekuwa kwa mfano waislam wanawachukia wakristo waislam wangevunja makanisa au wangechoma makanisa au wangewalipua wakristo. Wakati wa tukio la Mwembechai ndipo ambapo Polisi waliingia mskitini wakaua watu, wanawake wakateswa kwenye magereza na kadhalika, watu wakakaa miezi mitano gerezani bila kushtakiwa lakini hapakuwa na mtukio yoyote ya namna hii. Waislam na wakristo wa nchi hii ni wamoja. Wananchi wetu ni wa moja lakini sisi viongozi kwa kutoa kauli ambazo ni very irresponsible tunawagawa watu wetu na ni lazima tukatae hali hii. Tunafanya nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima twende mbele. Kwanza ni lazima sasa Serikali ijenge utamaduni wa kufuatilia grievances zote ambazo wananchi wanazo bila kujali dini zao. Pili turuhusu watu kuwa huru kusema. Nimesikia hapa watu wanasema kwamba maandamano ni tatizo nakadhalika. Maandamano si tatizo, ukimzuia mtu kuandamana akiweka hasira zake kesho atafanya nini? Atatoka na bomu. Turuhusu honest discussions miongoni mwetu kama wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu ni lazima sasa tuseme ya kwamba ni marufuku kuwa na kauli za chuki hate speeches. Kama hatuna vipengele vya kisheria tutunge sheria kwa sababu kumekuwa na hate speeches nyingi sana katika hii nchi na hakuna hatua ambazo zinachukuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, state, dola, ihakikishe inajiondoa kwenye shughuli za uendeshaji wa mambo ya kidini. Ijiondoe kabisa. Kwa mfano kuna lawama ya muda mrefu sana ya waislam kuhusu BAKWATA, Waislamu miaka mingi toka mwaka 1969 wakati Serikali imeunda BAKWATA wanalalamika. Leo hii Serikali ikitaka kuzungumza na waislam inafanya nini? Inaenda kuwaita BAKWATA. Hawana legitimacy ya waislam, hamtaweza ku-addres masuala ya waislam lakini ni rahisi sana kuweza kuongea na CCT kwa sababu CCT ni chombo ambacho kina uhuru wake. Kwa hiyo Serikali ijiondoe kwenye uendesheji wa shughuli za kidini. Hapa ndipo tutakapoweza kuhakikisha kwamba tunakuwa na nchi moja nchi ambayo ina amani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namaliza kwa kusema nchi hii si ya waislam peke yake, nchi hii si ya wakristo peke yake. Nchi hii si ya CCM au ya CHADEMA, CUF au ya NCCR-Mageuzi au TLP na kadhalika. Nchi hii ni moja, nchi hii ni ya Jamhuiri ya Muungano wa Tanzania. Lazima wote tusimame kuhakikisha tunailinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru sana asante.

Jasusi,

Kauli ya Zitto hii hapa.
 
Last edited by a moderator:
Kelelee weeee! We ni KAFIRI TU
Mkuu umemshtukia vizuri sana ... Mpuuzi kweli kweli eti na yeye anajinasibu kuwa ni mwislam! Adui Mkubwa kwa Waislam wa Tanzania anajulikana kuwa ni BAKWATA: chini yake mali za waislam zimeuzwa kama njugu, chini ya BAKWATA waislam tunaendelea kudhulumiwa katika kila nyanja za kimaendeleo, Watoto wa kiislam wanafelishwa, Waislam wananyimwa fursa za ajira katika taasisi nyeti za umma hadi ndani ya ikulu! Eti hakuna waislam waliosoma! waislam wa sasa tumesoma sana, tunauweledi mkubwa sana, tunachokihitaji ni fursa sawa kwa wote...
 
mi nadhani hapa issue inatetewa sana hoja, hoja uliyotoa feby ni kuwa waislam sana sana wa pwani wajipange wasome ili wawe kama wenzetu wakristo.
swali kwako je kwa sasa kwani waislam wasomi hakuna?
na je kama wapo je uwiano katika soko la ajira unalingana?
mimi nimemwelewa sana MOHAMED sasa unataka waislam wasome wakati necta ndio machinjioni, unakumbuka necta walikiri kukosea kusahihisha mitihani ya islamic knowledge? kwanini isiwe bible knowledge ?
wewe inawezekana ni muislam, lakini jiulize ni muumini?
je unaamrisha yale yote aliyotuamrisha ALLAH au tu wewe ni muislam kwa ajili familia na jina lako ni la kiislam.
shame be upon you.
 
Labda naomba msaada kwa Mohamed na vijana wake wanieleze, hivi akitokea Mwislam anamnajisi mwanamke kwa nguvu(kubaka) na mwanake huyo si Mwislam, je huyu mwislam aliyeona hilo anatakiwa amnusuru nani?
Amesema Mtume salalahu alayhi wasallam:
Mnusuru ndugu yako (Muislamu) aliyedhulumiwa au anayedhulumu, mtu mmoja aliyekuwepo akauliza:ninaelewa kumnusuru ndugu yangu aliyedhulumiwa lakini anayedhulumu (sielewi)?
Mtume salalahu alayhi wasallam akamwambia: Unaweza kumzuia asifanye (asiendeleze) dhulma, huo utakuwa ni msaada wako kwake (umemuondolea mzigo wa adhabu za Kiama)".mwisho wa hadith- (imepokelewa kwenye sahiihayn, Bukhari na Muslim)

*kwenye mabano ni tafsiri yangu jinsi nilivyoelewa mimi.
 
Mkuu umemshtukia vizuri sana ... Mpuuzi kweli kweli eti na yeye anajinasibu kuwa ni mwislam! Adui Mkubwa kwa Waislam wa Tanzania anajulikana kuwa ni BAKWATA: chini yake mali za waislam zimeuzwa kama njugu, chini ya BAKWATA waislam tunaendelea kudhulumiwa katika kila nyanja za kimaendeleo, Watoto wa kiislam wanafelishwa, Waislam wananyimwa fursa za ajira katika taasisi nyeti za umma hadi ndani ya ikulu! Eti hakuna waislam waliosoma! waislam wa sasa tumesoma sana, tunauweledi mkubwa sana, tunachokihitaji ni fursa sawa kwa wote...

Iboru1995.

Jina lako limenikumbusha skuli ya sekondari Ilboru iliyopo kule ARUSHA.

Ni mimi niliyepigania haki ya watoto wa kiislam pale Form One wasiingizwe katika kundi la kulisha nguruwe wa skuli.
Tukumbuke siku zote HAKUNA DHULMA YENYE KUDUMU. Na nafikiri sana ndio mnaenda ukingoni. Haki bin Haki ndio suluhisho. mambo ya dini fulani imesoma kuliko nyingine na hivyo wao wana fursa nyingi na hati miliki za uongozi wa nchi zimepitwa na wakti.

Unajua Mkuu wa skuli alikuwa anaitwa Mzee Mushi (maarufu kama Bino) alikuwa akiwataka form one wote wanakuwa na zamu za kulisha nguruwe wa skuli. Na watoto wa kiislam kazi zao zilikuwa kuleta chakula mpaka nje ya banda na wakristo ndio waliokuwa wanaingia ndani kulisha. Nilimfahamisha kuwa kufanya kazi zozote zile za nguruwe kuanzia kuleta chakule, kumlisha na mengineyo ni haramu kwa mwislam. nashukuru mzee huyo alikubali na ikawa kazi ya waislam ni kulisha ndama wa skuli. Hongera sana BONO na Mzc 611(hiyo ilikuwa namba ya gari lake)

Kinachotakiwa Pasu kwa Pasu. Na waachwe waislam wapumue kwa kujichagulia viongozi na taasisi waitakayo na sio kulazimishwa kujikita na BAKWATA.

Hongera sana Ilboru
 
Mkuu Barubaru umenikumbusha mbali sana, Nafurahi kuona wadau wengi sana wamepita pale Ilboru. Bino alikuwa Mwl na Kiongozi mzuri, enzi zetu tulikuwa tunapatiwa futari nzuri, alijitahidi kwa kweli...Back kwenye mada, mimi nakubaliana na wewe kwa 100%. Watu wengi hawataki kukubaliana na ukweli kuwa kama Taifa kuna mahali tulikosea! kuna kundi lilinyimwa fursa na sasa tayari limeshajiimarisha na linakataa kuendelea kudhulumiwa! wengine wanatamani waendelee kupokea check kutoka ikulu kwaajili ya kuwasomesha watu wao na kuendeleza miradi yao kwa gharama za walipa kodi wote bila ya kujali imani zao...Hii haikubaliki hata kidogo.
BAKWATA inajulikana kuwa haiko kwa maslahi ya Waislam wa Tanzania, Iko kuwatumikia waasisi wake zaidi... Mali za Waislamu zimewekwa chini ya chombo pandikizi BAKWATA! ndiyo maana kuna watu wanauziwa majengo na viwanja vyenye thamani kubwa kwa bei ya kutupa tena kimya kimya...Waislam wameikataa chombo hiki kwa nguvu zote lakini sana sana ninachokiona ni kesi za kubambikiwa zingine zikiwa za ugaidi na hujma za kuchoma makanisa ili mradi waislam tuonekane wakorofi wenye fujo... Tusikubali kuingizwa kwenye mitego ya kijinga, game wanalolicheza sisi tunalijua mwanzo mwisho! Nakubaliana na wewe kuwa sasa wamefikia mwisho na insha'allah tutafanikiwa kuunda chombo imara kitakacho hakikisha ustawi wa Jamii ya Kiislam hapa Tanzania...Tumuunge mkono Zitto et al kuikataa BAKWATA kwa Vitendo....
 
Mohamed Said,

Nimemsoma Zitto Kabwe hakihotubia bunge kaongea maneno mazito sana utadhani naye anafyonza Ilm kwenye huu Mnakasha.

Humu jamvini watu wanataka kuwapangia Waislam waongozwe na Bakwata ambayo ni chombo cha serikali.
Naomba niulize swali dogo tu. Kama Bakwata ni chombo cha serikali, na waislamu wengi hawakitambui, inakuwaje waislamu hao hao wanataka serikali hiyo hiyo iwaanzishie mahakama ya kadhi? Ni swali dogo tu.
 
Watatunga tu vijisababu hawanaga haya ya kusema hili ni kweli tulipotoka hapa ni kweli sio hivi kwao mashindano ndio utaratibu hata kama ni totaly wrong! Subiri jibu utaskia tu!
 
Back
Top Bottom