GOMBESUGU,
Asanta kwa uchambuzi wako kuhusu Uswahili, Kiswahili na Waswahili! umenikumbusha kisa Cha Mwalimu Nyerere na wageni wake Waswahili wa Moshi Mjini! mwanae Mwalimu alioa Mswahili na ndipo Mwalimu akawaalika wakweze Makongoro nyumbani kwake Butiama ili kufahamiana.
Wazee wa Kiswahili waliitikia mwaliko wa Baba wa Makongoro na kutua Kijijini kwa Mwalimu wakati wa jioni na kupumzika. Siku ya pili mnamo alfajiri sana Mwalimu aliamka huku kavaa kaptura na kubeba jembe kuelekea shambani kwake huku akiawaacha wageni wake wamelala!
Mwalimu alirudi nyumbani mnamo kwenye saa 4 asubuhi na kuwakuta wageni wake wanakunywa chai na kuanza kuwatania huku akicheka....haa haa haa Waswahili bwana haa haa yaani ndio mnaamka saa hizi! wale wazee ilibidi nao wacheke lakini kuna Mzee mmoja aliondoka na dukuduku moyoni na kujiuliza lengo la Mwalimu lilikuwa ni kuwaalika au kuwakebehi?
Kadogoo,
Salaam
Al Akhiy. Wallahi,nakusikia kwa utuvu.
Japo nalicheka hapa kiduchu kupitia baadhi ya
posts zako;ati unamrekebisha yule jamaa lile jina lake!ahaha!!
Ile mishikaki ya yule
Mzee Nasib,nami nilikua nikiipenda mno. Na pia nilikua nikipenda
Mama mmoja wa Kiswahili akileta sambusa zake murua pale kwenye ile
Restaurant kwenye lile jengo lilokua
CCM Mkoa pale karibu na ile round about nafikiri!?
Nilikua nikenda saana zamani hapo
Moshi hasa
Marangu. Maana nilipata mchumba,lakini ghafla nikatafutiwa masuala ya kuletwa huku na
Mzee wangu...sasa sijui labda nilifanyiwa kusudi!?ahaha!!
Nina khabari nyingi na
ndefu za Arusha na Moshi... Tukikutana nitakuchekesha mno
Al Akhiy! Na mpaka sasa tuna family/jamaa zetu pale Arusha miaka mingi mno wapo pale.
Nakumbuka zamani nikitoroka
JKT Mgambo Kabuku,basi nakimbilia
Arusha kwa Aunt yangu. Huku Mzee na Mother yangu wakijua ati nipo Jeshini nateseka!ahaha!!
Unajua
Mzee wangu alikataa kabisa mimi kukwepa
JKT;ati ndo uzuri nikapate ukakamavu na kuzidi kulipenda
Taifa!?ahaha!! Nafikiri pia ni labda kujisifu kwa wenzie huko makazini au mbele ya Nyerere. Si Unajua
"enzi ya Mwalimu" lazim uonyeshe yakuwa nyoote wewe na family yako mnaiabudu nchi na
fikra za Mwalimu!ahaha!!
Nakumbuka kuna wakati Salim Ahmed,wakati akiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Ulinzi na Jeshi. Ati wanasifia na Mzee wangu jinsi gani,tangia nimerejea toka
JKT nimebadilika na nimezidi ustaarabu!ahaha!! Hao Wazee yaani
Nyerere aliwadanganya saana pita kiasi. Yaani wangejua vile vituko vya huko
JKT nafikiri wasingethubutu kusema lolote,lakini mimi nilikua nawasikiliza tu!ahaah!! Mimi
Mswahili,ustaarabu nilizaliwa nao!ahaha!!
Nilipokuja na Wifey mara ya mwisho tulikua pale
Tengeru...pana
Lodge moja nzuri na tulivu mno. Tulikaa siku kiduchu maana mambo na safari zilikua nyingi mno. Nikija safari hii kama utakuwa hapo Afrika, basi italazim
Shariff Ritz anilete popote ulipo ili tucheke japo kiduchu vituko vya
Waheshimiwa Nguruvi3 na Mag3!ahaha!!
Insha Allah Al Akhiy,tutazungumza siku nyingine japo kiduchu. Je bado upo
Cairo au usharejea...karibu saana hapa
Al Habiby.
Shukran.