Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hilo lilitokea kweli na masheikh na Waislam kwa jumla walikereka sana.
Kanisa halikuwapo katika harakati za kupigania uhuru.
 
Hapo swadakta.. Narudi kidogo kwenye uhuru wa Tanganyika., Hili pia ningependa na Mzee wetu Mohamed Said alitolee ufafanuzi. Katika mojawapo ya maandiko ya wanazuoni nguli wa Zanzibar niliyopata kuyapitia kwa umakini mkubwa yanaelezea namna ambavyo Baba wa Taifa, akiwa katika TANU alivoanza kuwa na mgogoro na baadhi ya wazee wa kiislamu.

Anaeleza kuwa, mara tu baada ya Uhuru, mwalimu alikutana kwa siri na baadhi ya viongozi wa juu wa kanisa katoliki, hasa maaskofu na waliliweka Taifa la Tanganyika chini ya usimamizi wa Bikira Maria, na hii ikafanywa kuwa formal kabisa.

Baadae alipowaomba kuzikabidhi shule za makanisa chini ya Serikali haikuwa vigumu kwa kuwa tayari walikuwa "wanazungumza lugha moja". Tukio hili la kuliweka taifa chini ya Bikira Maria lilifanywa kwa siri kubwa, lakini kwakuwa ndani ya Serikali walikuwepo viongozi wa kiislamu kama vile akina Mzee wetu Mkwawa (R.I.P), Zilivuja na kuwafikia baadhi ya masheikh wakubwa Tanganyika hasa wa Tabora na Dsm..

Hawa wasingekubali kunyamaza, na huo ukawa mwanzo wa maelewano tete kati ya mwalimu na wenzake wa TANU, hasa wale waislamu. June 1962, masheikh hawa waliamua kuonana na Mwalimu ili kuweka wazi madukuduku yao.. Hata hvo, yasemekana mwalimu alikuwa na baadhi ya masheikh ambao "wangemtetea popote hata kupinga imani zao", na hata katika mazungumzo hayo, walisimama kidete kumtetea mwalimu.

Sina shaka hili pia lilihusishwa na uundwaji wa BAKWATA, na waliotengeneza BAKWATA ya mwanzo walikua hawa ambao waliiva katika chungu kimoja na Mwalimu, wakati wengine walipinga vikali uanzishwaji wake.


Hebu wanazuoni wangu naombeni mnichambulie vizuri hii habari ya Bikira Maria kufanywa msimamizi wa Taifa na mgogoro kati ya mwalimu na masheikh., pana ukweli ama ni porojo za kwenye gahawa?
Kwako
Yericko.
Mohamed Said,
Ritz,
Nguruvi na wengine wote...

Hiyo Tanzania kuwekwa chini ya BIKIRAMARIA ni habari mpya kwangu,

Lakini nitaitafsiri na kuipa majibu kwa uzani uleule iliyokuja nao hapa jamvini,

Kwanza niseme ni UONGO bila kupepesa juu ya madai hayo, ni yakufikirika kama zilivyo zingine za mitaani!

Baada yakupata uhuru, taasisi zote za kiroho zilizotambuliwa na mkoloni kwamaana ya zile zenye usajili kamili zililazimika kufika ikulu nakujitambulisha mbele ya kiongozi mpya wa nchi, hilo halina tofauti na ilivyo leo hii!

Taasisi hizo za kidini ni, Waislamu, Wakatoliki na muungano wa makanisa ya Kiruthelani

Hizo ndizo taasisi zinazotambuliwa hadi leo kisheria, na kila rais aingiapo madarakani taasisi hizo zina utaratibu wake wakwenda kumuona rais/kumpa hongera/nk!


Sasa zikiibuka hoja kuwa walizungumza nini katika makutano ya mwazo kabisa kati ya Julius Nyerere na Katoliki baada ya uhuru, Bila shaka zitaibuka hoja zingine za.

"Nyerere alipokutana na Mashehe katika kikao chao cha siri walikubaliana kuwa nchi iwe ya kiislamu"

Mimi binafsi ninasema hoja yako hapo juu ni yakufikirika tu!
 

gombesugu, mpaka dakika hii nashindwa kuamini ni wewe umeandika hayo maneno...ingawaje hayakulengwa kwangu lakini!...Anyway, hayo tuyaache. gombesugu, kumbuka humu kuna watu aina mbili; wanaofyonza ilmu kutoka kwa mtoa darsa Mohamed Said bila kuhoji na wale wanaozipokea kwa tahadhari huku wakihoji ukweli wake na zipo nyakati mtoa darsa amekuta kumbe ni yeye anapewa darsa!

Hapo nyuma nimewahi kuelezea kuhusu chaguzi mbili zilizofanyika Zanzibar mwaka 1961 na mwaka 1963 na kuambatanisha matokeo. Ajabu ni kwamba hata wewe gombesugu umeungana na wameza ngano kudai ushahidi lakini hapo hapo humu ndani hata mara moja sijakushuhudia ukihoji simulizi za maAl Akhiy @ Mohamed Said au Ritz, kulikoni A Akhiy gombesugu?

Muheshimiwa Mag3,

Salaam sana ndugu yangu.

Nilishawahi kukwambia mara kadhaa yakuwa wewe ni mmojawapo ya watu ninaowaheshimu hapa jamvini.

Na ndo maana nimeamua kukujibu kipande hiki.

Lakini naona umeamua kuleta somo la self-discipline,nami takujibu kiduchu ndugu yangu.

Kumbuka huyo unayejaribu kumtetea,hii siyo mara ya kwanza kuniadhibu kwa kejeli na kashfa. Tena sio ati kwa yeye kutoa hoja kwa kupinga hoja yangu,hasha! Najua wewe ni mmojawapo wa wafuatiliaji wa karibu katika huu mnakasha,kwa hiyo natumai wafahamu nikisemacho!?

Pia ninafahamu kwa kina distinction between Academic discipline, Self-discipline(pyschology of behavior/cognitive processes) and outside acceptable limits.

Haya majambo pia yanasomeshwa,kufafanuliwa kwa kina na kiundani kwenye Madrassa. Hili somo ambalo hu-cover topic nyingi linaitwa "Taratib Al Adab".

Kwa hiyo kabla ya kumnyooshea maneno huyo jamaa yako,ilinilazim kuzingatia vitu vingi mno kuliko wewe unavyohisi.

Kama unavyofahamu hapa jamvini,pana mambo mengi mno pita kiasi. Jambo ambalo si baya asilan,ni haki ya kila mmoja wetu. La muhimu ni ku-empathises na wenzetu watizamaji na sisi tuliomo humu kama wanajamvi.

Nakumbuka kuna wakati,Mwanakijiji katika kukazia hoja yake,akenda mbali zaidi na kutoa mifano kadhaa ya maisha yake utotoni(visiting memory lane) alipokua Tanga,na mpaka akataja alivyokua akipiga "Daku Kula" na marafiki zake wa KiIslamu. Jasusi,kama tujuavyo mara kadhaa anatupa mifano ya Family yao kina Nyerere.
Haya yoote ni mambo mazuri saana,maana kila mmoja wetu anakuwa free na kufunguka kwa kina,ndipo hoja inapoleta ukweli na kujengeka kwa kina na uelewo mwepesi.

Sasa,anapokuja kiwavi mwengine kutaka kunifanzia character deformation kisa ati nimegusia family yangu kiduchu ili ku-amplify ile hoja yangu kwako,halafu wewe Mag3 ati unaonyesha kunistaajabu mimi!?

Awali nilitaka kumu-ignore na kutojibu asilan,lakini nilipooona huyo jamaa jana ame-edit/update ndipo nilipobaini yakuwa kweli amenidhamiria kikweli.

Napenda kukuuliza masuali japo kiduchu. Wakati Mtume Muhammad na Allah walipokua anatukanwa kwa maneno machafu yaso kiasi wewe binafsi uliandika chochote japo kukemea au kumstaajabu huyo mtukanaji!?

Mtu mzima mwenzio Sheikh Mohammed Said anapotukanwa na kupewa kashfa za hali ya juu na vijana ambao wengine labda yaweza kuwa hata ni wajukuze,wewe ulishawahi kukemea!? Mifano kadhaa,ni kwamba wewe binafsi unajumuika nao au kuanzisha hilo zogo dhidi ya Sheikh mohammed.

Kwa kuwa mimi nakuheshimu mara fulani nishawahi kukuasa/kukukanya kwa dasturi hiyo mbovu. I hope you took that as a compliment

Kuhusu baadhi yenu, kuhisi yakuwa kila anaemkubali Sheikh Mohammed ni mbumbumbu na hajui atendalo;nilishawahi kujitetea.
Sina sababu ya kujichosha au kukuchosha wewe pia kwa kujieleza.Tafadhali kipata fursa pitia bayana zangu za awali japo kiduchu. Lakini kwa kifupi tu,kwangu mimi hiyo itakua ni kinyume na dasturi yangu na pia kinyume na maadili ya taratibu za kibarua/field yangu.

Hata huko Madrassa,usifikiri ati watu wanaitikia tu kila waambiwalo,hasha ndugu yangu. Uliza kwa kina utafahamishwa na nina hakika utastaajabu mno. Kuna ma-Ulamaa wengine wanatafsiri yakuwa ni kharam na ni kinyume cha Quraa'n kusikiliza tu jambo kwenye kusoma kitaaluma bila ya kuhoji kwa kina na kiundani,lakini huku ukitumia maadili mema na "adab sakhikh".

Naona hapo umetaja majina ya "ma-Akhiy wenzangu" ambao huwa sihoji hoja/bayana zao. Yawezekana ni kweli.

Sasa hapa ndugu yangu nahisi wataka kunitwisha lawama zisizo kiasi changu. Kwani wewe binafsi hii si ndo mara ya kwanza kukuomba/kukutaka ulete source ya statistics ulizoleta!?

Takupa mfano;tangia nimeingia hapa jamvini Nguruvi3 amezungumza vitu vingi mno nami binafsi kuna baadhi nilikua nikimwandikia kumwambia yakua namsoma kwa utuo.

Kumbuka huyohuyo Nguruvi3,alikua akizungumza khabari za Alhaj Rukara/WML na Bakwata in deep details,na hajawahi wala hatowahi kuleta kielelezo hata kimoja.
Mimi binafsi niliona baadhi ya vitu alonena vilikua vikileta sense,maana kuna baadhi ya vitimbi vya Bakwata navijua kiundani. Ndo maana nikawa namsikiliza kwa utuvu. Kwa sababu mimi napenda na najaribu mno kuwa-open minded na flexible katika kusikiza au kujifunza jambo nisilolijua.

Nina hakika zile khabari,kama angeleta mtu anaekubali hoja za Sheikh Mohammed,Wallahi ingelikua kitahanani hapa jamvini na nanga zingalipaa!!

Kitu cha mwisho kwako ndugu yangu,nakupa wasia kiduchu.
Unajua jana kule kwenye ile Thread ya "CCM imeshindwa kulinda tembo hata Kiswahili"? Niliona mchango wako kiduchu.

Lakini mbona ZeMarcopolo alipotoa hoja kuhusu vijana wa Bavicha;wewe badala ya kumjibu kwa ustaarabu na utulivu kama mtu mzima na mmojawapo ya waadilifu/wawakilishi wa Chadema humu JF...ukamwita mbwa na mpaka picha ukamwekea ya mbwa wawili mmoja ukamwita Marco na mwengine Polo!?

Je ule ni uungwana ndugu yangu,khasa ukizingatia umri wako ulonao!? Je vijana/watoto wakikutusi utalalama!? Nahisi mi ndie nalitakiwa nikustaajabu wewe kwa vitimbi vyako wala si the other way round!

Yale majedwali yako nimeyaona ndugu yangu,lakini nimeshikwa na vijishughuli kiduchu. Kipata fursa Insha Allah takuandikia

Nimependa tumewasiliana,nami binafsi tajifunza kwa mazuri ulonayo.

Shukran.

Cc;Ritz,ZeMarcopolo
 
Niwe radhi ndugu yangu maulaga, kwa kuchelewa kukujibu.

Source ya mipini hiyo imetoka kwa Mwalimu wetu wa historia Mohamed Said, pamoja na Masheikh na Wazee wetu ambao wengi wameishatangulia mbele ya haki mmoja wao tumemzika jana Ally Sykes.

Kama utapenda kufyonza Ilm zaidi bado wapo Wazee unaweza kumtafuta Mzee Abbas Sykes, Sheikh Bilal Waikela hawa wameishi zama hizo na Nyerere.
Nakushukuru sana ndugu yangu. Je sheikh Bilal Waikela ameandika maandishi yoyote? ni yule mzee aliyetoa ushahidi kwenye kesi ya Ponda hivi juzijuzi? kama ndie huyo naamini anaishi Tabora, nitamfikiaje kutoka huku Iringa!
 
Last edited by a moderator:
Muheshimiwa Nguruvi3,

Salaam.

Unafahamu nini maana ya Al Akhiy kwa utuvu,na kama unafahamu mbona unafanya tashtit zisizo maana "ndugu yangu wa Kicheba"!?

Napenda kukufahamisha yakuwa Al Akhiy Barubaru,siye pekee mwenye hiyo PhD hapa jamvini(kama PhD ndio kigezo chako cha kumuhishimu mtu na kumuona wa maana au msomi zaidi).

Hata hao "ma-Al Akhiy" unaowadharau na kuwabeza nao pia wanazo hizo "PhD zako" unazoziabudu.

Kama kuitendea haki "Club ya PhD",mbona unamuonea Barubaru peke yake!?

Kwani hujapata khabari kuna watu wa "Club" hiyohiyo ya PhD,wananyang'anya Wake za watu na kuwafanza Vimada wao...je ushawahi kuwaambia lolote!? Kumbuka udhaifu ni kwa mwana-Adam yeyote.

Hivi karibuni takujibu ile hoja yako,nisamehe nimezongwa na vijishughuli kiduchu.

Nashukuru kwa kunisikiza.

Shariff gombesugu,

Walaahi bayana zako zina tashtiti nyingi sana naona jamaa yako PhD kwake ndiyo kila kitu cha kushangaza hata kiongozi wao anaitendea haki PhD yake kwenye masuala yake ya kupora mke wa mtu ha haa haa. Bora tukae kimya siye watu wa mtaani ambao hatuna PhD tukifunga zaid4 walaahi jamvi litachafuka.
 
Last edited by a moderator:
Hilo lilitokea kweli na masheikh na Waislam kwa jumla walikereka sana.
Kanisa halikuwapo katika harakati za kupigania uhuru.

Mbona unaweka hisia zako nakuhalalisha kuwa ndio ukweli wa historia?

Harakati za ukombozi za mwaka gani ambazo kanisa/makanisa hayakujihusisha?

Nimekupa habari mpya katika uzi huo pale juu nikieleza ushiriki wa kanisa kuanzia 1927 sasa nini hujakielewa?

Hebu nenda pinga kwakila hoja unapinga kwa hoja katika yale yote niliyoyaeleza pale juu!

Nilikuuliza jambo dogo tu kuwa Shekhe Issa Bin Amir unafahamu habari zake? Lakini umekimbia jumla hoja hiyo unabaki kuhubiri uongo tu!
 
Hiyo Tanzania kuwekwa chini ya BIKIRAMARIA ni habari mpya kwangu,

Lakini nitaitafsiri na kuipa majibu kwa uzani uleule iliyokuja nao hapa jamvini,

Kwanza niseme ni UONGO bila kupepesa juu ya madai hayo, ni yakufikirika kama zilivyo zingine za mitaani!

Baada yakupata uhuru, taasisi zote za kiroho zilizotambuliwa na mkoloni kwamaana ya zile zenye usajili kamili zililazimika kufika ikulu nakujitambulisha mbele ya kiongozi mpya wa nchi, hilo halina tofauti na ilivyo leo hii!

Taasisi hizo za kidini ni, Waislamu, Wakatoliki na muungano wa makanisa ya Kiruthelani

Hizo ndizo taasisi zinazotambuliwa hadi leo kisheria, na kila rais aingiapo madarakani taasisi hizo zina utaratibu wake wakwenda kumuona rais/kumpa hongera/nk!


Sasa zikiibuka hoja kuwa walizungumza nini katika makutano ya mwazo kabisa kati ya Julius Nyerere na Katoliki baada ya uhuru, Bila shaka zitaibuka hoja zingine za.

"Nyerere alipokutana na Mashehe katika kikao chao cha siri walikubaliana kuwa nchi iwe ya kiislamu"

Mimi binafsi ninasema hoja yako hapo juu ni yakufikirika tu!

JF kuna vituko naona umeamua kuandika mwenyewe kisha unajijibu mwenyewe...ha ha haa.
 
Naam na znz yenu yenye maendeleo itapatikana mkiwa nje ya muungano!

Kwabahati mbaya hilo halitatokea kwasababu ninyi ndio waumini wa muungano wa Uswiss, Hong Kong na China n.k. Hamtaki kuondoka katika muungano mkifahamu wazi kuwa hayo ni maumivu tena makali.

Kuhusu wznz kupigwa, hilo halina taabu. Hakuna sababu za wnz kuandamana kudai znz.
Wanaweza kuipata znz bila tusi achilia mbali kurusha jiwe.

Ni hivi, mwambieni makamu wa rais aliyepatikana kwasababu ya uzanzibar, mawaziri waliopatikana kwasababu ya uzanzibar(na si weledi au usomi), wabunge walioko Dodoma kwasababu ni wzn, maafisa wanaofanyakazi katika serikali ya muungano kwasababu ni wznz, wanafunzi wanaosoma bure kwasababu ni waznz na wafanyabiashara, wote kwa pamoja waondoke warudi kuijenga znz yenye maendeleo. Hadi hapo muungano utakuwa umekufa.

Si hapo tu, washawishini wajumbe 15 wa tume ya warioba waondoke katika tume.
Mshaurini Maalim arudishe kitambulisho alichochukua Karimjee.
Fungeni biashara na mawasiliano na Tanganyika. Muungano utakuwa umekufa

Ima hayo ni magumu, nendeni katika baraza la wawakilishi mkiwa na mswada wa kuvunja muungano.
Kabla wabunge wa Dodoma hawajaondoka kurudi kwao, watoe mswada wa kuvunja muungano

Ima hawataki basi anayeng'ang'ania si Mtanganyika aliyeko nyumbani kwakwe ni mzanzibar aliyekuja kuhemea huku akiacha nchi ya neema na yenye maendeleo

Hadi hapo unajitaji maandamano ?

Kuhusu maendeleo, takwimu zipo wazi kuwa katika muungano mnachangia pato la billion 24.
Mapato ya znz kwa mwaka ni 120 billioni, bajeti ni 630 billioni, jilize hilo pengo anaziba nani?

Hapo ukae ukitambua kuwa hakuna bajeti ya ulinzi na usalama, elimu ya juu, na mishahara ya SMZ.

Mna hiari muondoke mkatafute maendeleo, hakuna anayewazuia. Ule muda wa kulia na kupewa pipi sasa basi.

Jaji Warioba, hawa watu wana 50% katika tume! tunakutahadhirisha kuwa kila jambo liangaliwe kwa 50% kama wanahitaji msaada wa kuwa nasi. Rasimu ya kumbeba mznz itakufa kabla ya kusomwa




Mkuu Nguruvi,

Maumivu gani tutakayoyapata nimekupa point kwamba sisi tumeonesha ishara kwamba tunataka kujitoa nyinyi hamna na wala hamtajaribu kua na mawazo ya kutoka katika muungano katika kuchangia hata scotland unajua wanachangia ngapi katika muungano wao fanya research utajua na bado wanataka kujitoa sisi hatuhitaji kua na muungano wa china wa wapi na wapi ila nionavyo munakua munanuna sana na kukereka na kutoa maneno makali mukiambiwa kuhusu muungano na pia kama kwenda baraza la wakilishi mbona tushaenda au hukuona yale maandamano japo lilikua kundi dogo lakini limetu present wazanzibar na bado tumejaribu


swali kama na nyinyi hamuutaki nini mulichojaribu ndo swali niloliweka mwanzo instead ya nyinyi kulalamika aah wanatunyonya hawalipi umeme?

Sina uwezo na wala hatuna uwezo wakuwalazimisha viongozi kua pamoja nasi tutakua kama egypt wamepigania uhuru wao wa mara ya pili bila ya kua na kiongozi wa serekali pembeni yao.

Tumeshafanya hilo la kwenda baraza la wakilishi.

Mkuu nguruvi nafikiri utakua unakumbuka miaka ya 1990s nyinyi mulikua munakuja kwetu munatufata sisi halafu kuna law ambazo zinaruhusu raia wengine kuishi nchi nyengine na hivyo hivyo ushuru unaojigambia nao nusu yake wazanzibar ndo wanaingiza sisi tunakuja munafaidika na kukupeni tax nyinyi munakuja munatufaidisha na nini



Nambokola
 
Mbona unaweka hisia zako nakuhalalisha kuwa ndio ukweli wa historia?

Harakati za ukombozi za mwaka gani ambazo kanisa/makanisa hayakujihusisha?

Nimekupa habari mpya katika uzi huo pale juu nikieleza ushiriki wa kanisa kuanzia 1927 sasa nini hujakielewa?

Hebu nenda pinga kwakila hoja unapinga kwa hoja katika yale yote niliyoyaeleza pale juu!

Nilikuuliza jambo dogo tu kuwa Shekhe Issa Bin Amir unafahamu habari zake? Lakini umekimbia jumla hoja hiyo unabaki kuhubiri uongo tu!

Yericko,

Nafikiri hapo nilipo-bold umekusudia Sheikh Hassan Bin Amir!?

Ukipata fursa jitahidi ukabadilishe na kule mwanzo wa hii Thread,maana pia hilo jina bado linasomeka kimakosa!

Ahsanta.
 
Yericko,

Nafikiri hapo nilipo-bold umekusudia Sheikh Hassan Bin Amir!?

Ukipata fursa jitahidi ukabadilishe na kule mwanzo wa hii Thread,maana pia hilo jina bado linasomeka kimakosa!

Ahsanta.

Hapana sijakosea wala sikubahatisha,

Issa Bin Amir alizaliwa 1846 katika viunga vya mchikichini Mzizima na kuhudumu katika wadhifa wa shekhe katika msikiti uliokuwa hapohapo viwanja vya nyumbani kwake akiwa na umri wa miaka 34 tu, hiyo ni mwaka 1880 hadi 1953

Nje ya kuhudumu katika uislamu, alikuwa ni mvuvi aliyevua pamoja na Ally Ramadhan mwekahazina wa kwanza wa AA,

Kabila Mzaramo na akiishi hadi kifo chake Mchikichini pale nyuma ya kilipo kiwanda cha bia leo (TBL)

Issa Bin Amir rafiki kipenzi wa Arestide Maranta na mzee wa hekima za kilele za zama hizo, mtu aliyekuwa kiungo muhimu kati ya uislamu na ukristu, Mtu ambae Klest Sykes, Cesil Matol na wengine waliokuwa AA walimheshimu sana kwa hekima zake!

GombeSugu sizungumzi ilimradi nimezungumza wala sibahatishi,

Chuki za kidini zimeletwa na Abdul Sykes kuanzia mwaka 1953 tu hivi majuzi, nyuma ya hapo nchi ilikuwa moja na watu wamoja kuanzia kaskazini ya Kenya mpaka Kusini ya Rodesia!
 
Mkuu,

Me maono yangu ni kwamba bado wanajidanganya mara ngapi wazanzibar wamedai kujitoa lakini vitisho na kuwauwa na kuwaweka chini ya ulinzi wengine ama vifungo vya ndani kwa kutaka kuuvunja muungano kama ni mzigo wazanzibar wameonesha ishara za dhati kutaka kujitenga lakini sijasikia na kushuhudia hata mara moja watanganyika(watanzania) wanaandamana ama wanapinga kuhusu muungano sijawahi kuona hadi hii leo.

Halafu mwengine anakuja anasema TANGANYIKA inachangia kiasi fulani iko wapi hiyo tanganyika yenyewe ifufueni kwanza, halafu sisi tunajuaje kama tanganyika inachukua mara mbili (Tanganyika + Tanzania) ndo maana tunasema yamuungano yawe ya muungano ya tanganyika ilokufa yawe ya tanganyika

Pia kama mlijua nchi ni ndogo na bado munajua kama ni ndogo kama sehemu ya ilala kwanini bado mupo nao pamoja ingieni barabarani mupinge na nyinyi TUMECHOKA KUONA ZANZIBAR YETU BILA YA MAENDELEO.

nambokola,

..lazima nikiri kwamba sisi wa-Tgk tumechelewa kudai haki zetu ndani ya muungano.

..pamoja na hayo tumeanza kuelimishana kama unavyoona tunavyofanya ktk media kama hizi.

..naamini kwamba tumeanza vizuri na huko tunakuoelekea Tanganyika itarudi tu.

..pamoja na kuirudisha Tanganyika, tunataka kuendeleza mashirikiano na Zanzibar kupitia East African Community.

..hatutaki muungano wa serikali 3, wala muungano wa mkataba, zaidi hatutaki any kind of bilateral relations. mashirikiano yoyote yale baada ya hapo lazima yawe kupitia multilateral organizations, na the most suitable one ni EAC.

..hizo data nilizokupatia ni taarifa za makusanyo toka Tanzania Revenue Authority. waandaaji wa ripoti wametumia jina Tanzania Bara, mimi nimeamua kutumia jina TANGANYIKA.

..mimi naomba utuletee data zinazoonyesha kwamba Tanzania Visiwani[zanzibar] inachangia zaidi ya Tanzania Bara[Tanganyika] ktk jambo lolote lile la muungano. that is a challenge kwa mtanzania visiwani yeyote yule anayedai muungano unawanyonya.

NB:

kwa heshima zote nikupatia link ya source ya data nilizotumia.

URT Joint Finance Commission: Joint Finance Commission

barua pepe kwa katibu wa Commission: katibu@jfc.go.tz

publications za commission:

http://www.jfc.go.tz/downloads/mapato.pdf

http://www.jfc.go.tz/downloads/gharamaa.pdf

cc: THE BIG SHOW, gombesugu, Nguruvi3, Wickama, Ritz, Kadogoo
 
Last edited by a moderator:
Nini chaajabu kwako hapo?

Ninaposema Mwalimu Nyerere ni Mzee wangu, Joseph Warioba ni mzeee wangu, Paul Boman ni Mzee wangu, Joseph Butiku ni Mzee wangu, Abdul Sykes ni Mzee wangu, Kingunge Ngombalemwiru ni Mzee wangu, unaelewa nini hapo?

Usiwe mkubwa wa mwili na umri tu lakini akili za kijiko cha chai!

Mohamed Said anaposema Shehe Hassan Bin Amir ni mzee wake unaelewaje?

Wewe unaposema Abdul Sykes ni mzee wako unaelewa maana yake!

Nilishasema huna Qualification za kujadiliana na mimi, nakustahi kwakuwa ni binadamu unaepumua!

Kimsingi nakupuuza! Na sitakujibu kwa upuuzi wako huo!


Poor young boy..!
Thats why nakuita wewe ni chakubimbi na mdandia nasaba za watu,kama hao wote unaowataja ni wazee wako kwanini sasa ukaja JF kujiverify na baba mmoja tuh ambae ni JULIUS KAMBARAGE NYERERE??Haitoshi mbona una mtukuza huyo tuh huku baba zako wengine ukiwaacha kwenye mataa??

Sasa kutufaham kwa surname ipi??

Yericko bin warioba?
Yericko bin paul bomani?
Yericko bin butiku??
Yericko bin Abdul sykes??
Yericko bin kingunge ngombaru mwiru??
Ipi hasa ni nasaba yako??hao wote wewe unasema ni wazee wako kama nyerere,iweje sasa uchague jina moja la julius kuja kujiverify JF??

Unavyofanya sivyooo..
Watu tunakuona hovyooo..
Tabia yako siyoo,kwenye jamii utaleta matatizoo,,
Sasa kwanin ufanye hivyoo??
Wakati unajua sivyoo??
Tabia yako siyoo kwenye jamii utaleta mkanganyikooo...
 
nambokola,

..lazima nikiri kwamba sisi wa-Tgk tumechelewa kudai haki zetu ndani ya muungano.

..pamoja na hayo tumeanza kuelimishana kama unavyoona tunavyofanya ktk media kama hizi.

..naamini kwamba tumeanza vizuri na huko tunakuoelekea Tanganyika itarudi tu.

..pamoja na kuirudisha Tanganyika, tunataka kuendeleza mashirikiano na Zanzibar kupitia East African Community.

..hatutaki muungano wa serikali 3, wala muungano wa mkataba, zaidi hatutaki any kind of bilateral relations. mashirikiano yoyote yale baada ya hapo lazima yawe kupitia multilateral organizations, na the most suitable one ni EAC.

..hizo data nilizokupatia ni taarifa za makusanyo toka Tanzania Revenue Authority. waandaaji wa ripoti wametumia jina Tanzania Bara, mimi nimeamua kutumia jina TANGANYIKA.

..mimi naomba utuletee data zinazoonyesha kwamba Tanzania Visiwani[zanzibar] inachangia zaidi ya Tanzania Bara[Tanganyika] ktk jambo lolote lile la muungano. that is a challenge kwa mtanzania visiwani yeyote yule anayedai muungano unawanyonya.

NB:

kwa heshima zote nikupatia link ya source ya data nilizotumia.

URT Joint Finance Commission: Joint Finance Commission

barua pepe kwa katibu wa Commission: katibu@jfc.go.tz

publications za commission:

http://www.jfc.go.tz/downloads/mapato.pdf

http://www.jfc.go.tz/downloads/gharamaa.pdf

cc: THE BIG SHOW, gombesugu, Nguruvi3, Wickama, Ritz, Kadogoo

Umefanya vema sana kuwapatia links hawa ndugu zetu,

Wasome na wapevuke hapa hapa!
 
Last edited by a moderator:
Wanajamvi,
Tuweke rekodi sawa, Huyu Sheikh Amir anayetajwa sana kufukuzwa na kudhalilishwa ndiye huyu huyu alipewa nafasi katika serikali akaikataa(Wickama kama siajakosea).

Badala ya yeye kuingia na kupigana na ‘’mfumo’’ alioona unatatizo kwa waislam, yeye aliamua kurudi misikitini na kuendeleza yale ya AMNUT ambayo waislam waliikataa mwishoni mwa 1950.

Kwangu mimi huyu si shujaa ni msaliti. Ni msaliti kwasababu hakutumia fursa kwa manufaa ya waislam. Hilo si Mohamed Said au Akhyi yoyote anayelisema.
Tunasikia kafukuzwa tu.

Gombesugu, Kicheba haijambo mashallah. Nimesoma post yako uliyonituhumu kuhusu WML ya Lukara kwa kusema sina kielelezo chochote.

Ullichosahau ni kuwa hakuna aliyepinga yale niliyosema akiwemo Mwalim Mohamed na Akhyi wake.

Nilikusikiliza sana uliposema ‘’leave pi as pi’’.
Naona unataka kulirudisha suala la WML kwa mlango wa uani, nadhani nina ufahamu mzuri tu juu yake.

Sasa kama ukitaka nilete kielelezo cha WML na Rukara, nitakueleza kuwa alikuwa na passport ya Tanzania na sasa ni seneta Burundi. Huoni kuna jambo hapo?

Hebu jiulize alipataje passport, wakati wa utawala wa nani na kwanini huyu mgeni aiwakilishe nchi licha ya ukweli kuwa alikuja kama mfanyakazi wa WML.

Zaidi ya hapo sijui unataka kielelezo gani kuhusu Usheikh wake.
Usheikh una heshima zake sasa unataka tuweke vielelezo vya ufuska?

Ninashukuru hakuna post yako utakayoweka bila kunitaja, nadhani sisi wa Magila, mwambani na Mabawa ndio utaratibu wetu wa kujuliana hali.

Je, haijambo. Khairi inshallah mjulie hali ahli na vijana wako.
 
Cool Runnings,

This is the second time you try to seek attention. It seems that you are reading me too much.

Well,I responded to you only once and this is the last.

I like offering candy as reward to a small child like you,for acting big and kind of like you know everything.

You really do write the biggest pile of random sh1t on here. Your words means nothing.

The reality is;it's what you feel on inside that you manifest on the outside...the end result for you is a lost person/an Idiot and a sad spectacle.

Your attitude is garbage. There will always be a$$holes,pompous nutters but I can out number all of you and over power your Clan through decency and kindness....HATE away!!

Ciao.

Cc;Ritz,

dude i think I was acting a little bit polite kukuita limbukeni na full of inferiority complex, truth hurts hahahaaaa!!! You know what? THe name tht suits u is a d..k head ooh yea yes u r in case u didn't know.
 
Nakushukuru sana ndugu yangu. Je sheikh Bilal Waikela ameandika maandishi yoyote? ni yule mzee aliyetoa ushahidi kwenye kesi ya Ponda hivi juzijuzi? kama ndie huyo naamini anaishi Tabora, nitamfikiaje kutoka huku Iringa!

Ndugu yangu maulaga, siku zote ukitaka kujifunza kitu lazima ukubali kupoteza muda wako inabidi uende Tabora ukamuone huyu mzee Bilal Waikela.
waikela_kisutu-court.jpg

MZEE Bilal Waikela (mwenye bakora) akitoka nje ya mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kutoa ushahidi wake katika kesi ya Sheikh Ponda
 
Tunaendela sehemu ya pili.

Mazishi ya Abdulwahid Sykes yalifanyika siku ya Jumapili tarehe 13 Okrtoba. Mazishi yake yalikuwa makubwa yasiyo kifani. Ukitoa mazishi ya mwaka 1950 ya Sheikh Idrissa bin Saad, muasisi na Khalifa wa Tariqa Askariya na mazishi ya Sheikh Kaluta Amri Abeid mwaka 1963, Dar es Salaam ilikuwa haijapata kushuhudia mazishi kama hayo. Gerezani yote ambako Abdulwahid aliishi katika utoto wake na mahali ambapo alianza harakati zake dhidi ya Waingereza ilikuwa kama vile imesimama hakuna kinachoendelea ila maziko ya Abdulwahid. Hii ilikuwa pamoja na sehemu nyingine zilizozunguka Kariakoo kama Misheni Kota na Kisutu.

Gerezani kwa hakika ilikuwa na mwito wa pekee. Ilikuwa ni kutoka Gerezani ndipo walipotoka wanaharakati wa mwanzo waliounda TANU ukimtoa John Rupia. Siku hiyo Gerezani ilikuwa imekuja kumzika shujaa wao. Watu walianza kukusanyika nyumbani kwa mama yake, Abdulwahid Bibi Mluguru bint Mussa mapema asubuhi ambako maiti ilipokuwa imepelekwa. Ilipofika adhuhuri ikawa kama vile Dar es Salaam nzima imekusanywa pale. Chifu wa Unyanyembe Abdallah Said Fundikira, ambae Abdulwahid alisomanae darasa moja katika shule ya serikali mjini Dar es Salam katika miaka ya 1930 na mtu ambae walikwenda wote kuhiji Maka alikuja Dar es Salaam kwa ndege kutokea Nairobi kuja kuhudhuria mazishi.
Inasemekana Nyerere hakutaka kuja kwenye mazishi ya Abdulwahid kwa kuwa wakati ule ndiyo kulikuwa na lile tatizo la EAMWS na masheikh walikuwa wakikamatwa nyakati za usiku na kutupwa jela. Usalama wa Taifa unasemekana ulimshauri Nyerere kwa usalama wake kutohudhuria mazishi yale kwa sababu mazishi ya Abdulwahid yatahudhuriwa na Waislamu wengi. Chuki za Waislamu dhidi ya Nyerere kwa wakati ule zilikuwa juu sana.
Rashid Kawawa aliyekuwa Makamo wa Rais alipopata habari zile kuwa Nyerere hatofika mazishini haraka alimwendea Nyerere na kumwabia kuwa kabla hajachukua uamuzi wa kutokwenda yeye atakwenda kuangalia hali ya mambo yalivyo pale msibani kisha atarudi kumpa habari kamili.
Aliporudi kwa Nyerere Kawawa alimwambia Nyerere kuwa umma uliokuja kumzika Abdulwahid haujapata kuonekana. Chifu Fundikira amekuja kutoka Nairobi kuja kumzika Abdulwahid. Watu wa Dar es Salaam hawatamwelewa kama yeye Nyerere yupo Dar es Salaam na ashindwe kwenda kwenye mazishi yake. Watu wa Dar es Salaam wengi wao wanakumbuka kwa mara ya kwanza kumuona Nyerere akiwa amefuatana na Abdulwahid na wanafahamu hisani aliyomfanyia Nyerere. Nyerere aliona busara ya Kawawa na palepale ikatoka amri kuwa ulinzi katika mazishi ya Abdulwahid uimarishwe na Nyerere atakwenda kumzika rafiki yake aliyempokea na kumuunga mkono wakati ule wa kipindi kigumu cha kuasisi TANU.

Rais Nyerere akawa mmoja wa watu waliokwenda kuomboleza kifo cha Abdulwahid. Akitembea kwa miguu Nyerere alilifuata jeneza la Abdulahid nyuma kutoka Mtaa wa Lindi, Gerezani hadi Msikiti wa Kitumbini maiti ilipokwenda kuswaliwa swala ya jeneza kama ilivyo ada ya Kiislamu.
Pale Kitumbini, Nyerere alisimama nje ya msikiti pamoja na Wakristo na wananchi wengine kungojea maiti ilitolewe nje. Mfanyabiashara mmoja wa Kiasia kuona rais amesimama wima, kwa ajili ya heshima alileta kiti na kumuwekea Nyerere akae. Nyerere alikataa kukaa na akawa amesimama pamoja na watu wengine. Kutoka Kitumbini msafara wa maziko ulielekea makaburi ya Kisutu kwa ajili ya mazishi.
Chifu Fundikira alikuwa mmoja wa watu walioingia kaburini kuupokea mwili wa Abdulwahid. Wakati huu wote wakielekea makaburini, Nyerere alikuwa nyuma ya jeneza kichwa chake amekiinamisha na kila wakati alionekana akifuta macho yake na kitambaa.
Nyerere alikuwa analia. Ilikuwa mwaka 1952 Abdulwahid alipofahamiana na Nyerere na yeye Abdulwahid akamjulisha kwa watu mashuhuri wa Dar es Salaam - Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Mwinjuma Mwinyikambi, Mohamed Jumbe Tambaza, Omar Londo, Rajab Diwani, Mshume Kiyate, Bibi Tatu bint Mzee, Bibi Asha Ngoma, Bibi Titi Mohamed, Bibi Hawa bint Maftah, Bibi Khadija bint Kamba, Said Chamwenyewe na wengi wengine. Ilikuwa na kutokana na msaada wa Abdulwahid na Waislam hawa ndiyo uliomuwezesha Nyerere kuwa katika siasa na kuchukua uongozi wa nchi miaka tisa baadae.
Hakuna aliyeweza kukisia ni mawazo gani yalikuwa yanapita katika fikra za Nyerere. Lakini ni wazi kuwa alikuwa akimfikiria Abdulwahid na jinsi pamoja walivyoweza kuanzisha harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Ilikuwa miaka kumi na tano iliyopita katika Ukumbi wa Arnatouglo, si mbali na pale alipokuwa, Nyerere aligombea urais wa TAA na rais aliyekuwa madarakani, Abdulwahid Sykes. Abdulwahid akiwa na umri wa miaka thelathini na Nyerere akiwa na miaka thelathini na mbili.
 
Hilo lilitokea kweli na masheikh na Waislam kwa jumla walikereka sana.
Kanisa halikuwapo katika harakati za kupigania uhuru.
Mkuu wangu Mohamed Said,unaonaje tukaliangalia jambo hili kwa mtazamo kwamba kanisa kama taasisi lisingeweza kujiingiza katika mzozo na serikali ya kikoloni(kwa mtazamo wake wa ya Kaisari aachiwe kaisari) lakini hata hivyo waumini wake ambao walikuwa wanatoka katika madhehebu mbalimbali na matabaka mbalimbali walishiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya ukoloni sambamba na watanganyika wenzao wa kiislam na imani nyingine.
 
Ndugu yangu maulaga, siku zote ukitaka kujifunza kitu lazima ukubali kupoteza muda wako inabidi uende Tabora ukamuone huyu mzee Bilal Waikela.
waikela_kisutu-court.jpg

MZEE Bilal Waikela (mwenye bakora) akitoka nje ya mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kutoa ushahidi wake katika kesi ya Sheikh Ponda
Mkuu wangu Ritz, mie sio mtafiti na wala sikusudii kuandika kitabu, nataka kufyonza ilm hapa na isitoshe sina rasilimali za kunifikisha huko Tabora hata kama ningependa kufanya hivyo! Mkuu, tupeane taarifa hapahapa kama inawezekana.
 
Back
Top Bottom