Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Sasa wewe dini huna hautambui uwepo wa Mungu wala dini, sasa umejuaje kama mimi mdini...ha haa ha
Kuri na maandishi yako ndio yalifanya nikutambue kuwa wewe ni mdini wa kutupwa! na unaposhindwa hoja hapa jamvini hukimbilia kuwaomba waislam wenzako wawashambulie wale walio kutwisha mipini ya NGUVU!
 
Haki ya Mungu hooooooo, Ritz, Unaniita? ndiyo maana unacheka. Umeanza, tarime, kisha SUA kasha umalizie JIKICHWA? ahahahahaha. Usipate shida na maeneo. Mimi na Tarime na Kavirondo kwenye zombies, haileti taabu kihivyo. Infact nakusifu mpaka sasa unafanya kazi nzuri. Mshikaji anaita BAYANA YAKO!!!!! Yaeleka hajui actual source yeye anajua unashusha vitu kiroho mbaya. Kisha kakutwanga LIKE, ilikuwa RIZK yako bwana. ahahahahah. Ama kuhusu SUA usipate shida. Dunia ina watu bilioni 5 wote. hawawezi kwenda kusoma Harvard. Na huko huko Marekani (haswa Silicon Valley-california) miaka ya karibuni wamekuwa wanaajiri sana (brain drain) computer programers toka INDIA na CHINA sio HARVARD au CHICAGO tena!!!!. Pana fumbo hapa.

Nisikusumbue wewe endelea na shughuli. Eti Ritz, utani pembeni Zali vipi jamani? Penality ilikuwa for how long? Mimi I loved our crossfire and the missiles Zali threw at me!!!! Nobody asked for a transfusion.

Ila sheikh wangu, ukishamaliza ku-paste page ya 500 kuna maswali hamjajibu. Labda urudie ku-paste kitabu upya.

Yericko, tafadhali mtunzie Ritz yale maswali hadi amalize anachofanya kwa sasa tusimchanganye (Kwa JKT-anakula shushi). MS asiguswe jamani. HAYUMO. Mzee MS heshima yako bwana!!!!!

cc; Nguruvi, Jokakuu, Mohammed Said, Jasusi, Hassanalis, BigShow

Wickama,

Wala unajihisi mie nilikuwa natoa mfano tu, lakini bahati mbaya ndugu yangu umenishambulia bure.
 
Last edited by a moderator:
Wanajamvi, hapa chini nawakumbusha tu kuhusu serikali aliyoiunda Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofuatia mapinduzi yaliyoutimua utawala wa Kisultani visiwani. Baraza la Mawaziri lililoundwa lilikuwa na wafuatao.

nyerere+baraza+la+mwaziri.jpg



  1. Mwalimu Julius Nyerere (Christian): President
  2. Abeid Karume (Muslim): 1[SUP]st[/SUP] Vice President and Minister responsible for Zanzibar affairs.
  3. Rashidi Kawawa (Muslim): 2[SUP]nd [/SUP]Vice President and Minister of Defence and National Service.
  4. Nsilo Swai (Christian): 1[SUP]st[/SUP] Minister of State for Economic Planning in the President’s Office.
  5. Abdulrahman Babu (Arab & Muslim): 2[SUP]nd[/SUP] Minister of State for Economic Planning in the President’s Office.
  6. Amir H. Jamal (Indian & Hinduist) 3[SUP]rd[/SUP] Minister of State for Economic Planning in the Presidet’s Office.
  7. Aboud Jumbe (Muslim): 1[SUP]st[/SUP] Minister of State in the 1[SUP]st[/SUP] Vice President’s Office.
  8. Lawi Sijaona (Muslim): 1[SUP]st[/SUP] Minister of State in the 2[SUP]nd[/SUP] Vice President’s Office.
  9. Bhoke Munanka (Christian): 2[SUP]nd[/SUP] Minister of State in the 2[SUP]nd[/SUP] Vice President’s Office.
  10. Said Maswanya (Muslim): Minister of Agriculture, forests and Animal Husbandry.
  11. Jeremiah Kasambala (Christian): Minister of Commerce and Cooperatives.
  12. George Kahama (Christian): Minister of Transport and Buildings.
  13. Paul Bomani (Christian): Minister of Finance.
  14. Oscar Kambona (Christian): Minister of Foreign Affairs.
  15. Job Lusinde (Christian): Minister of Internal Affairs.
  16. Tewa Said Tewa (Muslim): Minister of Lands, Settlement and Water.
  17. Kassim Hanga (Muslim): Minister of Industries and Mines.
  18. Solomon Eliufoo (Christian): Minister of Education.
  19. Derel Brycesson (British & Christian): Minister of Health.
  20. Michael Kamaliza (Christian): Minister of Labour.
  21. Amri Abeid (Muslim) Minister of development and Culture.
  22. Austin Shaba (Christian): Minister of Housing and Local Government.
  23. Hasan Moyo (Muslim): Minister of Law.
  24. Idris Abdulwakil (Muslim) Minister of Information and Tourism.

Wanajamvi wapendwa wakati huo Mwalimu alipendwa kikweli kweli na Watanzania wote bila kujali dini zao, rangi zao wala kabila zao...sura kwenye hili Baraza la Mawaziri mwaka 1964 ni ushahidi tosha kwamba Watanzania hawakubaguliwa wala kubaguana katika misingi yoyote ile. Mapokezi aliyokuwa anayapata Mwalimu kila alipofanya ziara visiwani hayakuwahi kuwa na mfanowe katika historia ya Zanzibar. Kama alikuwepo Mtanzania mwenye dukuduku lolote ni wale Waislaam wachache walioshindwa kuwashawishi Waislaam wenzao kuwaunga mkono hata kabla ya uhuru walipoanzisha chama cha AMNUT mwaka 1958.

Huu uchochezi tunaoushuhudia hivi leo ulikuja kujitokeza muda mfupi baadaye kutokana na chuki za baadhi ya wazee waliokataliwa katika hila zao za kutwaa madaraka kwa kupitia mgongo wa dini. Njama zilianza kufanyika kutaka kuvuruga umoja wa Watanzania kwa kupandikiza mbegu ya chuki ambayo hadi leo mtoto wa mmoja wa wazee hawa anaiendeleza kama tunavyoshuhudia ndani ya mnakasha huu. Swali la kujiuliza ni hili; hivi hawa Waislaam waliokuwa ndani ya hilo Baraza la Mawaziri kuanzia makamu wawili wa Raisi hadi Waziri wa Sheria walikuwa ni wasaliti kwa wananchi wa Zanzibar na Uislaam?

Je Abeid Karume, Abdulrahman Babu, Kassim Hanga, Amri Abed, Aboud Jumbe, Hasssan Moyo na Idris Abduwakil walikuwa ni wasaliti visiwani Zanzibar? Je Wazanzibari wanayathamini mapinduzi yaliyowaweka hawa madarakani? Je, kwa msingi wa madai ya wachochezi kama Mohamed Said, mapinduzi ya mwaka 1964 yalikuwa haramu? Je Waislam wa bara na visiwani wanawaona hawa kama wasaliti katika Uislaam? Je katika msingi huop huo viongozi wote wa juu wa Jamhuri ya Tanzania ambao wote ni Waislaam, kulingana na uchochezi unaoendelea ni wasaliti katika Uislaam? Je Kikwete, Dr. Bilal, Dr. Shein na Shariff ni wasaliti wa Uislaam?

Nimeipenda sana hii list ya baraza la mawaziri.

Mimi ningekushauri uiangalie kwa jicho la tatu list hiyo kwa kuwatoa wale kutoka Znz ambao wao kwa zaidi ya 99.9% ni waislam. na ubakishe waTanganyika kisha linganisha dini zao.

Hiyo itakupa picha halisi. Kumbuka kuwa Mmamlaka ya BAKWATA MWISHO CHUMBE hayajawahi kufika Znz hata siku moja.

Pole sana

 
Ritz,
Yericko bado yuko kule kule anadhani mie hapa
jamvini nazungumza na yeye wakati yeye ni "rabbit"
katika mbio ndefu ananisaidia mie kuvuta kasi.

Katika mashindano ya mbio kunakuwa na timu moja
labda ina wakimbiaji 4 wanashindana na timu pinzani.

Ili kupata mafanikio huwa hizi timu zinakuwa na pace setter
kuweka spidi ili wavunje rekodi na ushindi upatikane.

Hawa pace setters huitwa rabitts.
Hapa JF sungura wangu ni Yericko Nyerere.

Ananitia spidi ya kueleza mambo mengi ambayo bila yeye nisingeweza
kukwea mti huo.
 
Ritz,Yericko bado yuko kule kule anadhani mie hapajamvini nazungumza na yeye wakati yeye ni "rabbit"katika mbio ndefu ananisaidia mie kuvuta kasi.Katika mashindano ya mbio kunakuwa na timu mojalabda ina wakimbiaji 4 wanashindana na timu pinzani.Ili kupata mafanikio huwa hizi timu zinakuwa na pace setterkuweka spidi ili wavunje rekodi na ushindi upatikane.Hawa pace setters huitwa rabitts.Hapa JF sungura wangu ni Yericko Nyerere.Ananitia spidi ya kueleza mambo mengi ambayo bila yeye nisingewezakukwea mti huo.
Sheikh Mohamed, wewe ndiye uliyenisababisha mimi kujiunga na JF kutokana na hoja zako. So mimi ni mfuasi wako.Nakuomba kwa heshima na tahadhima mjibu Nguruvi3 na wenzie hayo maswali yao yanayohusu mapinduzi ya Zanzibar.Usipojibu maswali hayo utakuwa hujatutendea haki mimi na familia yangu hapa Mbagala, kwani nyumba mzima na majirani zetu wote tunafatilia mjadala huu na hasa hasa hoja zako wewe. Mjibu Nguruvi3 na wenzie kwa faida ya wakazi wa Mbagala.
 
Nimeipenda sana hii list ya baraza la mawaziri.

Mimi ningekushauri uiangalie kwa jicho la tatu list hiyo kwa kuwatoa wale kutoka Znz ambao wao kwa zaidi ya 99.9% ni waislam. na ubakishe waTanganyika kisha linganisha dini zao.

Hiyo itakupa picha halisi. Kumbuka kuwa Mmamlaka ya BAKWATA MWISHO CHUMBE hayajawahi kufika Znz hata siku moja.

Pole sana




Barubaru,

Salaam Al Habiby.

Wallahi,kama ulikuwamo ndani ya moyo wangu...maana nami nalitaka kuuliza suali hilo hilo tena kwa kunyambua zaidi.
Lakini haina neno Al Akhiy,sitaki kukuharibia hii shughuli ulomwanzia huyo jamaa yako Mag3.

Hii imbalance ya kwenye first Cabinet,inaashiria yakuwa Nyerere hapo hivyo vyeo/nafasi alikua akitoa kwa kuangalia zaidi Udini. Alisahau yakuwa hiyo nchi alokua akiungana nayo/Zanzibar ni Waislamu almost 100%...nafikiri hii fact huyo Nyerere alii-over look au alifanza kwa makusudi!

Kwa mtu yeyote mwenye maarifa na uelewa,ataangalia hiyo idadi ya Waislamu na Wakristo kutoka upande wa Tanzania Bara/Tanganyika,khalafu utajiuliza hao Waislamu wa Tanganyika wako wapi kwenye ile first Cabinet,mbona uwiano hauleti picha nzuri ya nchi/Taifa linalojinasibisha na u-Secular!?

Lakini najua kuna wale fidhuli wa asili na wajuba watatujibu,yakuwa woote walikua ni Makuli!ahaha!!

Hii hali imewaumiza mno Waislamu wa Tanganyika kwa miaka mingi,maana hizo nafasi zao/vyeo ndo imelazim wapewe/wachukue ndugu zao kutoka Zanzibar.

Katika maandiko/vitabu vyake nafikiri Sheikh Mohammed amejaribu kuelezea kwa kina na kiundani masuala haya,tena kwa ustaarabu mwingi mno.

Nafikri hawa jamaa kila khabari waletayo,ambayo wao hufikiri ni mpya miongoni mwao,hawajui yakuwa ndo wanazidi kujitia mwiba na majiti ya roho, na kusababisha masuali mengine mengi zaidi dhidi yao wao wenyewe.

Kwasisi wengine hizi khabari zoote ni za kawaida na ni za kitambo mno,ndo maana Sheikh Mohammed na nduguze wengine kufikia mpaka kuandika vitabu na kubainisha mengi kwa utuvu wa kitaaluma...mpaka leo ni yupi alotokea kuwajibu kitaaluma,zaidi ya tashtit na kebehi za kitoto!?

Insha Allah tuendelee na mnakasha Al Akhiy.

Ahsanta.

Cc;Ritz
 
Sheikh Mohamed, wewe ndiye uliyenisababisha mimi kujiunga na JF kutokana na hoja zako. So mimi ni mfuasi wako.Nakuomba kwa heshima na tahadhima mjibu Nguruvi3 na wenzie hayo maswali yao yanayohusu mapinduzi ya Zanzibar.Usipojibu maswali hayo utakuwa hujatutendea haki mimi na familia yangu hapa Mbagala, kwani nyumba mzima na majirani zetu wote tunafatilia mjadala huu na hasa hasa hoja zako wewe. Mjibu Nguruvi3 na wenzie kwa faida ya wakazi wa Mbagala.

[h=3]Multiple IDs at work...ha haa haa.[/h]
 
Sheikh Mohamed, wewe ndiye uliyenisababisha mimi kujiunga na JF kutokana na hoja zako. So mimi ni mfuasi wako.Nakuomba kwa heshima na tahadhima mjibu Nguruvi3 na wenzie hayo maswali yao yanayohusu mapinduzi ya Zanzibar.Usipojibu maswali hayo utakuwa hujatutendea haki mimi na familia yangu hapa Mbagala, kwani nyumba mzima na majirani zetu wote tunafatilia mjadala huu na hasa hasa hoja zako wewe. Mjibu Nguruvi3 na wenzie kwa faida ya wakazi wa Mbagala.


Pain Killer,

Poleni nyoote wana wa Mbagala,Mola takuzidishieni sabra kwa mustahamala mfanzao.

Sheikh Mohammed,kishatoa majibu yoote ya hayo masuali yao kwenye vitabu na maandiko yake mengi. Nina hakika utakua unayajua kwa kina kama kweli wewe ni "mfuasi wake" mtiifu kama unavyodai ndugu yetu. Japo nina hakika yeye hatopenda wewe kutumia neno hilo,na wala hajui na hajawahi kuwa na wafuasi popote pale!

Kinachotumika hapa ni technicalities tu,na kwakuwa Sheikh Mohammed ni Scholar/msomi wa hali ya juu,anafahamu mbinu na ujanja woote utumikao hapa.

Kumbuka yakuwa mpaka sasa huo uchochezi,ugaidi na uhaini bado haujathibitishwa popote pale!...sasa hii ilobaki ndo inajaribu kutumika kama bakora/fimbo ya kuthibitsha yayo.

Niwie radhi kwa kuingilia kati mawasiliano yako matukufu na Sheikh Mohammed,na pia niswamehe kwa huo uchechefu wangu.

Ahsanta sana.

Cc;Sheikh Mohammed Said
 
Sheikh Mohamed, wewe ndiye uliyenisababisha mimi kujiunga na JF kutokana na hoja zako. So mimi ni mfuasi wako.Nakuomba kwa heshima na tahadhima mjibu Nguruvi3 na wenzie hayo maswali yao yanayohusu mapinduzi ya Zanzibar.Usipojibu maswali hayo utakuwa hujatutendea haki mimi na familia yangu hapa Mbagala, kwani nyumba mzima na majirani zetu wote tunafatilia mjadala huu na hasa hasa hoja zako wewe. Mjibu Nguruvi3 na wenzie kwa faida ya wakazi wa Mbagala.

Ooooho my god!

Mungu awape nguvu na uvumilivu wakufuatilia uzi huu,

Bila shaka mzee wetu Mohamed Said atawatendea haki watz wenzake!
 
Wickama,

Wala unajihisi mie nilikuwa natoa mfano tu, lakini bahati mbaya ndugu yangu umenishambulia bure.


Shariff Ritz,

Salaam Al Akhiy.

Huyo jamaa yetu Wickama nafikiri yuko sensitive mno. Ni mtu wa kujishuku saana.
Lakini haina neno,mimi binafsi nampenda mno na tamwandikia sasa hivi nimuombe akaniongezee mke wa pili huko kwao Tarime na itakua uzuri kama ana Dadize walobaki japo kiduchu...labda ndo itasaidia ili atufahamu kwa kistaarabu!?ahaha!!

Ahsanta.
 
Ooooho my god!

Mungu awape nguvu na uvumilivu wakufuatilia uzi huu,

Bila shaka mzee wetu Mohamed Said atawatendea haki watz wenzake!

Yericko,

Mbona unajiandikia msgs/posts khalafu unajijibu mwenyewe ndugu yangu!?

Umekutwa na jakamoyo lipi!?

Cc;Ritz
 
GombeSugu,

Sio kweli kama unavyohalalisha kuwa 100% ya Wazanzibar ni Waislamu!

Makanisa yaliyopo Zanzibar unayaweka kundi gani la Wazanzibar?
 
Yericko,

Mbona unajiandikia msgs/posts khalafu unajijibu mwenyewe ndugu yangu!?

Umekutwa na jakamoyo lipi!?

Cc;Ritz

Kuna haja gani mpaka nifike mahali nijiandike na kujijibu mwenyewe?

Angalia IP address na Location kama ni Kigamboni Mbutu mtaa wa Mbarajange!

Hapa ndipo ninapoishi na mida hii nipo Nyumbani na shemeji yako keshanipikia maakuli ya Kizanaki hasaaaa!

Karibu ndugu!
 
Kujumuika ktk saumu haikuwa zawadi kwa Nyerere.Kijana msomi,mwenye hekina wa enzi hizo akiwa ktk kundi la makuli,masheikh na wengine waliokuwa hawana elimu dunia...Nyerere alikuwa superstar haraka kwa vile alikuwa na vionjo vilivyowafanya wazee wamhitaji.Waislama always wana mapingano ktk yao ,the third person alifanya bora wote wakose.

Pia hakuna ushahidi Kuwa Nyerere alifunga ramadhani:rejea hapa
1.walifunga ili kuomba kitu maalumu kwa ajili kitu fulani.Hii ni purely Judeo-Christian.

2.Walifunga ila Nyerere alikuwa kaifunga na kuomba, baadaye ktk kufuturu Nyerere alikuwa nao.Ila kuulizia dawa na si chakula wakati wa wengine wanafuturu ni wazi kuwa nyerere alikuwa anafunga christiani ways.Kufunga muda mefu bila futarii,ila mara chache kula kidogo kitoshacho kutunza uhai.Sasa hapa nyerere alikuwa kakosa maji na pengine na necessary ions kwa ubongo...


Naomba muwe analytical kuliko kuwa storage media.

Hawa ndugu zetu siku zote tuendelea kuwapa darsa pamoja kuwa wanatuletea kejeli na dhihaka kwa wazee wetu wazalendo amabao walikuwa na mapenzi makubwa na Nyerere anagalia hapa chini hizi kejeli.

Kujumuika ktk saumu haikuwa zawadi kwa Nyerere.Kijana msomi,mwenye hekina wa enzi hizo akiwa ktk kundi la makuli,masheikh na wengine waliokuwa hawana elimu dunia...Nyerere alikuwa superstar haraka kwa vile alikuwa na vionjo vilivyowafanya wazee wamhitaji
Wanaukumbi baada ya kumsoma huyu ndugu yetu hebu hapa chini tumsome Nyerere anawazungumziaje hawa Wazee wanaoitwa makuli.
Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa mguu; kila Jumamosi. Baadaye wazee wakanipa baiskeli nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu; kufanya mikutano.

Hivyo ndivyo tulivyofanya. Wazee wakaniamini upesi sana. Tukawa na uhusiano mkubwa sana. Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Abass Sykes (mdogo wake), Dosa Aziz – waliokuwa wengi ni wazee.

Katika kuhutubia mikutano yangu, nilikuwa nikisema: Wazee na Ndugu zangu! Wazee hasa ndio walikuwa na mikutano ya awali ya TAA na TANU.

Mashaalah hapa tumeona Wazee wetu makuli walijibana na vijisenti vyao na kuamua kumnunulia Nyerere baiskeli, mahaba mazito.

Pia hakuna ushahidi Kuwa Nyerere alifunga ramadhani:rejea hapa
1.walifunga ili kuomba kitu maalumu kwa ajili kitu fulani.Hii ni purely Judeo-Christian.
Hakuna alikuambia Nyerere alifunga Ramadhan Nyerere alifunga kwa ajili ya mapambano ya uhuru na kuwasaidia wengine ndiyo maana anasema tulikuwa tunafunga hebu msome Nyerere mwenyewe hapa chini.

Baadhi yetu mtakumbuka safari moja jamaa wa Kenya, hawa akina Tom Mboya (marehemu) walishitakiwa. Tukasema tuwasaidie. Tuwasaidie vipi? Tukasema tufunge. Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo. Tufunge! Tukafunga. Hakuna kula. Na siku ya kufunga tulikuwa na mkutano Bagamoyo. Tukaenda huko. Tukafanya mkutano hadi saa 12 jioni.

Wanakumbi hebu tuendelee kumsoma Nyerere mwenyewe anavyoielezea funga halafu tulinganishe na maneno ya huyu ndugu yetu.
2.Walifunga ila Nyerere alikuwa kaifunga na kuomba, baadaye ktk kufuturu Nyerere alikuwa nao.Ila kuulizia dawa na si chakula wakati wa wengine wanafuturu ni wazi kuwa nyerere alikuwa anafunga christiani ways.Kufunga muda mefu bila futarii,ila mara chache kula kidogo kitoshacho kutunza uhai.Sasa hapa nyerere alikuwa kakosa maji na pengine na necessary ions kwa ubongo...
Wanaukumbi hebu chini hapa tujitulize tumsome Nyerere mwenyewe anavyofafanua vizuri kuhusu walivyokuwa wanafunga.
Baada ya mkutano tukaenda nyumbani kwa Mzee Mohamed Ramia (marehemu). Hapa ndipo tulikuwa tumefikia. Mimi nikamuuliza mzee: Sheikh, una Aspro? Akajibu: Kwa nini unataka Aspro? Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kwelikweli. Akasema subiri.

Tulisubiri hadi saa ya kufuturu. Tukafuturu vizuri. Mzee Ramia akaniuliza: bado unataka Aspro? Nikajibu kichwa sasa hakiumi. Kumbe ilikuwa njaa.

Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka, tulishikamana sana. Tulishirikiana sana na wazee."'

Wanaukumbi nadhani mesoma wenyewe hali ilivyokuwa pamoja na kejeli na dhihaka kutoka kwa hawa ndugu zetu wanaowaita wazee wetu makuli lakini sisi bado tupo nao kama Watanzania wenzetu.
 
Wickama,

..wasikusumbue hao. wengine ni binamu wa Sultani Jamshid.

..kama ni lawama apewe Muingereza kwa kubakisha utawala haramu wa Sultani.

..wanadai Sultani alikaribishwa na wenyeji kumuondoa Mreno. lakini huo siyo uhalali wa yeye kukaa hapo miaka yote najuu yake kuuza watu weusi Utumwani.

..Tanzania na sisi tulikaribishwa na Waganda kumuondoa nduli Iddi Amini, lakini baada ya kumaliza shughuli hiyo tulifunga virago na kuondoka.



JokaKuu,

Nimechungulia ile post yako kwenye Thread fulani humu Jf,ati ukiamrisha na kutaka Wazanzibary woote wajikusanye na mizigo yao uwakute Port/s tayari kwa deportation!?ahaha!!...hata wewe JokaKuu ndugu yangu ni wa kusema yale!?ahaha!!...haina neno ndo mambo ya minakasha.

Hayo mambo ya Utumwa na vile Vita haramu na vya kinafiki vya Uganda,nafikiri kwa sasa tuiyaache ili tusiharibu hii mada...la muhimu turudi kwenye kuthibitisha kwa kina na kiundani "Uchochezi,Ugaidi na Uhaini".

Unasemaje "tulikaribishwa" na Waganda halafu kumaliza "shughuli" tukaondoka!?...kwa legitimacy ipi iliyokuwepo wakti huo hapo Uganda!?

Soote tunajua jinsi gani Nyerere alivyoingilia kiundani internal politics za Uganda.


Nafikiri kuna wakti hata Mzee Jasusi,pia aligusia na kuunga mkono baadhi ya yale nilokua nazungumzia /kuhoji...nina maana uhusiano wa hizo Ugandan gangs na Nyerere.

Nyerere alitumia rasilmali na jasho jingi la nchi yetu maskini, ili kuvilea na wakti huohuo kuvigombanisha vikundi mbalimbali vilivyokua chini ya wale wauaji,mafisadi,majangili, matapeli na "wanae vipenzi" kina Yusuf Kirunde Lule,Godfrey Binaisa,Obote na Yoweri Kaguta.

Tuyaache haya majambo kwa sasa...nakujibu ile bayana yako ya jana nafikiri ndugu yangu punde tu,maana leo nimapata kifursa kiduchu.

Ahsanta sana.
 
Multiple IDs at work...ha haa haa.
ID yangu ni moja tu na ni mara yangu ya kwanza kujiunga na JF. Kwani kosa langu ni nini?

Bado tunamuomba Sheikh Mohamed ajibu hayo maswali yanayohusiana na mapinduzi ya Zanzibar.

Kwani mnaposema huu mjadala unafatiliwa na watu 200,000 unamaanisha nini? Mbuzi au binadamu?

Kama unakubali hao wafatiliaji ni binadamu basi mimi ni mmoja wapo na nipo hapa kujifunza bila kuege
mea upande wowote.

Sheikh Mohamed siye ndugu zako tunasubiria majibu ambayo yatatufanya tutembee kifua mbele kwa kuwa na mwalimu kama wewe. Shukran
 
Shariff Ritz,

Salaam Al Akhiy.

Huyo jamaa yetu Wickama nafikiri yuko sensitive mno. Ni mtu wa kujishuku saana.
Lakini haina neno,mimi binafsi nampenda mno na tamwandikia sasa hivi nimuombe akaniongezee mke wa pili huko kwao Tarime na itakua uzuri kama ana Dadize walobaki japo kiduchu...labda ndo itasaidia ili atufahamu kwa kistaarabu!?ahaha!!

Ahsanta.

Al Habiby gombesugu,

Mwenzako mimi tayari nimeishafanya
[h=3] Masna , Nikah Tarime ha ha haaa.[/h]
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom