Sijui ni kwanini watu hawasomi na kuelewa point ya mtu.
Nadhani ni kwasababu wanaongozwa na hasira na jazba.
Niliposema Mohamed Said amejinukuu nina maana kuwa yeye anasema kuna source.
Mimi nasema hakuna source ya info zake isipokuwa source ni yeye kujinukuu na anadanganya kuwa kuna anonymous source. Angesena source ni yeye kusingekuwa na tatizo, tatizo ni kujikweza na kukweza jambo kama kawaida yake
Sasa hapa simwombi alete source ninachotaka ni kumdhihirishia kuwa yeye anadanganya jamvi kwa kusema zile taarifa za Zanzibar kuna mahali amezitoa na hapo ndipo hoja ilipo. Aliogopa kujinukuu akasingizia kuna source.
Ukinisoma nimesema hatuhitaji ataje jina, paper, kitabu, source au chochote bali atupe muda kazi hiyo ilipofanyika kwa range (1950-1970) basi
Hoja hapa si yeye aweke nukuu, hoja ni kuwa amejinukuu! hilo pia si tatizo, tatizo ni pale anapotaka kulifanya jamvi liamini kuwa hizo ni habari nyeti sana kutoka karika source maalumu huku tukijua kuwa ni yeye binafsi.
Muongo mkubwa huyu mzee na sijui urongo unamsadiia nini.
Naomba mnielewe hoja si yeye kuleta source, hoja ni kuwa anajifanya ana vyanzo muhimu sana ili kufunga akili zatu waamini kile anachokisema wakati tunafahamu kuwa ni maneno yake ametunga halafu anasema yametoka katika source.
Lengo ni kuonyesha kuwa haaminiki, hana credibility na hiyo ni tip of ice...
Narudia tena habari ya znz aliyonukuu ni yake personal hana source, I can prove it kwa maandishi na hoja zake.
Waheshimiwa Nguruvi3 na Mag3,
Salaam sana ndugu zangu. Tafadhalini pokeani hii bayana yangu kiduchu yenye
hishma na taadhima ilo kuu kwenu.
Kwanini au kitu kipi kinachokufanzeni nyinyi muone yakuwa mtu yeyote kuomba
source/s ya informations zenu binafsi au kutoka kwa
Yericko,ni kutokana na mtu huyo kuwa na jazba au hamaki fulani!?
Inakuwaje leo hamjiulizi yakuwa
Yericko,yuko hapa
takriban nusu mwaka tena huku akijinasibu yakuwa ana "khabar nyingi na ndefu mno" za
Historia ya Tanzania lakini bila ya kuthubutu hata siku moja kutaja "
source/s zake"!?ahaha!!
Lakini cha
kustaajabisha zaidi ni yakuwa, katakata hatoi/hataki na
"source/s zake" wala hapendi kuulizwa hilo suali...na cha
kuhuzunisha zaidi ni ile support mnayompa and all of you just keep follow him blindly and religiously!?ahaha!!
Hivi ndugu zangu,kutokana na usomi wenu wa hali ya juu mlionao na exeperience na exposure zoote za kitaaluma mlizonazo,hamuoni yakuwa mtu kuomba
source/s ya information au datas ni
legitimate question kwenye field yoyote ile muhimu duniani!?
Mimi binafsi,nimeanza kuomba
sources za khabar mletazo hapa
jamvini nyinyi wawili kitambo, tena kwa ustaarabu bila ya hamaki au jazba yeyote,na mpaka leo bado nasubiria
Insha Allah maana najua kwa ustaarabu wenu kamwe hamjanisahau ndugu yenu!?
Kwa hiyo si kweli ya kwamba ati tunafanza/ninafanza hivyo ili kulipiza kisasi kisa yakuwa nanyi mnaulizia baadhi ya
sources toka kwa
Sheikh Mohammed.
Jingine
Muheshimiwa Ngururvi3;usitumie nguvu zako nyingi mno kila wakti kuonyesha ati sisi hatukufahamu point/s zako au ni wazembe wa kufahamu jambo na mengineyo mengi, hasha ndugu yangu.
Mimi binafsi nilishakuambia mara kadhaa hapa
jamvini yakuwa nakusikiza na kukufuatilia
bayana zako tena kiuadilifu,bila ya kujali yakuwa mara nyingi tunajikuta/tunakuwa kwenye mitazamo tafauti!?
Yawezekana ni kweli hatujawahi kwenda Shule,hatujui kusoma wala kuandika,lakini pia tuna
"Tartib Al Adab" zetu zinazotuwezesha na kutusaidia kufahamu majambo mengi mno kwa kina kuliko vile wengi wenu mnavyokhis.
Yeyote kati yenu au atokaye kwenye wafuasi wenu,ni wajibu wake kitaaluma na pia ni haki kama
Mwanajamvi kuomba
source/s ya aina yeyote toka kwa
Sheikh Mohammed...
lakini pia ikumbukwe yakuwa
uamuzi wa mwisho ni wa huyo aombwae-
Sheikh Mohammed na maelekezo atoayo!?
Tukumbuke huyu mtu ni
Scholar/Historian mkubwa mno na pia ni maarufu kwa kiasi chake...kwa hiyo pia ni wajibu wake kufuata kanuni na
ethics za field yake,mojawapo ni
kuhifadhi source/s of information zake when deemed necessary!?
Nimefurahi kuzungumza nanyi kwa pamoja ndugu zangu. Niwieni radhi kwa huo uchechefu wangu kiduchu.
Ahsantani sana.
Cc;Ritz