Uchumba wetu ulikufa sababu ya dini ni tofauti

Uchumba wetu ulikufa sababu ya dini ni tofauti

Mkuu nakumbuka enzi zangu niliwahi kuwa na ukaribu na mtoto wa watu tena walikuwa wa ile iman ya kaptula ndefu ila nilikuja jinasua huko na nikapata somo la oa dini yako oa labila lako kupunguza mizozo ndani ya familia. Baada ya hapo nimekuwa nikishaur sana vijana kuhusu haya mambo
Hamkuwa tu na maelewano
Dini mkaiona ni sababu

Ndoa ni maridhiano si dini
 
Tukubaliane tu kuna makabila bila kuyataja hayastarabika, watu wanapoowana kwa kuchanganya makabila inampa faida mmoja wapo kuadapt ustaarabu na kizazi chake kitastaarabika pia.

Wajinga Wawili wakiowana ni tatizo, na hili ndio tatizo linawakabiri Waarabu, wako wenyewe wana makabila yao kuna mabedui hawezi kuolewa na Kabila lingine, Sasa ikitokea uko Fulani ni wajinga basi ni kizazi chote.

Nioneshe Mwarabu gani uliyesoma naye alikuwa Kipanga darasani?
Nimesoma na waraabu ambao ni vipanga kibao ..kaangalie matokeo ya mtoto wa bakhessa mpaka akapewa scholarship.

Kwa bongo huwezi kuwajua maana Wanasoma elimu tofauti na sisi kama unabisha kaangalie pilots wengi hapa bongo ni jamii gani na mabaharia.
 
Sema hamkupendana
Dini sio tatizo mkiridhiana
Usidanganywe na mtu yeyote, kwenye primitive society kama Tanzania dini ni factor kubwa sana, ni mapenzi ndio yanatiaga watu upofu tu.

Ni either mwanamke abadili dini akufuate imani yako (ndivyo inavyotakiwa iwe) au mwanaume ufuate dini ya mwanamke ( uzuzu huu)
 
Hii ya kuhusu kabila ina sides mbili. Usihitimishe kwa kusema oa/ olewa na mtu wa kabila lako.
Mimi kama mtu niliyeoa mtu wa kabila tofauti kwa miaka 10 sasa ntakukatalia, tena kwa hoja thabiti. Habari za chakula, mila na desturi haijawahi kuwa sehem ya changamoto yetu.

Hata hivyo, kuna waliooa/olewa na watu wa makabila tofauti wanakabiliwa na changamoto za chakula, mila na desturi/ lugha n.k.

Ndio maana nasema, hii hoja ina ambiguity.
Mkuu maswala ya dini na kabila inasaidia kupunguza migongano ambayo si ya lazima ila si kwamba ukioa au kuolewa na mtu wa kabila ama dini moja ndo uko salama la hasha unapunguza migongano tu
 
Mkuu maswala ya dini na kabila inasaidia kupunguza migongano ambayo si ya lazima ila si kwamba ukioa au kuolewa na mtu wa kabila ama dini moja ndo uko salama la hasha unapunguza migongano tu
Dini nakubaliana na wewe, lakini kabila, No! Najitolea mimi mfano.
 
Nimesoma na waraabu ambao ni vipanga kibao ..kaangalie matokeo ya mtoto wa bakhessa mpaka akapewa scholarship.

Kwa bongo huwezi kuwajua maana Wanasoma elimu tofauti na sisi kama unabisha kaangalie pilots wengi hapa bongo ni jamii gani na mabaharia.
Uko mbali na ukweli, mtu anasoma IST unategemea atakuwa kilaza?

Naongelea hawa Waarabu wa buguruni Madenge kama sisi.
 
Wewe ulikuwa haupendwi na vile mlevi hauna swagga ,wengi kama walevi mnakuwaga na sura za kizee wakati bado watoto wadogo.
Kawaida mke ndo anamfuata mume basi angekufuata Kwa namna yeyote ile.
 
Hamkuwa tu na maelewano
Dini mkaiona ni sababu

Ndoa ni maridhiano si dini
Nilipima nikaona siwez ishi na mtoto wa mtu kama nimetorosha mwanafunzi. Kaptula ndefu wanatenga mtoto kama akijiamulia kwenda upande mqingine sasa nikaona nisusiwe mtoto wa watu jw likitokea tatizo ambalo wao ndo wanajua ufumbuzi wakeeeee?
 
Uko mbali na ukweli, mtu anasoma IST unategemea atakuwa kilaza?

Naongelea hawa Waarabu wa buguruni Madenge kama sisi.
Hamna mwarabu wa ovyo nimesoma nao nakuambia hivi nimekaa na jamii izo nazitambua snaa Labda kwa upande wa wanawake ila wanaume mmoja wapo ni rafiki yangu damu kabisa ni daktari mkubwa wa upasuaji.

Ninachokueleza ni ukweli na hata kweny biashara hakuna jamii hapa bongo inawakaribia ..Ngumu sana kuwakuta vyuo vikuu maana hawa wengi ni wazee wa short course na kupenda kusoma book keeping and commerce.

Ukitaka kujua ni wengi nenda chuo kama NIT kweny automobile ukawaone.
 
Ushauri wangu kwa vijana
Oa au olewa na mtu wa dini yako
Oa au olew na mtu wa kabila lako.
Daima utajanishukuru
Narudia
Oa au olewa na mtu wa dini yako
Oa au olewa na mtu wa kabila lako.
Utakuja nishukuru
Mimi maoni yangu ni vizuri kuoana mkiwa na imani moja mambo ya kabila sijui nini si lazima sana,mkatoliki aoane na mkatoliki mwenzake,msabato pia,mlokole halikadhali hii inaimarisha upendo sana
 
Nilipima nikaona siwez ishi na mtoto wa mtu kama nimetorosha mwanafunzi. Kaptula ndefu wanatenga mtoto kama akijiamulia kwenda upande mqingine sasa nikaona nisusiwe mtoto wa watu jw likitokea tatizo ambalo wao ndo wanajua ufumbuzi wakeeeee?
Ishu sio kutenga je akifa atazikwa vip? Kwa taratibu za dini gan?
 
Kwenye dini hapo naweza kukubali maana hata mie ilinikuta , kila mtu akashika njia yake, ila kabila hapana tunaweza kuipa nusu kwa nusu, kuna kijana alikuwa akimcheka kaka yake na kumsema kwanini kaoa kabila tofauti na yakwao, kaka mtu akatulia alipooa yeye sasa ndoa yao hata sijui iliishia wapi hata miezi 6 haikufika waliishia kupata mtoto 1 anayelelewa na Mama Baba haeleweki, kaishia kujilaumu kwanini nimeoa mapema[emoji16][emoji16]
 
Nilipima nikaona siwez ishi na mtoto wa mtu kama nimetorosha mwanafunzi. Kaptula ndefu wanatenga mtoto kama akijiamulia kwenda upande mqingine sasa nikaona nisusiwe mtoto wa watu jw likitokea tatizo ambalo wao ndo wanajua ufumbuzi wakeeeee?
Ungempa mimba
Undugu haukataliwi
 
Usidanganywe na mtu yeyote, kwenye primitive society kama Tanzania dini ni factor kubwa sana, ni mapenzi ndio yanatiaga watu upofu tu.

Ni either mwanamke abadili dini akufuate imani yako (ndivyo inavyotakiwa iwe) au mwanaume ufuate dini ya mwanamke ( uzuzu huu)
Endeleeni
Siku mkikutana humo ndani moto unawaka ndo mtajua dini si kila kitu
 
Mimi maoni yangu ni vizuri kuoana mkiwa na imani moja mambo ya kabila sijui nini si lazima sana,mkatoliki aoane na mkatoliki mwenzake,msabato pia,mlokole halikadhali hii inaimarisha upendo sana
Mnaoana wakatoliki wote, baadaye Mme hajulikani lini alienda kanisani mke naye anahamia kawe ha ha ha
 
Back
Top Bottom