Uchumi Unao, Umeukalia....


Sawa kabisa Pascal,kwa sasa hivi mambo yanayoendelea nchini hata mtoto mdogo anafahamu vile tunauchakata uchumi wetu, je, tunaweza kutabiri kuwa baadae ya muda gani matokeo ya kuchakata uchumi yataleta tija kwa wananchi hadi filed wa chini na kumfanya apate mahitaji yake muhimu (chakula,malazi na makazi?).

Pongezi nyingi sana kwa mkuu wa nchi kuhamasisha uchakataji hasa kwa upande wa miradi hii mikubwa, je shughuli hizi zinamfikia raia hadi wa chini? Simaanishi ajar bure na aletewe mahitaji muhimu na serikali laa hasha,namaanisha mjasiriamali anayejishighulisha kufanya shughuli ndogondogo kujikwamua kiuchumi, anasonga au anakandamizwa na uchumi wa nchi husika?
 
Duh! Kazi kweli kweli!
It's true ni kazi kwelkwel, ila ni kazi halali na ndio ajira inayoongoza duniani kuliko ajira nyingine zote, hivyo sisi wapigania haki huru, hata hawa tinawapigania.

P
 


Eeenheeee, nilikuwa nataka uchakataji huu, na idadi yetu bado ni milioni 55?

Hivi tunakwama wapi? Tukitaka kukaa mahindi nchi jirani walau tupate pesa mipaka inafungwa, Hata humu ndani watu wengi wamekuja na mada za kukatishwa tamaa na juhudi walizozifanya kwenye kujikwamua kiuchumi matokeo yake wamepoteza mitaji yao huko....

Mabenki yapo yanatoa mikopo, shida ni nini? Tunahitaji masters degree na PhD ili tuuchakate uchumi wetu kuleta maendeleo kwa kila mwananchi? Na hii ilete chachu kwa wananchi waliokata tamaa kujituma hasa wakiona jirani amefanikiwa...

Natamani kitu kifanyike ila najikuta nakwama, elimu ya hamasa na research zilizofanyika zikiletwa kwa wananchi zitawaamsha kujituma na hapo serikali pia itakusanya mapato yake. Naona kuna LAXITY mahali, nachelea kusema siasa zinavuruga Mambo haya sababu sijajikita sana kwenye siasa na hii haimaanishi kuwa nimejikita kwenye uchumi las hasha bali Mahaba yamenichosha pia.... Labda na umri nao umenisonga....

Kasinde Matata.
 
Kwa vile kazi ya Kujenga uchumi huwa inachukua muda mrefu, kusema ukweli miaka kumi haitoshi, ndio maana wengine tumeshauri, tukitaka kumfaidi Magufuli, tumuongezee muda, tumpe muda wa Kutosha, akiondoka, aondoke ametuachia Tanzania ya uchumi wa kati.

P
 


Okay, hapo sawa kwa upande wa nchi kwa ujumla na miradi yake kutokana na rasilimali za nchi.

Je, na wananchi wa hali ya chini nao wasubirie miaka 10 ili kuanza kujikwamua kiuchumi?

Naona kiswahili kigumu halafu nashindwa kuandika kilichopo akilini mwangu, sina shida na kiongozi kukaa madarakani hata miaka 30, ila kuna mahali nilisikia (sijui kama ni uzushi au laah) ila uchumi wa nchi ulipimwa kwa kiwango cha mwananchi kuweza kujimudu gharama zake za siku nikimaanisha mtu huyo anaishi kwa shilingi ngapi kwa siku?

Tuchukulie kibarua aliyeajiriwa kwenye kiwanda cha kukamua mafuta ya kupikia, malipo yake ni ya siku (sina takwimu wanalipwaje) ila akirudi nyumbani ana gharama za kuendesha maisha zinamsubiria... Kodi ya pango, chakula, kama ameoa watoto na mke, elimu ya wanae, nayeye ajiendeleze walau aweke akiba au aanzishe kamradi n.k n.k.

Kipindi cha mzee Mkapa ilisemekana mtu wa hali ya chini anaishi kwa shilingi 1,000/- natamani kujua kwa sasa ni shilingi ngapi.

Nilijaribu kupitia tovuti ya takwimu, benki kuu na wizara ya fedha ila sikufanikiwa kuona kitu.

Anyways uchumi ni mpana sana, na una vigezo vya kuzingatia wakati wa kuuchakata. Eehehehee nimekumbuka elimu ya sekondari.... Ceteris Paribas... Other things remains constant....

Eeehhh acha nikachakate muhogo uchumi ushanivuruga, na hivi wengine hatuna huo uchumi.... Majangaa.
 
Hapo ulipoanza na maneno ya kumuomba Mungu umenikumbisha huu wimbo.


Yeah uchumi ukitumika vizuri huleta manufaa ila ukiutumia vibaya inakuwa sawa na kuukalia tuu, unajikuta unabaki Kuwa masikini.
hahahaaaaaa niko Kijiweni na mzee mmoja hapa tunausikiliza huu wimbo na nakuja hapa naukuta umeuweka imenibidi nifurahi tu.
 
Hongera kwa hamasa yako kubwa kwangu
 

Tafuta mbebez mwenye hela kama Lemutuz aokoe jahazi. Hii ilisababisha dada tunayependana anikimbie. Sababu eti sina future
 
Mabwana wadogo wa instagram na twitter hawawezi kukuelewa unamaanisha nini.

Sisi wahenga tumekosoma vyema. Mwalimu Nyerere alikwenda Zanzibar, akawaambia uchumi mnao lakini mmeukalia. Wazanzibari wakahamaki, yakheee umetutukana yakheee.

Mwalimu akawaambia mmenielewa vibaya, namaanisha maliasili tunazo halafu tunalalamika umaskini.
 


Heheheheheheee uchumi huu unaleta shida... Kauli ni tungo tata kidogo hehehehee.
 
Times change and speak volumes. Maisha mtihani sana. Mambo yakikugomea unaokoka kama konki ili kuepusha shari


Wengine majina yetu ni nafuu ya shari....

Haikwepekii, umeukaliiiaaaaaa....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…