Uchumi Unao, Umeukalia....

Uchumi Unao, Umeukalia....

Kasie

Platinum Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
22,379
Reaction score
41,294
Habari za kuikaribisha wikiendi....na poleni na majukumu ya kutwa nzima na wiki nzima.

Kichwa cha uzi ni usemi uliovuma sana miaka hiyoo niko jeshini...na waliotamka usemi huo walikuwa na maana tofauti tofauti.

Tukichukulia kama sentensi ilivyo, mtu anashangaa unakuwaje masikini wakati umezungukwa na bahari,mito,maziwa,misitu yenye wanyama kama vivutio,milima, madini, ardhi yenye rutuba na kustawi mazao mengi...haingii akilini unakuwaje masikini na kula ya wananchi wa nchi husika ni ya sintofahamu....

Wanawake...ilikuwa fumbo kwao, utasikia mtu anamwambia mwanamke, unalia lia shida wakati uchumi unao na umeukalia.....
Siku hizi siusikii huu usemi, nimekumbuka zamani.

Kwa wale wahenga wenzangu, wewe unafahamu maana ipi?

Kasinde
 
Kwanza Tuombe Mungu, Baba yetu utupe mkate wetu wa kila siku, Tunajua kuna kupata na kukosa sisi waja wako watenda dhambi utusamehe.

Nguvu,Ulimi,Uchumi unao unaukalia tu? Hasa dada zetu walipenda sana kupeana motisha kwa maneno haya. Kuna walotumia vyema Uchumi wao wakafanikiwa na kuna wengine waliishia kupata mabalaa makubwa.
 
Umenikumbusha mbali sana! Enzi hizo mwanamama akiwa na shida unamwambia unahangaika kwa nini wakati uchumi unao na unaukalia, na hasa akiwa na makalio makubwa. Enzi za magangwe, watenmi, wasela nondo, nk
 
Hapo ulipoanza na maneno ya kumuomba Mungu umenikumbisha huu wimbo.

Yeah uchumi ukitumika vizuri huleta manufaa ila ukiutumia vibaya inakuwa sawa na kuukalia tuu, unajikuta unabaki Kuwa masikini.
 
Semi za zamani balaa kabisa. Wakenya walimwambia hayati mzee Jomo Kenyatta ‘Harambee. Tuko nyuma yako baba.’ Yeye akawajibu ‘Pambaf...zenu.Huko nyuma yangu mnafanya nini?

Aaahahahahahahaa
 
Umenikumbusha mbali sana! Enzi hizo mwanamama akiwa na shida unamwambia unahangaika kwa nini wakati uchumi unao na unaukalia, na hasa akiwa na makalio makubwa. Enzi za magangwe, watenmi, wasela nondo, nk

Hapo bolded in red ni sawa kabisa, na kuna wanawake baadae ya kusikia hivyo waliutumia haswa uchumi wao.

Japo nchi haina makalio, Ila pia usemi huu unaugusa nchi, uchumi umejaa tele ila wananchi wameukalia uchumi huo..... Hakika sentensi tata hii heheheee
 
Vijana amkeni vijana amkeni tujenge taifa vijana amkeni tufukuze umaskini sisi ndio viongozi wa baadaye na serikali ndio inayotutegemea kufanya makubwa huwa nikiwaza hili jambo linanitia hamasa katika kupamba na maisha Mungu uliyebinguni tunaomba utusamehe makosa yetu kama nasi wanaotukosea na utupe mkate 🍞 wetu kila siku tupe amani umoja upendo na mshikamano kulisogeza taifa letu maskini lakini lenye utajiri wa mali asili Mungu naomba utusaidie Amina
 
Duh....!. Umenikumbusha mbali!.
P

Karibu Pascal, umekumbuka kipi haswa?

Vipi kwa nchi yetu, bado tumeukalia uchumi au tumeshainuka kuutumia? Je, uchumi wetu unatunufaisha au pamoja na kuutumia/ kuuchakata bado haina tofauti na kuukalia?

Wanawake wa siku hizi hawaujui huu usemi hehehehee.

Kasinde.
 
Habari za kuikaribisha wikiendi....na poleni na majukumu ya kutwa nzima na wiki nzima.

Kichwa cha uzi ni usemi uliovuma sana miaka hiyoo niko jeshini...na waliotamka usemi huo walikuwa na maana tofauti tofauti.

Tukichukulia kama sentensi ilivyo, mtu anashangaa unakuwaje masikini wakati umezungukwa na bahari,mito,maziwa,misitu yenye wanyama kama vivutio,milima, madini, ardhi yenye rutuba na kustawi mazao mengi...haingii akilini unakuwaje masikini na kula ya wananchi wa nchi husika ni ya sintofahamu....

Wanawake...ilikuwa fumbo kwao, utasikia mtu anamwambia mwanamke, unalia lia shida wakati uchumi unao na umeukalia.....
Siku hizi siusikii huu usemi, nimekumbuka zamani.

Kwa wale wahenga wenzangu, wewe unafahamu maana ipi?

Kasinde
Wewe tu muhenga umepitwa na wakati lakini Vibinti vya 18-25 vinatumia UCHUMI wao vizuri sana.
 
Vijana amkeni vijana amkeni tujenge taifa vijana amkeni tufukuze umaskini sisi ndio viongozi wa baadaye na serikali ndio inayotutegemea kufanya makubwa huwa nikiwaza hili jambo linanitia hamasa katika kupamba na maisha Mungu uliyebinguni tunaomba utusamehe makosa yetu kama nasi wanaotukosea na utupe mkate 🍞 wetu kila siku tupe amani umoja upendo na mshikamano kulisogeza taifa letu maskini lakini lenye utajiri wa mali asili Mungu naomba utusaidie Amina

Maombi yafaa yaendane na kunyanyuka na kuuchakata uchumi ili ulete Tina na mabadiliko kwa wananchi wake.

Raia wa nchi nyingi wanatushangaa, tunakuwaje masikini ilhali uchumi tunao? No kiasi cha kuuchakata ipasavyo na kila mwananchi apate sehemu ya mahitaji muhimu, CHAKULA, MAVAZI na MALAZI/MAKAZI. Elimu ni muhimu ila si lazima iwe elimu ya mfumo wa mkoloni. Hata elimu asilia ya namna ya kutumia rasilimali zetu pia ni elimu tosha.

Wananchi wakipata elimu namna ya kulima kilimo cha kisasa,namna ya kuhifadhi mazao kwa muda mrefu, namna ya kutumia ardhi yenye rutuba bila kutumia mbolea na kuizeesha ardhi, namna ya kuvua samaki na kuacha waendelee kuzaana, namna ya kusindika vyakula na kuboresha miundombinu ili maeneo yenye ukame na uhaba wa maliasili wazipate na maisha Kuwa bora kwa kila mtanzania.....

Tunakwama wapi?
Mbona uchumi tunao??! Tena wa asilia tuu.

Hapo hujagusa madini.....
 
Wewe tu muhenga umepitwa na wakati lakini Vibinti vya 18-25 vinatumia UCHUMI wao vizuri sana.

Kwa kweli nimepitwa, ila zana ya kutumia uchumi ni ukuletee maendeleo, hao mabinti wameendelea kwa kuutumia uchumi wao?

A nchi je? Bado tumeukalia uchumi au tunachakata mapumba?
 
Karibu Pascal, umekumbuka kipi haswa?

Vipi kwa nchi yetu, bado tumeukalia uchumi au tumeshainuka kuutumia? Je, uchumi wetu unatunufaisha au pamoja na kuutumia/ kuuchakata bado haina tofauti na kuukalia?

Wanawake wa siku hizi hawaujui huu usemi hehehehee.

Kasinde.
Kwa upande wa uchumi wa taifa, Tanzania tunapaa, midege angani, mabarabara ya juu kwa juu, SGR, Stigler Gorge, Tanzania ya Viwanda tukielekea kuwa nchi ya uchumi wa kati, uchumi wa gesi na Tanzania kugeuka a donor country.

Kwa upande wa ule uchumi ule wa Dada zetu wale wanaokalia, mimi nimewapigania sana ile biashara yao irasimishwe, ihalalishwe, iwekewe utaratibu, itengewe maeneo rasmi, watu wafanye kazi walipe kodi. Jijini Dar Massage zimetapakaa watu wanakuwa Massaged asubuhi, mchana, jioni na usiku kucha, lakini serikali hazipati chochote.

P
 
Kwa kweli nimepitwa, ila zana ya kutumia uchumi ni ukuletee maendeleo, hao mabinti wameendelea kwa kuutumia uchumi wao?

Wanaendelea vizuri kula vichwa watu na BAHATI zao Kasie.

A nchi je? Bado tumeukalia uchumi au tunachakata mapumba?

Kama nchi Uchumi ulishamalizwa, kipindi cha Nyerere ndio tulikuwa tumekalia Uchumi.
 
Kwa upande wa ule uchumi ule wa Dada zetu wale wanaokalia, mimi nimewapigania sana ile biashara yao irasimishwe, ihalalishwe, iwekewe utaratibu, itengewe maeneo rasmi, watu wafanye kazi walipe kodi. Jijini Dar Massage zimetapakaa watu wanakuwa Massaged asubuhi, mchana, jioni na usiku kucha, lakini serikali hazipati chochote.
Duh! Kazi kweli kweli!
 
Uchumi tumeukalia kwa asilimia mia.Fursa hatuzioni.Tanzania tuna upungufu wa mafuta ya kula kwa asilimia 75% lakini Tuna zaidi ya ekari millioni zenye rutuba ya kulima Karanga,Alizeti,Ufuta,mawese nk tunanunua mafuta kwanye Nchi yenye visiwa Malaysia na isiyo na rutuba.Wengi wanatamani kwetu na wakija wanapiga hela sisi hatuoni fursa.Hicho ni kimoja tu kati ya vingi.Au mpaka waje wakolini tena?
 
Back
Top Bottom