Angalia mwamerika huyu anayeishi kwenye nchi yenye uchumi wa juu
View attachment 1510546
Nafikiri kuna haja ya kuiandikia Benki ya Dunia barua ya kupinga kuwa Tanzania haijafikia uchumi wa kati.
Ni tofauti kabisa kumlinganisha yule bibi na huyo Mmarekani.
Huu ni mfano wa hovyo kabisa wa kulinganisha.
Lakini mimi nayaona matumaini makubwa sana kwa yule bibi na familia yake.
Kwanza nyumba yake kuezekwa kwa nyasi si hoja. Hiyo nyumba ilivyo haimuonyeshi kuwa hali yake ya kipato ni duni. Kuna vitu vingine kwenye picha hiyo vinavyoweza kuonyesha kupungukiwa kwa bibi na watu wake
Dar es Salaam yetu ya leo pale kariakoo ni tofauti kabisa na Dar es salaam ya miaka michache iliyopita. Ukitafuta picha za Uhuru 1961, utaiona Kariakoo ile ikiwa na vijumba vya makuti. Magomeni nzima kuondoa 'kota' ilikuwa ni makuti tupu. Leo huyaoni tena.
Na hizi nyuma huko vijijini zimeanza kupotea, ndio maana nadhani hata mleta mada akaona aitumie kama mfano wa hoja yake (ambayo kwa bahati mbaya ni kinyume cha anayoyashikia bango).
Sio hivyo tu, hiyo hiyo Marekani, rudi nyuma miaka 30 tu uangalie hali za maisha ya wananchi wake ni tofauti kabisa na hawa unaowaona leo.
Tanzania yetu hii, ikitulizana, ikaacha kufanya mambo ya hovyo hovyo yasiyofaa (nazungumzia viongozi waliolewa madaraka na kukandamiza wananchi bila ya sababu zozote); ipe miaka kumi, (inawezekana huyo bibi akawa hayupo wakati huo, lakini hilo ni kudra za Mwenyezi Mungu); Lindi hiyo itakuwa tofauti sana na hii Ruangwa ya leo.
Tumefikia kwenye 'inflection point' ambapo tunatakiwa kuanza kuona mabadiliko ya maisha ya watu yakitokea kwa haraka sana.