KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Unazunguka zunguka kote huko kujaribu kukimbia mfano ulioutoa hapo wa hao watu wawili, Bi Kizee wa Ruangwa na huyo omba omba wa Marekani.Unejitahidi kuandika, lakini sioni unachojaribu kueleza kuhusiana na picha hiyo. Utajiri wa taifa hauna maana ya utajiri wa mtu mmoja mmoja. Taifa tajiri kama marekani nalo lina maskini kama huyo na vivyo hivyo hata sis tulipokuwa uchumi wa chini bado pia tulikuwa matajiri wengi tu. Uchumi wa nchi nunapimwa kwa averages, na ni lazima kuna watu wenye uchumi wa hini sana, na wale wenye uchumi juu sana lakini kipimo kinachoongelewa ni average tu. Kutafuta watu maskini na kuwatumia kwa extrapolation kuwa nchi yote ni masikini ni ufinyu wa mawazo, kwani unaweza pia kutafuta matajiri wachache akina Bakhressa na kuwa kuwatumia kusema nchi ni tajiri.
Ni mfano usioshabihiana kabisa kwa kila namna yoyote. Ni mfano wa hovyo.