Ndiyo hapo naona mwanamke akifanya kazi au biashara pesa yake haina msaada kama mwanamme bado yupo ,itakuja kuwa na msaada endapo m/me akifariki.jamaa mambo yakamzidia kwani alikuwa na marejesho ila bado alitakiwa kufanikisha mahitaji yote ya ndani kwa 100%
Huo ni ubinafsi uliopitiliza. Kama umemsoma vizuri mtoa mada, aliingia madeni ya mkopo ili mke apate mtaji wa biashara. Baada ya kujipata, hata hakumbuki aliyemuwezesha huo mtaji wa biashara ambao leo hii aniringia ulitoka kwa mume wake.Mwanaume kipato cha mwanamke daima hakikuhusu.
Mwanaume simama na majukumu yako otherwise utanena kwa lugha humo ndani ya jela yako.
Watu wameoa mawaziri na bado huduma zipo pale pale na wanaambiwa kabisa baba naomba hela 😆 🤣 baba tuletee vitu friji limekuwa jeupe!!!!
Ningependa kupinga hii dhana kwamba mwanaume ndiye anayepaswa kubeba kila jukumu la kifamilia wakati mwanamke ana kipato chake. Zamani mfumo huu ulikuwa na mantiki kwa sababu wanawake wengi hawakuwa kwenye ajira rasmi, hivyo mwanaume alibeba sehemu kubwa ya mahitaji ya familia. Lakini dunia imebadilika; wanawake sasa wanasoma, wanafanya kazi na wanapata kipato, na hilo ni jambo zuri.Mwanaume kipato cha mwanamke daima hakikuhusu.
Mwanaume simama na majukumu yako otherwise utanena kwa lugha humo ndani ya jela yako.
Watu wameoa mawaziri na bado huduma zipo pale pale na wanaambiwa kabisa baba naomba hela 😆 🤣 baba tuletee vitu friji limekuwa jeupe!!!!
UmemalizaHuo ni ubinafsi uliopitiliza
Huo ni ubinafsi uliopitiliza. Kama umemsoma vizuri mtoa mada, aliingia madeni ya mkopo ili mke apate mtaji wa biashara. Baada ya kujipata, hata hakumbuki aliyemuwezesha huo mtaji wa biashara ambao leo hii aniringia ulitoka kwa mume wake.
aisee pole sana kaka ila wanawake sisi hatuelewi tunataka ninina wanaume pia hamutuelewi mpka siku tunaingia kaburinUzi bora kabisa huu kwa wanaume mimi mwenyewe ishanitokea hii huko nyuma kuna dili la pesa nilipiga kwa kampuni niliyokuwa nafanya kazi kwa muhindi ile pesa nikafanya kosa nikamfungulia biashala kubwa sana ya vipodozi wife maeneo ya kinondoni dah ishu job ikawa kubwa kesi mahakamani nikapigwa segelea miezi 6 kuja kutoka namkuta wife yupo na mtu mwingine na mimba juu
Hivi ndivyo inapaswa kuwa lakini itachukua muda sana ubinafsi wa ke uje kueleweshwa kuhusu hili. Hatusemi biashara yake iwe ya familia bali mnaweza kujadili na mkaelewana mkafungua joint A/c ambayo kila mmoja atachangia ustawi wa maendeleo ya familia. Hii itapunguza ile dhana ya changu ni changu (ubinafsi)ni suala la watu wawili wanaojenga familia moja kushirikiana, kujadiliana na kusaidiana kwa ajili ya ustawi wa familia yao.
Unayosema yote hayo ni sawa.Ningependa kupinga hii dhana kwamba mwanaume ndiye anayepaswa kubeba kila jukumu la kifamilia wakati mwanamke ana kipato chake. Zamani mfumo huu ulikuwa na mantiki kwa sababu wanawake wengi hawakuwa kwenye ajira rasmi, hivyo mwanaume alibeba sehemu kubwa ya mahitaji ya familia. Lakini dunia imebadilika; wanawake sasa wanasoma, wanafanya kazi na wanapata kipato, na hilo ni jambo zuri.
Sisemii kwamba kila kitu katika familia kigawanywe 50/50. Hapana. Mwanaume anapaswa kusimama kwenye majukumu yake na kuwa tayari kuihudumia familia yake. Lakini inapojitokeza changamoto au hitaji fulani la kifamilia, wanandoa wanapaswa kukaa pamoja na kuangalia namna watakavyolitatua kwa kutumia uwezo na rasilimali walizonazo wote.
Pia, tunapozungumzia usawa wa haki, tusichague tu sehemu zinazotunufaisha. Kama tunatetea haki sawa katika elimu, ajira, fursa na kujitegemea kiuchumi, basi tunapaswa pia kuwa tayari kukubali kwamba katika maisha ya familia, kila mmoja anaweza kuwa na nafasi ya kuchangia pale inapohitajika. Hii haimaanishi kwamba mwanamke lazima abebe majukumu sawa na mwanaume, bali ina maana tusitumie “usawa” pale unapokuwa na faida upande mmoja, halafu tunapofika kwenye majukumu tuseme hayo ni ya upande mwingine tu.
Kama tumeamua kuishi kama familia moja na kusema tumeungana kuwa kitu kimoja, basi lengo linapaswa kuwa ustawi wa familia, si nani amebeba asilimia ngapi. Mwanamke ana haki ya kufanya kazi na kutumia kipato chake, lakini anapokuwa na uwezo wa kusaidia familia wakati wa uhitaji, si vibaya kufanya hivyo. Hili si suala la mwanaume kumtegemea mwanamke, wala si suala la 50/50; ni suala la watu wawili wanaojenga familia moja kushirikiana, kujadiliana na kusaidiana kwa ajili ya ustawi wa familia yao.
Mwanamke yoyote usijichanganye kwamba akiwa vizuri kimaisha inaleta nafuu kwako, hasa hawa wafrika ingawa na wazungu wapo hiviWajumbe naona mnavyochakarika kuuinua uchumi wa nchi na kuhakikisha mkono unaenda kinywani kongole sana.Niende moja kwa moja kwenye jambo letu.
Tumekuwa tukishuhudia jinsi ambavyo wanamke(baadhi🤔) wanajitahidi kuhakikisha wanayapambania maisha na hata kushiriki kutatua changamoto za kifamilia hasa kiuchumi.Hongera sana🫲Shida inakuja pale uchumi wa mwanamke unapoinuka ghafla migogoro nayo hiyooo.Mara mwanamke anakuwa na misimamo yake ,hamtii mume na hata wakati mwingine unakuta mume anafanya project zake mke naye anafanya zake, kila mtu anaspend bila kushirikishana as family.
Nalisema hili huku nikirefer experience from my best friend's life style.
Rafiki yangu alioa mwaka 2022 mwezi wa6,mke alikuwa hana kazi akamtupia mtaji wa kueleweka biashara ikazaa maradufu.
Du ghafla si mambo yakabadilika ndani humo, kukurukakara huku na kule wife akaanza makeke. Mara ghafla wife kabadilika , mara hoo wife hamskilizi mume, mara ooh utaniambia nini?
Siku zimesogea biashara ikawezazalisha mara 2 ya anachozalisha mume. Mume alikuwa mwajiriwa so alikuwa na mikopo kadhaa katika hali ya kujiendeleza ikiwa ni pamoja na mkopo wa ujenzi na aliomfungulia mkewe biashara.Aloooo inaniuma mpaka natamani niishie hapa nisielezeee tena ila waswahili husema maji ukiyavulia nguo huna budi kuyooga ngoja tu nimalizie.
Sasa bwana jamaa mambo yakamzidia kwani alikuwa na marejesho ila bado alitakiwa kufanikisha mahitaji yote ya ndani kwa 100% Kwa vile mtaji wa mke uliendelea kukua akamwomba amsaidie kupunguza marejesho aliyo nayo kwenye baadhi ya taasisi.Akamchomolea nje.
Hajakaaa sawa akaambiwa kwanza wewe si type yangu.Du ukizingatia jamaa alikuwa amepeleka watoto medium schools(walikuwa wamepata watoto kabla ya kufunga ndoa hivyo wakati wanafunga ndoa walikuwa na watoto wakubwan wanaosoma) mzigo ulimuwia mkubwa hivyo kuomba msaada wa mkewe huku akiambiwa kwamba mwanaune ndiye kichwa cha familia atende wajibu wake kama inavyoagizwa kwenye vitabu vya Mungu kwani mke yeye anatekeleza wajibu wake kadiri ya maandiko yaani ku .............kwa uchungu.
Jamaa mara kadhaa amekuja kuomba ushauri kwangu huku akitamania sana mambo yangu yanavyoenda vizuri huku tukishirikishana na wife kukokotoa mambo mbalimbali ya familia.
Kiufupi rafiki yangu huyu anaona kuinuka kwa uchumi wa mke wak ndyo chanzo cha familia yake kuingiliwa na migogoro kwani wife keshamwambia kama mbwai iwe mbwai,Yuko tayari kuanzisha safari mpya.
Aloooooo nitaendelea baadae hebu kwanza nimalizie kazi flani hapa then nitaendelea ila najiuliza kukua uchumi wa mke si ni baraka kwa familia iweje igeuke msumari wa moto wa kuyadhuru mahusiano ya wanandoa hata wakati mwingine kuisambaratisha🥱🤔🫢
Hahaha wanazipata baada ya kusota kwa muda mrefu. Lakini sasa kwa Afrika yetu wanawake ambao sio maskini wanapatikana wapi?Shida ya kuoa mwanamke masikini au kuwa na mahusiano na mwanamke masikini.
Wanawake masikini ni washenzi kupindukia siku wakipata mafanikio.