Uchumi wa Tanzania: Je, Ni Kitendawili au Ni Mazingaombwe Kwa Maskini?

Uchumi wa Tanzania: Je, Ni Kitendawili au Ni Mazingaombwe Kwa Maskini?

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Posts
4,850
Reaction score
9,434
Katika dunia ya leo, mataifa mengi yaliyopiga hatua kubwa kiuchumi na kimaendeleo na kupelekea maisha bora kwa wananchi wake, hasa kuanzia awamu ya pili ya karne ya ishirini (i.e. 1950s) yamefanikiwa kupiga hatua ya maendeleo kutokana na kufuata mikakati na sera zenye mtazamo wa nje kuliko wa ndani – i.e. "outward looking strategies" – kwa maana ya "Export Promotion Strategies". Mataifa haya ni pamoja na yale yanayojulikana kama "East Asian Tigers" – kwa mfano South Korea Malaysia. Katika kundi la nchi hizi zilizopiga hatua kutokana na ‘outward looking/orientation' ni pamoja na nchi kama vile Chile ya Amerika Kusini, lakini pia nchi tatu kutoka barani Afrika - Botswana, Tunisia na Mauritius. Vile vile, mataifa yanayoibuka kwa kasi kiuchumi leo hii duniani (mfano China na Brazil) pia mafanikio yao ymekuwa yanategemea sana exports kwenda soko la dunia.

Angalizo:

Nchi pekee barani afrika ambayo imefanikiwa kuingia katika mapinduzi ya kweli ya viwanda barani afrika (nje ya afrika kusini) ni nchi ya Mauritius.

Mastaajabu ya uchumi wa Tanzania

Cha kustaajabisha ni kwamba kwa Tanzania ni kwamba – performance yetu in terms of exports imekuwa kubwa sana kwa kipindi cha Zaidi ya miaka kumi mfululizo, ambapo katika kipindi cha miaka 2000 – 2012, tuliwashinda wafuatao in terms of export performance:

  • Brazil
  • South Korea
  • Thailand
  • Tunisia &
  • Mauritius
Ni nchi chache sana duniani zilikuwa bora Zaidi kuliko Tanzania katika kipindi husika, ikiwemo China.

Undani wa Export Performance yeetu (2000 – 2012)

Total merchandise of our exports (Tanzania) iliongezeka Zaidi ya mara tano, na kufikia Dollar za Kimarekani billion kumi na mbili ($12 billion dollars) kufikia mwaka 2012. Such growth of exports zilichangiwa na factors zifuatazo:

  • Bei nzuri ya traditional exports zetu kwenye soko la dunia (e.g. Coffee, Tobacco, Cotton & Sisal).
  • Kukua kwa sekta ya madini nchini ambapo exports ya madini iliongezeka kwa kasi kubwa i.e. kutoka $380 million mwaka 2002, na kufikia $2 Billion (two billion dollars) mwaka 2012.
  • Kukua kwa manufacturing sector nchini (Tanzania) kutoka 7% of total merchandise exports mwaka 2002, na kufikia 20% of total merchandise exports in 2012.
  • Diversification yetu katika masoko ya nje ya nchi, kwa mfano, kupungua kwa destination ya mazao yetu kwenda Jumuiya Ya Ulaya (EU) kutoka 50%, na kufikia 30%; Kuongezeka kwa destination ya exports zetu kwenda Asia - kutoka 23%, na kufikia Zaidi ya 30%; Pia muhimu hapa ni kuongezeka kwa exports zetu barani Afrika - kutokea 10% hadi kufikia 30%.
Katika mazingira ya kawaida, kasi hii kubwa ya mauzo ya bidhaa zetu za nje inatakiwa kuwa ni Habari njema, hasa kwa wale ambao walipingana na ‘inward looking' policies wakati wa Mwalimu Nyerere i.e. Import Substitution Strategy, ambao wamekuwa wanaunga mkono Zaidi Export Promotion Strategies. Vile vile, katika mazingira ya kawaida, such an outstanding export performance maana yake ni kwamba katika kipindi hiki, makampuni ya ndani ya nchi (local/domestic/indigenous companies/firms) yamefaifika na fursa zilizojitokeza, kwa mfano:

  • Ongezeko la masoko nje ya nchi kwa wazalishaji wetu (makampuni) kutokana na ufinyu wa soko nchini/limited domestic market.
  • Makampuni ya nyumbani kuongeza ubora na ufanisi wao kutokana na kujifunza from their foreign suppliers, marketing networks & global value chains in general.

Lakini kinyume chake, haya yote hayajajitokeza kwa sababu kadhaa ikiwa ni pamoja na:

  • Moja ni ukweli kwamba concentration ya exports za Tanzania ilikuwa Zaidi kwenye Dhahabu (Gold), which accounted over 40% of the total exports. Matokeo yake ni kwamba, kushuka kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia kunaleta madhara makubwa nay a moja kwa moja katika thamani ya jumla ya mauzo ya bidhaa zetu kwenye soko la dunia.
  • Pili, sehemu kubwa ya bidhaa tunazouza nje hazina thamani kubwa – yani ‘low value-added products' kama vile unprocessed minerals and unprocessed agriculture goods ambayo hayana impact yoyote ya maana katika uchumi wetu kwama maana ya – kuzalisha ajira za maana na zenye kuhitaji utaalam wa Tanzania, lakini pia, kutokana na udogo wa thamani ya bidhaa hizi tunazouza nje, tumekosa fursa ya kufaidika na technology development – technology diffusion and transfer ambayo ingeleta impact yenye manufaa kwa uchumi wa ndani (domestic economy).
Matokeo yake ni kwamba watanzania walio wengi wanazidi kuishi katika lindi la umaskini, huku wengi (hasa vijijini) wakiwa na hali zao zile zile kwa miaka 50 ya uhuru. Kwa mfano, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Afrobarometer unaelezea two main facts:

First Fact:

Kwa mujibu wa Afrobarometer, "Lived Poverty" in Tanzania has increased over the past ten years (2002 – 2012), na kujadili kwamba ‘for the past ten years, economic growth has benefited the wealthy, leaving the poor stuck in poverty, or even getting poorer'. What is more interesting in these findings ni kwamba, ‘lived poverty' katika nchi nyingine ndani ya ripoti husika imepungua – kwam mfano: Botswana, Malawi, Gambia, Ghana.

Second Fact:

Kwa mujibu wa Afrobarometer, "Going without" some basic essentials is more common in Tanzania than in most of the rest of Africa." Afrobarometer wanatoa takwimu zifuatazo:

  • 62% of Tanzanians went without clean water in the past 12 months, compared to an average of 49% across Africa.
  • 71% of Tanzanians went without medicines or medical care in the past 12 months, compared to an average of 53% across Africa.
  • 55% of Tanzanians went without enough food in the past 12 months, compared to an average of 50% across Africa.

Tanzania imepitia inward looking strategies kama njia za kukuza uchumi na kupunguza umaskini (1967 – 1985) ambayo wapo watu wengi wanaojenga hoja kwamba haikumsaidia mtanzania wa kawaida kujikwamua kutoka kwenye lindi la umaskini. Kutokana na hoja hii, nchi yetu ikaingia katika mageuzi ya kiuchumi mkakati mpya wa ‘outward looking' (Export Promotion Strategy) ukaanza kutumika kama njia ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini. Kutokana na uzoefu wetu chini ya mkakati huu, pamoja na matokeo yake ambayo nimeyajadili awali, watanzania tumebakia na maswali mengi sana ya kujiuliza, hasa kuhusiana na suala zima la matumizi ya export promotion strategy kama njia ya kukuza uchumi na kumkomboa mtanzania wa kawaida:

  • Je, kuna haja ya kufanya export promotion kuwa kipaumbele cha taifa kiuchumi?
  • Je, kuna haja ya kulenga bidhaa Fulani Fulani, Sekta Fulani Fulani au masoko Fulani Fulani katika matumizi ya mkakati huu wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini i.e. export promotion strategy?
  • Je, nini ni vikwazo vikubwa kwa makampuni ya nyumbani (domestic companies) katika suala zima la kufaidika na mkakati huu i.e. export promotion strategy?
  • Mwisho, tofauti na Import Substitution Strategy, je, tunakabiliwa na risks gani katika matumizi ya ‘outward-looking strategy'/Export Promotion Strategy katika kufanikisha kukua kwa uchumi wenye manufaa kwa walio wengi?

Sources:

WorldBank Reports & Afrobarometer.

cc. Nguruvi3, Zitto, Zakumi, Ben Saanane, JingalaFalsafa, Jasusi, JokaKuu, Zinedine, ZeMarcopolo, MwanaDiwani, chama, Ritz, zomba, Kobello, Invisible, AshaDii, MTAZAMO, Ngongo, Kimbunga, Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba, HKigwangalla et al
 
Nadhani ni kitendeawili.

Ukuaji wa exports hautakuwa na maana iwapo asilimia chache ndiyo inapatikana for redistribution.
 
Mkuu Mchambuzi ina maana gani kukua kwa uchumi wakati asilimia 55 % wanaenda bila kuwa na uhakika wa mlo wa siku na bado asilimia 71% hawana uhakika wa matibabu au huduma za matibabu au hata hizo hospital na zahanati hazina dawa wala wataalam na vifaa vya kutosha
 
Last edited by a moderator:
Kama tutaendelea kuamini kuwa hatuna uwezo wa kushikilia njia za uchumi sisi wenyewe kwa ushirikiano kiasi na wadau wengine duniani na kuwaachia wageni washikilie njia zote kuu za uchumi, basi kukua kwa uchumi kutabaki kwenye makaburasha ya serikali pamoja na familia chache za madalali wa njia za uchumi.

Mbegu inayopandwa kwamba mtanzania HAWEZI ni sumu kubwa na inasikitisha kuona kuwa inazidi kumea!!!

If you believe that you can not, then you will never be able to. If you believe you can, MAY BE you will be able to.

Choice is ours to make...
 
Hii takwimu sio sahihi.


Mkuu ZeMarcopolo naamini uko kwenye field ya medicine may be au uko kwenye nafasi nzuri ya kusema ni takwimu gani iko sahihi ambayo tunaweza kuichukua inayohusiana na huduma za afya kwa sasa na ikitegemewa ziwe huduma bora sio bora huduma na sio zile za mgonjwa kuandikiwa dawa akanunue pharmacy au kwenda kwenye kituo ambacho hakina hata umeme au hakina doctor kina mhudumu wa afya au kiko kilometer kadhaa kutoka makazi anayoishi na hakina hata usafiri
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ZeMarcopolo naamini uko kwenye field ya medicine may be au uko kwenye nafasi nzuri ya kusema ni takwimu gani iko sahihi ambayo tunaweza kuichukua inayohusiana na huduma za afya kwa sasa na ikitegemewa ziwe huduma bora sio bora huduma na sio zile za mgonjwa kuandikiwa dawa akanunue pharmacy au kwenda kwenye kituo ambacho hakina hata umeme au hakina doctor kina mhudumu wa afya au kiko kilometer kadhaa kutoka makazi anayoishi na hakina hata usafiri

Takwimu sahihi hazipo ila asilimia ya watu wasiopata huduma bora ya afya wanayostahili haiwezi kuwa chini ya 90% kwa sababu Tanzania hakuna hospitali hata moja inayotoa huduma bora ya afya katika viwango vinavyostahili, kwahiyo wale wote wanaopata huduma hiyo wanaifuata nje ya nchi. Asilimia ya watanzania wanaoweza kusafiri nje ya nchi kwa matibabu haiwezi kuzidi 10, ndio maana nasema wasiopata hawawezi kupungua 90%.

Siku tukifikia asilimia 71 kama ulivyoandika tutajipongeza na tutaiambia dunia yote.
 
Takwimu sahihi hazipo ila asilimia ya watu wasiopata huduma bora ya afya wanayostahili haiwezi kuwa chini ya 90% kwa sababu Tanzania hakuna hospitali hata moja inayotoa huduma bora ya afya katika viwango vinavyostahili, kwahiyo wale wote wanaopata huduma hiyo wanaifuata nje ya nchi. Asilimia ya watanzania wanaoweza kusafiri nje ya nchi kwa matibabu haiwezi kuzidi 10, ndio maana nasema wasiopata hawawezi kupungua 90%.

Siku tukifikia asilimia 71 kama ulivyoandika tutajipongeza na tutaiambia dunia yote.


Asante sana kwa ufafanuzi wako mkuu ZeMarcopolo mawazo yangu yalikuwa tofauti kidogo maana niliamini wewe unapingana na mtoa uzi kuwa huduma ni bora zaidi kumbe huduma ni mbovu zaidi ya hata takwimu za mtoa mada
Na tunakoelekea badala ya kupungua hizo asilimia ndio zinazidi kuongezeka na huduma zinazidi kuwa mbovu maana hakuna mkakati wowote uliondaliwa unaweza kunyanyua huduma hizo
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi ,

Kwanza kabisa mara nyingi nakosa imani na hizi data zetu mara nyingi haziko sawa lakini hii si hoja.

Kwanini tunafanya vizuri kwenye export lakini bado wananchi wengi ni masikini ?.
a. Tanzania ina export kwa wingi dhahabu lakini utashangaa hakuna uhusiano na ustawi wa taifa kwa ujumla hii inasababishwa na aina ya mikataba ambayo taifa liliingia na makampuni ya nje kwaajili ya uchimbaji wa dhahabu.Nimewahi kusikia taifa linafaidika na kodi kama PAYE,SDL, Corporate Tax na Royality 3% tu.Ukienda kwa wenzetu Botswana utakuta serekali yao ni wabia wa migodi kitu ambacho Tanzania inakikosa.Sasa we fikiria mgodi xyz umeuza tons 150 za dhahabu kwa mwaka unaambulia 3% mwekezaji anatafuna 97% !!!!!!.Kibaya zaidi mwekazaji ni mgeni faida anayoipata anawekeza kwao wakija wataalamu wa uchumi wanakokotoa hesabu pamoja na za mgeni tunaambiwa Tanzania tumeuza dhahabu tons 150 halafu unashangaa kwanini wananchi wengi hawana access ya maji,madawa,elimu.... Naambiwa Mwl Nyerere alianzisha STAMICO pengine hawa wangekuwa wabia wa migodi yote ya dhahabu hata kwa 30% tu tungeshuhudia mabadiliko makubwa na mapato katika sekta ya madini yangekuwa na mchango mkubwa.Unapotegemea SDL,PAYE kama mchango wa sekta ya madini tegemea matatizo makubwa.

b. Serekali inakosa nidhamu ya matumizi ya fedha na sera mahususi zinazolenga kupunguza au kumaliza umasikini badala yake mara nyingi imejikuta ikianzisha programs mbali mbali (MKURABITA.MKUKUTA....) ambayo zinatumia fedha nyingi katika utawala na kuwaacha walengwa wakuu (wanavijiji) bila msaada wa maana.Mfano unaweza kukuta mradi xyx ujenzi wa bwala la kuogesha mifugo umetengewa 500 milioni wataalamu wetu wananyofoa 300 milioni kwaajili ya ununuzi wa gari la msimamizi wa mradi Land Cruiser VDJ,posho za safari,ukaguzi wa mradi 50 milioni,semina elekezi 70 milioni,matengenezo ya magari 50 milioni hapa bado sijaweka wizi mdogo mdogo utajakuta fedha zinazomfikia mlengwa ni chini ya 15%.

c.Tanzania imekosa dira ya maendeleo ya muda mrefu na muda wa kati nchi inajiendeea yenyewe kusikojulikana.Najua watakuja watu na vitabu vilivyojaa vumbi toka wizara mbali mbali.Ukweli ni kwamba sera nyingi zinatengenezwa na wataalamu wetu lakini zinabaki katika mawizara badala ya kupelekwa kwa wahusika ambao ni wananchi kwaajili ya utekelezaji.Uandaaji wa sera lazima ushirikishe wananchi ngazi ya kaya kabla ya kutekelezwa.Matokeo yake ni huu umasikini usiokwisha kila uchao.

d.Tanzania inapata fedha nyingi kutokana na mauzo ya bidhaa za nje lakini fedha hizo hazipelekwi katika maeneo yanayoweza kuondoa au kupunguza umasikini lau kama zinapelekwa basi zinapelekwa kidogo sana.Fedha nyingi zinaelekezwa kama matumizi ya kawaida ya uendeshaji wa serekali.Tunaweza kuongeza bidii kuuza mazao mbali nje ya nchi lakini serekali nayo inaongeza matumizi ambayo yangeweza kuepukwa.Mfano leo hakuna tofauti ya gari anayotumia Rais na mkuu wa wilaya,RPC au wakurugenzi wa mashirika ya umma.Ebu fikiria Tanzania ina wilaya ngapi ?.Serekali imekuwa ikizalisha wilaya na mikoa kwa jinsi inavyotaka kwa kisingizio eti inasogeza maendeleo kwa wananchi !.Wananchi masikini hawana haja na wakuu wa mikoa au wilaya wananchi wangependa kusogezewa huduma za afya karibu na maeneo yao,wangependa kuhakikishiwa soko la uhakika la mazao yao,wangependa kupata huduma ya maji karibu na maeneo yao na si madoido ya mkuu wa wilaya na L/C VDJ.


Mwisho nadhani "outward looking strategies" ni nzuri lakini mapato yetu lazima yaelekezwe katika maeneo yenye kupunguza umasikini.Lazima taifa liwe na tafsiri moja ya umasikini na si kuwa na mipango mingiiiii progarms nyingi majina mengiiiiii.Tuwe na vipaumbele vichache tunavyoweza kuvisimamia na matokeo yake yakaonekana wazi pasipo ghilipa za statistics za kuunga unga.Serekali ipunguze matumizi ya kawaida badala yake ipeleke fedha nyingi katika matumizi ya maendeleo.
 
Last edited by a moderator:
Asante sana kwa ufafanuzi wako mkuu ZeMarcopolo mawazo yangu yalikuwa tofauti kidogo maana niliamini wewe unapingana na mtoa uzi kuwa huduma ni bora zaidi kumbe huduma ni mbovu zaidi ya hata takwimu za mtoa mada
Na tunakoelekea badala ya kupungua hizo asilimia ndio zinazidi kuongezeka na huduma zinazidi kuwa mbovu maana hakuna mkakati wowote uliondaliwa unaweza kunyanyua huduma hizo

Hakuna mkakati kwa sababu siasa imeshika hatamu.

Mambo ya kitaalamu waachiwe wataalamu.

Kama wanasiasa watakuwa waamuzi wa mambo ya kitaalamu na wataalamu wanabaki kutekeleza tu maamuzi ya wanasiasa, basi hakutakuwa na mkakati wowote endelevu.

Mwansiasa thinking yake iko ndani ya election circles. Anafikiria kimiaka mitano mitano na jinsi ya kupata kura. Mambo ya kitalaamu hayawezi kuendelezwa na mtu ambaye kipaumbele chake ni kupata kura kwa kuwaonyesha watu kuwa "anajali" hata kama jambo analofanya sio endelevu.
 
"Kukua kwa manufacturing sector nchini (Tanzania) kutoka 7% of total merchandise exports mwaka 2002, na kufikia 20% of total merchandise exports in 2012"

Kukua huku kwa manufacturing sector hakujasaidia sana kupunguza umaskini kwasababu bidhaa tunazouza nchi za nje sio extension ya mahitaji yetu hapa hapa nchini in other words these exportss are not an extension of our domestic market! Ingekuwa tunazalisha viwandani mahitaji yetu wenyewe kwanza hii ingekuwa na multiplier effect in terms of employment kwa wananchi na serikali ingepata kodi zaidi lakini hivyo sivyo; we target external demand/market which has no relationship to our domestic demamd/market. Ili kupata maendeleo ya manufacturing sector hakuna budi viwanda kwanza vizalishe mahitaji ya humu ndani halafu ziada ndio iuzwe nchi za nje in the process we shall create employment,save forex and also earn from our exports!!!
 
Mkuu Mchambuzi, Mipango ya Nyerere ilikuwa ni kujenga msingi (foundation) ya uchumi, iliangalia vyote viwili (Inward looking na outward looking.

  1. Inward looking: import substitution,kujitosheleza kwanza na kutengeneza ajira ili kuifikia jamii haraka.
  2. Outward looking: export ya processed good ili kuongeza thamani na kuleta forex

Majibu ya maswali uliyoyaleta mwishoni

Je,tunahitaji kipaumbele cha export promotion kama kipaumbele?
Jibu: hapana! export promotion ni lazima si suala la kipaumbele. We must do!

Je kuna haja ya kulenga bidhaa Fulani .sekta Fulani au masoko Fulani?

Jibu ni definite na hili ndilo tatizo letu kubwa. Japan wapo katika viwanda zaidi kuliko Kilimo. Wamelenga masoko makubwa na madogo. Toyota inatembea Washington, Kwimba hadi Baidoa.


Korea kusini ni kilimo , baada ya kujenga uwezo wamerudi katika viwanda.
Wajerumani ni katika machines zaidi ya kitu kingine. Botswana ni madini. Mauritius ni Utalii zaidi.


FAO inatabiri tatizo la chakula miaka 10 ijayo. Tanzania ina arable land madini na utalii.
Hatutegemei kuwa na viwanda kabla ya kujenga uwezo kwanza.
Umuhimu ni kujikita katika Kilimo, madini na utalii ni muhimu sana. Advantage kubwa kuliko Botswana na Mauitius


Kwanini kilimo? Tuna masoko tayari. Kipindi cha 2002-2012 tumesafirisha chakula katika nchi za Afrika mashariki.
Jana Kenya wameomba tani za kutosha. Bado hatukidhi soko la Afrika mashariki.

Utalii: Tuna upper hand kuliko sehemu nyingi za bara hili. Tunaweza kuwa world destination kama tutajipanga.Utalii ni sehemu muhimu ya uchumi wa Kenya na South Afrika, kwanini sisi wenye rasilimali zaidi tuhitaji promotion bada ya mkakati( kuna tofauti za mkakati na promotion)

Tulenge bidhaa gain? Chakula ni bidhaa isiyohitaji mjadala hasa Nafaka.

Mazao kama Mkonge yafufuliwe kwasababu dunia inarudi katika katani kutoka Nylon/plastic. Kuna potential in the future.
Tuangalie masoko ya Ulaya kwa bidhaa kama Matunda na mazao yatokanyo na kilimo kama Maua.

Nini tatizo la viwanda vya Nyumbani kutoka na mkakati uliosema?
Jibu: utegemezi wa viwanda kama sehemu ya mapato. Viwanda vinashindwa ushindani kwasababu ya kodi za juu na gharama za uzalishaji zitokanazo na vitu kama nishati na maji. Bidhaa zetu zinakuwa gahali kuliko za ku import


Kuna risk gain katika ezport stategy?

  1. Kwanza lazima tuwe competitive vinginevyo tunaweza kuwekeza na kutopata return tarajiwa.
  2. Utegemezi wa export peke yake unaweza kuumiza uchumi. Ezport strategy inafanywa na network ya dunia. Mtikisiko kama uliotokea miaka miwili unaweza kumaliza ndoto kabisa za investment
Kabla sijaendelea zaidi kuhusu mada hii, niwashukuru Ngongo na ZeMarcopolo kwa hoja zao zilizonigusa. Nitazichangia baadaye.

Nitajadili mikakati.

 
Mchambuzi:

Kwa kuongozea tu. Kwa miaka mingi tulitegemea soko la Ulaya ambalo halina ongezeko ya idadi ya watu. Kwa sasa hivi ukuaji wa uchumi wa China na India umeongeza idadi ya people with disposable income, the middle class. Hivyo uchumi wa Tanzania utaendelea kukua.

Kuhusiana na analysis zako za inward and outward strategies, it doesn't make sense to me.

Unapokuwa na jamii ambayo haina skilled labour ni lazima ufanye export raw materials or natural resources ambazo zinaweza kukusaidia kununua expertise, attract talents and capital. Hivyo inward strategy didn't make sense back then na hatuna sababu ya kumtetea Mwalimu kwa sababu uchumi sio sayansi.

Outward strategy inayoendelea sasa makes sense to me. Lakini hatuitumii vizuri kwa sababu kile kidogo kipatikanacho hakitumiki ku-build expertise, attract talents and accumulate internal capital ambayo ingetumika kujenga uchumi imara.

Kwa sasa hivi uchumi wa Tanzania sio kitendawili kwa sababu ingridients zipo. Kinachokosekana ni mpishi tu.
 
Mkuu Mchambuzi, tunashukuru kwa uchambuzi japo yaleyale "Research-less system" ndiyo iliyopo nchini kwetu. Kwamba Serikali haiongozwi kwa tafiti, bali kwa mazoea na siasa. Na hili litatu-cost kwa muda mrefu sana kama hatutobadilika. Kama ikitokea mtu akapitia mabandiko yako yote ya humu JF na maoni yake, basi inatosha kupata wayforward ya maendeleo yetu, But we read everything and understand nothing.

Nikirejea kwenye maswali chokozi uliyoyatoa, kimsingi Nguruvi3 ameshajibu maswali haya ila nami nitaongezea kidogo tu.
Kwanza, hatuna budi kujua tofauti ya System na Strategies. Nchi yetu, kwa maana ya Serikali yetu inatumia terms hizi interchangeably ima kwa makusudi au kwa kutojikita kwenye research ili kujua usahihi wa matumizi yake. System ni kama machinery, ukishaiweka basi yenyewe yaweza kujiendesha kwa muda unaotaka wewe bila ww kuwepo kwenye eneo la machine, lakini strategy hauko hivyo. Unapoweka mkakati hauna budi ya kuusimamia kwa 100% mpaka uwe. Kwa msingi huo, Economic Liberalization ni mfumo lakini Export/Outwards promotion ni Strategy, Import/Inwards promotion pia ni strategy kwamba ufanisi wake unategemea usimamizi uliopo. Sasa kinachoonekana katika nchi yetu, tunadhani tukiwa na Document safi nzuri inayoitwa "Tanzania Export Strategy" basi hapo tumeshamaliza na tunasubiri kuvuna/ku-win.

Export Promotion Policy, kwanza nakubali kwamba ni mkakati mzuri na kama ulivyobainisha umeleta matokeo chanya kwa nchi nyingi hasa zile za Asia Tigers(Korea, Taiwan, Singapore, Hong Kong) na wenzi wao pia wanafanya vizuri Malaysia, Thailand, China, India, hata Indonesia si mbaya sana). Lakini kufanikisha mkakati wa kukuza mauzo ya nje unategemea na parameters nyingi lakini kubwa ni hizi mbili:-
1. Trade Policy na 2. Industrial Policy
Nikieleza kwa uchache kuhusu Trade Policy, kwa muda mrefu, nchi za dunia ya nne(LDCs) tumekuwa hatuna mkakati wowote wa ku-win katika Trade Policy chini ya GATT now WTO; ushiriki wetu una agenda kuu mbili tu:
i) Kuendelea kupewa Special and Differential Treatment katika utekelezaji wa makubaliano ya WTO pamoja na kuongezewa Aid for Trade) na;
ii) Kuendelea kuomba kunufaika na (Generalized System of preferences) kupitia Unilateral Agreements (EPA, EBA, AGOA etc). Lakini mikakati hii yote inadhihirisha "ujinga" walionao wataalamu wetu ambao naamini unasababishwa na umasikini wetu. Kwanini? Preferences tunazozipigania hazina maana sana kwasababu mbili muhimu
a) Tunapigania/tunapewa Market Access ya kuuza bidhaa zetu kwenye masoko ya Nchi zilizoendelea kwa kupewa msamaha wa Kodi (tariff free), lakini je Tariff rates za Nchi zilizoendelea ni kiasi gani? Nyingi ni chini ya 4%!
b) Preferences tunazopata kwenye masoko hayo nyingi zao hazihusishi bidhaa za Kilimo kwani sekta ya Kilimo ambayo ina tariff rates kubwa katika Nchi zilizoendelea lakini imekuwa ikilindwa mno (Rejea Doh Breakdown) hivyo kwa kiasi fulani hizi GSP hazina maana sana kwa nchi zetu kwa sasa.

2. Industrial Policy,
Kiukweli industrial policy ndiyo ilizozitoa hizi nchi za Asia Tigers pamoja na Kiranja wao Japan. Nchi hizi zote zina uchumi wa Viwanda, (kitu ambacho kinazidi kuziweka kwenye uimara madhubuti kwa muda mrefu) tofauti na Ulaya(ukitoa Ujerumani) ambao walikuja na mkakati wa kuhama kwenye (Manufacturing). Lakini Je swali la kujiuliza, hii Industrial Policy ya nchi hizi iko nzuri kiasi gani hata wao ikawatoa lakini sisi kwetu mtihani? Jibu ni kwamba Industrial Policy "document" yetu ni "nzuri" kuliko yao lakini Industrial "Strategy" yao ni nzuri kuliko yetu, na wanafahamu tofauti ya "system" na "Strategy".

Industrial Policy yaweza kuwa na approach mbili:
2.1 Industrial Policy ku-promote specific sectors (Kilimo, Viwanda, Huduma nk)
2.2 Industrial Policy ambayo imejikita kwenye "market promotion policies". Hii inajumuisha masuala kadhaa ya msingi kama vile Labor Market Policies (job cration, incentive programs. labor mobility, subsidies nk), Capita market policies kwa ajili ya kuimarisha mitaji na sera za ushindani (competition policies). Ni approach yenye lengo au pia mkakati wa ku-influence different industries kutumia our factor markets. Ni approach gani sisi kama Tanzania tunaifuata, mie sijui labda Nguruvi3 atakuja kutufahamisha kuhusu hili.

Je kwanini Tanzania hatufikii Lengo la Industrial Policy au Trade Policy?
>The role of Government ndipo inapohitajika. Tuchuke mfano wa Nchi moja katika zile za Asia Tigers; Tuseme Korea. Walitekelezaje mkakati wao wa Viwanda na Sera ya Biashara?

1. Korea iliamini kwamba, ubinafsishaji hauna maana ya kujiondo kwa Serikali katika jukumu la kusimaia na ku-control uchumi, hivyo serikali ilisimamia kikamilifu katika namna (baadhi zifuatazo)
i) Serikali ilibuni na kutekeleza sera wezeshi ili kuhakikisha kwamba uwekezaji unakuwa na manufaa kwa wawekezaji na wawekwezaji;

ii) Serikali ilikuwa na jukumu la kuangali all externalities zinazohusiana kila sekta
iii) Serikali ilitoa strategic support KWA LENGO LA KUANZISHA/KUIMARISHA NA KUENDELEZA DOMESTIC FIRMS. KUANZISHA/AU KUIMARISHA NA KUENDELEZA DOMESTIC FIRMS ILI KUZIFANYA ZIWE GLBAL COMPANIES (creation of oligopolistic market, domestic firms should able to capture larger share of international trade kwa kutumia Joint Industrial and Trade Policy.) Kumbuka Korea ilikuwa outward-protective policy country-hii ndiyo sera yao ya Biashara. Chini ya Mkakati huu wa kuendeleza na kuimarisha Wafanyabiashara/firms za ndani, Korea ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kiasi ya kwamba Makampuni yote yalichangia maendeleo ya nchi hiyo ni ya wazawa au ya nyumbani. Nikiyataja machache hapa (Hyundai Elecronics Co. Ltd, LG Semiconductor, Sumsung Petrochemical, Hanwha Energy Production, Daewoo Heavy Industries, Hanji Heavy Indusries, Korea heavy Industries, POSCO Heavy Industries). Iliyaendelezaje makampuni haya, itafuata mbele.

iv) Serikali ilihakikisha uwepo wa taasisi wezeshi (Sio BRELA ambayo akienda Mtanzania nayetaka kuonana na Mkurugenzi Mtendaji anaambiwa "yuko bussy" au "yuko mkutanoni" then akienda mhindi anaambiwa "pita" huu ni upuuzi wa akili fupi tulizonazo waafrika). Kwamba Serikali ilihakikisha inaweka discipline kwenye supporting institutions zinazo-deal na wafanybiasha, hususan wanaouza bidhaa nje ili kuleta ufanisi wa hali ya juu.

v) Serikali ilihakikisha uwepo wa instrumets ambazo zitachangia katika kushusha kwa gharama za uzalishaji ili kuzifanya bidhaa zao ziwe competitive katika bei.

vi) Makampuni yaliyokuwa na dhamana ya kuuza bidhaa nje yalipewa misamaha kadhaa (kumbuka hapa kwetu msamaha unatolewa kwa makampuni yanayo-import)

vii) Hakukuwa na export tariffs (sijui kama Tanzania tuntoza export tariff au vipi)
viii) Serikali kupitia Taasisi za kifedha ilitoa "punguzo maalum la kupata mkopo kwa makampuni ya ndani yanayouza bidhaa nje);

ix) Serikali ilianzisha tunzo ya wauza bidhaa nje ya nchi (Exporter's awards)

x) Rais wa Nchi alikuwa na mkakati wa kukutana na wafanyabiashara, mawaziri kila mwezi BILA KUKOSA ili kupata "live comments" wapi wamekutana na ugumu, wapi? wapi wanapata changamoto? Wizara gani taasisi iliyo chini yake imezembea au haina ufanisi. Wafanyabiashara walipewa uhuru wa kusema mbele ya Rais na yeye aliweza kuchukua hatua mara moja za ku-rectify Taasisi husika. (Hope hili lingekuwepo hapa kwetu, Taaisis kama Brela, TRA, TIC, TBS, TFDA ambazo kwao ufanisi ni kama msamiati, wafanyakazi wake wasingekuwa na majibu jeuri kwa Watazania au wasingecheza game muda wa kazi) [Samahani kisa kidogo: Siku moja nilikuwa Temeke TRA, kulikuwa na foleni kubwa ya wateja waliokuwa wakitaka TIN, then ilipofika mchana kama saa 6.30; yule mfanyakazi wa TRA akawaambia wateja "Khaa, pumzikeni nimechoka nataka nile kwanza" mje saa 8"-Can you imagine mtu wa namna hii ndio tunaowategemea kusimamia ukusanyaji wa mapato].

xi) Education and Human Resources intervention.

xii) Serikali iliweka mkakati maalum wa kuwapeleka vijana wake wakasome US na Ulaya ili kujiandaa na technology exchange. Je Nchi yetu inasimamia lipi katika haya?

Ukiangalia mtiriko wa niliyoeleza hapo juu, utabaini kwamba tuna matatizo zaidi ya ndani kuliko ya nje. Tanzania ni LDCs, ambayo kimsingi iko "exempted" kwenye treatmaents nyingi za WTO hivyo inaweza kutekeleza baadhi ya vipengele vyake vya sera ya biashara in differential basis hivyo kujiweka katika mazingira mazuri. Hata hivyo, kwa kupitia hizi figure za uongo, huenda ikaondoka hilo kundi la LDCs kisiasa halafu ikapata matatizo makubwa zaidi.

Nitarejea kuendelea na sehemu ya pili, ila kwa muhtasari kuwa na Wafanyabiashara wakubwa wa ndani watakaokuwa 'major shareholders' ndio kipaumbele cha kwanza cha kufanikisha maendeleo. Ni wazi kwamba mchango wa watu kama Mengi au Bahkressa katika maendeleo ya Tanzania ni mkubwa, mimi nilitarijia Rais angekuwa na Vikao vya kila mwezi na wafanyabiashara hawa wazalendo ili kupata changamoto zao, na ikiwezekana kuwadhamini katika vyombo vya fedha vya kimataifa ili wawe chachu ya maendeleo. Lakini kitendo cha Rais kuungana na wanaodai kwamba watanzania hawawezi kuwekeza katika baadhi ya sekta, ni anguko baya kabisa kwa uchumi wa maendeleo yetu. Ulaya haikuendelea kwa Makampuni ya Marekani. Marekani haikundelea kwa makampuni ya Ulaya, Japan haikuendelea kwa makampuni ya Ulaya au Amerika, Asia hikuendelea kwa makampuni ya Marekani au Ulaya. Hata Afrika Kusini, ina makampuni mkakubwa mabayo ni ya Afrika Kusini yenyewe, vivyo hivyo Australia, Newsland, German. Kila Asian Tiger alijidhatiti kuyandeleza makampuni yake ambayo Serikali ilipata uwezo kubwa wa kuya-kabili na kushauriana pindipo panapotokea "kind crisis". Sasa Leo, kukitokea crisis, unadhani ni rahisi Serikali kukaa na "BP" ili kulitatua "in favor of Tanzania". Wapi tunapata huu ushauri ndugu zangu waafrika? WB au IMF? Hizi Taasisi zimeanza kujiingiza kwenye mipango ya maendeleo ya Afrika toka miaka ya 50, mbona mpaka leo hali ni mbaya.
Inshaaallah, next time nitakuja kuchangia tena kidogo kwenye mada hususan, juu ya athari za kutegemea uwekezaji wa nje katika kuendeleza uchumi wa Tanzania/Afrika kwa ujumla.

 
Naomba mniwie radhi kwa kutorudi kwa wakati kuchangia mawazo yangu kutokana na hoja za wadau mbalimbali;Naomba nianze na bandiko #9 la Ngongo:

Kimsingi nakubaliana na hoja zako kuhusiana na kwanini "export orientation strategy" au "outward looking/orientation" haimsadii mwananchi wa kawaida kuinuka; Vile vile nakubaliana na hoja yako juu ya umuhimu wa kupeleka mapato ya exports zetu kwenye miradi itakayotusaidia kutokomeza umaskini;Pamoja na umuhimu wa haya, tunakabiliwa na changamoto kadhaa kufikia huko ikiwa ni pamoja na:

*Kwanza, ingawa kwa mfano exports zetu za gold mwaka 2012 zilikuwa dollar billioni mbili ($2 Billion), kilichopatikana ilikuwa sio zaidi ya 5 percent ya royalty fee ambayo sio zaidi ya dollar za kimarekani milioni mia moja;kwahiyo tusijipongeze sana kwa figure ya $2 Billion; Swali linalofuatia hapa pia ni:

* Je - export earnings hizi zinatumikaje kuendeleza wananchi kufuatana na mapendekezo yako kwenye bandiko #9 ?

Hakuna majibu ya moja kwa moja kwani sina takwimu kamilifu ila naweza kusema kwa kujiamini kwamba:

Moja, hakika mapato haya hayarudi yalipotoka - mfano ukanda wa uzalishaji madini kwani hata miundo mbinu ya barabara tunayojipongeza nayo, mingi inatokana na mikopo ya wahisani (barabara za tanroads) huku barabara ndani ya manispaa zikijengwa kwa mapato yatokanayo na kodi za wananchi; Inasikitisha sana kusikia pia kwamba hata meli ya MV Victoria ambayo inasua sua kihuduma, inasubiri mkopo wa Norway ambapo mradi huo utakamilika 2017;hii ni taarifa iliyotolewa bungeni na serikali leo katika kipindi cha maswali na majobu asubuhi;

Pili, Tanzania ina debt to export ratio kubwa sana, ambapo its present value is over 50 percent, ikiwa na maana kwamba, zaidi ya nusu ya mapato yetu ya exports yanaenda to service deni la nje;Mwaka 2012, exports zetu zilifikia karibia $9 Billion, hivyo ina maana kwamba karibia $5 billion ilienda kulipa madeni ya nje;

Kilichobakia kinatumika kwa ajili gani? Ni kama ulivyoainisha - kinaenda kwenye matumizi ya kawaida (karibia 70percent of the budget) kwa ajili ya magari ya kifahari, posho, mishahara, semina, na kujaza makabati na mafriji ya taasisi mbalimbali kwa ajili ya kunyweshana togwa na kahawa huko maofisini;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Wakuu Nguruvi3 & Zakumi:

Naomba nijibu hoja zenu kwa pamoja;

Kumekuwa na utamaduni wa wanasiana wengi kutumia mafanikio ya nchi kama south korea kujenga hoja kwamba na sisi tunaweza kuendelea kwa kuwatumia south korea kwa mfano as a model; Hii inatokana na ukweli kwamba kuingia 1960, South Korea ilikuwa nyuma kimaendeleo kuliko mataifa mengi ya Afrika kwa wakati ule; Na jinsi nchi ya south korea, pamoja na Taiwani na wengine wachache walivyoweza to tranform from economic baskets to economic powerhouses remains to be a brain-teaser to many policy makers and alike;

Kimsingi, kilichotokea ni kwamba nchi ya south korea na taiwan ziliingia katika traditional import substitution approach to development, pamoja na kuweka multiple exchange rates, high levels of trade protectionism, and a suppressed domestic financial sector; Ilipofikia late 1960s, kila nchi ikawa imesha exhaust hatua muhimu za awali za import substitution; Mbali na hili, katika kipindi hicho hicho, foreign Aid kwenda nchi hizi zikaanza kupungua kutokana na geo political reasons za wakati ule; Tukumbuke kwamba foreign aid toka marekani ilikuwa ni chanzo kikuu cha excellent export performance za south korea na taiwan since early 1960s;
Lakini ni vigumu kuja na conclusion yenye mashiko kwamba export orientation per se played a significant causal role in the growth of countries kama south korea; Kwa mfano, if you measure faida za exports za south korea in the 1960s, utaona kwa urahisi sana kwamba exports per se hazikuwa significant to account for the phenomenal export boom;kwa maana nyingine, exports were not the end in themselves; isitoshe, exports zilikuwa ni ndogo sana to have a significant effect on aggregate economic performance;hapa, hoja ya Ngongo inahusika ambapo kwa kuongezea, - faida za exports hazitakiwi kutumika tu ovyo bila a proper economic development planning chini ya serikali yenye "political will"; kwa mfano, nchini kwetu, kwa miaka kumi na mbili (2000-2012) of tremendous exports growth and performance, hapajakuwa na mkakati wowote wa serikali kuhakikisha performance on the macro level delivers to the meso and micro levels;

Tukiangalia south korea kwa mfano, kufuatia financial resources constraints zilizoanza kujitokeza in late 1960s, tayari walikuwa wameshajenga misingi ya import substitution scheme, hivyo kilichofuatia ikawa ni kufanya the right investments, hasa on human capital, infrastructure pamoja na policies za kusaidia technology diffusion and transfer toka nje; kwa maana nyingine, kufuatia mabadiliko ya Aid profile, south korea walitumia changamoto hii kuwa more innovative kwa maslahi ya taifa; unlike viongozi wetu ambao wanaona lack of financial resources as a major obstacle to innovation (rejea kauli za kasungura kadogo), viongozi wa south korea wakachukulia financial resources constraints as a catalyst and source of innovation - wakawekeza kwenye social infrastructure (elimu, afya)and physical infrastructure (hasa reli na bandari);

Leo hii, lugha kuu south korea sio english, lakini bado, kwa mujibu wa recent rankings za excellence/quality of education among countries in the world, south korea wapo juu sana, zaidi, kama sio karibia na english speaking countries kama UK & USA;Je sisi na kiswahili chetu tulishindwa wapi? Je, ni kweli matumizi na uelewa mdogo wa lugha ya kingereza ni kikwazo kwetu cha kutoweza shiriki kikamilifu kwenye global knowledge chains and networks? Wakorea, wachina, wanawezaje?

Wenzetu waliwekeza na bado wanawekeza sana kwenye primary education kwani huko ndio pa kuanzia - kujenga the right attitude, confidence, culture, literacy, numeracy, Sciemce and technology driven mindsets za watoto tangia wadodo;kwa mfano, ni aibu sana kwa mchina au mkorea kutojua hesabu hata kama hajaelimika vya kutosha; Sisi tunakwepa kuwekeza kwa watoto wetu tangia ngazi ya msingi, na tunakimbilia kwenye sekondari ambazo literary, tunatengeneza mfumo wa kupokea quantity na sio quality ili kujilinda kisiasa; ni jambo la ajabu sana kwa viongozi wetu to deal with quantity challenges badala ya quality challenges linapokuja suala la elimu nchini;

Pia badala ya kuwekeza kwenye miuondo mbinu yenye significant effect to economic efficiency kama reli na bandari, tunapoteza fedha nyingi kwenye mabarabara ambayo pamoja na umuhimu wake, ni more costly kwa mwananchi in terms of maintenance, na more expensive in terms of usafirishajo watu na mizigo; kwa mfano, wataalamu wa transport economics wanatueleza kwamba usafiri wa barabara ukizidi kilometa mia sita, unakuwa ni wa hasara unlike reli (least expensive, ikifuatiwa na usafiri wa maji);

Sisi, viongozi wetu wamebakia na makelele ya BIG RESULTS NOW
na PRESIDENTIAL DELIVERY UNIT ambazo zinapoteza tu muda na kodi za wananchi, badala ya kuunda ECONOMIC INTELLIGENCE UNIT ya kushughulika na masuala kama haya tunayojadili;


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi
Tulizembea katika Model aliyokuja nayo Nyerere iliyoshabihiaba na ile ya Korea.
Kwasasa hatuwezi kurudi nyuma, speed ya dunia ni kubwa kutoa mnafasi ya sisi kuanza kutambaa.
Miaka 10 iliyopita imebadilisha dunia kuliko karne moja ya industrial revolution.
Ni lazima tukimbie na wenzetu na hivyo kuchukua model zote kwa pamoja.

Kuhusu Lugha, tatizo si lugha bali wataalam na wanasiasa walioizaidi ya utaalamu.
Jana wameondoa div 0 kila mmoja afaulu ili kupata takwimu nzuri za elimu.
Je, hilo linasaidia taifa? kwamba mtu asipoandika hata jina katika mtihani huyo anapewa daraja!!!

Takwimu kutoka nchi za magharibi zinaonyesha walimu wengi huenda Asia majira ya joto kufundisha lugha.Wenzetu wamewekeza katika lugha bila kuathiri zao.

Hivi kwanini iwezekane mtu aweze kuongea lugha kifaransa , Kiswahili, kiingereza na isiwezekane katika shule zetu. Tatizo ni lile lile nani ananagalia hili kutoka angle nyingine.
Hebu angalia wahindi, kwanini wanaweza kuwa na lugha zaidi ya moja bila kuwaathiri.

Dunia ya leo lugha haikwepeki, Marekani wanafundisha kiswahili/kishispani/ kiarabu n.k. kwa nguvu kuliko sisi.
Lugha ni nyezo na si fahari kama ilivyokuwa siku za nyuma.

Bado tunaweza kufundisha kwa lugha moja na watu wakajifunza lugh nyingine na kupata mafanikio tarajiwa. Mfano, wazee wetu waliwezaje kufanya hilo sisi tushindwe.

Tatizo lipo katika mkakati wa ku link lugha na shughuli za jamii ikiwemo uchumi na wala si kwasababu ya lugha moja. Vipi tumeshindwa kuondoa kipindu pindu kwa kiswahili lakini tuamini tunaweza ku infuse teknolojia kwa lugha hiyo hiyo.

Kuhusu ujenzi wa miundo mbinu, hili umeniwahi nilikuwa nilijadili na ahasante kwa maelezo yako.
Hakuna nchi dunia inayoendelea au iliyoendelea bila miundo mbinu kama reli.
Marekani, Australi, Canada, China n.k. wanawekeza katika hilo.Reli inarahisisha na kupunguza gharama.

Katika mkakati niliosema hapo juu kuhusu kilimo, reli ni muhimu kwa kupeleka na kuchukua bidhaa, mfano wa bolea na kuchukua mazao kwa mauzo au viwanda.

Lazima tukiri kuwa hatuna economic intelligence unit. Miundo mbinu yetu si ujenzi ni ukarabati na nyongeza kidogo. Utashangaa tunakijikita katika barabara ambazo ni ghali kujenga, maintainance na 'life span' yake ni fupi. Nini kinaendelea reli ya kati kati ya 2002-2012! Nini kinaendelea Tazaara!

Muhimu zaidi ni kuwa unapokuwa na serikali kubwa kama alivyosema Ngongo unakaribisha mambo haya
1. Corruptions
2. Mismanagement
3. Lack of vision kwasababu ya distraction zinazotokana na 1 na 2 hapo juu.

Kuna kitu umenigusa sana. Nchi za wenzetu vitengo vya economic intelligence hutoa dira na mikakati ya uchumi . Marekani wanaamini uslama wa nchi ni uchumi. Pamoja na vitengo vya intelejensia kuna kitu wanaita 'think tank' . Hiki kina watu wenye uzoefu na wasomi wa hali ya juu sana wanaoshauri serikali kuhusu uchumi.

China wana kitengo cha intelejensia, siku za karibuni kimeleta tabu UK.
Walikuwa wanapeleka wanafunzi wa PhD kama undergraduate UK.
Kumbe hawakuwa wanafunzi walikuwa wanafanya intelejensia ya teknolojia na kuiba kurudisha kwao. UK wamewapiga marufuku na wanaosoma wanafuatiliwa. Mfano huu ni kuonyesha wenzetu wapo seerious kiasi gani.
Tanzania hatuna na tumeshindwa kubaini hata intelejensia kwa majirani.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu Nguruvi3 & Zakumi:

Naomba nijibu hoja zenu kwa pamoja;

Kumekuwa na utamaduni wa wanasiana wengi kutumia mafanikio ya nchi kama south korea kujenga hoja kwamba na sisi tunaweza kuendelea kwa kuwatumia south korea kwa mfano as a model; Hii inatokana na ukweli kwamba kuingia 1960, South Korea ilikuwa nyuma kimaendeleo kuliko mataifa mengi ya Afrika kwa wakati ule; Na jinsi nchi ya south korea, pamoja na Taiwani na wengine wachache walivyoweza to tranform from economic baskets to economic powerhouses remains to be a brain-teaser to many policy makers and alike;

Kimsingi, kilichotokea ni kwamba nchi ya south korea na taiwan ziliingia katika traditional import substitution approach to development, pamoja na kuweka multiple exchange rates, high levels of trade protectionism, and a suppressed domestic financial sector; Ilipofikia late 1960s, kila nchi ikawa imesha exhaust hatua muhimu za awali za import substitution; Mbali na hili, katika kipindi hicho hicho, foreign Aid kwenda nchi hizi zikaanza kupungua kutokana na geo political reasons za wakati ule; Tukumbuke kwamba foreign aid toka marekani ilikuwa ni chanzo kikuu cha excellent export performance za south korea na taiwan since early 1960s;
Lakini ni vigumu kuja na conclusion yenye mashiko kwamba export orientation per se played a significant causal role in the growth of countries kama south korea; Kwa mfano, if you measure faida za exports za south korea in the 1960s, utaona kwa urahisi sana kwamba exports per se hazikuwa significant to account for the phenomenal export boom;kwa maana nyingine, exports were not the end in themselves; isitoshe, exports zilikuwa ni ndogo sana to have a significant effect on aggregate economic performance;hapa, hoja ya Ngongo inahusika ambapo kwa kuongezea, - faida za exports hazitakiwi kutumika tu ovyo bila a proper economic development planning chini ya serikali yenye "political will"; kwa mfano, nchini kwetu, kwa miaka kumi na mbili (2000-2012) of tremendous exports growth and performance, hapajakuwa na mkakati wowote wa serikali kuhakikisha performance on the macro level delivers to the meso and micro levels;

Tukiangalia south korea kwa mfano, kufuatia financial resources constraints zilizoanza kujitokeza in late 1960s, tayari walikuwa wameshajenga misingi ya import substitution scheme, hivyo kilichofuatia ikawa ni kufanya the right investments, hasa on human capital, infrastructure pamoja na policies za kusaidia technology diffusion and transfer toka nje; kwa maana nyingine, kufuatia mabadiliko ya Aid profile, south korea walitumia changamoto hii kuwa more innovative kwa maslahi ya taifa; unlike viongozi wetu ambao wanaona lack of financial resources as a major obstacle to innovation (rejea kauli za kasungura kadogo), viongozi wa south korea wakachukulia financial resources constraints as a catalyst and source of innovation - wakawekeza kwenye social infrastructure (elimu, afya)and physical infrastructure (hasa reli na bandari);

Leo hii, lugha kuu south korea sio english, lakini bado, kwa mujibu wa recent rankings za excellence/quality of education among countries in the world, south korea wapo juu sana, zaidi, kama sio karibia na english speaking countries kama UK & USA;Je sisi na kiswahili chetu tulishindwa wapi? Je, ni kweli matumizi na uelewa mdogo wa lugha ya kingereza ni kikwazo kwetu cha kutoweza shiriki kikamilifu kwenye global knowledge chains and networks? Wakorea, wachina, wanawezaje?

Wenzetu waliwekeza na bado wanawekeza sana kwenye primary education kwani huko ndio pa kuanzia - kujenga the right attitude, confidence, culture, literacy, numeracy, Sciemce and technology driven mindsets za watoto tangia wadodo;kwa mfano, ni aibu sana kwa mchina au mkorea kutojua hesabu hata kama hajaelimika vya kutosha; Sisi tunakwepa kuwekeza kwa watoto wetu tangia ngazi ya msingi, na tunakimbilia kwenye sekondari ambazo literary, tunatengeneza mfumo wa kupokea quantity na sio quality ili kujilinda kisiasa; ni jambo la ajabu sana kwa viongozi wetu to deal with quantity challenges badala ya quality challenges linapokuja suala la elimu nchini;

Pia badala ya kuwekeza kwenye miuondo mbinu yenye significant effect to economic efficiency kama reli na bandari, tunapoteza fedha nyingi kwenye mabarabara ambayo pamoja na umuhimu wake, ni more costly kwa mwananchi in terms of maintenance, na more expensive in terms of usafirishajo watu na mizigo; kwa mfano, wataalamu wa transport economics wanatueleza kwamba usafiri wa barabara ukizidi kilometa mia sita, unakuwa ni wa hasara unlike reli (least expensive, ikifuatiwa na usafiri wa maji);

Sisi, viongozi wetu wamebakia na makelele ya BIG RESULTS NOW
na PRESIDENTIAL DELIVERY UNIT ambazo zinapoteza tu muda na kodi za wananchi, badala ya kuunda ECONOMIC INTELLIGENCE UNIT ya kushughulika na masuala kama haya tunayojadili;


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums


Mchambuzi:

Katika kujibu na kuongezea ulichosema, nitatumia vigezo vichache vifuatavyo. Cha kwanza, constructs za taaluma ya uchumi sio stable kama zile za sayansi. Katika sayansi unaweza kutumia mathematical models kutengeneza mechanical system itakayokwenda Mwezini na kurudi dunia salama.

Katika taaluma za uchumi zipo mathematical and historical models ambazo nchi inaweza kuzitumia katika masuala ya ujenzi wa uchumi. Tatizo ni kuwa models hizi sio stable au deterministic. Model aliyotumia Nyerere haikuwa mpya duniani. Warusi walitumia hiyo. Vilevile World Bank ilitumia hiyo katika miaka ya 60 na 70 kujaribu kuziletea nchi ya kiAfrika maendeleo bila mafanikio.

Miradi iliyopo Tanzania, ilikuwepo Kenya, Zaire, Zambia n.k. Na kila nchi ilikuwa na sera ya kulinda uchumi wake. Lakini kulikuwa hakuna mafanikio. Kushindwa kwetu kuitumia model hii ilitokana na ukweli kuwa hatukuwa na ingridients au chachu za maendeleo. Na kutokana na msingi huu kutumia mfano wa South Korea bila kuwa na ingridients za mafanikio ni kujiangamiza sisi wenyewe.

Kigezo cha kwanza kinanileta kwenye kigezo cha pili. Kutokana na constructs za kujenga uchumi kutokuwa statics au stable ni lazima nchi au jumuia ifanye investment in human capital. Mfano mzuri ni nchi hizo tunazoziita Asian Tigers. Kwa mfano mafanikio ya China yanachangiwa na mfumo mzuri wa primary education. Mfumo huu umeweza kutoa educated and skilled cheap labour. India hawana mfumo mzuri wa primary education, lakini universities zao zinatoa graduate wazuri katika service sectors. Nguruvi ametoa mfano mzuri wa waChina kupeleka wanafunzi kusoma UK. Watanzania inabidi tujiulize, katika miaka 50 ya uhuru, je tumefanya nini katika kuimarisha Human Capital?

Kigezo cha pili kinanileta kwenye kigezo cha tatu. Unapokuwa na Human Capital nzuri the rest is commentary. Tungekuwa na Human Capital nzuri, mjadala wa inward, outward, export, import usingekuwepo.


Tukirudi kwenye masuala ya elimu, kiswahili sio tatizo. Attitude ni tatizo. Habari kutoka sources nyingi zinasema kuwa Rwanda wanataka nchi yao iwe hub ya information Technology katika Africa mashariki na kati na kuna vyuo vikuu kama vitatu vimeshafunguliwa katika kipindi cha miaka kumi. Miaka mitano inayokuja, watakuja kama IT professionals wenye kuzungumza kifaransa, kiingereza na kiswahili. Je tutawanyima kazi wakati sisi tumekalia masuala ya ardhi katika EA?
 
@Zakumi nikushukuru kwanza kwa mabandiko yako mawili.
Model ya Nyerere kama ilivyotumika na nchi nyingine haikushindwa. Kilichoshindwa ni kuiendeleza kwasababu za kukosa watu makini wenye maono.
Hebu soma habari hii hapa chini kwanza

[TABLE="width: 1013"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]na Mwandishi wetu, Dodoma


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF"]

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR="bgcolor: #ffffff"]
[TD]SERIKALI imetakiwa kueleza ni kwanini imeua kiwanda cha kutengeneza redio aina ya Philips kilichoko mjini Arusha.
Hoja hiyo iliibuliwa bungeni jana na mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema (CHADEMA).
Mbunge huyo aliitaka serikali itoe maelezo ni kwa nini iliamua kuua kiwanda hicho na kusababisha kuagiza redio kutoka nje.
Katika swali la msingi, mbunge wa Mji Mkongwe, Muhammad Ibrahim Sanya (CUF), alitaka kujua kama serikali haioni kuwa umefika wakati wa kutafuta mwekezaji ili kuwepo kiwanda cha kutengeneza betri za redio zenye viwango.
"Wananchi wengi hususan vijijini ambao njia pekee ya kupata taarifa mbalimbali za masuala yanayohusu kilimo, afya, uchumi na maendeleo hupatikana kupitia matangazo ya redio na redio hizo hutumia betri ambazo huingizwa kutoka nje ya nchi, lakini zikiwa katika viwango hafifu na zisizodumu muda mrefu.
"Je, serikali haioni kuwa umefika wakati wa kutafuta mwekezaji ili kuwepo kiwanda cha kutengeneza betri za redio zenye viwango," alihoji mbunge huyo.
Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Gergory Teu, alikiri idadi kubwa ya Watanzania hususan wanaoishi vijijini wanapata taarifa mbalimbali kupitia matangazo ya redio zinazotumia betri.
Teu alisema kwa sasa Tanzania ina upungufu wa betri milioni 15 kwa mwaka tofauti na mahitaji halisi ambayo ni betri milioni 250 kwa mwaka.
Alisema kuna kiwanda cha Panasonic Battery (T) Co.Ltd ambacho kinazalisha betri milioni moja kwa mwaka wakati mahitaji ni zaidi ya betri milioni 250.
Alisema kuwa kutokana na mahitaji ya betri kuwa makubwa nchini kampuni ya Tiger Head kutoka China imeingia mkataba na serikali wa kujenga kiwanda nchini cha kuzalisha betri

Mchunguzi kasema zipo model mbili za inward na outward. Katika hizo inward looking (import subsitution) tulikuwa tumeshaanza. Kwanini kiwanda cha Philips kilifungwa, Matsushita iliyokuwa inatengeneza betri bora Afrika mashariki, general tyre n.k.

Leo waziri anafunga safari kwenda kualika wawekezaji wakati kuna mahitaji ya betri milioni 250 nchi achilia mbali nchi za jirani. Je hapa haturidi nyuma kweli. Korea kusini wanaweza kurudi nyuma kwa kufanya yale ya mwaka 1960 na 70 kama tufanyavyo?

Kuna somo kuhusu maswali ya Mchunguzi. Ile hoja ya kuchagua sekta fulani na kwa soko fulani inaingia hapa. Pengine leo tungekuwa wasambazaji wazuri sana wa betri za matsushita. Je kwa kuona kuwa tuna mahitaji ya betri milioni 250 , je hiyo peke yake haitoshi kuona uwezekano wa soko kubwa zaidi ya hilo katika ukanda wetu?

+


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Nguruvi3,

Shukrani kwa kuleta hoja kuhusiana na mjadala wa kiwanda cha philips jana bungeni;Binafsi nilisikia mjadala huo, na ni kama ulivyoripotiwa kwenye source uliyotuwekea hapo juu; Swali langu ni je, iwapo wapo waliopingana na Mwalimu kuhusiana na infant industry argument under the inward looking strategies za wakati ule, je, katika zama hizi za outward looking strategies, ambapo kiwanda hiki na vingine vingi vimekufa, hoja yao ya msingi kutetea mafanikio ya outward looking strategies being implemented in Tanzania ni nini?

Mwalimu alifuata strategies za inward looking kama zilivyofanya nchi nyingi sana zilizokuwa zinaendelea baada ya vita vya pili vya dunia, kuanzia bara la latin america, asia, sehemu za europe na africa, so alichofanya wasn't new nadhani kama alivyojadili Zakumi au wewe hapo juu; Justification for infant industry protection ilikuwepo kwa maana moja tu - viwanda vipya vinahitaji kufikia a certain threshold to gain experience za aina nyingi before letting them out of the wild; Na njia kuu ya kufanikisha hili ilikuwa ni kupitia trade regime (restricting imports fulani fulani so that they don't distort domestic production and consumption); Swali linalofuatia ni je, kwa tanzania: did the long run benefits justify the short run costs of starting up an initially high cost infant industrial base?

Sina jibu la moja kwa moja, lakini naweza kusema kwamba the test on validity ya infant industry can be simple and straightforward ambayo ni kuangalia ratio ya input per output - input being labour, capital and raw materials;if input per unit of output inaanguka kwa kasi zaidi katika protected industries, basi justification inakuwepo, and vice versa holds;

Tukiangalia takwimu zetu za miaka ya sitini na sabini, protected industries did not experience rapid increase in output per unit of input, kwahiyo kulikuwa na tatizo, suala ambalo Nguruvi3 ameligusia kwa mbali kidogo; Je, kilitokea nini? Inawezekana our trade regime provided the wrong incentives, au we lacked data realiable for planning, au hatukuwa na wataalam, au my favourite - mapato ya viwanda hayakurudi kuwekeza kwenye kilimo, badala yake yalielekezwa zaidi kwenye huduma za kijamii, and the list can go on and on; Vinginevyo kuna uwezekano kwamba under different incentive structures, output per unit of input inhaweza kukua kwa kasi kubwa kwenye protected industries kuliko ilivyotokea; Kwa kifupi - tunaweza hitimisha kwamba at least in our case, protectionism under inward looking strategies haikupelekea growth in output per unit of input kwa viwango vya kurudhisha, and since hapo ndio proponents of infant industry usually base their claim for protectionism, katika hilo walianguka; Lakini swali la msingi linajirudia tena, kwamba, fine, tulishindwa to take off under the inward looking strategies, je, viwanda vingi vya wakati ule kuwa sasa ni machaka ya chatu, maghala ya wahindi kuhifadhi mazao ya kilimo na bidhaa zao kutoka nje, under the outward lokking strategies za nyakati hizi, inatueleza nini?

Cc Zakumi,
Zinedine una hoja za msingi sana #14 , nitakurudia;


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom