Uchumi wa Tanzania: Je, Ni Kitendawili au Ni Mazingaombwe Kwa Maskini?

Uchumi wa Tanzania: Je, Ni Kitendawili au Ni Mazingaombwe Kwa Maskini?

Lakini swali la msingi linajirudia tena, kwamba, fine, tulishindwa to take off under the inward looking strategies, je, viwanda vingi vya wakati ule kuwa sasa ni machaka ya chatu, maghala ya wahindi kuhifadhi mazao ya kilimo na bidhaa zao kutoka nje, under the outward lokking strategies za nyakati hizi, inatueleza nini?

Cc Zakumi,
Zinedine una hoja za msingi sana #14 , nitakurudia;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Mkuu Mchambuzi hili swali ni kama nimeligusia kwenye mchango wangu na. 14. Hofu ya outward looking policy ni namna nzima ya kulinda sekta zako ambazo uti wa mgongo wa Taifa. Ukweli ni kwamba WTO regimes inatoa nafasi kubwa tu kwa hizi nchi ndogo kutumia hizo trade remedies lakini tatizo lililopo ni kwamba Hizi nchi zetu hazijui kutumia hizi kitu. Leo hii China wanatumia sana trade remedies na masharti kibao, mengine yako ndani ya WTO regimes (lakini mengine wanakiuka) kwasababu China ni Middle income country hivyo wana limitations fulani, lakini kwa nchi yetu ambayo ni LDCs ina loophole nyingi ya kutekeleza outward-protective policy kwani hatuko binded sana na WTO standards, bali Serikali haina mpango wa kutumia wataalamu wa Biashara kucheza na hizi kitu. Kwa mfano, Korea mpaka leo hataki kutambuliwa kama Developed country kwasababu akifanya hivyo itabidi baadhi ya trade remedies asizitumie. Nchi hiyohiyo inalinda sekta ya kilimo kwa nguvu zote hususan mchele wao,(Labda waondoshe miaka michache hii), ni kwasababu wanaweza kusoma documents za mwenendo na sheria za Biashara duniani na kuzitumia. Wataalamu wetu kwa kuwa hawasikilizwi, wanacheza karata tu ofisini, hakuna Ofisi inayofanya research nowdays.

Hivyo, bado Serikali ina nafasi kubwa ya kulinda viwanda vyake huku bado ikawa na nafasi ya kuuza nje, kwani hata retalitaion measures zenyewe kutoka kwa mataifa makubwa kwa nchi hizi zinalindwa (to a given
threashold). Hii nchi kinachoua ni USHAMBA na 10%, kuna watu wanahongwa vitu vidogo sana ili ku-divert national plans au strategies, Tuisheni fee kwa watoto wao, safari za kitalii nje ya nchi basi, zinawafanya wapitishe vitu vya ajabu sana. Makamu wa Rais wa Zambia Guy Scott, alialikwa na wachina (call investors) kwa ajili ya Lunch (luncheon), alipotoa neno la shukrani aliwaambia, anashukuru kwa lunchi lakini ile lunch yeye haisaidii Zambia, Zambia imeita wachina na wageni wengine kwa ajili ya mambo mawili tu. Waweze kuongeza ajira kwa wazambia na ku-raise mapato ya Serikali si vinginevyo, wala sio lunch! Wachina wakainamisha vichwa chini. Je Makmu wetu au Waziri Mkuu wetu anaweza kuwaambia "wawekezaji" waliomualika lunch. Ukifuatilia maisha ya Guy Scott wa Zambia, kuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwa Mzambia/mzungu huyu. (sorry kwa kutoka kwenye mada kidogo).
 
Kwa mara ya kwanza Tanzania tunaongelea trend ya ukuwaji wa uchumi kwa miaka 17 mfululizo, haijawahi kutokea.

Usitegemee kuwa uchumi utakuwa kwa uwiano sawa katika sekta zote na katika tabaka zote. Hakuna economist duniani anaeweza kufanya miujiza hiyo.

Hata muwe hamfanyi kazi na mnangoja kupewa tu hisa za migodi na mafuta na gas, pia hamtaweza watu million 45 kuwa na uwiano sawa wa kiuchumi.

Ndio maana asilimia zinazotajwa ni uwiano.

Msingi mkubwa faida kidogo; Mfano, ukiwfanya biashara ya millioni 200 ukapata faida ya 5% hapo una millioni 10 faida.

Msingi mdogo faida kubwa; Ukifanya biashara ya 100,000 ukapata faida faida 100% hapo una faida ya 100,000.

Utaona kwa mfano huo ingawa mwenye msingi mkubwa kapata faida kubwa lakini kibiashara / kimahesabu kapata faida ndogo, asilimia 5 tu. Na yule mwenye msingi mdogo kapata faida ndogo ya laki moja tu lakini kimahesabu huyu kafanya vizuri sana.
 
Mkuu Mchambuzi hili swali ni kama nimeligusia kwenye mchango wangu na. 14. Hofu ya outward looking policy ni namna nzima ya kulinda sekta zako ambazo uti wa mgongo wa Taifa. Ukweli ni kwamba WTO regimes inatoa nafasi kubwa tu kwa hizi nchi ndogo kutumia hizo trade remedies lakini tatizo lililopo ni kwamba Hizi nchi zetu hazijui kutumia hizi kitu. Leo hii China wanatumia sana trade remedies na masharti kibao, mengine yako ndani ya WTO regimes (lakini mengine wanakiuka) kwasababu China ni Middle income country hivyo wana limitations fulani, lakini kwa nchi yetu ambayo ni LDCs ina loophole nyingi ya kutekeleza outward-protective policy kwani hatuko binded sana na WTO standards, bali Serikali haina mpango wa kutumia wataalamu wa Biashara kucheza na hizi kitu. Kwa mfano, Korea mpaka leo hataki kutambuliwa kama Developed country kwasababu akifanya hivyo itabidi baadhi ya trade remedies asizitumie. Nchi hiyohiyo inalinda sekta ya kilimo kwa nguvu zote hususan mchele wao,(Labda waondoshe miaka michache hii), ni kwasababu wanaweza kusoma documents za mwenendo na sheria za Biashara duniani na kuzitumia. Wataalamu wetu kwa kuwa hawasikilizwi, wanacheza karata tu ofisini, hakuna Ofisi inayofanya research nowdays.

Hivyo, bado Serikali ina nafasi kubwa ya kulinda viwanda vyake huku bado ikawa na nafasi ya kuuza nje, kwani hata retalitaion measures zenyewe kutoka kwa mataifa makubwa kwa nchi hizi zinalindwa (to a given
threashold). Hii nchi kinachoua ni USHAMBA na 10%, kuna watu wanahongwa vitu vidogo sana ili ku-divert national plans au strategies, Tuisheni fee kwa watoto wao, safari za kitalii nje ya nchi basi, zinawafanya wapitishe vitu vya ajabu sana. Makamu wa Rais wa Zambia Guy Scott, alialikwa na wachina (call investors) kwa ajili ya Lunch (luncheon), alipotoa neno la shukrani aliwaambia, anashukuru kwa lunchi lakini ile lunch yeye haisaidii Zambia, Zambia imeita wachina na wageni wengine kwa ajili ya mambo mawili tu. Waweze kuongeza ajira kwa wazambia na ku-raise mapato ya Serikali si vinginevyo, wala sio lunch! Wachina wakainamisha vichwa chini. Je Makmu wetu au Waziri Mkuu wetu anaweza kuwaambia "wawekezaji" waliomualika lunch. Ukifuatilia maisha ya Guy Scott wa Zambia, kuna mengi sana ya kujifunza kutoka kwa Mzambia/mzungu huyu. (sorry kwa kutoka kwenye mada kidogo).

Zizou;

Tatizo lililopo ni kuwa sera ya viwanda ya Tanzania katika kipindi cha miaka ya 60 na 70 ilikuwa chini ya serikali. South Korea na Taiwan sera zilikuwa chini ya private sekta. Na wajapan walianza kwa kuimarisha private sekta.

Ukichukua matajiri wetu wakubwa: Mengi na Bakhresa. Walianza na mitaji midogo kuliko mashirika ya umma. Mashirika ya umma yamekufa wao bado wanapeta. Na vizuri zaidi wamefanya diversification ya biashara zao.

Nina uhakika kuwa kama tungekuwa na sera za kukuza private, tungekuwa mbali.
 
Mkuu Zinedine, Ningependa kujadili kidogo kuhusiana na experience ya South Korea; Kufikia late 1960, taifa hili lilikuwa limejitengenezea a well educated labour force relative to their physical capital, suala ambalo liliwatengenezea mazingira mazuri ya kupata "high return to capital"; Kwa Tanzania, hali yetu in terms of a well educated labour force ilikuwa ni kinyume kabisa, na mbaya Zaidi, miradi mingi ya maendeleo – hasa viwanda na mashirika ya umma, yalikuwa chini ya wanasiasa kuliko wataalam. Pia kwa wenzetu Wakorea, ruzuku (subsidies) & coordinated investment decisions kupitia effective polices (ambazo Zinedine umegusia baadhi), ziliwezesha serikali to engineer significant in private returns to capital; Vile vile, serikali iliweka in place equality of income and wealth ili kuiokoa jamii from sent seeking behavior; Tanzania tulijaribu hili kupitia azimio la arusha bila ya mafanikio ya msingi;

Nakubaliana na Zinedine kwamba kwetu Tanzania, it is ‘business as usual'; tutakabiliwa na a huge deficit in policy making – tunajaribu kukimbilia maendeleo kwa kuiga wengine wamefanya nini as if tumeambiwa kwamba development is path dependent while it's really not!; Kila taifa lililoendelea leo limefikia hatua husika kupitia njia mbalimbali, sio kwa kuiga wengine wamefanya nini; Hata hizi East Asian Tigers zilibezwa sana na World Bank et al kwa kufanya mambo nje ya ushauri wao, only to be embarrassed baadae; Hadi leo, World Bank anaongea kwa aibu sana juu ya mafanikio ya South Korea; Cha msingi hapa ni kwamba kuna umuhimu wa kuchukua experience za wenzetu na kuchanganya na akili zetu wenyewe; na katika hili, tunahitaji sana kuwa na uongozi wa nchi ambao upo reform – minded, wenye' political will' katika kuleta mageuzi yenye maslahi ya taifa (sio maslahi ya wawekezaji au mitaji ya nje pekee); Tumekuwa ni taifa maarufu kwa kusua sua sana in terms of reforms zenye manufaa kwa wananchi walio wengi, na hata katika suala zima la EAC, vurugu zote hizi zinatokana na ukaidi wa viongozi wetu; Ni bahati mbaya sana wananchi wengi wanazidi kuaminishwa kwamba wakorofi ni majirani zetu; Pia Zinedine ana hoja ya msingi sana pale anapojadili juu ya viongozi wetu kujichanganya between mfumo na mkakati; mfano, rejea porojo za Big Results Now, Presidential Delivery Unit, yote haya lengo lake ni to distract wananchi wasiweze kuona mapungufu ya serikali katika utendaji wa kuhudumia wananchi;

Vile vile, ana hoja nyingine ya msingi sana inayojadili juu ya ukosefu wa mikakati ya kukuza mazao ya nje; Hii ni kweli, na kuna mwanazuoni mmoja (Robert Calderisi) anaelezea vizuri sana jinsi gani mawaziri wa Trade kutoka Africa walivyoshiriki kukwamisha trade negotiations kwa maslahi ya Africa kule Cancun; Kwa mujibu of his account ambapo alikuwepo kwenye mkutano ule, ukumbi ulilipuka na makofi kutoka kwa mawaziri wengi wa Africa, kitendo ambacho kiliacha NGOs zilizoenda kushinikiza Africa ipewe fursa, wakibakia midomo wazi na wasijui la kufanya; Inasemekana, hata Waziri wa Tanzania wa wakati huo alikuwa miongoni mwa viongozi kutoka Africa walioshiriki kuangusha bara letu la Africa; Ni watanzania wachache sana ambao they have knowledge jinsi gani taifa letu linakosa masoko ya nje kutokana na njama za makusudi za viongozi wenyewe; Hapo awali nilijadili kwamba ‘economic development ‘isn't path dependent, kwani tumeona jinsi gani nchi mbalimbali zikitumia njia mbalimbali kujikwamua kutoka kwenye umaskini – kwa mfano tukitazama East Asian Tigers, Brazil, Chile, Vietnam, India, China, na hata Botswana na Mauritius barani afrika, zote hizi zimepitia njia mbalimbali, tukiachilia mbali mataifa makubwa kama vile Ujerumani, UK, USA n.k;

Katika nyakati hizi, njia pekee iliyopo ni viongozi wetu kukubali kuleta mageuzi ya kisiasa na kiuchumi (reforms) wakiwa na mioyo ya uzalendo, lakini pia huku wakiwa waangalifu kwamba such reforms zisifanywe ndio conditionality of AID; Isitoshe, suala la AID kwa kiasi kikubwa ni letu wenyewe Tanzania na nchi nyingi za Africa kujitakia; Hivi inaingia akilini kweli kwa taifa kama Tanzania, kuwa tegemezi kwa donors in terms of bajeti za maendeleo? Jibu ni hapana. Na maelezo pekee juu ya kuendelea kwa tabia hii ni kwamba Tyrants love AID, kwani it helps them remain in power na pia enrich themselves for political gain binafsi lakini vile vile kwa wale wanaopanga kuwarithisha; Kwanini nchi nyingine ndogo ndogo tu Afrika zimefanikiwa kujikwamua (mfano Botswana na Mauritius)? Ni kwa sababu, nchi kama Botswana and Mauritius are the only true reformers in the continent, na wakiendelea na mwendo wao wa sasa, haitakuwa ajabu tukasikia wapo njiani kuelekea mafanikio ya East Asian Tigers; Tukichukulia nchi kama Mauritius, hawa hawana any natural resources lakini they have the highest income per capita in Africa; Mauritius hawana any meaningful amount of raw materials za kukukuza maendeleo ya viwanda vyao, lakini as of today, this is the only country in Africa (outside South Africa) for the past 50 yesrs, ambayo imefanikiwa to undergo an industrial revolution (outside South Africa); Vile vile, nchi hii haina vivutio vingi vya kitalii kama Tanzania lakini inasemekana inapokea mapato mengi kuliko Tanzania kutoka sekta ya utalii;

Kwanini wenzetu hawa waweze, na sisi tushindwe? Jibu ni kwamba tumekosa intelligent leadership, na wakipatikana, wanapigwa vita na fitina wasionekane ni wa maana, mara nyingine hata wananchi maskini nao wakishiriki katika mipango hiyo; Inavyoonekana sasa chini ya CCM, ili mtu uwe influential in terms of leadership, experience, uadilifu, uzalendo, education and wisdom havipewi kipaumbele kama kipimo cha ubora wa uongozi, badala yake mtu utapendwa CCM na kupewa madaraka na watawala iwapo utakuwa na sifa kuu zifuatazo:

  • Ignorance
  • Dishonesty
  • Stubbornness

Hizi ndio common features of leadership under CCM ambazo kimsingi ndio zinazorotesha uchumi wetu from their micro and meso perspective; ni wehu kupigia mafanikio ya kiuchumi at macro level wakati the macro success doesn't tricle down to the meso and micro; Nitarejea kujadili zaidi juu ya suala zima la industrial policy…

Cc Nguruvi3, Zakumi
 
Last edited by a moderator:

Kama nimetafsiri vibaya nitaomba mnisamehe, lakini nilichokibaini hapa mjadala uliopo kwa sasa si policy gani kama nchi ni nzuri kuifuata kati ya "export promotion" na "import substitution" na vilevile hatuna tatizo kubwa la direct external influence, bali ni tatizo la internal reforms and capcity kutekeleza chochote nchi iliyojipangia. Mchambuzi umekuja na ukweli huu baada ya kuonyesha kwamba reforms zetu ziko kwenye makaratasi kwa kukosa intelligence leadership ambayo inazaa weak management ya kusimamia mipango tuliyonayo. Binafsi sioni umuhimu wa kuwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kama overall coordinating office, Tume ya Mipango, Wizara ya Fedha na Uchumi yenye Idara ya Sera, hapo hapo panaanzishwa Presidential Delivery Unit/Bureau, hii si tu kwamba kuonyesha namna ofisi ya Waziri Mkuu inavyoshindwa kusimamia taasisi zilizopo kuleta tija katika uzalishaji, lakini pia ni uharibifu wa fedha za kutekeleza uzalishaji. Hii pia italeta fragmentation katika policy implementation na finacing options hivyo kutoleta matunda tarajiwa. Ni mfano kama wa fedha za mradi zinazoishia kwenye posho za viongozi wa mradi badala ya kununua mahitaji ya mradi.

Nikirejea kwenye mada, hivyo swali la msingi ni vipi kama nchi iko tayari katika kutekeleza na kusimamia reforms na policy zake. Hili ndilo suala la msingi ambalo binafsi linanitatiza kwani nadhani kwamba hakuna "focus" moja miongoni mwa watendaji wetu au mihimili yetu. Wako watendaji au mihimili ambao wanataka kuwatumikia wananchi lakini wanakutana na "equal and opposite" group lisilotaka kuwatumikia watendaji hivyo nchi kujikuta inapiga mark-time. Ukiangalia yanayotokea kwenye maeneo kama Bungeni ambako nilitarajia kuona watu wakijitoa mhanga kupendekeza kupunguziwa stahili zao, ndio kwanza kila Kikao huwa kinakuja na Agenda za kuongeza maslahi yao huku wakiwa wamejiziba masikio na macho juu ya hali ya Wananchi ambayo kwa kweli kwa dunia ilivyo, hazistahili. Je ni namna gani au mbinu gani zitumike kuwafanya watendaji wetu au mihimili yetu kuwa focused na jambo moja tu la kuwatumika wananchi? Tuna tatizo la capital financing, Je ni njia gani tunaweza kutumia kupata capital financing?

Kitatokea nini ikiwa Serikali itaaanzisha "compusory contributions" kutokana na stahili za viongozi wote nchi nzima ili kujenga maabara walau kila baada ya miezi mitatu? Tunajua kuna wabunge wanatumia asilimia kadhaa za mishahara yao katika kuboresha elimu katika majimbo yao (volutarirly) na haiwafanyi kushindwa kuishi. Maana hatuna budi ukweli tuukubali kwamba hali yetu kama Taifa ni mbaya sana, isiyohitaji unpredictable financing kutoka nje, na hata zikija zinaishia kwenye mifuko ya watu. Rwanda ilipopunguziwa misaada miaka michache iliyopita, ilianzisha "compusory contribution" kwa kupunguza stahili kadhaa za wafanyakazi wake hususan wa juu, na iliweza kufadhili baadhi ya shughuli za Serikali.

cc Nguruvi3, gfsonwin, Zakumi,
 
Neno moja tu: uongozi

Mengineyo ni pamoja na absence of sound economic policies, absence of real law enforcement mechanisms and the rule of law, presence of high illiteracy rates.

Mwisho wa yote: Uongozi una mata sana
 
Kwa wanaodhani kuwa sera za mwaka 1967 hadi 1987 zilzioachwa miaka 30 iliyopita ndizo zilizosababisha yote hayo rudini nyuma mfikiri kwa akili timamu tena.

Uganda iliyokuwa chini ya Amini hadi mwaka 1980 ikavurugwa sana na vita ya wenyewe kwa wenyewe hadi ilipoanza kuongoza na mseveni miaka 30 iliyopita kwa nini yenyewe iwe na uchumi bora kuliko wetu sisi?. Rwanda iliyouana wenywe kwa wenyewe hadi ikawa kama hakuna taifa tena miaka 20 iliyopita hadi walipoanza kutawaliwa na kagame miaka kama kumi na sita iliyopita inakuwaje iwe na uchumi mzuri kuliko Tanzania tena ukizingantia kuwa ni nchi ndogo yenye raslimali kiduchi sana.

Sera hizo hizo zilizokuwa zinafuatwa na Tanzania ndioz pia zilikuwa zinafuatwa na China, inakuwaje China leo ambayo bado ina mashirika ya umma tena mengi sana lakini ina uchumi wa pili kwa ukubwa duniani leo.

Tatizo la Tanzania ni sisi wenyewe siyo Nyerere wala Mkoloni wala bahati mbaya bali ni ujinga wetu wa kuendelea kukubali kutawaliwa na viongozi wasiofanya kazi na halafu hatuwawajibishi.

Huko China ukiiba mali ya umma au ukishikwa na rushwa ama unayongwa au unafungwa maisha. Pale kwa Kagame mtu akidokoa mali ya umma au akitumia madaraka ya umma vibaya anapelekwa kusikojulikana kimya kimya. Kwa mazingira yao, kumekuwa na discipline ya kufanya kazi kwa manufaa ya nchi siyo kama kwetu hapa ambapo kila mtu anataka kujaza mapesa uswisi na kujenga maghorofa ya familia yake kwa kutumia mali za umma kama ilivyo kwetu.
 
Wanabodi hongeren sana kwa hoja nzuri zenye kujaa changamoto nyingi ambao kila mmoja wenu amejaribu kuaninisha kwa nafasi yake hali halisi jinsi ilivyo. Mchambuzi nakupongeza zaid kwa hoja iliyojaa reference za kutohsa ili kubainisha hali halisi ilivyo hapa kwetu.

Nimeona kuna hoja kubwa ya msingi zaid ambayo bado haijatajwa kama msingi wa maendeleo na ukuaji uchumi wa taifa hili na hili si tu kukuza uchumi wa nchi bali hata kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja.

maendeleo na ukuaji wa sayansi na teknolojia ndiyo nyenzo pekee ambayo sasa nchi yetu kama nchi inatakiwa iitizame kwa jicho la tofauti kidogo lenye upendeleo.Ukuaji wa sayansi na Teknolojia ndiyo njia pekee ambayo hata nchi kama South Africa ni nchi ambayo kwa hapa Africa imepiga hatua sana kwenye sekta hii ya sayansi na technolojia na lleo hii ndiyo nchi pekee Africa ambayo inazalisha bidhaa kutokana na raw material zilizoko nchini mwao na kuuza nje ya nchi yao.

Tukiongelea export of low value goods or rather unprocessed goods tunaongelea mitaji amikubwa sana kwa wengine. Manake think of how many time, money, agri medics have been used ili kuweza kuitoa hiyo raw material?? ni wazi kwamba mkulima ametumia mtaji mkubwa sana sana sasa kwann bidhaa hii kwenye soko la dunia ikanunuliwe kwa bei ya kutupa?? Jibu linabaki kuwa kwamba technology ndiyo tunayokwenda kuuziwa.

je ni kweli kwamba sisi hatuwez kuwa na technolojia yetu na ikazalisha bidhaa nzurri na za kisasa kwa ajili ya biashara za kimataaifa?? Je wasomi wetu wanaosoma sayansi uhandisi hasa wa viwandani je ni kweli kwamba hawawez kuwa na hii technolojia??

je kwa nini serikali isijitolee kukuza taasisi kama TIRDO na za kufanana na hizi ili kuweza kukuza technolojia nchini mwetu??

Sioni mantki ya kuwapa vipaumbele wabunge wetu ilihali wao sio watendaji lijapo swala la kukuza uchumi akasahaulika kijana anayesoma chemical processing ambaye angeweza kugharamiwa kufanya project ambayo ni technology innovation.Leo hii nenda kwenye vyuo vikuu mwaka wa 4 mtu anafanya project ni amesoma MECHE eti badala ya kwenda kwenye technical field akaonyeshe ujuzi wake anapelekwa kwenda kusimamia fundi mwendesha catapiller la STRABAG ama napelekwa TICS kumsimamia mwendesha crane la kupakua makontena. sasa kweli hii ndiyo kazi ya huyu mtu?? je hapo unategemea atakuja na ujuzi gani??

TIRDO leo hii ikifufuliwa, ingesimamia viwanda kama machine tools, nyumbu na vinginevyo wanafunzi kama hawa wanapelekwa kule wao kazi yao ni moja tu wawe na ubunifu hasa kwenye mashine ungeona leo tuko wapi.angalia tasisi kama SAAST ya SOUTH AFRICA inavyojitahd kuhakikisha kwamba vijana wakiwa vyuoni wanavyo deliver na wanahikisha wote kwamba they do things in a practical way.

kwa jinsi hii iliwafanya vijana wengi watumike viwandani na viwanda vingi vianzishwe ili waweze kuwatumia na mpaka wa leo south africans wanauza madawa ambayo ni patent yao wenyewe wala hata si generic.

Ifike mahali sasa siasa iwekwe mbali watu wawe na nia ya kuona nchi kama nchi inapiga hatua ya kweli kwenye ukuaji wa sayansi na technolojia ili kuweza kukuza viwanda vyetu.
nitarudi baadae.
 
Last edited by a moderator:
Kwa wanaodhani kuwa sera za mwaka 1967 hadi 1987 zilzioachwa miaka 30 iliyopita ndizo zilizosababisha yote hayo rudini nyuma mfikiri kwa akili timamu tena.

Uganda iliyokuwa chini ya Amini hadi mwaka 1980 ikavurugwa sana na vita ya wenyewe kwa wenyewe hadi ilipoanza kuongoza na mseveni miaka 30 iliyopita kwa nini yenyewe iwe na uchumi bora kuliko wetu sisi?. Rwanda iliyouana wenywe kwa wenyewe hadi ikawa kama hakuna taifa tena miaka 20 iliyopita hadi walipoanza kutawaliwa na kagame miaka kama kumi na sita iliyopita inakuwaje iwe na uchumi mzuri kuliko Tanzania tena ukizingantia kuwa ni nchi ndogo yenye raslimali kiduchi sana.

Sera hizo hizo zilizokuwa zinafuatwa na Tanzania ndioz pia zilikuwa zinafuatwa na China, inakuwaje China leo ambayo bado ina mashirika ya umma tena mengi sana lakini ina uchumi wa pili kwa ukubwa duniani leo.

Tatizo la Tanzania ni sisi wenyewe siyo Nyerere wala Mkoloni wala bahati mbaya bali ni ujinga wetu wa kuendelea kukubali kutawaliwa na viongozi wasiofanya kazi na halafu hatuwawajibishi.

Huko China ukiiba mali ya umma au ukishikwa na rushwa ama unayongwa au unafungwa maisha. Pale kwa Kagame mtu akidokoa mali ya umma au akitumia madaraka ya umma vibaya anapelekwa kusikojulikana kimya kimya. Kwa mazingira yao, kumekuwa na discipline ya kufanya kazi kwa manufaa ya nchi siyo kama kwetu hapa ambapo kila mtu anataka kujaza mapesa uswisi na kujenga maghorofa ya familia yake kwa kutumia mali za umma kama ilivyo kwetu.

Mkuu Kichuguu:

Sio sera za mashirika ya umma za Chairman Mao ndizo zilizoleta maendeleo China. Katika miaka ya 1967-1987, karibu nchi zote za dunia ya tatu zilikuwa na uchumi unaotegemea mashirika ya umma. Kenya, Uganda, Zambia, Tanzania, Msumbiji, Cuba, Vietname n.k

Ukitaka kufanya mlinganisho mzuri, basi usilinganishe Tanzania na China tu. Linganisha Tanzania na nchi zingine na utaona kuwa tatizo linajirudia na hakuna nchi iliyoweza kutumia sera hizo kuleta maendeleo.

China was a sleeping giant. Hivyo tatizo lilikuwa ni kumwamsha aliyelala. Vilevile ana majirani waliondelea kama vile Japan. Vilevile business model yao inawapa competitive advantage. China ina idadi kubwa ya watu walioelimika ambao ni low cost skilled labour. These are economic ingridients we don't have.

Turudi kwenye mada kamili. Pamoja na kuwa na uongozi mbaya uchumi wa Tanzania unakuwa. Kitu hiki kilikuwa ni kitendawili wakati wa enzi ya uongozi bora na siasa safi. Hivyo tunaweza kusema kuwa uongozi bora na siasa safi sio sababu pekee za kukua kwa uchumi.

Matatizo yaliopo Tanzania kwa sasa ni distribution of wealth. Katika nchi masikini tunaiangalia katika utoaji wa huduma za jamii kama vile elimu, afya, na miundo mbinu ya mawasiliano na nishati. Vilevile vyanzo vya mapato ya taifa kwa sasa sio sustainable. Na hapa ndipo nakubaliana na wewe kuwa nchi inatakiwa kuwa na viongozi makini.

Viongozi makini ambao watakuwa na sera zinazobadilika kutokana na wakati na mazingira. Katika kipindi hiki cha mabadiliko ya technologia na globalization, economic and business cycles zinabadilika haraka haraka sana na Tanzania haiwezi kutumia sera za 1967-1987 kwa maendeleo yake.
 
Kuhusu uchumi wa china, nadhani unausoma kijuu juu tu. Uchumi wa china umetokana na state investment. Mwaka 1994 walileta ujumbe mzito sana pale Japan kutafuta msaada kwa kutumia mkondo wa kiserikali kuwezesha kujenga reli ya haraka - Chinkasen, na teknolojia ya multimedia computers wakati huo. Mwaka huo huo wakatuma ujumbe mwingine mzito sana wa kiserikali huko Marekani kuomba bidhaa za nchi yao zipewe upendeleo katika soko la Marekani ili kuwasaidia kupambana na umaskini; walifanya hivyo pia katika nchi kadhaa za Ulaya hasa Ufaransa na Ujerumani. Kuanzia mwaka huo huo wakawa wanawekeza sana katika kununua government bonds za marekani. Maelezo yanayofuata hapo ni marefu kidogo, ila miaka 15 baadaye wakawa waliweza kufumua ile treni waliyotoa Japan na ile waliyotoa Ufaransa na kuunda yao ambayo ilikuwa ni ya kasi kuliko zile ya Japan na Ufaransa. Short cut tunayotumia kueleza mafanikio ya China si sahihi, tunaweza kuijadili njia yao kwa kirefu lakini chini ya yote kuna factor moja kubwa sana ya uongozi.

Kuhusu China kuwa na educated population nalo ni jambo jingine tunaloweza kulijadili. Educated population ya china inatokana na investment ya serikali katika education. Zamani sana wakati Tanzania haina uongozi makini tulikuwa na investment kubwa sana katika education lakini baada ya uongozi wenye sera mbovu kuondoka madarakani, literacy rate ya Tanzania iliporomoka kwa kasi sana kutoka zaidi ya 85% hadi kufikia 67% leo tukiwa chini ya majirani zetu wote.

Kuhusu uongozi bora siyo tabia tu bali pia ni ule uwezo wa kujua kutumia opportunities zinazokuja kama ambavyo wachina walivyofanya. Opportunities na chellenges zilizokuwapo wakati wa Nyerere siyo zilizoko leo.

Ninajua Anti-Nyerere wengi hutumia Nyerere kama scapegoat ya kueleza matatizo yetu; kiongozi wetu leo alishatoa mifano mingi sana ya kulinganisha hali ya leo na wakati wa Nyerere ambao hata calculator haikuwapo lakini bado wanataka kulinganisha kuwa leo tuna kompyuta ambazo hamkuziona wakati wa Nyerere: blindness kubwa sana hiyo inapotoka kwa kiongozi mjue mna matatizo; hamjui muendoko.

Tujifunze kukubali ujinga wetu, halafu tuamue kuufuta. Kutafuta sababu za kuhalalaisha failures zaetu ni kutudidimiza zaidi. Bila kwenda huko mbali China au Vietnam, tujiulize tu kuwa kwa nini Rwanda inaendela kwa kasi kuliko sisi iwapo tuko katika mazingira yale yale na wao walipitia wakati mgumu sana na wala hawana raslimali kama sisi.

Tunaweza kuja na maelezo marefu sana ya kujaribu kuthibitisha kuwa sera za Nyerere za mashirika ya umma ndizo zilizofanya Tanzania iwe maskini leo, ila tutakuwa hatuwatendei haki wasomaji wetu kutokana na sababu nyingi ila mojawapo nyepesi ikiwa ni ile wanasheria wanayoita statue of limitations. Miaka 30 Nyerere aliyoondoka madarakani ni muda mrefu sana kuliko miaka 26 aliyotawala. Alianza kutawala nchi ikiwa na wataalamu wa kuhesabu, wakati anaondoka aliacha kukiwa na wataalamu kibao na vyuo vingi sana. Alituachia nafasi yote ya kurekebisha mabaya yake lakini bado tumelala tu mpaka leo tunamuota Nyerere. Hii inaonyesha jinsi gani sisi watanzania tulivyo watu wa namna gani iwapo hata sisi wataalamu bado tunadai kuwa makosa yote ni ya Nyerere. Hatukubali responsibility; tumejijenga kuwa watu wanaoamini entitlement. Ndiyo maana tukiwa na tatizo ama tunaomba msaada au tunatafuta mwekezaji wa kutufanyia.

Pale China mpaka leo Makampuni makubwa mengi ni yale yaliyoundwa na Mao au yaliyoundwa tena na serikali chini ya dhana ile ile ya Mao ila mfumo ukiwa imeboreshwa vizuri zaidi kuruhusu private investment. Mao alipokufa walifanya kazi ya kurekebisha makosa yake bila kuua mashirika yao; angalia list hii. Walikaribisha makapuni ya nje halafu makampuni yao yakawa yanajifunza kutoka kwa hayo yaliyokaribishwa. Sisi tunakaribisha makampuni ya nje ama kwa kuua ya kwetu au kwa kuwagawia wachukue hayo ya kwetu.

Siyo lazima tufuate njia ya China lakini kwanza ni lazima tujikomboe kimawazo kutambua kuwa maendeleo huletwa na watu wenyewe, hayaletwi na historia wala watu wa nje bali ni sisi wenyewe.
 
Kuhusu uchumi wa china, nadhani unausoma kijuu juu tu. Uchumi wa china umetokana na state investment. Mwaka 1994 walileta ujumbe mzito sana pale Japan kutafuta msaada kutumia mkondo wa kiserikali kuwezesha kujenga reli ya haraka Chinkasen, na teknolojia ya multimedia computers. Mwaka huo huo wakatuma ujumbe mwingine mzito sana wa kiserikali huko Marekani kuomba bidhaa za nchi yao zipewe upendelea katika soko la Marekani ili kwasaidia kupmbana na umaskini; walifanya hivyo pia katika nchi kadhaa za Ulya hasa Ufaranza na Ujerumani. Kuanzia mwaka huo huo wakawa wanawekeza sana katika kununua government bonds za marekani. Maelezo yanayofuata hapo ni marefu kdiogo, ila miaka 15 baadaye wakawa waliweza kufumua ile treni waliyotoa Japan na ile waliyptoa Ufaranza na kuunda yao ambayo ilikuwa ni ya kasi kuliko ile ya Japan na ya Ufaransa. Short cut tunayotumia kueleza mafanikio ya China si sahihi, tunaweza kuijadili njia yao kwa kirefu lakini chini ya yote kuwan factor moja ya uongozi.

Kuhusu China kuwa na educated poupulation nalo ni jambo jingine tunaloweza kulijadili. Educated population ya china inatokana na investment ya serikali katika education. Zamani sana wakati Tanzania haina uongozi makini tulikuwa na investment kubwa sana katika education lakini baada ya kupata uongzi wenye sera mbovu kuondoka literacy rate ya Tanzania iliporomoka kutoka zaidi ya 85% hadi kufikia 67% leo tukiwa chini ya majirani zetu wote.

Kuhusu uongozi bora siyo tabia tu bali pia ni ule uwzo wa kujua kutumia opportunities zinazokuja kama ambacyo wachina walifanya. Opportunities na chellenges zilizokuwapo wakati wa Nyerere siyo zilizoko leo.

Ninajua Anti-Nrere weni hutumia Nyerere kama scapeogoat; kiongzi wetu leo alishatoa mifano mingi sana ya kulinganmisna leo na wakati wa Nyerere ambao hata calculator haikuwapo lakini bado wanataka kulinganisha kuwa leo tuna kompyuta ambazo hamkuziona wakati wa Nyerere.

Tujifunze kukubali ujinga wetu, halafu tuamua kuufuta. Kutafuta sababu za kuhalalaisha failures zaetu ni kutudidimiza zaidi. Bila kwenda huko mbali China au Vietnam, tujiulize tu kuwa kwa nini Rwanda inaendela kwa kasi kuliko sisi iwapo tuko katioka mazingira yale yale na wao walipitia wakati mgumu sana na wala hawan raslimali kama sisi.

Tunaweza kuja na maelezo marefu sana ya kujaribu kuthibitisha kuwa sera za Nyerere za mashirika ya umma ndiyzo zilizofanya Tanzania iwe maskini leo, ila tutakuwa hatuwatrndei haki wasomaji watu kutokana na sababu nyingi ila mojawapo nyepesi ikiwa ni ile wanasheria wanayoita statue of limitations. Miaka 30 Nyerere aliyoondoka madarakani ni muda mrefu sana kuliko miaka 26 aliyotawala. Alianza kutawala nchi ikiwa na wataalamu wa kuhesabu, wakati anaondoka aliacha kukiwa na wataalamu kibau na vyuo vingi sana. Alituachia nafasi yote ya kurekebisha mabaya yake lakini bado tumelala tu mpaka leo tunamuota Nyerere. Hii inaonyesha jinsi gani sisi watanzania tulivyo watu wa namna gani iwapo hata sisi wataalamu bado tunadai kuwa makosa yote ni ya Nyerere. Hatukubali responsibility, ni tumejijenga kuwa watu wanaoamaini entintlement. Ndiyo maana tukiwa na tatizo ama tunaomba msaada au tunatafuta mwekezaji wa kutufanyia.

Pale China mpaka leo Makampuni makubwa mengi ni yale yaliyoundwa na Mao. Lakini Mao alipokufa wakafanya kazi ya kurekebisha makosa yake bila kuua mashirika yao; angalia list hii. Walikaribisha makapunia ya nje halafu makamupni yao yakawa yanajifunza kutoka kwa hayo yaliyokaribishwa.

Siyo lazima tufuate njia ya China lakini kwanza ni lazima tujikomboe kimawazo kutambua kuwa maendele hulewa na watu wenyewe, hayaletwi na historia.

Mkuu Kichuguu:

Nitaanza na paragraph yako ya mwisho. Unasema tujikomboe kimawazo na kutambua kuwa maendeleo yanaletwa na watu. Njia moja ya kujikomboa ni kuacha kufikiri kuwa makampuni au viwanda are prerequisite for economic growth. Nchi nyingi za kiafrika zilizopata uhuru miaka ya 50, 60 na 70 zilikuwa na sera za viwanda kama za Tanzania wakati wa Nyerere na zote zili-fail.

Kwa mfano Kaunda naye ali-implement sera zake za viwanda. Na yeye alitumia investment kubwa kwenye viwanda kuliko Nyerere aliyotumia. Lakini hakuna mafanikio yoyote yaliopatikana kule Zambia. Miaka ya 60, GDP ya South Korea ilikuwa ni mara mbili ya Zambia. Sasa hivi ni mara 40. Kama sera ya viwanda ni prerequisite for economic growth basi GDP ya Zambia ingekuwa nusu au robo ya South Korea.

Kuhusu Rwanda, vita vilileta mabadiliko ya uongozi na muundo wa uongozi. Rwanda na Burundi zinafanana karibu kwa kila kitu.Kama Rwanda inaendelea kwanini Burundi inasuasua. Rwanda inaendelea kwa sababu kuna Kagame. Tanzania nayo ikipata kiongozi mwenye kufanya kazi kwa kutumia common sense nayo ina nafasi ya kuendelea kwa sababu ina ingridients za maendeleo lakini wanakosekana wapishi.
 
Hiyo point ya tatu ndiyo ninayozungumza na nafurahi unakubaliana nami. Siyo historia inayotufanya tuwe maskini leo wakati opportunities zimekuwa nyingi sana leo hii, kinachotufanya kubaki maskini ni uongozi wetu. Uongozi una mata sana. China walikuwa na uongozi mzuri wakaendelea kwa kasi; Tanzania tuna wababaishaji tumebaki pia kuwababaishababaisha tu.

Samahani kwa typos nyingi zilizokuwa kwenye post yangu ya hiyo; nimezirekebisha
 
Hiyo point ya tatu ndiyo ninayozungumza na nafurahi unakubaliana nami. Siyo historia inayotufanya tuwe maskini leo wakati opportunities zimekuwa nyingi sana leo hii, kinachotufanya kubwaki maskini ni uongozi wetu. Uongozi una mata sana. China walikuwa na uongozi mzuri wakaendelea kwa kasi; Tanzania tuna wababaishaji tumebaki pia kuwababaishababaisha tu.

Samahani kwa typos nyingi zilizokuwa kwenye post yangu ya hiyo; nimezirekebisha

Kichuguu:

Uchumi unakuwa na kuporomoka. Hata kwa nchi zilizoendelea hii phenomenon hipo. Hivyo hata kama Nyerere angefuata siasa nazopenda mimi, ingefika kipindi hizo siasa zinge-experience fatique na uchumi ungeboronga. Hivyo cha muhimu sio kumlaumu Nyerere, bali kukusanya data hili matatizo yaliotokea wakati wa kipindi chake yasirudiwe.

Ukusanyaji na matumizi ya data sio kitu kinachofanyika. Na inasikitisha kuona kuwa kwenye sekta muhimu kama elimu tunarudia makosa yaleyale. Ufunguzi wa shule za sekondari za kata ni sawa mpango wa UPE. Tunaongeza enrollment wakati quality ya elimu inaporomoka.

Umefika wakati nchi ipate mtu wa kusema enough is enough. Uchumi wa Tanzania unakuwa lakini wanaofaidika ni wachache. Elimu nzuri ndio itakayosaidia katika tatizo la distribution of wealth.
 
mkuu umegusa mtima wangu kwa swala la elimu, umetaja utitiri wa shule za kata ukasahau utitiri wa vyuo vya kata vinavyoendelea kuanzishwa kila mwaka, hata sasa kama una jengo lako linaloonekana kama darasa ukienda TCU na bahasha yako ya kaki unaweza ukapata usajili wa chuo kwa kuwatumia wanafunzi wale wale waliotoka shule za kata kwa division zao 5 na wakifika chuo hiki kipya watakutana na vijana wenzao ambao watakuwa ndo walimu wao wapya waliomaliza vyuo vile vile vya kata na kupata First Class toka vyuo vile vile kwa njia wanazojua wao, loh! lakini pia wanafunzi hawa wapya wa chuo hiki kipya watabahatika sana kwa kumpata lecture wa UDSM anaekuja kwa part time ili ajiongezee kipato maana pesa za research now zinaishia mikononi mwa wajanja, nalia mimi, dah, yote hayo hayatokei kwa bahati mbaya, yamepangwa ili vijana wengi wapate vyeti vya degree na mwisho wa siku wanasiasa wapate cha kuongea kipindi cha campaign kwa takwimu nyingi nyingi, so sad,
 
Hiyo ndio "BIG RESULTS NOW".

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ndugu Mchambuzi,

Imenibidi tena nirudi hapa ukumbini kwa sababu maalum nayo ni kukata kiu cha watu hapa kuhusu UCHUMI wa nchi yetu na watu wameandika kila wanalofikiria lakini ukweli utabakia kwamba Tanzania kama nchi inayotembea kwa magongo haiwezi kufanikiwa ktk mfumo huu wa UBEPARI kamwe!

Nitasema ukweli daima na kama ilivyo signature yangu natazama hali halisi kwanza, kabla sijamtafuta mchawi. Kwanza tujiulize huu mfumo wa KIBEAPARI umetokana na fikra gani za Kiuchumi?. UBEPARI hauna kauli kubwa zaidi ya kuwepo vitu viwili, navyo ni 1. WaKOPOSHAJI (Financial Institutions) 2. WAKOPAJI (Inventors/investors)na ndipo hili neon - macro economic linapoweza kutumika kifasaha na ukayaona mabadiliko ya kiuchumi.

Kwa wana falsafa wa kiuchumi wanasema kwamba hizi itikadi mbili kati ya Ujamaa na Ubepari tofauti zake kubwa ni kama kusema hiv - Ubepari ni kuishi kwa madeni (mikopo) unajijenga taratibu tokana na uwekezaji na Ujamaa ni kuishi kwa fedha ulokuwa nayo mfukoni. Na ukitazama kwa undani kuna ukweli mkubwa ktk falsafa hizi mbili maana Wajamaa hawapendi kumtegemea mtu mwingine kifehda, bali wanaanzia pale walipo na kile walichonacho wakati MABEPARI maisha yao ni ya mikopo toka serikali zao hadi wananchi wake tunaishi kwa mikopo na hivyo inatakiwa nidhamu ya hali ya juu sana ktk Ubepari.

Sasa turudi nyuma, Ukiangalia nchi za magharibi huwezi kwenda mbele pasipo mokopo. Ubunifu wowote hutegemea kuna mwezeshaji ndani ambaye ataitazama idea yako, soko lake na hivyo kukopeshwa fedha za kufungua mradi ama hata ukitaka kununua nyumba hutazama kipato chako, kazi unayoifanya na kuhakikisha utaweza kumudu malipo ya nyumba hiyo. lakini tazama kwetu sasa, mtu anakopesha fedha benki sii kwa sababu ametazama soko na mahitaji ya jamii ili awekeze isipokuwa huchukua mkopo kwa sababu yeye mwenyewe anahitaji kitu kile..

Ndio maana nyumbani mtu akiomba mkopo wa nyumba, banki haitazami uwezo wa mwombaji isipokuwa rehani gani ameweka, iwe kiwanja, shamba au mali zake ambazo zinazidi thamani ya mkopo. Lengo la mikopo hii ni Ubeparimamboleo - Kuwaibia wananchi ardhi namashamba yao, ni kuwaingiza ktk umaskini zaidi kwa sababu benki zinajua hutaweza kulipa madeni ulokopa. Vivyo hivyo ukienda ktk Utaifa wetu, sisi kama nchi hupewa mikopo ama nisema misaada kwa njia hiyo hiyo ya kukimu matatiz yetu na ndio maana wanasema tunapewa AID. Wao hutazama watafaidika vipi na mkopo yao maana wanajua uwezo wa kuilipa hatuna, na kwa bahati mbaya mikopo yote tunayochukua sii kwa mtazamo wa soko bali kukimu mahitaji yetu sisi wenyewe ili hali tunauza umiliki wa ardhi kwao.

Kwa hiyo mkuu wangu ukitazama hizo nchi za Asia au South Amerika, hawa wameweza kuondokana na adha hizi kwa sababu kwanza wamejifunza Principals za Ubepari ambao kwanza mnatakiwa wenyewe kuwa na WAKOPESHAJI (Financial Institution) ambazo zitawawezehsa wananchi uwekezaji ktk ubunifu wao kulingana na mahitaji ya vitu mama mali ndani na nje. Hivyo wakaunda chombo hiki kwanza kasha mikopo haikutoka kwa kutazama matatizo ya watu wake bali uwekezaji wa miradi ya uzalishaji ambayo itauza mali zake ndani na nje.

Kina sisi hadi leo hii tunategemea Financial Institution kutoka nje, wawekezaji nao kutoka nje.. kasha tunajiuliza kwa nini hatujaendelea?. Sielewi wasomi wetu wamejifunza nini kuhusu Ubepari, maana binafsi nayasema haya kwa sababu ndio maisha ninayoishi na namshukuru Mungu ukijua jinsi unavyofanya kazi basi hata wewe ukiingia nchi hizi kesho, unaweza kutoka kirahisi maadam unaweza kubuni uwekezaji tokana na mahitaji ya watu (necessities).

majuzi Kiongozi wetu JK alizungumza kuhusu miradi ya gas na watu wamempongeza sana wengine kumlaumu lakini ukitazama kwa makini ukweli unabakia palepale. Sisi hatuna uwezo na hivyo kuwapa wageni uwekezaji na ukopeshaji hatujengi lolote zaidi ya kujiingiza ktk Ubeparimamboleo. Hakuna nchi yoyote ya Kibepari ambayo raisi wake angeweza kusema aloyasema JK kwa sababu nchi hizo tayari zina Financial Instituion zinazowawezesha wananchi kuwekeza na wananchi weke wana uwezo wa kuendesha mradi huo. Hivyo tunachokifanya ni kinyume kabisa cha Ubepari na haikubaliki ktk nchi yoyote ya kibepari.

Mwisho ni kusema kwamba Ujamaa wetu wakati wa Nyerere Ulishindikana kutokana na sisi wenyewe kutamani maisha ya juu ambayo hatukuwa na uwezo nayo. Ujamaa wa Nyerere ulikuwa tujikune tunapoweza, tutayatafuta maendeleo kwa fedha tulokuwa nayo mfukoni yaani tunaanza nauwezo tulokuwa nao badala ya kutegemea mikopo aua kuiga maisha ya nchi nyinginezo zilizoendelea. Sawa kabisa leo hii mimi Mkandara nifuate njia alizofanya Bakhresa kutajirika wakati ni maskini omba omba nayetazama kujikimu miye mwenyewe badala ya mahitaji ya watu wenignine, hivyo ukinipa mkopo miye nitafikiria kwanza nijenge nyumba yangu ya kuishi mimi na wanangu. Hivyo pamoja na kuwa na nyumba yangu ya kuishi matatizo yangu bado yako palepale maana sina kipato chochote na deni limenikalia kooni..

haya ndio maisha ya Tanzania yetu, siku zote tunapewa Mikopo ikiwa kama msaada maana sisi wenyewe ndio wenye shida na hivyo mikopo hiyo inatzama kuondoa matatizo yetu badala ya mikopo hiyo kutuwezesha sisi kuuza mali zetu nje kulingana na mahitaji ya soko la dunia, hivyo hata nyumba zetu zitajengwa kutokana na faida ya mauzo.
 
Mchambuzi, Nirejee tena baada ya kuwasoma wanajamvi walionigusa kwa namna moja au nyingine.

Mkandara : Nakubaliana na dhana yako ya ujamaa na ubeapri.

Kwa bahati mbaya sisi hatupo katika sehemu ya yote mawili. Kundi letu ni la 'kuchanganyikiwa'

i)Ubepari-kuishi kwa mikopo. Tumechagua ubepari na tunaishi kwa mikopo,hatutumii mikopo hiyo kujikwamua. Robo inakwenda Uswiss au kuonekana katika ofisi za CAG. Hakuna public investment bali ni tumbo street

ii)Ujamaa- kuishi kwa kile ulichonacho. Hatuishi hivyo kwasababu tuna vitu kama serikali kubwa, tumeua viwanda hata vya sabuni au kahawa. Tunatumia fedha nyingi kufuja na marupurupu n.k.

Hakuna saving kwa kile tulicho nacho.

Maswali ya Mchambuzi yanakuja; Endapo tuna resources kama human capital na natural resources wapi tatizo letu lilipo?Kichuguu katoa jibu moja rahisi sana na muhimu sana, Uongozi

Zakumi
; Sera za Nyerere kuhusu viwanda zilishindwa.
Sikubaliani na hili. Ninakubaliana na Kichuguu tulishindwa kuendeleza sera nzuri kwa kuzifanyia maboresho.

i)Leo tunaagiza nyama kutoka Uarabuni na Brazili,tunauza ng'ombe huko na bado tunao wengi.
Je, Tanganyika packers haikupaswa kufanyiwa maboresho badala ya kufanywa 3 star hotel.

ii) Tunanunua viberiti kutoka Pakistan. Kwanini hatukufanyia maboresho Kibo match kwa kutumia Sao hill?

iii) Tumeua Kilimanjaro machine/Mang'ula, je hatuhitaji vipuri hadi tuagize sub satndard kutoka China?

iv) Tumeua Maturabai Morogoro na Moshi tanneries, tunaagiza maturabai kutoka china na tunauza ngozi ili tuletewe bidhaa za ngozi kwa bei ya laki 2 kwa pair. Hapo Nyerere alishindwa nini. n.k n.k

gfsonwin- Hakuna investment kwa kutumia resources zetu. Tatizo letu ni kutokuwa na mipango ya nini kiwe kipaumbele na kwa njia gani kama alivyouliza Mchambuzi.

Tunatakiwa tupange kama kilimo ndio njia yetu basi madini yanaweza kutupatia investment katika elimu, utalii katika afya n.k. Lazima tuwe na mkakati tunalenga nini na kwasababu zipi. Sasa hivi hatujui tunafanya nini ndio maana wataalamu wanafikiria sigara na bia kukidhi bajeti. Kama si aibu sijui ni kitu gani.

Zakumi, ukitaka kuua taifa lolote usitumie silaha utaonekana mbaya, peleka kifo cha elimu.

Badala ya kufikiria kupandisha viwango vya elimu ili kupata competitive students tunashusha kwa div 5 kwasababu za kisiasa. Impact ya jambo hili i kubwa katika uchumi kuliko inavyodhaniwa.

Taifa kubwa kama Marekani linaposhtuka kuhusu elimu sisi hatupaswi kuwa na waziri anayefaulisha kwa kiwango cha div 5. Jibu la tatizo hili kama sehemu ya uchumi analo Kichuguu nalo ni Uongozi.

Nimalizie kwa kusema hakuna awamu iliyofanya vema katika uchumi kuliko awamu ya kwanza.
Hakuna taifa lililoendelea bila kwanza kuanza kujiendeleza ndani hasa katika elimu na miundo mbinu.

1) Elimu; viongozi wa sasa ni investment ya awamu ya kwanza na hata vizazi vyao ni sehemu ya investment hiyo
2) Miundo mbinu: Awamu ya kwanza ndiyo iliyowahi kujenga miundo mbinu kuliko awamu zote tatu zilizofuata kwa pamoja.

i) Uwekezaji katika nishati ya umeme
ii)Ujenzi wa reli na barabara.

Kuna tofauti ya ujenzi na ukarabati. Ukarabati hufuatia ujenzi na wala siyo ujenzi.

iii) Uwekezaji katika viwanda vidogo kwa ajili ya matumizi ya ndani, kukuza ajira na kuongeza tahamani za bidhaa ziuzwazo nje.

Nini kifanyike
a) Lazima tubadilike na tupate uongozi wenye mission and vision plus commitment
b)Tufanye specialization ya kile tunachokusudia kiuchumi
c)Tuishi kulingana na hali yetu ikiwa ni pamoja na serikali ndogo yenye tija isiyo na gharama
d)Tuwe na ujasusi wa kiuchumi na si delivery unit isiyotoa mchango bali tathmini.

mkuu umegusa mtima wangu kwa swala la elimu, umetaja utitiri wa shule za kata ukasahau utitiri wa vyuo vya kata vinavyoendelea kuanzishwa kila mwaka, hata sasa kama una jengo lako linaloonekana kama darasa ukienda TCU na bahasha yako ya kaki unaweza ukapata usajili wa chuo kwa kuwatumia wanafunzi wale wale waliotoka shule za kata kwa division zao 5 na wakifika chuo hiki kipya watakutana na vijana wenzao ambao watakuwa ndo walimu wao wapya waliomaliza vyuo vile vile vya kata na kupata First Class toka vyuo vile vile kwa njia wanazojua wao, loh! lakini pia wanafunzi hawa wapya wa chuo hiki kipya watabahatika sana kwa kumpata lecture wa UDSM anaekuja kwa part time ili ajiongezee kipato maana pesa za research now zinaishia mikononi mwa wajanja, nalia mimi, dah, yote hayo hayatokei kwa bahati mbaya, yamepangwa ili vijana wengi wapate vyeti vya degree na mwisho wa siku wanasiasa wapate cha kuongea kipindi cha campaign kwa takwimu nyingi nyingi, so sad,

mkuu zumbemkuu hapa kwenye swala la elimu naomba nianze hivi Kenya walianzisha shule za kata almost 20+ yrs back na lengo lao halikuwa tofauti na lile ambalo serikali yetu iliona na kuamua kuanzisha shule hizi maiak 5 iliyopita.

Ngoja nikwambie Kenya waliweza kupeleka wanafunzi kwenye hizi shule,changamoto ya waalimu, maabara na mabweni ilionekana hivyo serikali ikasema hawana budi kuinvest kwenye elimu zaidi. Serikali ya kenye wakati huo walijivika mikanda wakaanza kazi ya kutrain waalimu, kuboresha maabara na kuhakikisha mabweni mazuri yanakuwepo na mwisho wa siku walianza kuona ufaulu unakua.

Hapa kwetu tanzania hatua ya kwanza ambayo Lowassa aliiasisi ilikuwa ni kujenga shule na kupeleka wanafunzi, nafikiri hatua ya pili ilipasa kuimarisha mazingira a kufundishia, maabara, waalimu na mabweni katika shule hizi. (mabweni yanaweza yakawa sio ya msingi sana) sasa srikali ilipokosea ni pale ambapo tayari wanafunzi wako shulen halafu hakuna mwalimu wala kitabu wala hata chak ya kuandikia ubaoni.

Mim ni victim wa hii hali, manake niliwah kupelekwa kwenye shule ya kata ya kuanzisha nasema ukweli inaitwa shule ya seondari MAKURUNGE iko kisarawe mkoani pwani. nilikuwa nalazimika kwenda MINAKI kuomba vitabu, mpaka chaki manake nimepelekwa kwenye shule darasa ni moja lenye wanafunzi 85 kidato cha kwanza. imagine hakuna chaki, kitabu wala maji katika shule hivi wewe mwl unafundishaje hawa watoto??

Niliandika sio mara moja wala mbili kusema kama tumefanikiwa kujenga shule ikiwa bado changa basi tuinvest kwenye waalimu, mazingira bora ya kufundishia vitabu nk. I stayed for a yr pasi kupata hata kopi moja ya kitabu. Nikaletewa form one mwaka uliofuata wakiwa 75 nikaa na jumla ya wanafunzi 150 lakin hali ikawa mbali kuliko kwanza.

sasa jiulize miaka 2 mwanafunzi kukaa shule afundishwe na waalimu 3 vitabu vya kuomba utawezaje kuwafaulisha?? Ndio maana mimi nilidiriki kusema kwamba SHULE ZA KATA ZILILETWA KWAAJILI YA DEMOGRAPHIC CONTROL lkn sio kwa sababu ya kukuza watoto wetu kielimu.

Jiulize toka zianzishwe shule ipi ambayo imewekewa vifaa vya lab?? ipi ambayo ina waalimu wa kutosha hasa kw amasomo ya sayansi?? ipi ambayo wanafunzi wanaona kweli wako shule?? hakuna jamani hakuna.

serikali ifike mahali waone kwamba kuna haja ya kubadili mfumo wa elimu na kuinvest kwenye elimu kwa dhati zaidi.

Wakati tunapata uhuru literacy rate ilikuwa 65% kwa juhudi za NYERERE elimu ya watu wazima. elimu ya kujitegemea vilikuwa ndi msingi wa nchi na matokeo yake watanzania wengi walipata nafasi ya kusoma nje wakiwa considered kama best candidates, leo hii illiteracy rate ni 50% miaka 50 baada ya uhuru idadi ya wajinga inakuwa badala ya kupungua?? hii ni nini??

Haya kuona kabisa idadi ya wajinga inakuwa bado serikali ikatilia msisitizo kabisa wa kuua elimu hii kwa kupunguza kiwango cha ufaulu what a shame?? kwa kiwango kipya cha ufaulu kwa taznaia tunakuwa nchi ya kwanza yenye kiwango cha chini kabisa cha ufaulu duniani this position us kwenye idadi ya nchi iliyo na mambumbu wengi zaid duniani kote.

Yumkini 5 yrs huyu Mlugo hatakuwepo je unafikir impacta yake haitaonekana?? Kumbukeni Mungai alivyoleta uozo kwenye elimu na kuanzisha voda fasta matokeo yake yalidhihirika 4 yrs baada tu ya wale waalim kuingia sokoni, Kapuya nae ondoa elimu ya biashara, sijui ondoa masomo ya michezo baada ya miaka 4 tu impact ikaonekana. sijui kwann bado hatuajifunzi kutokana na haya tuliyokosea mwanzoni.

Nimeandika kwa uchungu sana manake this is my career na nimeiishi kwa hiyo naona matokeo yake mbelen. Sikufichi itafika wakati professionals wote tutahire toka nje na hatutakuwa na competent professionals kabisa.

sasa wananchi tuamke tu line up kukataa hali hii ya siasa kuwa ndio inayoamua kila kitu. tuamue lets say no to this tunahitaj elimu nzuri kwa tanzania ijayo.
 
Last edited by a moderator:
Iwapo serikali ina viongozi ambao wana elimu ya kuungaunga, na wengine wana vyeti vya kununua unategema watu hao wanajua maana ya elimu? Wao wanadhani kuwa ule ujanja ujanja uliowaweka madarakani niyo mafanikio yenyewe, kila mtu anatakiwa afanye hivyo. Ndio wanapopweakusaini mkataba kwa niaba ya serikali wala hata hawausomi kujua una maana gani.
 
mkuu gfsonwin pole sana, kama mkuu Kichuguu alivyosema tatizo ni uongozi, kwa kuthibitisha hilo tumtizame waziri mulugo mteule huyu wa serikali ya ari zaidi, kasi zaid na nguvu zaidi, kama kiongozi huyu mwenyewe hayupo serious na elimu yake, atawezaji kuwa serious na Elimu ya wengine? atawezaji kuongoza taasisi ya elimu ikiwa elimu yake binafsi aliyoipata haimuongozi?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom