Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Tawire baba! nimekusikia.Nyerere atabaki katika historia ya Taifa hili miaka yote kwa vile ndiye aliyekuwa Rais wa wake wa Kwanza. Ni kama ambavyo Stalin na mao walivyoko katika historia ya nchi za Urusi na China. Wenzetu huko wanaendelea tena kwa kasi sana na hawana ngonjera za Mao wala Stalin; sisi tusipogundua makosa hayo tutabaki kuwa walalamikaji dhidi ya Nyerere huku tukiwa hatuoni makosa yenyewe. Tutabaki na viongozi wanaoficha mafedha ya umma usiwsi wakati serikali inahsindwa kulipia majukumu yake halafu bado tukalalamika tena kuwa makosa yote ya serikali kukosa hela ni kutokana na Nyerere. Tena afadhali kabisa Nyerere alijitahidi kujenda viwanda vya ndani, alichokosea ni namna ya unedeshaji wa viwanda hivyo kwani uongozi wake baadaye ukwa kama vile wa kisisa badala ya kuwa uongozi wa kibishara. Tungefanya marekebishao hayo ya kuvifanya viwanda hivyo vijiendesha kibiashara kwa mfano kuuza hisa kwa watu binafsi tungesaidia sana kuimarisha viwanda hivyo. Lakini badala yake sisi tuliposikia neno privatization hatulichukulia kwa maana yake pana ya Private Sector, sisi tukalichukulia kwa maana finyu ya private individual. Kwa hiyo tukawa tunamtafuta mtu mmoja tajiri sana wa kumwuzia ambaye alikuwa anatafutwa kutoka nje ya nchi. Kenya pale walipo-privatize Kenya Airways waliuziana hisa wakenya wenyewe kwa wenyewe na leo unajua shirika hilo liko wapi. Kuuza kiholela viwanda vile vya Nyerere hakukuwa ni kurekebisha bali kulikuwa ni kubomoa kabisa ndiyo maana nchi leo ipo ipo tu ikiwa kama mwendawazimu. Tutaendelea hivi hivi mpaka tukome wenyewe.
Mimi nimeona kuwa swali lililotolewa hapa ni Uchumi wa Tanzania leo, siyo Historia ya Uchumi wa Tanzania Miaka 50 iliyopita. na Hivyo sioni kabisa nafasi ya sera za uchumi alizofuata Nyerere katika maisha ya watanzania wa leo
lakini kama wimbo vile; shule hazina vitendea kazi kwa sababu ya Nyerere. Migodi ya madini inachimbwa lakini serikali haipati chochote kwa sababu ya Nyerere. Miradi ya ujenzi wa miundo mbinu serikali inatolewa kinyemela kiasi kuwa ujenzi wake unakuwa ni substandard kwa sababu ya Nyerere. Manunuzi ya serikali yanakuwa ni ghali sana kuliko thamani halisi, kwa mfano ile rada tulilipa hela nyingi sana, kwa sababu ya Nyerere.
Kosa lililofanyika wakati ule lilikuwa la uchumi kuingiliwa na siasa. Hata hivyo bado nafasi ya kurekebisha ilikuwepo.
Badala ya kutumia fursa hiyo kuendelea tunatumia fursa hiyo kulaumu historia tena iliyojenga misingi mingine mizuri. Hatutumii historia kupata ufumbuzi bali kumtuhumu mtu na wala si sera.
Leo akina Zakumi hawatoi credit kuhusu miundo mbinu iliyoachwa na ambayo haitumiki.
Mfano, Tumeshindwa kutumia TAZARA kuinua uchumi tunalalamika Nyerere kuwekeza katika TAZARA? Inaingia akilini kweli.
Katika mashirika 400 yaliyobinafsishwa sijui ni mangapi yamefanikiwa hadi sasa(PCSRC).
Nimempa Zakumi mifano miwili ya viwanda vya sigara na bia, ameikataa kwasababu anasema hivyo ni vitu vinavyopatikana popote.
Naendelea kumpa mifano
Katika mashirika 400 yaliyobinafsishwa zilikuwepo benki.
CRDB walikwenda kuchukua hisa kwa Mwalimu Butiama.
Hawakuuzwa kwa mwekezaji, wakabaki kuwa benki ya walala hoi.
Leo CRDB ni moja ya benki kubwa katika ukanda wetu.
Nimesoma taarifa ipo katika mabenki 100 ya Afrika.
Tukauza NBC kwa makaburu. Kipande kidogo kikamegwa na kuitwa NMB. Hiki ndicho cha wazawa.
NMB inafanya vizuri sana na mwaka jana ilitoa gawio katika serikali kubwa kuliko benki zingine.
Zakumi, kwanini Tanganyika packers igeuzwe kuwa hotel wakati ng'ombe tunao bado?
Je,ni kiu ya kula nyama za majuu au ndio ujinga tunaoongelea huo wa viongozi wetu.Kwanini isiwe 'CRDB'
Kwanini tununue majembe feki yaliyotengenezwa uani kule china na si UFI Dar es Salaam?
Kwanini tununue spea 'generics' kutoka middle east na siyo Mang'ula au Moshi machine tools.
Kulikuwa na sababu gani za kutelekeza Mang'ula na kuwa ghala la chumvi badala ya kuifanya iwe kama CRDB!
Kuna sababu gani za kiwanda cha Mbolea Tanga kufa na si kiwanda cha Saruji!
Kwanini Saruji Tanga na Wazo hill havikufa kama ilivyokufa Mutex na Mwatex katika mazingira yale yale ya kukosa wasomi na poor management unayozungumzia.
Nitajie ni mashirika mangapi katika yale 400 yaliyofanya vema kuliko ilivyokuwa wakati yanajengwa.
Na kwanini wakati huu tukiwa na business oriented people tunalipa umeme ghali unaoathiri uzalishaji kuliko wakati wa nyuma ili hali mabwawa ya umeme yaliyojengwa na Mwalimu ni yale yale na tena kuna gesi.
Kwanini tushindwe! wasomi wapo, rasilimali zipo tena zaidi kwanini tunashindwa
Last edited by a moderator: