Uchumi wa Tanzania: Je, Ni Kitendawili au Ni Mazingaombwe Kwa Maskini?

Zakumi naona sasa hoja umeihamishia kwangu japo ni mfano unaotaka kulenga ubovu wa sera za mwalimu.

Kitu kimoja tu unashindwa kuelewa kwamba nia na lengo ya sera za mwalimu ilikuwa kwanza tujitosheleze sisi wenyewe kwa mahitaji yetu. Na sisi walanguzi hatukuwa ktk kundi la wahujumu uchumi isipokuwa tuliviwezesha viwanda vyetu kuuza mali zao. kumbuka tu tulinunua mali zile viwandani na kwenda kuziuza nje kasha fedha zinarudi nyumbani. Na ktk mzunguko huo wavuvi walifaidika, viwanda vilifaidika japo wananchi wengi walikosa huduma hizo wakipanga mawe ktk foleni madukani.

Hivyo usinilalamikie miye kiuchumi isipokuwa tulifanya isivyotakiwa wala haikupangiwa mali ile kuuzwa nje. Pato la viwanda au mashirika lilibakia pale pale maana waliuza mali zao japo sii kwa walengwa... Nitaendelea kumtetea Nyerere kwa sababu alikuwa na nia nzuri na alielewa uwezo wa wananchi ktk uzalishaji. Wakulima ambao walikuwa asilimia 80 hawakuwa na uwezo mkubwa wa kununua mali ktk kiwango chake na ndio maana kila kitu kilikuwa karibu na bure..Utawala wa Nyerere ulikuwa kama NGO kutuhudumia wananchi wasiojiweza, hilo tukubali tusikubali.

China, South Korea na Taiwan wameweza kuendelea kwa sababu wameunda mfumo mpya wa kuuza mali zao nje badala ya wao kuwa wahitaji tu. Uchumi wowote utakuwa zaidi ikiwa unauza zaidi ya unavyotumia lakini sisi toka Enzi hatukuweza kumudu mahitaji yetu ya ndani na kwa bahati mbaya zaidi tumeingia ktk imports zaidi ya Exports. bado fikira zetu ni kukidhi mahitaji yetu na ndio maana tunakula hadi mbegu.

Na kinachotuangusha sasa hivi ni kutegemea wawekezaji kutoka nje ambao hakuna mzunguko wa fedha ndani zaidi ya wao kuchota na kupeleka nje iwe mashirika ya simu au migodi ya dhahabu na gas. Nenda TRA utaambiwa hadi leo hii serikali yetu inategemea imports ktk makusanyo ya kodi zake kuliko exports tena mara 10 pamoja na kuwa na miradi mikubwa. Sisi ni Taifa tegemezi kwa njia zote za kiuchumi hivyo kutufanya mateja badala ya wazalishaji..

Mkandara;

Kwikwikwi. Nimehamishia hoja kwako kuonyesha kuwa ungekuwa China enzi za Mao ungepigwa risasi. Bila kujijua ulihusika kuhujumu viwanda.

Hili kufanya bidhaa ziwe zinauzika katika shughuli muhimu za maendeleo, kulikuwa na ruzuku iliyotoka serikalini iliyofanya bei ya bidhaa hizo kuwa chini. Kwa mfano mbolea. Iliuzwa kwa ruzuku hili wakulima wa Tanzania waweze kuzalisha zaidi na kuletea Taifa mapato.

Baadhi ya wafanyabiashara kama Mkandara walichukua mbolea kutoka Tanzania na kuuza nje. Ni kweli Matendo kama haya hayakuathiri vitabu vya mahesabu za viwanda. Kwani viwanda vilipata kile kilichotakiwa kuuzwa.

Lakini kitaifa uuzaji wa mbolea nje ya Tanzania ulileta matatizo. Mkulima wa Tanzania hakufaidika na ruzuku ambayo ingeipa taifa mapato. Hakuweza kuzalisha mazao ya kutumika katika viwanda vya Tanzania hili kuongeza kodi ambayo ingetumika kwenye ruzuku.

Hivyo pamoja na kumtetea Nyerere, ulikuwa ni adui wa siasa zake.
 
nakubaliana na jinga la falsafa na Kichuguu kwamba ifike mahali tutenge kati ya siasa na utendaji wa serikali.

lakini pia tufike mahali wananchi tutake kujua nini ndio matokeo na wala sio nini kitakachofanywa. sijui kama kweli watu wana nia ya dhati ya kutaka maendeleo mid set zetu siye tuwe wartu wakutaka kutenda matokeo yaonekane.

Ngoja niwashangaze jambo moja mradi wa STEHP uliodhaminiwa na WB ulikuwa na nia njema kwa maendeleo ya elimu ya juu sayansi na teknolojia. nimeshangazwa sana kitendo cha hata wale ambao runawategemea wawe result oriented nao wanachemsha kwenye utendaji wao. eti chuo kabisa cha elimu ya juu kinampeleka mtu wa miaka 55 PHd??

hivi huyu mtu umgharamie zaid ya 100mil ada tu kusoma nje ya nchi hujaweka bima ya afya, housing allowanze na subsistance allowance kwa huyu mtu,. sasa tizama gharama kama hii inaingia kwa serikali kisha huyu mtu anamaliza shule na kustafu kweli ameweza kulete tija kwa taifa??

kitu ambacho mie siwez kukijua lkn napejnda nijue ni hivi hizi fedha za wafadhili iwe tumekopeshwa ama tumepewa bure nani anatakiwa kuhakikisha zinatumiwa ipasavyo? je huwa kweli zinafanyiwa auditing?
 
Last edited by a moderator:
Zakumi,

Katika bandiko # 91 umekuja na hoja ifuatayo:

Kama sijaendelea, ningependa kukuuliza swali moja. Maendeleo yanaletwa na watu.

Bila shaka;

Je unaweza kunitajia viwanda au mashirika yaliokuwa na mafanikio na viongozi wake na vitu walivyofanya kuleta mafanikio katika viwanda au mashirika hayo? Ka
ti ya mashirika na viwanda 400 anavyopigia domo Nguruv3, nipe orodha ya majina kumi 10 tu;

Nilitarajia focus yako iwe kwenye WATU - from the Human Capital perspective, kwani hata ukiwa na wakuu wa mashirika wenye leadership skills, best educated, uzalendo, commitment, lakini wafanyakazi wengine wakakosa haya, ni kazi bure; Mjadala wetu utakuwa na manufaa zaidi iwapo focus yetu itakuwa katika WATU from Human Capital point of view; Vinginevyo ukitaka nikutajie tu majina ya mashirika na viongozi waliofanya vizuri chini ya Mwalimu, wapo kadhaa - kuna Amon Nsekela na NBC, Kuna Gibbons Mwaikambo na NIC, kuna Kasambala na Tanesco, Kuna Philip Magani na TRDB (later CRDB), kuna George Kahama na mwingine jina limenitoka ambao walisimamia uanzishwaji wa NDC, shirika ambalo lilisimamia ujenzi wa viwanda mbalimbali nchini - hasa vile vya mass goods production ambavyo mpaka sera za privatization zinaingia, vipo kadhaa ambvavyo vilikuwa vinaendeshwa kwa faida; Pia yupo Sylvester Barongo ambae alianzisha shirika la TPDC ambalo lilifanikiwa kufikia kiwango cha kuwa na uwezo wa kuikopesha serikali fedha za bajeti n.k. n.k; Lakini yote haya hayana maana zaidi ya Human Capital Base iliyokuwepo;

Pengine tuangalie mtazamo wa nyerere katika kipindi kile ili tupime tulikosea wapi, ili wewe uje na alternative scenario kwa kipindi kile; Bear in mind, wananchi walikuwa wanataka kuona matunda ya uhuru kwa maana ya access to social services, employment (income) among other things; Mwalimu alitamka haya sometime in 1970s:

over the last ten years we have done quite well in spreading basic social services to more and more people in rural areas; More remains to be done; but we shall only be able to do it if we produce more wealth

Kuna masuala mawili muhimu hapa:

*Kwanza, suala la extension of social services lililenga to improve our Human Capital Bases ambayo kimsingi ni elimu na afya katika population; Je:
-Kwa mtazamo wako, ilikuwa ni kosa kwa mwalimu kuweka kipaumbele katika hili?

*Pili, ni suala la kasi kubwa ya ongezeko la watu ambapo as of 1961, Tanzania ilikuwa na jumla ya watu milioni tisa, 90% wakiwa in the rural sector; Kwa zaidi ya miaka 20 ya uhuru, kasi ya ongezeko la watu lilikuwa sio chini ya 3% kwa mwaka, na hali hii iliwasumbua sana policy makers and donors alike katika muktadha wa kutafuta resources za kujenga human capital base sustainable katika nchi ambayo ilikuwa ipo nyuma sana kiuchumi relative to nchi kama Kenya n.k; Je:
-Kwa mtazamo wako, alternative scenario ya kukabiliana na hali hii ingekuwa nini?

Mwalimu anazidi kusema kwamba:

And we have not been doing very well on that front
akimaanisha 'wealth creation';

World conditions had not been helpful; Import prices were high and export prices too low
;

Mkuu Zakumi, kumbuka hoja yako ya awali bandiko #13 kwamba:
Kuhusiana na analysis zako za inward and outward strategies, it doesn't make sense to me.

Unapokuwa na jamii ambayo haina skilled labour ni lazima ufanye export raw materials or natural resources ambazo zinaweza kukusaidia kununua expertise, attract talents and capital. Hivyo inward strategy didn't make sense back then na hatuna sababu ya kumtetea Mwalimu kwa sababu uchumi sio sayansi.

Outward strategy inayoendelea sasa makes sense to me. Lakini hatuitumii vizuri kwa sababu kile kidogo kipatikanacho hakitumiki ku-build expertise, attract talents and accumulate internal capital ambayo ingetumika kujenga uchumi imara.

-Je: Unaijadili vipi hoja yako hii against this background?

Mwalimu anaendelea kusema:

But we should not use that or the drought years as an excuse for our own failures. The country was not being efficient. State companies were absorbing wealth, not creating it. Productivity was falling. We employ some sales managers who sit in their offices and wait for customers to search for them. We have virtually eliminated the discipline of fear; it is quite hard for a manager or employer to dismiss a worker, or even suspend or fine him for dereliction of duty; But in Tanzania it is not unusual for a manager to be locked out by the workers

Yapo mengi ya kuangalia kwa kina katika kauli hii:

Kwanza - Mwalimu admits failure, na wengi wetu humu sio kwamba tunaona mwalimu alikuwa mungu mtu kama unavyotujadili kupitia hoja zako, bali tatizo ni kwamba hoja zako zimejaa mashambulizi dhidi ya mwalimu bila ya kuangalia mazingira ya wakatiule yalikuwaje, lakini mbaya zaidi, bila ya kuwa na alternative solutions; Unakuwa unajenga hoja kama za republicans dhidi ya Obamacare i.e. "Obamacare is a total failure, Scrap the damn thing and lets start all over", wakiulizwa whats the alternative, wanabakia kuduwaa na kupiga porojo za siasa;

Pili - somo la pili hapa ni kwamba katika nyakati hizi za export orientation, hakuna kiongozi anayekubali kuwa na mapungufu au kufeli, viongozi wa sasa actually ndio miungu mtu;

Tatu - kuna hoja kwamba the state was absorbing wealth than creating it; Hii ilitokana na mambo makuu mawili - lengo la kuhakikisha kwamba watanzania wengi wanapata huduma za kijamii kujenga human capital base sustainably; Na pili, kujaribu kuwapatia watanzania income (wale walio nje ya kilimo) kwa kuwapatia ajira kwenye mashirika ya umma, serikalini n.k; Lengo halikuwa baya, tatizo wa the means towards that end, hivyo tulijadili hilo, sio 'end';

Nne - Mwalimu anazungumzia suala la ukosefu wa work ethics miongoni mwa wakuu wa mashirika; Hii ni moja ya sababu kubwa kwanini mashirika mengi yalifeli; Lakini tujiulize, je, baina ya nyakati hizi na zile za mwalimu, ni nyakati ipi kulikuwa na political will and commitment kurekebisha hilo? Na je, kwa wakati ule wa mwalimu, angefanya nini kama kiongozi wa nchi kutatua tatizo hili zaidi ya alivyofanya kupitia miiko ya uongozi ambayo ilikuja vunjwa for good chini ya azimio la zanzibar?

Tuelewe pia kwamba sio kwamba Mwalimu alikuwa haoni matatizo yaliyojitokeza, kwani mara nyingi alijadili jinsi gani alikuwa anakerwa na ukuaji wa sekta ya umma kwa kasi kuliko the rest of the economy, kupelekea matatizo ya bajeti; Wakati wa Mwalimu, foreign AID was funding 60% of the development budget; Mwalimu anasema hivi juu ya hili la Foreign AID(in the 1970s):

This is too high, it can be justified as an emergency operation to increase production, not to supplement our living standards. The intelligent farmer does not eat his seed-corn, and especially not borrowed seed. Our friends are willing to help us only because they respect our determination to help ourselves, and try to build a society based on human equality and dignity

Mwaka 1997, miaka 30 baada ya Azimio la Arusha, World Bank ilifanya its annual aid meeting in DSM; Miaka 30 baada ya Azimio la Arusha, serikali ilikuwa inaomba mikopo zaidi huku pia ikiomba misamaha ya madeni! Donor countries katika mkutano huu wakaombwa wachangie twice the amount to serve the same original purpose; Rais Mkapa aidha kwa kudhamiria au lah akasema yafuatayo:

Disengagement from donor dependency will not be accomplished in the twinkle of an eye;
Then akaja na takwimu za utafiti vijijini ambazo zilionyesha kwamba only one in five households walikuwa wanahisi kwamba maisha yao yamekuwa bora zaidi kutokana na mabadiliko ya kiuchumi ambayo Zakumi umekuwa unayapigia debe na kutumia kama platform kujenga hoja zako - Liberalization, Privatization and Marketization; Karibia 40% said they were worse off tofauti na miaka ya ujamaa; Je:

-Hii inatuambia nini kuhusiana na export promotion strategy inayoendelea kwa miaka mingi tu sasa?

May 1998, Mwalimu Nyerere alialikwa na Vice President of the World Bank pale Washington; Kwa mujibu wa mtu aliyekuwa na Mwalimu katika hafla ile, the VP akamueleza mwalimu kwamba: "he had become interested in Africa and Development because of Nyerere; Mwalimu akajibu "ah...kwa kicheko na kujiweka sawa kwenye kiti chake; Senior economists mwingine akasema
I have been re-reading your speeches from the 1960s and they still ring true;Obviously, there was nothing wrong in your vision; Where did we go astray?

Mwalimu akatafakari kidogo kisha kujibu:

i don't have a full answer to that question; some things certainly went right - we knitted a nation together, gave it a pride and educated a large number of our children and adults; But some ideas needed to wait their proper time; People weren't ready; But you (young Africans who are in here now have a chance to give those ideas new life

Mkuu Zakumi:
-Nini mtazamo wako kuhusiana na majibu ya Mwalimu hapo juu ?
Kumbuka hoja yangu ya awali hapo juu kuhusiana na maendeleo kuletwa na WATU;
Pia katika bandiko #29 ulijadili kwamba:

Matatizo yaliopo Tanzania kwa sasa ni distribution of wealth

Na pia bandiko #44 ulijadili kwamba:

Nchi zote wanazotolea mifano hapa kama China, Taiwan,South Korea zilianza na watu wenye strong personalities and results oriented. Toka Tanzania imepata uhuru, viongozi wanatoa maamuzi baada ya maamuzi lakini hawafuatilii utekelezaji wake. Na hilo ndio tatizo kubwa.

Nakubaliana na hoja zako mbili hizi, of which i shall discuss next...

cc: Nguruvi3, Kichuguu, zumbemkuu, JingalaFalsafa, Zinedine, gfsonwin, Mkandara, Ngongo
 
Last edited by a moderator:
Kwanza - Mwalimu admits failure, na wengi wetu humu sio kwamba tunaona mwalimu alikuwa mungu mtu kama unavyotujadili kupitia hoja zako, bali tatizo ni kwamba hoja zako zimejaa mashambulizi dhidi ya mwalimu bila ya kuangalia mazingira ya wakatiule yalikuwaje, lakini mbaya zaidi, bila ya kuwa na alternative solutions; Unakuwa unajenga hoja kama za republicans dhidi ya Obamacare i.e. "Obamacare is a total failure, Scrap the damn thing and lets start all over", wakiulizwa whats the alternative, wanabakia kuduwaa na kupiga porojo za siasa

Kwanza kabisa naomba niseme hivi mwalimu kwa wakati wake jamani alifanya aliyofanya kwa kiwango chake. Kwa miaka 26 aliyokaa madarakani alijitahidi sana.

Tukumbuke kwamba aliweza kuanzisha viwanda, ambavyo vilikuwa ndio tegem,eo letu na vilitutosha kwa kutukuza kwa wakati ule. Hivi leo hii machine tools iko wapi?? je inafanya nini?? na kwann Zakumi hakumwona Mwinyi kama mtu aliyekosea ili na kukubali kufisha viwanda vyetu? a;liposema RUKSA watu kuingiza bidhaa toka nje na kufisha viwanda vyetu je alikuwa sahihi??
 
mwalimu gfsonwin nakusoma, nadhani wale wanaomshambulia mwalimu wanasahau kufeli kwake pia kumesababishwa na ile vita kubwa aliyokuwa anapambana nayo vita ya Ujinga na ile ya Uganda.
 
Last edited by a moderator:
nakubaliana na @jinga la falsafa na Kichuguu kwamba ifike mahali tutenge kati ya siasa na utendaji wa serikali.

lakini pia tufike mahali wananchi tutake kujua nini ndio matokeo na wala sio nini kitakachofanywa. sijui kama kweli watu wana nia ya dhati ya kutaka maendeleo mid set zetu siye tuwe wartu wakutaka kutenda matokeo yaonekane.

Ngoja niwashangaze jambo moja mradi wa STEHP uliodhaminiwa na WB ulikuwa na nia njema kwa maendeleo ya elimu ya juu sayansi na teknolojia. nimeshangazwa sana kitendo cha hata wale ambao runawategemea wawe result oriented nao wanachemsha kwenye utendaji wao. eti chuo kabisa cha elimu ya juu kinampeleka mtu wa miaka 55 PHd??

hivi huyu mtu umgharamie zaid ya 100mil ada tu kusoma nje ya nchi hujaweka bima ya afya, housing allowanze na subsistance allowance kwa huyu mtu,. sasa tizama gharama kama hii inaingia kwa serikali kisha huyu mtu anamaliza shule na kustafu kweli ameweza kulete tija kwa taifa??

kitu ambacho mie siwez kukijua lkn napejnda nijue ni hivi hizi fedha za wafadhili iwe tumekopeshwa ama tumepewa bure nani anatakiwa kuhakikisha zinatumiwa ipasavyo? je huwa kweli zinafanyiwa auditing?

Kama Tanzania itandelea na jitihada zake za kuboresha western democracy, haitaweza kutenganisha serikali na siasa. Hiyo hoja yenu ni wishiful thinking, but haiwezakani. Nenda kwenye ukumbi wa siasa uone jinsi wapenzi wa CCM na CDM wanavyomwaga utumbo. Hao ndio viongozi wa nchi wa kesho.

Huwezi kuwa na matokeo bila kuwa na njia ya kufikia matokeo hayo. Matatizo makubwa ya watanzania ni kuwa na nia bila kuwa na njia za kufanikisha nia hizo. Wana nia ya kujenga ujamaa. Nia ya kufuata ujinga. Nia ya kutoa elimu bure. Nia ya kukopesha mabilioni. Nia ya kujenga viwanda. Nia ya kubinafsha viwanda. Nia ya kunondoa umasikini. The list goes on and on.

Kuhusiana na huyo mtu aliyekwenda kuchukua Phd, kama ana nia ya kulisaida taifa kwa kutumia elimu yake sioni tatizo lolote lile. Tatizo ni kitu gani anakileta mezani kwa kutumia elimu na uzoefu wake wa kazi.
 
Kwanza - Mwalimu admits failure, na wengi wetu humu sio kwamba tunaona mwalimu alikuwa mungu mtu kama unavyotujadili kupitia hoja zako, bali tatizo ni kwamba hoja zako zimejaa mashambulizi dhidi ya mwalimu bila ya kuangalia mazingira ya wakatiule yalikuwaje, lakini mbaya zaidi, bila ya kuwa na alternative solutions; Unakuwa unajenga hoja kama za republicans dhidi ya Obamacare i.e. "Obamacare is a total failure, Scrap the damn thing and lets start all over", wakiulizwa whats the alternative, wanabakia kuduwaa na kupiga porojo za siasa

Kwanza kabisa naomba niseme hivi mwalimu kwa wakati wake jamani alifanya aliyofanya kwa kiwango chake. Kwa miaka 26 aliyokaa madarakani alijitahidi sana.

Tukumbuke kwamba aliweza kuanzisha viwanda, ambavyo vilikuwa ndio tegem,eo letu na vilitutosha kwa kutukuza kwa wakati ule. Hivi leo hii machine tools iko wapi?? je inafanya nini?? na kwann Zakumi hakumwona Mwinyi kama mtu aliyekosea ili na kukubali kufisha viwanda vyetu? a;liposema RUKSA watu kuingiza bidhaa toka nje na kufisha viwanda vyetu je alikuwa sahihi??

Gfsonwin;

Sijamshambulia mwalimu. Nimeshambulia baadhi ya sera zake. Hicho ni kitu cha kawaida in politiking. Katiba ya Tanzania ina nipa haki ya kufikiri, kutoa mawazo na kushiriki katika politiking.

Kuhusiana na hoja yako kuwa tulitegemea viwanda ni sawa na kumpa mtoto wa darasa la kwanza Phd. Uzalishaji wa viwanda haukukidhi mahitaji ya taifa. Bidhaa nyingi zilikuwa na kiwango cha chini. Na mapato ya viwanda hivyo hayakufikia 10% ya pato la taifa.

Ukweli wa mambo mapato yaliotokana na misaada yalikuwa zaidi ya mara 5 ya mapato ya viwanda. Hivyo tulitegemea misaada. Mlete Mchambuzi au Mkandara wabishe hii point.

Kuhusiana na RUKSA, let me say am a libertarian and free marketer and also believe that people are inherently greedy.
 
Nguruv3;

Soma posti zangu uelewe. Kama Wewe na Mchambuzi mngekuja na Novel Approachies za kuendeleza viwanda Tanzania ningekubaliana na nyinyi. Unavyoleta ni vile alivyoacha Nyerere.
Zakumi , Mchambuzi ameuliza maswali kuhusu sera za kiuchumi za sasa na tatizo letu lipo wapi.

Nilimjibu kuwa export ni lazima siyo chaguo kwa nyakati tulizo nazo (outward strategy).
Hata hivyo export lazima ianze kujenga uwezo wa sisi kujitegemea. Nikasema clearly serikali iweke mazingira mazuri ya kuendeleza inward strategy. Nilitolea mfano wa utalii ambao sijui nao ni sehemu ya viwanda kama unavyoonyesha!!

Hili suala la sera za 60 na 70 umelileta wewe. Chanzo ni kulaumu kuhusu miundo mbinu, viwanda na uwekezaji katika nishati kama fashion. Tulichojaribu kukuambia ni kuwa kuna mambo yalifanyika kwasababu ni lazima.
Unaposema kujenga mabwawa ya kutoa nishati ni fashion, sijui ni uchumi upi unakusudia ujengwe! sijui.

Kama basi miaka ya 60 na 70 haikuwa na skilled labor na sasa ipo kwanini serikali isijenge mazingira(hapa elewa tofauti ya kujenge mazingira na viwanda, ndipo panakupa tabu) ya sisi kuanza kujitegemea kwa kile kidogo tunachoweza?

Kama unadhani tunapaswa kufanya export ya malighafi, lazima utambue kuwa mali ghafi inahitaji kuwa processed pia ili ipate thamani. Huwezi kuuza pamba isiyochambuliwa, utapata thamani ndogo sana kuliko mwenzako aliyejaribu kuisafisha. Sasa hizo processing industry za malighafi utazikwepaje?

Au kuuza malighafi unakozungumzia ni kule kwa makontena ya mchanga kupelekwa nje kama 'raw material'!!!
 
Last edited by a moderator:
Zakumi,

Katika bandiko # 91 umekuja na hoja ifuatayo:

Bila shaka;

Nilitarajia focus yako iwe kwenye WATU - from the Human Capital perspective, kwani hata ukiwa na wakuu wa mashirika wenye leadership skills, best educated, uzalendo, commitment, lakini wafanyakazi wengine wakakosa haya, ni kazi bure; Mjadala wetu utakuwa na manufaa zaidi iwapo focus yetu itakuwa katika WATU from Human Capital point of view; Vinginevyo ukitaka nikutajie tu majina ya mashirika na viongozi waliofanya vizuri chini ya Mwalimu, wapo kadhaa - kuna Amon Nsekela na NBC, Kuna Gibbons Mwaikambo na NIC, kuna Kasambala na Tanesco, Kuna Philip Magani na TRDB (later CRDB), kuna George Kahama na mwingine jina limenitoka ambao walisimamia uanzishwaji wa NDC, shirika ambalo lilisimamia ujenzi wa viwanda mbalimbali nchini - hasa vile vya mass goods production ambavyo mpaka sera za privatization zinaingia, vipo kadhaa ambvavyo vilikuwa vinaendeshwa kwa faida; Pia yupo Sylvester Barongo ambae alianzisha shirika la TPDC ambalo lilifanikiwa kufikia kiwango cha kuwa na uwezo wa kuikopesha serikali fedha za bajeti n.k. n.k; Lakini yote haya hayana maana zaidi ya Human Capital Base iliyokuwepo;

Pengine tuangalie mtazamo wa nyerere katika kipindi kile ili tupime tulikosea wapi, ili wewe uje na alternative scenario kwa kipindi kile; Bear in mind, wananchi walikuwa wanataka kuona matunda ya uhuru kwa maana ya access to social services, employment (income) among other things; Mwalimu alitamka haya sometime in 1970s:

Kuna masuala mawili muhimu hapa:

*Kwanza, suala la extension of social services lililenga to improve our Human Capital Bases ambayo kimsingi ni elimu na afya katika population; Je:
-Kwa mtazamo wako, ilikuwa ni kosa kwa mwalimu kuweka kipaumbele katika hili?

*Pili, ni suala la kasi kubwa ya ongezeko la watu ambapo as of 1961, Tanzania ilikuwa na jumla ya watu milioni tisa, 90% wakiwa in the rural sector; Kwa zaidi ya miaka 20 ya uhuru, kasi ya ongezeko la watu lilikuwa sio chini ya 3% kwa mwaka, na hali hii iliwasumbua sana policy makers and donors alike katika muktadha wa kutafuta resources za kujenga human capital base sustainable katika nchi ambayo ilikuwa ipo nyuma sana kiuchumi relative to nchi kama Kenya n.k; Je:
-Kwa mtazamo wako, alternative scenario ya kukabiliana na hali hii ingekuwa nini?

Mwalimu anazidi kusema kwamba:

akimaanisha 'wealth creation';

;

Mkuu Zakumi, kumbuka hoja yako ya awali bandiko #13 kwamba:

-Je: Unaijadili vipi hoja yako hii against this background?

Mwalimu anaendelea kusema:

Yapo mengi ya kuangalia kwa kina katika kauli hii:

Kwanza - Mwalimu admits failure, na wengi wetu humu sio kwamba tunaona mwalimu alikuwa mungu mtu kama unavyotujadili kupitia hoja zako, bali tatizo ni kwamba hoja zako zimejaa mashambulizi dhidi ya mwalimu bila ya kuangalia mazingira ya wakatiule yalikuwaje, lakini mbaya zaidi, bila ya kuwa na alternative solutions; Unakuwa unajenga hoja kama za republicans dhidi ya Obamacare i.e. "Obamacare is a total failure, Scrap the damn thing and lets start all over", wakiulizwa whats the alternative, wanabakia kuduwaa na kupiga porojo za siasa;

Pili - somo la pili hapa ni kwamba katika nyakati hizi za export orientation, hakuna kiongozi anayekubali kuwa na mapungufu au kufeli, viongozi wa sasa actually ndio miungu mtu;

Tatu - kuna hoja kwamba the state was absorbing wealth than creating it; Hii ilitokana na mambo makuu mawili - lengo la kuhakikisha kwamba watanzania wengi wanapata huduma za kijamii kujenga human capital base sustainably; Na pili, kujaribu kuwapatia watanzania income (wale walio nje ya kilimo) kwa kuwapatia ajira kwenye mashirika ya umma, serikalini n.k; Lengo halikuwa baya, tatizo wa the means towards that end, hivyo tulijadili hilo, sio 'end';

Nne - Mwalimu anazungumzia suala la ukosefu wa work ethics miongoni mwa wakuu wa mashirika; Hii ni moja ya sababu kubwa kwanini mashirika mengi yalifeli; Lakini tujiulize, je, baina ya nyakati hizi na zile za mwalimu, ni nyakati ipi kulikuwa na political will and commitment kurekebisha hilo? Na je, kwa wakati ule wa mwalimu, angefanya nini kama kiongozi wa nchi kutatua tatizo hili zaidi ya alivyofanya kupitia miiko ya uongozi ambayo ilikuja vunjwa for good chini ya azimio la zanzibar?

Tuelewe pia kwamba sio kwamba Mwalimu alikuwa haoni matatizo yaliyojitokeza, kwani mara nyingi alijadili jinsi gani alikuwa anakerwa na ukuaji wa sekta ya umma kwa kasi kuliko the rest of the economy, kupelekea matatizo ya bajeti; Wakati wa Mwalimu, foreign AID was funding 60% of the development budget; Mwalimu anasema hivi juu ya hili la Foreign AID(in the 1970s):

Mwaka 1997, miaka 30 baada ya Azimio la Arusha, World Bank ilifanya its annual aid meeting in DSM; Miaka 30 baada ya Azimio la Arusha, serikali ilikuwa inaomba mikopo zaidi huku pia ikiomba misamaha ya madeni! Donor countries katika mkutano huu wakaombwa wachangie twice the amount to serve the same original purpose; Rais Mkapa aidha kwa kudhamiria au lah akasema yafuatayo:

Then akaja na takwimu za utafiti vijijini ambazo zilionyesha kwamba only one in five households walikuwa wanahisi kwamba maisha yao yamekuwa bora zaidi kutokana na mabadiliko ya kiuchumi ambayo Zakumi umekuwa unayapigia debe na kutumia kama platform kujenga hoja zako - Liberalization, Privatization and Marketization; Karibia 40% said they were worse off tofauti na miaka ya ujamaa; Je:

-Hii inatuambia nini kuhusiana na export promotion strategy inayoendelea kwa miaka mingi tu sasa?

May 1998, Mwalimu Nyerere alialikwa na Vice President of the World Bank pale Washington; Kwa mujibu wa mtu aliyekuwa na Mwalimu katika hafla ile, the VP akamueleza mwalimu kwamba: "he had become interested in Africa and Development because of Nyerere; Mwalimu akajibu "ah...kwa kicheko na kujiweka sawa kwenye kiti chake; Senior economists mwingine akasema

Mwalimu akatafakari kidogo kisha kujibu:

Mkuu Zakumi:
-Nini mtazamo wako kuhusiana na majibu ya Mwalimu hapo juu ?
Kumbuka hoja yangu ya awali hapo juu kuhusiana na maendeleo kuletwa na WATU;
Pia katika bandiko #29 ulijadili kwamba:

Na pia bandiko #44 ulijadili kwamba:

Nakubaliana na hoja zako mbili hizi, of which i shall discuss next...

cc: Nguruvi3, Kichuguu, zumbemkuu, JingalaFalsafa, Zinedine, gfsonwin, Mkandara, Ngongo

Mchambuzi:

Kwanza nishukuru kwa kutumia muda kutafuta reference ambazo zinaonyesha kuwa Nyerere mwenyewe alikubali kuwa sera zake zilikuwa na mapungufu ya kiufundi. Na moja ya rejea hiyo inaonyesha kuwa ni amekabidhi mwenge kwa kizazi kipya (The cheateh generation) kutafutia ufumbuzi wa matatizo hayo.

Tukirudi kwenye mada, nilikuomba unipe orodha ya kampuni au mashirika 10 ya kiserikali yaliokuwa na mafanikio. Naona zoezi hilo limekuwa gumu sana. Katika makampuni na mashirika 400,kushindwa kuja na orodha ya makampuni kumi inaonyesha kuwa mambo hayakuwa mazuri.

Kama mtanzania anaweza kutoa listi ya makampuni ya kichina ya kiserikali yaliofanya vizuri na kushindwa kufanya hivyo kwa nchi yake, something is wrong.

Kuhusiana na rejea za mwalimu ulizotoa kuonyesha kwanini kulikuwa na matatizo, Mwalimu aliona kasoro za kiutendaji. Lakini kiundani kulikuwa na kasoro nyingine: zikiwemo za formulation za sera zenyewe. Kwa mfano formulation ya sera za vijiji vya ujamaa ilikuwa na kasoro kubwa. Na matokeo yake ni kushuka kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo ambayo yalitegemewa na viwanda. Uzalishaji wa korosho uliathirika sana na formulation ya sera hii. Elimu ya UPE na Operasheni maduka ni miongoni mwa sera mbovu pia.

Katika posti zilizopita ulisema kuwa state capital ndio iliyotumika zaidi. Katika posti hii unasema kuwa foreign aid ilichangia 60% ya development aid. Naomba jamaa wa kambi yako waisome hiyo. Watu msiendelee kung'ang'ania tulijenga hiki na kile, wakati misaada ya kutoka nje ndiyo iliyotoa impetus ya mabadiliko na sio resources za Tanzania.

Tukibaki kwenye misaada,takwimu zinaonyesha kuwa hakuna nchi iliyoendelea kwa kutegemea 60% ya misaada kutoka nje. Asian Tiger zilitegemea chini ya asimilia 2% misaada kutoka nje. Hivyo dependency ya misaada ilikuwa ni chanzo cha failures za sera kwa sababu mbili. Kwanza misaada iliwafanya viongozi wetu kuwa na kiburi. Pamoja na nia yao nzuri, wao na wahisani walitupangia (Top down approach).

Pili misaada ni matokeo ya kuvutia washirika wakati wa vita vya baridi. Misaada mingi ilikuja Tanzania ilitoka kwenye serikali zilizofuata mkondo wa kushoto. Hivyo Nyerere alikuwa naive kwa kuamini kuwa walitusaidia kwa sababu ya juhudi zetu. Walitusaidia kwa sababu walitaka tuwe upande wao.

Tukirudi kwenye kasoro za sera, toka TANU na mtoto wake CCM ishindwe kuelezea mafanikio ya maendeleo, wanatumia kusomesha wanafunzi kwa idadi kubwa kama ni mafanikio. Ukweli wa mambo takwimu za maendeleo hazionyeshi uwiano wowote wa idadi kubwa ya wanafunzi na maendeleo ya jamii. Maendeleo ya nchi yanaletwa ubora wa elimu inayotolewa. Hivyo massive enrollment of students in 70s didn't translate to anything.

Kwa kifupi huo ni mtazamo wangu kuhusu majibu ya mwalimu. Aliyaona matatizo ya utekelezaji wa sera kwa kuangalia utendaji. Lakini kulikuwa na matatizo ya formulation ya sera zenyewe, funding ya sera, na social traps.

Tukirudi kwenye mada kamili. Watanzania watajikomboa kwa kutumia human and natural resources zao vizuri. Kama huna skilled workforce inward and outward strategies are just fancy words. Utaendelea kupokea misaada na kunyonywa tu.
 
@Zakumi , Mchambuzi ameuliza maswali kuhusu sera za kiuchumi za sasa na tatizo letu lipo wapi.

Nilimjibu kuwa export ni lazima siyo chaguo kwa nyakati tulizo nazo (outward strategy).
Hata hivyo export lazima ianze kujenga uwezo wa sisi kujitegemea. Nikasema clearly serikali iweke mazingira mazuri ya kuendeleza inward strategy. Nilitolea mfano wa utalii ambao sijui nao ni sehemu ya viwanda kama unavyoonyesha!!

Hili suala la sera za 60 na 70 umelileta wewe. Chanzo ni kulaumu kuhusu miundo mbinu, viwanda na uwekezaji katika nishati kama fashion. Tulichojaribu kukuambia ni kuwa kuna mambo yalifanyika kwasababu ni lazima.
Unaposema kujenga mabwawa ya kutoa nishati ni fashion, sijui ni uchumi upi unakusudia ujengwe! sijui.

Kama basi miaka ya 60 na 70 haikuwa na skilled labor na sasa ipo kwanini serikali isijenge mazingira(hapa elewa tofauti ya kujenge mazingira na viwanda, ndipo panakupa tabu) ya sisi kuanza kujitegemea kwa kile kidogo tunachoweza?

Kama unadhani tunapaswa kufanya export ya malighafi, lazima utambue kuwa mali ghafi inahitaji kuwa processed pia ili ipate thamani. Huwezi kuuza pamba isiyochambuliwa, utapata thamani ndogo sana kuliko mwenzako aliyejaribu kuisafisha. Sasa hizo processing industry za malighafi utazikwepaje?

Au kuuza malighafi unakozungumzia ni kule kwa makontena ya mchanga kupelekwa nje kama 'raw material'!!!

Nguruv3:

Kwanza si kweli kuwa suala la sera za miaka ya 60, 70, na 80 nimelileta mimi. Ukisoma utangulizi wa thread utaona Mchambuzi analilisema.

Tanzania imepitia inward looking strategies kama njia za kukuza uchumi na kupunguza umaskini (1967 – 1985) ambayo wapo watu wengi wanaojenga hoja kwamba haikumsaidia mtanzania wa kawaida kujikwamua kutoka kwenye lindi la umaskini. Kutokana na hoja hii, nchi yetu ikaingia katika mageuzi ya kiuchumi mkakati mpya wa ‘outward looking’ (Export Promotion Strategy) ukaanza kutumika kama njia ya kukuza uchumi na kupunguza umaskini nchini. Kutokana na uzoefu wetu chini ya mkakati huu, pamoja na matokeo yake ambayo nimeyajadili awali, watanzania tumebakia na maswali mengi sana ya kujiuliza, hasa kuhusiana na suala zima la matumizi ya export promotion strategy kama njia ya kukuza uchumi na kumkomboa mtanzania wa kawaida:

Kwanaza watanzania sio wabunifu. Kushindwa kwa serikali kutotatua matatizo kumefanya watu kulilia sera za Nyerere hata zile zilizoboronga. Hivyo kuna umuhimu kuweka sawa.

Pili umeshindwa kuleta idadi ya viwanda au Mashirika 20 kuonyesha kulikwa na mafanikio. Hivyo na mshikaji wako Mchambuzi bado mnatumia imaginary viwanda kujenga hoja. Naona Mkandara amekimbia baada ya kumwambia kuwa vitendo vyake vya ulanguzi vilihujumu the eco-system ya maendeleo ya viwanda.

Tukirudi kwenye posti. Tupo kwenye ukurasa mmoja kwa export katika kipindi cha sasa ni muhimu. Katika uchumi tunaangalia michango ya sekta mbalimbali. Utalii ni sekta ya uchumi. Nikiuliza kwanini sekta hii haikundelezwa miaka ya 60, 70, na 80 nitaambia namlaumu Nyerere. Ukweli wa mambo it was an opporunity that we didn't take.

Misingi ya mazingira mazuri kwa inward or outward strategy ni hilehile. Na mingi inahitaji serikali kufanya vitu vya kawaida vya kijamii kwa ufanisi mkubwa. Hakuna siku maalumu ya kusema kuwa mazingira yetu yanafaa kwa inward strategy. Kwa maoni yangu inward and outward strategies co-exist. Kinachotofautisha ni hipi dominant.

Kuna uwezekano mkubwa kuwa nchi tunazozitaja kama mfano wa mafanikio, hazikujipangia outward strategy. Zilijipangia ku-take opportunities zilizojitokeza na wakafanikiwa. Na Tanzania nayo ikiangalia opportunities zinazojitokeza inaweza kufanikiwa zaidi bila kujali makosa yaliofanyika miaka ya nyuma.
 
@Zakumi nimekuuliza hapo nyuma, hebu weka swali lako la mashirika katika muktadha unaoeleweka kwanza.
Kwasasa lipo vague kwasababu halieleweki unataka nini hasa.

Pili, umezungumzia kufeli kwa sera za mwalimu kunatokana na unskilled workforce.
Sasa hivi kuna skilled workforce ukilinganisha na zama hizo.
Ni kipi unachoweza kutuomyesha kuwa for the past 30 years kuna tofauti na 26 years before

Tatu, kwavile umesema mkakati uwe kusafirisha malighafi kwa maana ya pamba zenye magugu, korosho zisizobanguliwa na makontena ya dhahabu, Tanzanite na almasi, je huoni kuwa katika soko la dunia lenye ushindani utauza sh10 mwenzako anauza 100 kwa kitu kile kile? Hebu fafanua hakuna ukweli hapo?

Nne, hebu tueleze baada ya kuuza yale mashirika 400 ya 'hovyo' nini kimefanyika kama mbadala na nini matokeo ya mauzo hayo ambayo kiuchumi tunaweza kusema yameleta afueni?
Je kugeuza kiwanda kuwa ghala la chumvi ndio uchumi ndio inward strategy

Tano, kama sera za sasa ni kuuza malighafi(hata kama ni chafu) kwanini tuite wawekezaji kutoka nje kuja kuwekeza nchini. Kwanini tusiwaambie wafanyabiashara waje kubeba pamba yenye masonyo na magugu kama malighafi tuachene na textile company n.k.

Sitta, kama unakubali kuwa inward na outward zina co-exist, vipi tena utakuwa na inward wakati umeamua kuuza makontena ya mchanga ukatengenezwe huko huko?
Vipi tena zina co-exist wakati inward inaangalia zaidi ustawi wa ndani.
Je, unaweza kuuza makontena ya mchanga wa dhahabu ukasema hiyo ni inward strategy.
 
Tukirudi kwenye mada, nilikuomba unipe orodha ya kampuni au mashirika 10 ya kiserikali yaliokuwa na mafanikio. Naona zoezi hilo limekuwa gumu sana. Katika makampuni na mashirika 400,kushindwa kuja na orodha ya makampuni kumi inaonyesha kuwa mambo hayakuwa mazuri. Kama mtanzania anaweza kutoa listi ya makampuni ya kichina ya kiserikali yaliofanya vizuri na kushindwa kufanya hivyo kwa nchi yake, something is wrong.

Mkuu Zakumi,

Nimekupa majina ya makampuni kadhaa ya huduma za kifedha na bima pamoja na viongozi wake; Vile vile nimekueleza kwamba dhamana ya industrialization ilikuwa chini ya National Development Corporation, na yapo makampuni kadhaa (sio yote) ambayo yalianzishwa na pia kuendeshwa with formidable success - mass goods industries kwani ni haya ndio yalikimbiliwa haraka sana na wawekezaji kutoka nje following the wave of privatization; nadhani unajichanganya katika hili kwani ni makampuni hayo hayo ambayo siku chache zilizopita ulikubali kwamba yalifanikiwa lakini ukayabeza kwamba hayana thamani yoyote ya maana kwa taifa kwa vile yanazalisha tu pombe, tumbaku; Na hapa naomba nikuulize: Kwa mtazamo wako, je kulikuwa na maana ya kuanzisha viwanda vya korosho mtwara miaka ile? Kwanini vilikufa? Kwanini leo under export promotion strategy mtazamo uliopo ni kwamba viwanda hivi ni muhimu?
Kuhusiana na rejea za mwalimu ulizotoa kuonyesha kwanini kulikuwa na matatizo, Mwalimu aliona kasoro za kiutendaji. Lakini kiundani kulikuwa na kasoro nyingine: zikiwemo za formulation za sera zenyewe. Kwa mfano formulation ya sera za vijiji vya ujamaa ilikuwa na kasoro kubwa. Na matokeo yake ni kushuka kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo ambayo yalitegemewa na viwanda. Uzalishaji wa korosho uliathirika sana na formulation ya sera hii. Elimu ya UPE na Operasheni maduka ni miongoni mwa sera mbovu pia.

Binafsi sijakataa kwamba sera chini ya Mwalimu zilikuwa na mapungufu; Lakini naomba unieleze katika nchi za africa, ni wapi walifanikiwa na Kilimo baada ya uhuru, kilimo ambacho kiliweka wazawa at the centre sio wazungu)? Ukitazama kwa makini, utagundua kwamba pamoja na failures zetu, approach yetu ilikuwa ni nafuu kuliko nchi nyingi, lakini muhimu zaidi ni kwamba, misingi iliyowekwa wakati ule inatupatia fursa ya kuanza tena bila ya major disruptions kwani sehemu kubwa ya ardhi bado ipo mikononi mwa wananchi aidha directly au indirectly; Lakini kwa bahati mbaya sana, haya yote huyatazami, badala yake ni kutazama mapungufu tu; Isitoshe, katika suala hili la sera za Mwalimu, bado sijaona approach mbadala kutoka kwako inayojitosheleza zaidi ya kuja tu na erratic statements;

Katika posti zilizopita ulisema kuwa state capital ndio iliyotumika zaidi. Katika posti hii unasema kuwa foreign aid ilichangia 60% ya development aid. Naomba jamaa wa kambi yako waisome hiyo. Watu msiendelee kung'ang'ania tulijenga hiki na kile, wakati misaada ya kutoka nje ndiyo iliyotoa impetus ya mabadiliko na sio resources za Tanzania.
Zakumi, nadhani huelewi hoja yangu ya msingi hapa ni nini; Huko nyuma nilieleza kwamba much AID went into provision of social services, huku chache zikienda kwenye maeneo mengine ya maendeleo; Hapa ni kuangalia proportion ya capital iliyotumika, kama nilivyojadili awali; Sasa kwa vile Mwalimu hapo juu hakuchanganua suala hilo katika maelezo yake, wewe umetumia fursa hiyo kusisitiza kwamba our mass good industries (leather, oil, Textiles...), fedha iliyotumika zaidi ilikuwa ni misaada kuliko STATE CAPITAL; Kafanye utafiti juu ya hilo; Zakumi - mass goods industrialization like oil, leather, textiles zilitumia more state capital (plus a little bit of local private capital) kuliko foreign capital; Kafanye utafiti mzuri juu ya hili; A smaller proportion ilitoka from foreign public loans pamoja na private management contracts;

Tukibaki kwenye misaada,takwimu zinaonyesha kuwa hakuna nchi iliyoendelea kwa kutegemea 60% ya misaada kutoka nje. Asian Tiger zilitegemea chini ya asimilia 2% misaada kutoka nje. Hivyo dependency ya misaada ilikuwa ni chanzo cha failures za sera kwa sababu mbili. Kwanza misaada iliwafanya viongozi wetu kuwa na kiburi. Pamoja na nia yao nzuri, wao na wahisani walitupangia (Top down approach).
Sio kweli; Hoja yako inaonyesha jinsi gani haupo in touch with reality on what transpired in South East Asia wakati wa Cold War; Bila ya massive AID, South Korea isingefanikisha yaliyofanikishwa, thats the bottom line; Kilichotokea ni kwamba uongozi wa nchi ulitumia fursa hii kikamilifu; Kwa hili pia nashauri ufanye utafiti;

Pili misaada ni matokeo ya kuvutia washirika wakati wa vita vya baridi. Misaada mingi ilikuja Tanzania ilitoka kwenye serikali zilizofuata mkondo wa kushoto. Hivyo Nyerere alikuwa naive kwa kuamini kuwa walitusaidia kwa sababu ya juhudi zetu. Walitusaidia kwa sababu walitaka tuwe upande wao.

Sio kweli; Unajua wachangiaji wa World Bank ni kina nani? Unajua kiasi gani World Bank ilichangia katika misaada? Unajua story ya McManara (World Bank President wa wakati wa Ujamaa) na Tanzania? Pia nashauri ufanye utafiti ili uweze kuelewa tofauti baina ya bilateral and multilateral donors; Wewe unazungumzia bilateral donors kama Sweden etc, lakini unapuuzia the multilateral front (e.g. Role of the World Bank ambamo wenye control na funds sio leftists);

Tukirudi kwenye kasoro za sera, toka TANU na mtoto wake CCM ishindwe kuelezea mafanikio ya maendeleo, wanatumia kusomesha wanafunzi kwa idadi kubwa kama ni mafanikio. Ukweli wa mambo takwimu za maendeleo hazionyeshi uwiano wowote wa idadi kubwa ya wanafunzi na maendeleo ya jamii. Maendeleo ya nchi yanaletwa ubora wa elimu inayotolewa. Hivyo massive enrollment of students in 70s didn't translate to anything.

Katika hili mkuu, pia unaonyesha mapungufu yako niliyoeleza awali kwamba unajadili industrialization kwa jicho la Privatization, Liberalisation and Marketization - ambayo haikuwepo in 1960s; Hata kwa marekani na uingereza, dhana hii ilikuwa baadae sana chini ya Thatcher (UK) na Reagan (USA) - late 1970s; Fanya utafiti mdogo tu kubaini haya; Lakini muhimu zaidi (kuhusu investment in UPE), nahisi kama vile huwa unalazimisha hoja wakati common sense tells us kwamba - kwa kipindi kile, hapakuwa na jinsi bali kuanza na elimu ya msingi, kwani all over the LDCs, it was necessary to invest in primary education kwani there were substantial returns to education to be reaped all over the newly independent states, especially kwa nchi changa kiuchumi na kimaendeleo; Wewe ulitaka investment ianzie wapi, Secondary? Vyuo vikuu? In a country where 90% was rural and almost illiterate? Cha kujadili hapa ni kwamba je, kulikuwa na vikwazo gani kwa Tanzania na sera yake ya elimu yenye manufaa kwa uchumi miaka ile?

Kwa kifupi huo ni mtazamo wangu kuhusu majibu ya mwalimu. Aliyaona matatizo ya utekelezaji wa sera kwa kuangalia utendaji. Lakini kulikuwa na matatizo ya formulation ya sera zenyewe, funding ya sera, na social traps.

I agree, lakini hizi zilikuwa ni changamoto in most contexts, sio Tanzania tu; Jiulize, kwanini nchi nyingi zilikumbana na changamoto hizi? Ukitafiti kidogo tu utabaini kwamba pamoja na mapungufu ya Mwalimu, kufikia 1985, Tanzania was better off lilipokuja suala la kuanzia pale Mwalimu alipoishia relative to mataifa mengi ya Afrika ambayo kufikia 1985 mambo yalikuwa yameshaharibika kwa namna nyingi - hasa poor governance, corruption, social hatred etc; Hata Nguruvi3 amekuuliza, je kipindi cha post Mwalimu tumekitumia vipi kumletea mtanzania maendeleo relative to prior 1985? Kama kawaida, majibu kwa hili hauna; Vinginevyo iwapo nakutafsiri sawa, unakubali kwamba the vision (the end) was justified, na kama kulikuwa na matatizo, basi ilikuwa kwenye means towards that end;

Tukirudi kwenye mada kamili. Watanzania watajikomboa kwa kutumia human and natural resources zao vizuri. Kama huna skilled workforce inward and outward strategies are just fancy words. Utaendelea kupokea misaada na kunyonywa tu.
I agree, lakini hoja hii kwa kiasi fulani contradicts with your earlier position kwamba ili tuendelee, we must specialize on exportation of raw materials and natural resources tu na kwamba mengine tuachane nayo; Nguruvi3 katika hili akakueleza kwamba you cant just have such a policy expecting mambo yatakuwa mazuri kwani kuna suala la value of your exports, suala ambalo in your exports approach, you tend to ignore; Hapa ndio umuhimu wa processing industries unajitokeza; Kwa kweli unaniacha na maswali mengi kuliko majibu pale unapoamua kupuuza umuhimu wa agriculture valued added, approach ambayo imekuwa ni standard all over the developing world;
 
Last edited by a moderator:
Gfsonwin;

Sijamshambulia mwalimu. Nimeshambulia baadhi ya sera zake. Hicho ni kitu cha kawaida in politiking. Katiba ya Tanzania ina nipa haki ya kufikiri, kutoa mawazo na kushiriki katika politiking.

Kuhusiana na hoja yako kuwa tulitegemea viwanda ni sawa na kumpa mtoto wa darasa la kwanza Phd. Uzalishaji wa viwanda haukukidhi mahitaji ya taifa. Bidhaa nyingi zilikuwa na kiwango cha chini. Na mapato ya viwanda hivyo hayakufikia 10% ya pato la taifa.

Ukweli wa mambo mapato yaliotokana na misaada yalikuwa zaidi ya mara 5 ya mapato ya viwanda. Hivyo tulitegemea misaada. Mlete Mchambuzi au Mkandara wabishe hii point.

Kuhusiana na RUKSA, let me say am a libertarian and free marketer and also believe that people are inherently greedy.

ni kweli uchumi wa nchi wa wakati tunapata uhuru ulitegem,ea zaid misaada sawa lakin pia hata mtotom aliyezaliwa hupewa maziwa yasiyoghoshiwa nikiwa na maana kwamba utoto huanza kwa kukaa kisha kutambaa na ndipo usimame.

hivi Mchambuzi na Mkandara watanibishia kwamba hakukuwa na sababu ya kuwa na viwanda ama kuwa na viwanda kwa wakati ule ilikuwa ni makosa??

binafsi unless kwamba am getting old na uwezo wangun wa kufikiri unazidi kudumaa but the truth is mwl did the right thing kwa wakati huo, lets name viwanda vilivyokuwapo ingawa vilipata changamoto ya ujinga uliokuweppo miongonui mwa wengi lkn it was much better manake that was one way ya kuelekea kukuza taifa liwe na uchumi huru.

nafikiri tukianza kutaja tyoka enzi za RTC, MAGUNIA, COFFEE CURING, URAFIKI, TANZANIA PACKERS, TANARIES ETC huoni kama hata kama havikuwa na mchango mkubwa kiuchumi but vilitakiwa kuendelezwa ili vije vitufae baadae??

unaona sera ya Mwinyi free market ilikuwa sawa na mimi naikubali but unapoongelea free je ni free market ya kuagiza tu ama na wewe una supply??
manake angesema free markert huku na siye tunasupply ingekuwa sawa ila free market kwa kuingiza tu thats bull shit to me......

hebu kwanza tuangalie % ya import na export enzi za mwl kisha tuje tukompee na za mzee ruksa tuone.

Ukweli ni kwamba misingi ya mwl kwa enzi zile ilikuwa ni mizuri sana na kama tungepata maboresho kidogo toka pale ilipokuwa tungekuwa mbali sana lkn kuua kabisa ile misingi ndio chanzo cha matatizo yetu leo. imagine hata kiberiti tunaagiza nje from kenya?? kiberiti cha kibo match hakina ubora hadi unajiuliza hivi mwl aliondoka na akili za watu ama ilikuwaje??

Sikatai sera za mwl kukosolewa lkn pia napingana zaid na kukosolewa kwa sera zake kwa aina ya kuzikaa na kuzifisha bila kuziboresha ili ziweze kwenda na wakati.

Mimi nakupa mfanio mdogo tu nimezaliwa kijijini sana huko Hai machame nazaliwa nakuta home kwetu kijijini kuna simu lile la kuzungusha la mezani, ila baada ya tu ya mzee ruksa kuingia alianza na posta na simu wakati huo kuifanya anachojua yeye sile idara ya simu ikahujumiwa ikafa ikawa nyaya zake ndizo tunazoanikia nguo na kibaya zaid mtu akitaka kupiga simu basi anakwenda kufunua lile handaki la cable anapiga simu kwa kuchezea hadi simu ikawa mufilisi. thanks to Mkapa alokuja kuifufua na kuifanya kuwa ni kitebgo kinachojitegemea na sio posta na simu tena.

sasa hii inanipa picha kwamba hata kama mwl alikuwa na mapungufu but aliweza kusimamaia vitu vikaonekana na vikawepo ila wanasiasa wa leo wote wanasimamia matumbo yao tum na hakuna anyejali hata mmoja.

sera za mwl zikirekebishwqa kuwenda na wakati zingeyytufikisha mbali ila kwa kufuata sera za dunia sijui dunia inaenda wapi na sisi tunaenda tu kama vipofu hatufiki. kwanza sion sababu ya kucopy na kila aina ya uchumi wa dunia unavyoenda cant we be creative kwa kiasi cha kuwa na mfumo wetu ambao kwenye mfumo wa mwenendo wa uchumi duniani unafiti lkn pia kwetu sisi unatupa maisha bora zaid??
 
Last edited by a moderator:
[FONT=comic sans ms [USER=12016]Zakumi[/USER] nimekuuliza hapo nyuma, hebu weka swali lako la mashirika katika muktadha unaoeleweka kwanza.
Kwasasa lipo vague kwasababu halieleweki unataka nini hasa.

Pili, umezungumzia kufeli kwa sera za mwalimu kunatokana na unskilled workforce.
Sasa hivi kuna skilled workforce ukilinganisha na zama hizo.
Ni kipi unachoweza kutuomyesha kuwa for the past 30 years kuna tofauti na 26 years before

Tatu, kwavile umesema mkakati uwe kusafirisha malighafi kwa maana ya pamba zenye magugu, korosho zisizobanguliwa na makontena ya dhahabu, Tanzanite na almasi, je huoni kuwa katika soko la dunia lenye ushindani utauza sh10 mwenzako anauza 100 kwa kitu kile kile? Hebu fafanua hakuna ukweli hapo?

Nne, hebu tueleze baada ya kuuza yale mashirika 400 ya 'hovyo' nini kimefanyika kama mbadala na nini matokeo ya mauzo hayo ambayo kiuchumi tunaweza kusema yameleta afueni?
Je kugeuza kiwanda kuwa ghala la chumvi ndio uchumi ndio inward strategy

Tano, kama sera za sasa ni kuuza malighafi(hata kama ni chafu) kwanini tuite wawekezaji kutoka nje kuja kuwekeza nchini. Kwanini tusiwaambie wafanyabiashara waje kubeba pamba yenye masonyo na magugu kama malighafi tuachene na textile company n.k.

Sitta, kama unakubali kuwa inward na outward zina co-exist, vipi tena utakuwa na inward wakati umeamua kuuza makontena ya mchanga ukatengenezwe huko huko?
Vipi tena zina co-exist wakati inward inaangalia zaidi ustawi wa ndani.
Je, unaweza kuuza makontena ya mchanga wa dhahabu ukasema hiyo ni inward strategy.[/FONT]
Nguruvi3 hebu nisaidien jambo hapa mimi naona hata hawa skilled labour force iliyopo kwa miakam hii 30 ni hovyo kabisa manake badala ya kukuza nchi tumefifisha nchi.

kwanza labda Zakumi aseme je kwasasa hivi nchi yetu kama ilivfyo inasafirisha nini nje ya nchi kama bidhaa?? je sisi kama nchi tuna viwanda gani ambavyo vinaweza kukompete na vyenye mnitaji mikubwa?

hivi kuuza juice na maziwa na ice cream ndicho ambacho tunakitegema as a nation?? hivi kuuza sigara na bia ndo kitu pekee for 30yrs kweli??

Nauliza swali kwann leo hii hatuna BORA kile kiwanda cha viatu ambacho kilikuwa kinatumia ngozi za tanarries?? hvim kuh=na sababu ya mtanzania wa leo kuvaa mtumba kiatau licha ya kwamba klila siku idadi kubwa ya ng'ombe na mbuzi, swala wanachinjwa?

ipo wapi sababu ya mtu kutumia malindi salt licha ya uvunza yetu kuwa na uwezo wa kutoa chumvi ya kutosha?

nauliza ipo wapi sababu ya kuagiza daftari toka Kenya licha ya KIBO paper kuwepo?

ipo wapi sababu ya kuagiza tiles na gypsum toka nje ilihali gypsum powder ipo hapo bagamoyo na tanga??

kuna haja gani ya kutumias spanmish ama italian tiles ilihali tunazo tanga stones na montemorillonite clay?? tunayo ceramic powder kweli tuagize vigae nje?? baada ya miaka 50 ya uhuru?? unless tuko wapumbavu na kuna watu wanafurahia upumbavu wetu na yumkini ndio maana tumekuja na kipengele kwamba hakunaga mtu anayepata sifuri tukafuta div 0 na kukubali kuwa nchi ya kwanza duniani yenye alama ndozo kabisa za ufaulu.

hivi kwa ukubwa wa eneo la bahari tulio nao kweli kuna haja ya sisi kuwa hapa tullipo?? marine scientist can tell tuna kiasi kikubwa sana marine resources nyingi sana, kila siku meli za kichina zinaondoka na pearls sasa hivi kwan sisi hatuhitaj hizi pearls?? nani amewah kusemea hili jamani nyie hamjui tu lkn ukweli ni the most expensive kito cha kwenye maji na huuzwa kwa thaman kubwa sana lkn sasa sisi tuko kimyaa wachina wanaenda kutengeneza na kuuza ulaya imekuwa kama enzi zile za watu kuchezea almasi mdako?? baada ya miaka 30 ya tunao waita wenye sera nzuri??
 
Last edited by a moderator:
wanabodi mie nina swali kwenu moja tuu ambalo nataka kujibiwa kwa ufasaha kabisa,

hivi hapa tunaujadili uchumi wa mtanzania mmoja moja ama wa taifa kwa ujumla?? hivi tunajadili juu ya kuboresha maisha ya mtanzania mmoja moja ama wote??

najiuliza maswali haya as nimeingiwa na simanzi sana nafsini mwangu, siku ya leo. achilia mbali kwamba nimeharibikiwa na siku toka saa mbili asbh maeneop ya Ilala klabu ya wazee baada ya kushuhudia watu 3 wakipoteza maisha yao kama jana lidondokavyo juu ya mti kwa kutumia bunduki ambazo zilinifanya niione westgate ndani ya Ilala kwa muda wa sekunde chache.

lakini siku yangu hii imeharibiwa na kile nilichokikuta KKOO sehem ambayo ndipo wengi huenda kujipatia mahitaj yetu ya kila siku.

Najiuliza hivi kweli ni hizo sh laki 6 -770 hawana ama ni makusudi wanayofanya hawa wafanya biashara?? ama wao ni akina nani ambao wanaweza kuilazimisha serikali ifanye kile wanachokitaka wao pasi kuangalia ukweli uko wapi??
Nguruvi3, Mchambuzi. Zakumi nijibuni tafadhali hivi hasara ambazo serikali inazipata kwa kushindwa kukusanya kodi vizuri toka kwa hawa wafanyabiashara nani anayeilipia??

nimejiuliza sana labda zumbemkuu utakuwa na jibu, hivi kwann serikali atoka tupate uhuru wa nchi hii, haijawah kuwa na uhakika wa kukusanya kodi ipasavyo na kwa halali zaid ya kodi wanayokusanya kutoka kwa mfanyakazi awe wa umma ama wa sekta binafsi.

naumia manake sijawah kuona siku salary imekuja pasi tozo la payee lkn wenzetu hawa hawatak kuwa fair na wao kulipa kodi kwa uaminifu??

yaani kkoo maduka yamefungwa eti hawataki mashine za risiti za TRA lkn wanaona wanayohaki ya kukwepa kulipa kodi na hivyo kuhujumu uchumi sasa naomba Kichuguu unijibu huu uchumi tunaudiscuss hapa ni wa mtu mmoja mmoja mfukoni ama ni wa taifa?

naumia zaid kuona delay ya siku 2 ya biashara kutokufanyika ni sawa na kuzuia kwa siku 2 serikali isikusanye mapato jambo ambalo linarudisha uchumi nyuma wa taifa hili.

mbona wafanya kazi wa maofisin na viwandani wako radhi kulipa kodi regardless kipato chao kidogo?? kwann hawa wenye mitaj mikubwa tena ambao wanakopesheka hata kwenye mabenki wanakataa kulipa kodi?

kwann wafanya biashara wanaona sawa tu kuhujumu uchumi wa nchi hii?? ni kweli kwamba hawana hizo hela za kununua hizo mashine? ama je ni kazi ya serikali kuwanunulia naombeni majibu.

am pissed off kwakweli
 
Last edited by a moderator:
@Zakumi nimekuuliza hapo nyuma, hebu weka swali lako la mashirika katika muktadha unaoeleweka kwanza.
Kwasasa lipo vague kwasababu halieleweki unataka nini hasa.

Pili, umezungumzia kufeli kwa sera za mwalimu kunatokana na unskilled workforce.
Sasa hivi kuna skilled workforce ukilinganisha na zama hizo.
Ni kipi unachoweza kutuomyesha kuwa for the past 30 years kuna tofauti na 26 years before

Tatu, kwavile umesema mkakati uwe kusafirisha malighafi kwa maana ya pamba zenye magugu, korosho zisizobanguliwa na makontena ya dhahabu, Tanzanite na almasi, je huoni kuwa katika soko la dunia lenye ushindani utauza sh10 mwenzako anauza 100 kwa kitu kile kile? Hebu fafanua hakuna ukweli hapo?

Nne, hebu tueleze baada ya kuuza yale mashirika 400 ya 'hovyo' nini kimefanyika kama mbadala na nini matokeo ya mauzo hayo ambayo kiuchumi tunaweza kusema yameleta afueni?
Je kugeuza kiwanda kuwa ghala la chumvi ndio uchumi ndio inward strategy

Tano, kama sera za sasa ni kuuza malighafi(hata kama ni chafu) kwanini tuite wawekezaji kutoka nje kuja kuwekeza nchini. Kwanini tusiwaambie wafanyabiashara waje kubeba pamba yenye masonyo na magugu kama malighafi tuachene na textile company n.k.

Sitta, kama unakubali kuwa inward na outward zina co-exist, vipi tena utakuwa na inward wakati umeamua kuuza makontena ya mchanga ukatengenezwe huko huko?
Vipi tena zina co-exist wakati inward inaangalia zaidi ustawi wa ndani.
Je, unaweza kuuza makontena ya mchanga wa dhahabu ukasema hiyo ni inward strategy.

Nitakujibu point kwa point.

1. Swali lilikuwa nipe orodha ya makampuni au mashirika kumi yaliofanikiwa na viongozi wake. Nimesema mara kadhaa kuwa viwanda na mashirika yanaendeshwa kukidhi business imperatives. Na hili yafanikiwe ni lazima viongozi wake watumie business and industrial best practices. Kama kiongozi alitumia best practices na kufanikiwa katika sehemu moja atafanikiwa katika sehemu nyingine. Na vilevile atarithisha excellence kwa vizazi vijavyo .

2. Nimesema sera zili-fail kwa sababu ya unskilled labour force. Vilevile niliongezea kasoro zingine. Moja ikiwa formulation ya sera zenyewe. Nyingine ikiwa funding ya sera zenyewe. Sera zilitegemea sana foreign aid. Vilevile kulikuwa na social traps.

3. Unavuna ulichopanda. Tulikazania elimu ya msingi na elimu hiyo ilikuwa duni ambayo haiongezi values katika bidhaa za kuuza nje. Hii ni moja ya sababu ya kuuza malighafi. Vilevile elimu mbovu inachangia uzalishaji mdogo. Kwa heka moja ya pamba wakulima watanzania wanatoa kiwango kidogo sana hata kwa standard za kiafrika.

4. Makampuni na mashirika yamekufa kwa sababu ya Business Darwinism.

5. Kama Tanzania inaweza kuwekeza kwa kutumia internal investors, isingekaribisha external investors. Hivyo hili ni suala la capabilities za nchi.

6. Uchumi unaangaliwa kwa kutumia sectors and segments. Hivyo applications ya inward na ourward strategies zinatofautiana katika segments mbalimbali za uchumi. Kwa mfano ni kitu kinachowezekana kuwa inward strategy katika sector ya uzalishaji na usindikaji wa chakula. Kuhusu utengenezaji wa viatu labda itakuwa na manufaa kuuza ngozi.
 
Kama Tanzania itandelea na jitihada zake za kuboresha western democracy, haitaweza kutenganisha serikali na siasa. .
Hewala Mkuu wangu! Na kama hatutaweza kutenga serikali na siasa, basi kila kitu tutakachofanya ni kazi bure. Ukombozi wa Mtanzania utakuwa Ndoto za alinacha.

Mkuu wangu Mchambuzi hii aya uliyoitupia hapa inabeba uzito mkubwa sana kwangu, na nadhani inatoa majibu mengi sana tunayojiuliza juu ya Mwalimu na sera zake.
"I don't have a full answer to that question; some things certainly went right -(ni wazi alitambua kuna vilivyokwenda wrong) we knitted a nation together, gave it a pride and educated a large number of our children and adults; (akatupa sababu ya baadhi ya mambo kwenda mrama) But some ideas needed to wait their proper time(TIMING);People weren't ready(ATTITUDE); But you (young Africans who are in here now have a chance to give those ideas new life" (Declaration of War, Go ahead to the Soldiers)

Sera bora ni zile zenye nia njema kwa mwananchi, hata kama zilifanyiwa bad timing haiwezi kuondoa ukuu wake. Ni wajibu wetu leo kusimama pamoja kupiga hatua. Huwa tunajidanganya sana na neno UHALISIA wa dunia, basi kufuata mambo hovyo ovyo kwa kigezo cha Time Factor (Dunia ndivyo inavyotaka). Ipo siku Dunia mnayosemea itataka kuua kizazi chetu chote kuifanya iendelee kuwepo, sidhani kama kuna atakayekuwa mstari wa mbele kunyoosha shingo yake kisu kipite kutii Matakwa ya dunia. Tusipotahadhari ni lazima yatukute hayo.

Ili kufikia maslahi yao Walitupora Nguvu zetu, walipoona haitoshi wakatupora UTU wetu. Kilichobaki ni Uhai wetu, nasi tunawakenulia meno eti ndivyo dunia inavyotaka. -------!

Time Will Tell - We Are The Time.
Mungu wetu yu hai, tayari kutushindia vitani.
Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Zakumi,

Nimekupa majina ya makampuni kadhaa ya huduma za kifedha na bima pamoja na viongozi wake; Vile vile nimekueleza kwamba dhamana ya industrialization ilikuwa chini ya National Development Corporation, na yapo makampuni kadhaa (sio yote) ambayo yalianzishwa na pia kuendeshwa with formidable success - mass goods industries kwani ni haya ndio yalikimbiliwa haraka sana na wawekezaji kutoka nje following the wave of privatization; nadhani unajichanganya katika hili kwani ni makampuni hayo hayo ambayo siku chache zilizopita ulikubali kwamba yalifanikiwa lakini ukayabeza kwamba hayana thamani yoyote ya maana kwa taifa kwa vile yanazalisha tu pombe, tumbaku; Na hapa naomba nikuulize: Kwa mtazamo wako, je kulikuwa na maana ya kuanzisha viwanda vya korosho mtwara miaka ile? Kwanini vilikufa? Kwanini leo under export promotion strategy mtazamo uliopo ni kwamba viwanda hivi ni muhimu?

Binafsi sijakataa kwamba sera chini ya Mwalimu zilikuwa na mapungufu; Lakini naomba unieleze katika nchi za africa, ni wapi walifanikiwa na Kilimo baada ya uhuru, kilimo ambacho kiliweka wazawa at the centre sio wazungu)? Ukitazama kwa makini, utagundua kwamba pamoja na failures zetu, approach yetu ilikuwa ni nafuu kuliko nchi nyingi, lakini muhimu zaidi ni kwamba, misingi iliyowekwa wakati ule inatupatia fursa ya kuanza tena bila ya major disruptions kwani sehemu kubwa ya ardhi bado ipo mikononi mwa wananchi aidha directly au indirectly; Lakini kwa bahati mbaya sana, haya yote huyatazami, badala yake ni kutazama mapungufu tu; Isitoshe, katika suala hili la sera za Mwalimu, bado sijaona approach mbadala kutoka kwako inayojitosheleza zaidi ya kuja tu na erratic statements;

Zakumi, nadhani huelewi hoja yangu ya msingi hapa ni nini; Huko nyuma nilieleza kwamba much AID went into provision of social services, huku chache zikienda kwenye maeneo mengine ya maendeleo; Hapa ni kuangalia proportion ya capital iliyotumika, kama nilivyojadili awali; Sasa kwa vile Mwalimu hapo juu hakuchanganua suala hilo katika maelezo yake, wewe umetumia fursa hiyo kusisitiza kwamba our mass good industries (leather, oil, Textiles...), fedha iliyotumika zaidi ilikuwa ni misaada kuliko STATE CAPITAL; Kafanye utafiti juu ya hilo; Zakumi - mass goods industrialization like oil, leather, textiles zilitumia more state capital (plus a little bit of local private capital) kuliko foreign capital; Kafanye utafiti mzuri juu ya hili; A smaller proportion ilitoka from foreign public loans pamoja na private management contracts;

Sio kweli; Hoja yako inaonyesha jinsi gani haupo in touch with reality on what transpired in South East Asia wakati wa Cold War; Bila ya massive AID, South Korea isingefanikisha yaliyofanikishwa, thats the bottom line; Kilichotokea ni kwamba uongozi wa nchi ulitumia fursa hii kikamilifu; Kwa hili pia nashauri ufanye utafiti;

Sio kweli; Unajua wachangiaji wa World Bank ni kina nani? Unajua kiasi gani World Bank ilichangia katika misaada? Unajua story ya McManara (World Bank President wa wakati wa Ujamaa) na Tanzania? Pia nashauri ufanye utafiti ili uweze kuelewa tofauti baina ya bilateral and multilateral donors; Wewe unazungumzia bilateral donors kama Sweden etc, lakini unapuuzia the multilateral front (e.g. Role of the World Bank ambamo wenye control na funds sio leftists);

Katika hili mkuu, pia unaonyesha mapungufu yako niliyoeleza awali kwamba unajadili industrialization kwa jicho la Privatization, Liberalisation and Marketization - ambayo haikuwepo in 1960s; Hata kwa marekani na uingereza, dhana hii ilikuwa baadae sana chini ya Thatcher (UK) na Reagan (USA) - late 1970s; Fanya utafiti mdogo tu kubaini haya; Lakini muhimu zaidi (kuhusu investment in UPE), nahisi kama vile huwa unalazimisha hoja wakati common sense tells us kwamba - kwa kipindi kile, hapakuwa na jinsi bali kuanza na elimu ya msingi, kwani all over the LDCs, it was necessary to invest in primary education kwani there were substantial returns to education to be reaped all over the newly independent states, especially kwa nchi changa kiuchumi na kimaendeleo; Wewe ulitaka investment ianzie wapi, Secondary? Vyuo vikuu? In a country where 90% was rural and almost illiterate? Cha kujadili hapa ni kwamba je, kulikuwa na vikwazo gani kwa Tanzania na sera yake ya elimu yenye manufaa kwa uchumi miaka ile?

I agree, lakini hizi zilikuwa ni changamoto in most contexts, sio Tanzania tu; Jiulize, kwanini nchi nyingi zilikumbana na changamoto hizi? Ukitafiti kidogo tu utabaini kwamba pamoja na mapungufu ya Mwalimu, kufikia 1985, Tanzania was better off lilipokuja suala la kuanzia pale Mwalimu alipoishia relative to mataifa mengi ya Afrika ambayo kufikia 1985 mambo yalikuwa yameshaharibika kwa namna nyingi - hasa poor governance, corruption, social hatred etc; Hata Nguruvi3 amekuuliza, je kipindi cha post Mwalimu tumekitumia vipi kumletea mtanzania maendeleo relative to prior 1985? Kama kawaida, majibu kwa hili hauna; Vinginevyo iwapo nakutafsiri sawa, unakubali kwamba the vision (the end) was justified, na kama kulikuwa na matatizo, basi ilikuwa kwenye means towards that end;

I agree, lakini hoja hii kwa kiasi fulani contradicts with your earlier position kwamba ili tuendelee, we must specialize on exportation of raw materials and natural resources tu na kwamba mengine tuachane nayo; Nguruvi3 katika hili akakueleza kwamba you cant just have such a policy expecting mambo yatakuwa mazuri kwani kuna suala la value of your exports, suala ambalo in your exports approach, you tend to ignore; Hapa ndio umuhimu wa processing industries unajitokeza; Kwa kweli unaniacha na maswali mengi kuliko majibu pale unapoamua kupuuza umuhimu wa agriculture valued added, approach ambayo imekuwa ni standard all over the developing world;

Mchambuzi:

Bado unaboronga. Hili makampuni yawe na mafanikio ni lazima ya-pass stress tests. Makampuni yako hayakuweza kustahimili ujio wa makampuni binafsi. Hivyo mafanikio unayong'ang'ania yalikuwa artificially induced wakati wa Ujamaa. Kwa mfano kazi zote zilizofanywa na mabenki ya kiserikali,zinafanywa na benki binafsi tena kwa ufanisi mkubwa.

Wawekezaji kukimbilia haraka baadhi ya makampuni fulani, ni potential ya makampuni hayo. Hivi kwanini Nyerere alikimbilia haraka kutaifisha mabenki binafsi mwaka 1967? Walichofanya wawekezaji ni kilekile kilichofanywa na serikali wakati inataifisha.

Kuhusu kwanini nchi nyingi za kiAfrika kuboronga, nimeeleza kwenye posti mbalimbali. Sera zilizokuwepo Tanzania hazikuwa Unique. Nchi mbalimbali zilifanya hivyo na nchi mbalimba zilianguka kwa sababu zilezile. Tatizo kubwa ni capabilities. Huwezi sema kuwa Tanzania imeboronga kwa unafuu bila kutumia measurable approach.

Mkuu hiyo state capital itabidi uifanyie utafiti vizuri. Kuanzia 1974 uzalishaji katika sekta mbalimbali ulianza kuboronga na mfumuko mkubwa wa viwanda ulitokea mwishoni mwa 70. Hivyo hiyo state capital ilitoka wapi? mikopo, grants, or misallocation of resources?

Kuhusiana misaada kwa asian tigers, unaangalia misaada ya nje ni asilimia ngapi ya bajeti ya nchi. Nchi yenye kupokea asilimia 2% inajitegemea tayari. Hivyo maendeleo ya nchi hizo hayakutegemea kuwepo au kutokuwepo misaada. Nchi hizo tayari ilikuwa kwenye trajectories za maendeleo kwa sababu ziliweza kumudu gharama za chachu za maendeleo.

Kwa upande mwingine Tanzania haikuwa kwenye trajectory ya maendeleo. 1961 misaada ilikuwa 9% na kufikia 70 ilikuwa above 40%. Hii inaonyesha kuwa uzalishaji na matumizi yetu ulikuwa haulingani.

Kuhusiana na viwanda naona unalazimisha. Kwa kifupi serikali ya Tanzania ilikuwa haina shughuli ya kufungua viwanda au kufanya umachinga (period).

Kulikuwepo na alternative. Wataalamu wa elimu wa ndani na nje walimpa mwalimu model ambayo ingekuza kiwango cha elimu kwa kipindi cha miaka 20. Mwalimu alikataa model hiyo na kutangaza Azimio la Musoma ambalo lilitaka kufuta ujinga kwa miaka saba.

The rest is commentary.
 
wanabodi mie nina swali kwenu moja tuu ambalo nataka kujibiwa kwa ufasaha kabisa,

hivi hapa tunaujadili uchumi wa mtanzania mmoja moja ama wa taifa kwa ujumla?? hivi tunajadili juu ya kuboresha maisha ya mtanzania mmoja moja ama wote??

najiuliza maswali haya as nimeingiwa na simanzi sana nafsini mwangu, siku ya leo. achilia mbali kwamba nimeharibikiwa na siku toka saa mbili asbh maeneop ya Ilala klabu ya wazee baada ya kushuhudia watu 3 wakipoteza maisha yao kama jana lidondokavyo juu ya mti kwa kutumia bunduki ambazo zilinifanya niione westgate ndani ya Ilala kwa muda wa sekunde chache.

lakini siku yangu hii imeharibiwa na kile nilichokikuta KKOO sehem ambayo ndipo wengi huenda kujipatia mahitaj yetu ya kila siku.

Najiuliza hivi kweli ni hizo sh laki 6 -770 hawana ama ni makusudi wanayofanya hawa wafanya biashara?? ama wao ni akina nani ambao wanaweza kuilazimisha serikali ifanye kile wanachokitaka wao pasi kuangalia ukweli uko wapi??
Nguruvi3, Mchambuzi. Zakumi nijibuni tafadhali hivi hasara ambazo serikali inazipata kwa kushindwa kukusanya kodi vizuri toka kwa hawa wafanyabiashara nani anayeilipia??

nimejiuliza sana labda zumbemkuu utakuwa na jibu, hivi kwann serikali atoka tupate uhuru wa nchi hii, haijawah kuwa na uhakika wa kukusanya kodi ipasavyo na kwa halali zaid ya kodi wanayokusanya kutoka kwa mfanyakazi awe wa umma ama wa sekta binafsi.

naumia manake sijawah kuona siku salary imekuja pasi tozo la payee lkn wenzetu hawa hawatak kuwa fair na wao kulipa kodi kwa uaminifu??

yaani kkoo maduka yamefungwa eti hawataki mashine za risiti za TRA lkn wanaona wanayohaki ya kukwepa kulipa kodi na hivyo kuhujumu uchumi sasa naomba Kichuguu unijibu huu uchumi tunaudiscuss hapa ni wa mtu mmoja mmoja mfukoni ama ni wa taifa?

naumia zaid kuona delay ya siku 2 ya biashara kutokufanyika ni sawa na kuzuia kwa siku 2 serikali isikusanye mapato jambo ambalo linarudisha uchumi nyuma wa taifa hili.

mbona wafanya kazi wa maofisin na viwandani wako radhi kulipa kodi regardless kipato chao kidogo?? kwann hawa wenye mitaj mikubwa tena ambao wanakopesheka hata kwenye mabenki wanakataa kulipa kodi?

kwann wafanya biashara wanaona sawa tu kuhujumu uchumi wa nchi hii?? ni kweli kwamba hawana hizo hela za kununua hizo mashine? ama je ni kazi ya serikali kuwanunulia naombeni majibu.

am pissed off kwakweli

Gfsonwin:

Katika nchi kuna shared values au common good. Na values ambazo individuals watazifuata kwa matakwa yao. Education,hospital, umeme, maji, barabara n.k ni sehemu ya sommon good.

Nchini Marekani, tajiri kama Bill Gates na homeless wanatumia chanzo kimoja cha maji na umeme. Na wanafanya hivyo kwa sababu vyombo vya kiserikali vipo tayari kuendeleza na kuboresha vyombo hivyo.

Kwa Tanzania, vyombo vya kiserikali vinashindwa kutoa huduma za kuimarisha shared values au common good. Na wasimamizi wa vyombo hivyo wako tayari kujichimbia visima vyao vya maji. Kuwa na majenereta yao. Hapa ndipo matatizo yanapoanza

Unapoelewa umuhimu wa common good au shared values, utaelewa kwanini ni lazima ulipe au ukusanye kodi.
 
Zakumi, haya ni majibu yangu kwa bandiko lako #18 :

Mchambuzi:
Bado unaboronga. Hili makampuni yawe na mafanikio ni lazima ya-pass stress tests. Makampuni yako hayakuweza kustahimili ujio wa makampuni binafsi. Hivyo mafanikio unayong'ang'ania yalikuwa artificially induced wakati wa Ujamaa. Kwa mfano kazi zote zilizofanywa na mabenki ya kiserikali,zinafanywa na benki binafsi tena kwa ufanisi mkubwa.

Mkuu Zakumi,
Its obvious kwamba wewe ndio unaboronga kwani nitajirudia tena: Unaangalia suala zima la industrialization in Tanzania kwa jicho la Liberalization, Marketization and Privatization, suala ambalo halikuwepo miaka hiyo; Katika dunia ya tatu, main anthem was developmental state ambapo nchi zilijengwa under STATE CAPITALISM (including the current Asian Tigers); Hivi unaelewa jinsi gani mataifa makubwa (yaliyoendelea) yalifanikiwa kufanya hivyo kupitia protectionism? Do you understand anything about the argument for infant industries? Hata hawa asian tigers tunaowajadili hapa, sio kwamba walifungua milango kwa njia ya "RUKSA" bila mipaka; Zakumi, You have to wake up and smell the Coffee;
Bila ya wewe kujinasua toka katika giza hili (i.e. kuishi dunia ya Liberalization, Marketization and Privatization – as if it has always been there, kamwe hauta appreciate malengo yaliyokusudiwa chini ya Ujamaa, let alone mafanikio katika maeneo kadhaa; Fanya utafiti uelewe kwanini donors walimiminika kwa wingi in terms of misaada na uwekezaji baada ya kutangazwa kwa azimio la Arusha, na sio kabla ya hapo;

Na hoja yako awali kwamba kilichofanyika Tanzania wasn't something new ni ishara kwamba haufanyi utafiti wa kutosha; Tanzania iliwavutia west na Ujamaa na Kujitegemea kwasababu it was a unique approach: Ujamaa opposed capitalism and shunned Marxism; Kwa wakati ule, kulikuwa na njia kuu mbili za kupiga hatua kimaendeleo kwa nchi maskini: Aidha accelerate integration of your economy into the global capitalist system (the colonial way), of which mkuu Zakumi, without reservations, unaona hiyo ndio njia sahihi OR, disengage/delink from this system through socialist policies; Again, the fact that Ujamaa opposed Ubepari and at the same time Shunned Marxism ilivutia watu wengi sana, na hata wewe ungekuwa unaishi nyakati zile, hakika usingepingana na hili; tatizo ni kwamba unafanya analysis "baadae sana";

Hoja yako juu ya "stress test" katika nyakazi zile za ujenzi wa taifa na uchumi baada ya maafa ya ukoloni haina mashiko kabisa, kwani again, unaishi katika muktadha ambao haupo sahihi kufanya such an analysis. Naomba nijirudie tena kwamba - hata kwa nchi kama Marekani na Uingereza, Sekta ya Umma ilipewa kipaumbele kuliko sekta binafsi kwa kipindi kirefu sana kufuatia kumalizika kwa vita vya pili vya dunia (1945), na mageuzi makubwa yalikuja letwa na Thatcher (UK) na Reagan (USA); Nini uchambuzi wako wa stress test kwa wenzetu hawa? Kumbuka, hata sekta ya umma kwa mataifa haya ilianza kupata misuko suko, lakini tofauti na sisi, mbali ya wao kuwa na uwezo mkubwa kiuchumi na utaalamu katika masuala ya sera, pia yalipata fursa to reform at their own pace vinginevyo yangeanguka; Mwalimu Nyerere aliomba kufanya the same na ndio maana Tanzania ilikuwa ni moja ya nchi za mwisho kabisa kupokea Structural Adjustment Policies spearheaded by the World Bank and IMF;

Wawekezaji kukimbilia haraka baadhi ya makampuni fulani, ni potential ya makampuni hayo.

Nashukuru umekuja na hoja hii, kwani inapingana na hoja yako ya awali ambayo ulibeza sana viwanda ambavyo wengi wetu tulijadili kwamba vilikuwa na umuhimu licha yaw ewe kuviponda kama viwanda visivyokuwa na maana katika uchumi – sigara, bia n.k; Kumbuka, hivi vilikuwa ndio viwanda kwanza kukimbiliwa na wawekezaji, na ndio kwa kiasi vimekuwa bado sustained na ni miongoni mwa tax payers wakubwa nchini; kama alivyojadili Nguruvi3, viwanda vingine vingi vimeishia kuwa maghala ya kuhifadhia chumvi, na akakuhoji kwanini, huku wewe ukitokomea bila ya majibu;

Hivi kwanini Nyerere alikimbilia haraka kutaifisha mabenki binafsi mwaka 1967? Walichofanya wawekezaji ni kilekile kilichofanywa na serikali wakati inataifisha.

Hivi kwanini Mkapa alikimbilia kubinaifisisha mabenki yaliyokuwa chini ya umma katika awamu yake? Kwa kiasi kikubwa, wanachofanya wawekezaji ni kilekile kilichokuwa kinafanywa na wakoloni.

Kuhusu kwanini nchi nyingi za kiAfrika kuboronga, nimeeleza kwenye posti mbalimbali. Sera zilizokuwepo Tanzania hazikuwa Unique. Nchi mbalimbali zilifanya hivyo na nchi mbalimba zilianguka kwa sababu zilezile. Tatizo kubwa ni capabilities. Huwezi sema kuwa Tanzania imeboronga kwa unafuu bila kutumia measurable approach.

Haupo in touch with reality; hata a simple search on google itakueleza kwamba our approach to development chini ya sera ya ujamaa na kujitegemea ilikuwa "UNIQUE"; Mengine nimejadili hapo juu;

Mkuu hiyo state capital itabidi uifanyie utafiti vizuri. Kuanzia 1974 uzalishaji katika sekta mbalimbali ulianza kuboronga na mfumuko mkubwa wa viwanda ulitokea mwishoni mwa 70. Hivyo hiyo state capital ilitoka wapi? mikopo, grants, or misallocation of resources?

Utafiti niliofanya ni kwamba – we experienced growth in the industrial sector late 1960s to mid 1970s ambapo mchango wa sekta hii kwa pato la taifa (GDP) ulifikia peak ya 13%; Hapo awali ulikuja na takwimu zisizo sahihi kwamba hatujawahi kuwa na mchango wa sekta hii kwa GDP ya Zaidi ya 7%; Kwahiyo nukuu yako hapo juu kuhusu uzalishaji wa sekta mbalimbali kuanza kuborongo in mid 1970s ni sahihi, na ndio maana STATE CAPITAL ikadumaa, lakini sio kabla ya hapo;

Kuhusiana misaada kwa asian tigers, unaangalia misaada ya nje ni asilimia ngapi ya bajeti ya nchi. Nchi yenye kupokea asilimia 2% inajitegemea tayari. Hivyo maendeleo ya nchi hizo hayakutegemea kuwepo au kutokuwepo misaada. Nchi hizo tayari ilikuwa kwenye trajectories za maendeleo kwa sababu ziliweza kumudu gharama za chachu za maendeleo.

Hivi kweli unaelewa role of Foreign AID katika maendeleo ya nchi kama South Korea?

Kwa upande mwingine Tanzania haikuwa kwenye trajectory ya maendeleo. 1961 misaada ilikuwa 9% na kufikia 70 ilikuwa above 40%. Hii inaonyesha kuwa uzalishaji na matumizi yetu ulikuwa haulingani.

Ni kweli kwamba uzalishaji na matumizi yetu havikulingana; Lakini jiulize why? Ni kwa sababu (na hii ipo all over the development literature – Tanzania ilijaribu to capture the peasants without coercion; Nchi nyingi zilizofanikiwa na viwanda, hata Britain, walifanya kinyume; Rejea matukio ya enclosure system ambayo ilikuwa ni very chaotic; Ni baadae sana Mwalimu akashawishika kufuata approach hii pale alipoanzisha vijiji vya ujamaa kwa nguvu, lakini baada ya muda mfupi, he abandoned this strategy kwani pia ikawa counterproductive; So capturing peasants (kisera) ikawa tatizo, na not capturing peasants (kisera), inaendelea kuwa tatizo hadi leo; So hoja yako kuhusu matumizi kuwa makubwa kuliko vipato ni kwa sababu – Mwalimu ilibidi atumie method nyingine, hasa ile ya kuwashawishi to engage in production of marketable surplus in exchange of free social services (elimu, afya, maji&#8230😉; Hii ikapelekea failure to produce a marketable surplus; Hoja ya msingi hapa mkuu Zakumi ni kwamba, pamoja na mapungufu ya Mwalimu kisera, mengi are justified kwani we have structural weaknesses in our economy, na ndio maana hadi leo serikali imekwama – inapinga ujamaa wa Mwalimu lakini haiji na mbadala wa kweli wa kumuinua mwananchi; na wewe kwa bahati mbaya upo in the same wagon;

Kuhusiana na viwanda naona unalazimisha. Kwa kifupi serikali ya Tanzania ilikuwa haina shughuli ya kufungua viwanda au kufanya umachinga (period).

Kwa kweli, ni wewe ndio unalazimisha, lakini muhimu Zaidi, mtazamo wako sio sahihi na unashangaza kidogo; For any country, industrialization ni muhimu sana kutokana na mambo kama vile high economic returns, greater production, employment linkages and productivity improvement kupitia technological adaptation; Malengo ya Mwalimu na viwanda ilikuwa to disengage from international capitalism kama milivyojadili awali ili tuweze ku gain economic independence (tofauti na mfumo ulioacha na mkoloni) i.e. mkakati wa ku restructure uchumi wetu ambao ulikuwa based in primary commodity that aimed to serve former colonial powers; Zakumi, kwa wakati ule, mtazamo huu ulikuwa na tatizo gani?
Juhudi za industrialization zililenga kwenye processing ya mazao ya kilimo na pia import substitution ya basic industries – hasa viwanda ambavyo vinge promote our capacity kuwa self reliane in industrial production pamoja na viwanda ambavyo vinge fulfill basic needs za binadamu kwa watanzania walio wengi – food, shelter, clothing etc; Viwanda vya namna hii were envisaged not only kuwa the corner stone of our county's industrial structure upon which viwanda vingine vingeweza endelezwa, bali pia kutengeneza linkages muhimu ambazo zinge penetrate katika uchumi kama vile employment n.k;

Mambo hayakuwa mabaya mpaka ilipofikia mid 1970s kama ulivyojadili hapo juu, lakini ni bahati mbaya sana unajadili mapungufu yaliyojitokeza domestically na kupuuza masuala yaliyokuwa yanaendelea in the international scene;

Kulikuwepo na alternative. Wataalamu wa elimu wa ndani na nje walimpa mwalimu model ambayo ingekuza kiwango cha elimu kwa kipindi cha miaka 20. Mwalimu alikataa model hiyo na kutangaza Azimio la Musoma ambalo lilitaka kufuta ujinga kwa miaka saba.

Unaweza kuja na hiyo model waliyopendekeza kwenye sekta ya elimu kisha ufanye analysis ingetusaidiaje relative to mafanikio chini ya sera ya mwalimu?

Vinginevyo katika suala la maendeleo ya uchumi, mwalimu alichukua ushauri wa hao unaowaitia utalaam: Moja ya makubaliano baina ya mkoloni (Britain) na Nyerere ilikuwa ni sisi kuendelea na sera zile zile za mkoloni; Na utambue pia kwamba 5 years development plan adopted in 1962 ilikuwa imeandaliwa na wataalam unaowazungumzia, lakini matokeo yake kiuchumi yakawa disastrous; Nitarudi kujadili hili kwa kina na kwa takwimu, vinginevyo kufeli kwa utaalam huu wan je pamoja na maugomvi makubwa ya cold war yakapelekea external assistance kwa nchi nyingi duniani (including Tanzania) kuanza kukauka; Hapo ndipo Mwalimu akaamua kuja na Azimio la Arusha ambalo liliamsha interest za donors kuliko kipindi cha awalil Nikipata nafasi, nitarudi kujadili haya kwa kina;
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom