Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Zakumi ni ngumu sana mtu kukuelewa unasimamia wapi katika hoja, samahani kusema hivyo.JLF;
Nimeikubali posti yako na hususa ujumbe wa kubadili attitudes za wabongo. Attitude ya sasa ya kuamini kuwa serikali is a gigantic enterprise with unlimited resources ni lazima iondoke. Serikali ni lazima ifanye vitu inavyoweza kuvifanya kwa ufanisi. Kuiongezea serikali mamlaka katika shughuli ambazo haina uwezo nao kwa kisingizio cha kufuta umasikini ni kujiongezea umasikini.
Tukirudi kwenye majibu ya hoja zangu, kuna alternatives. Lakini kila kitu kina gharama zake. Moja ya alternatives ni kutumia mikopo. Nchi inaweza kutumia mikopo kutoka nje kujenga viwanda. Na baadhi ya viwanda vilivyojengwa kati ya 60-80 vilitumia mikopo. Matatizo ya mikopo ni kuongeza deni taifa. Viwanda vinaposhindwa kutimiza majukumu yake ya kurudisha pesa, ulipaji wa madeni na riba unaweza kuiletea nchi umasikini.
Alternative nyingine ni kutumia misaada ya kutoka nje. Misaada mingi ina masharti yake. Na vilevile tukumbuke kuwa wahisani wana watu wengi wa kuwasaidia. Cha muhimu zaidi kuhusu misaada ni donor fatique. Nchi za scandinavia zilitusaidia, lakini zilipochoka zilianza kutushinikiza kufanya reforms.
Mara nyingi hapa tunatoa mifano ya maendeleo ya viwanda ya China na South Korea. Nchi hizi na zingine za Asian Tiger zilikuwa zinategemea sehemu ndogo ya misaada kutoka nje (2%). Na vilevile hawakuwa na uwiano mbaya wa madeni kutoka nje. Hivyo shinikizo la kutoka nje linakuwa dogo.
Hivyo kwa maoni yangu binafsi si vibaya nchi kuanza kwa kutumia resources zake kwanza. Japokuwa mapato yanaweza yasiwe makubwa, matumizi mazuri ya kipato hicho yataleta mafanikio baadaye. Chukua mfano wa Tanzania. Kwa zaidi ya miaka 30 tuna mashule mengi ambayo hayana waalimu wazuri au wa kutosha. Haya ni matumizi mabaya ya kile kidogo tunachopata. Hii ni kwa sababu wahitimu wa shule hizo hawana manufaa ya kuleta mabadiliko.
Kwanza, umeungana na baadhi yetu kwa kusema serikali itoe nafasi kwa sekta nyingine kuchangia uchumi. Ukisoma bandiko la mwanzo kabisa la Mchambuzi hicho ndicho alichokisema. Akauliza je tutumie mkakati gani katika kuinua uchumi? Inward looking au outward looking. Tena kuna mahali ameta private sectors na SME kwa maana ya nje ya serikali
Ukisoma bandiko nililochangia kuhusu hoja hiyo nikasema serikali ijitoe katika utendaji lakini ijenge mazingira mazuri ya private sectors kutekeleza majukumu yake. Nikasema hakuna sababu serikali ikashiriki katika kutangaza utalii, kinachotakiwa ni serikali kuandaa mazingira ya wadau wa sekta husika kushiriki katika kutangaza utalii.
Lakini serikali haiwezi kujitoa kabisa katika majukumu yake. Mfano, balozi zetu zinaweza kutumika kutoa taarifa za maonyesho ya utalii au maeneo yenye potential za kukuza utalii. Serikali iwasiliane na wadau kwa kuwapa fursa kushiriki na kutangaza utalii.
Pamoja na hayo ili private sector ifanye vema lazima kuwe na incentives kwasababu compettition haitegemei maarifa inatgemea mazingira pia. Kwanini tutoe tax break kwa makampuni ya madini tushindwe kutoa tax break kwa kampuni zitakazotangaza utalii na kweli kufanya hivyo. Je hapo serikali haina jukumu.
Zakumi nadhani unajenga hoja za nguvu na siyo nguvu za hoja. Kama ungefuatilia vema historia ungegundua kuwa miradi mingi iliyofanyika kati ya 60 na 70 ilikuwa misaada kwa kuzingatia kuwa kipindi hicho kilikuwa post independence na nchi nyingi zilishiriki.
Kwa viwanda vilivyojengwa kwa mikopo, mikopo hiyo ilikuwa na masharti nafuu na mingi ilirudishwa mapema sana. Mfano, Mchina alijenga Urafiki, mfaransa akajenga Mutex. Kibaha education ilijengwa na msaada, kama ilivyo reli ya Tanga-Dar n.k.Nimeyaona haya.Hivyo hoja yako kuhusu mikopo ya 60 na 70 haina mantiki.
Na mwisho umetuunga mkono tena kwa kusema tutumie rasilimali zetu kuanza kujenga uwezo wetu. Wote wamesema hilo na Mchambuzi kasema je kuna haja ya specialization ya maeneo ya uchumi? Nilichangia kwa kusema ipo na itasaidia kuejenga uwezo wetu hata kuwa na viwanda.
Nikasema kama tuna kipaumbele kuwa fedha za madini ziwekezwe katika elimu, fedha zitokanazo na gasi ziwekezwe katika miundo mbinu na tuongeze mazao ya biashara na chakula, upo uwezekano wa kujenga uwezo wenyewe. Hoja hiyo ndiyo waliochangia akina gfsonwin na zumbemkuu kuwa elimu ni sehemu ya uchumi.
Basically unakubaliana na hoja nyingi sijui wapi lakini kuna wakati unageuka kama nitakavyokuonyesha bandiko lifuatalo
Last edited by a moderator: