Zakumi, haya ni majibu yangu kwa bandiko lako
#18 :
Mkuu
Zakumi,
Its obvious kwamba wewe ndio unaboronga kwani nitajirudia tena: Unaangalia suala zima la industrialization in Tanzania kwa jicho la
Liberalization, Marketization and Privatization, suala ambalo halikuwepo miaka hiyo; Katika dunia ya tatu, main anthem was developmental state ambapo nchi zilijengwa under STATE CAPITALISM (including the current Asian Tigers); Hivi unaelewa jinsi gani mataifa makubwa (yaliyoendelea) yalifanikiwa kufanya hivyo kupitia protectionism? Do you understand anything about the argument for infant industries? Hata hawa asian tigers tunaowajadili hapa, sio kwamba walifungua milango kwa njia ya RUKSA bila mipaka;
Zakumi, You have to wake up and smell the Coffee;
Bila ya wewe kujinasua toka katika giza hili (i.e. kuishi dunia ya
Liberalization, Marketization and Privatization as if it has always been there, kamwe hauta appreciate malengo yaliyokusudiwa chini ya Ujamaa, let alone mafanikio katika maeneo kadhaa; Fanya utafiti uelewe kwanini donors walimiminika kwa wingi in terms of misaada na uwekezaji baada ya kutangazwa kwa azimio la Arusha, na sio kabla ya hapo;
Na hoja yako awali kwamba kilichofanyika Tanzania wasnt something new ni ishara kwamba haufanyi utafiti wa kutosha; Tanzania iliwavutia west na Ujamaa na Kujitegemea kwasababu it was a unique approach: Ujamaa opposed capitalism and shunned Marxism; Kwa wakati ule, kulikuwa na njia kuu mbili za kupiga hatua kimaendeleo kwa nchi maskini: Aidha accelerate integration of your economy into the global capitalist system (the colonial way), of which mkuu
Zakumi, without reservations, unaona hiyo ndio njia sahihi OR, disengage/delink from this system through socialist policies; Again, the fact that Ujamaa opposed Ubepari and at the same time Shunned Marxism ilivutia watu wengi sana, na hata wewe ungekuwa unaishi nyakati zile, hakika usingepingana na hili; tatizo ni kwamba unafanya analysis baadae sana;
Hoja yako juu ya stress test katika nyakazi zile za ujenzi wa taifa na uchumi baada ya maafa ya ukoloni haina mashiko kabisa, kwani again, unaishi katika muktadha ambao haupo sahihi kufanya such an analysis. Naomba nijirudie tena kwamba - hata kwa nchi kama Marekani na Uingereza, Sekta ya Umma ilipewa kipaumbele kuliko sekta binafsi kwa kipindi kirefu sana kufuatia kumalizika kwa vita vya pili vya dunia (1945), na mageuzi makubwa yalikuja letwa na Thatcher (UK) na Reagan (USA); Nini uchambuzi wako wa stress test kwa wenzetu hawa? Kumbuka, hata sekta ya umma kwa mataifa haya ilianza kupata misuko suko, lakini tofauti na sisi, mbali ya wao kuwa na uwezo mkubwa kiuchumi na utaalamu katika masuala ya sera, pia yalipata fursa to reform at their own pace vinginevyo yangeanguka; Mwalimu Nyerere aliomba kufanya the same na ndio maana Tanzania ilikuwa ni moja ya nchi za mwisho kabisa kupokea Structural Adjustment Policies spearheaded by the World Bank and IMF;
Nashukuru umekuja na hoja hii, kwani inapingana na hoja yako ya awali ambayo ulibeza sana viwanda ambavyo wengi wetu tulijadili kwamba vilikuwa na umuhimu licha yaw ewe kuviponda kama viwanda visivyokuwa na maana katika uchumi sigara, bia n.k; Kumbuka, hivi vilikuwa ndio viwanda kwanza kukimbiliwa na wawekezaji, na ndio kwa kiasi vimekuwa bado sustained na ni miongoni mwa tax payers wakubwa nchini; kama alivyojadili
Nguruvi3, viwanda vingine vingi vimeishia kuwa maghala ya kuhifadhia chumvi, na akakuhoji kwanini, huku wewe ukitokomea bila ya majibu;
Hivi kwanini Mkapa alikimbilia kubinaifisisha mabenki yaliyokuwa chini ya umma katika awamu yake? Kwa kiasi kikubwa, wanachofanya wawekezaji ni kilekile kilichokuwa kinafanywa na wakoloni.
Haupo in touch with reality; hata a simple search on google itakueleza kwamba our approach to development chini ya sera ya ujamaa na kujitegemea ilikuwa UNIQUE; Mengine nimejadili hapo juu;
Utafiti niliofanya ni kwamba we experienced growth in the industrial sector late 1960s to mid 1970s ambapo mchango wa sekta hii kwa pato la taifa (GDP) ulifikia peak ya 13%;
Hapo awali ulikuja na takwimu zisizo sahihi kwamba hatujawahi kuwa na mchango wa sekta hii kwa GDP ya Zaidi ya 7%; Kwahiyo nukuu yako hapo juu kuhusu uzalishaji wa sekta mbalimbali kuanza kuborongo in mid 1970s ni sahihi, na ndio maana STATE CAPITAL ikadumaa, lakini sio kabla ya hapo;
Hivi kweli unaelewa role of Foreign AID katika maendeleo ya nchi kama South Korea?
Ni kweli kwamba uzalishaji na matumizi yetu havikulingana; Lakini jiulize why? Ni kwa sababu (na hii ipo all over the development literature Tanzania ilijaribu to capture the peasants without coercion; Nchi nyingi zilizofanikiwa na viwanda, hata Britain, walifanya kinyume; Rejea matukio ya enclosure system ambayo ilikuwa ni very chaotic; Ni baadae sana Mwalimu akashawishika kufuata approach hii pale alipoanzisha vijiji vya ujamaa kwa nguvu, lakini baada ya muda mfupi, he abandoned this strategy kwani pia ikawa counterproductive; So capturing peasants (kisera) ikawa tatizo, na not capturing peasants (kisera), inaendelea kuwa tatizo hadi leo; So hoja yako kuhusu matumizi kuwa makubwa kuliko vipato ni kwa sababu Mwalimu ilibidi atumie method nyingine, hasa ile ya kuwashawishi to engage in production of marketable surplus in exchange of free social services (elimu, afya, maji
); Hii ikapelekea failure to produce a marketable surplus; Hoja ya msingi hapa mkuu
Zakumi ni kwamba, pamoja na mapungufu ya Mwalimu kisera, mengi are justified kwani we have structural weaknesses in our economy, na ndio maana hadi leo serikali imekwama inapinga ujamaa wa Mwalimu lakini haiji na mbadala wa kweli wa kumuinua mwananchi; na wewe kwa bahati mbaya upo in the same wagon;
Kwa kweli, ni wewe ndio unalazimisha, lakini muhimu Zaidi, mtazamo wako sio sahihi na unashangaza kidogo; For any country, industrialization ni muhimu sana kutokana na mambo kama vile high economic returns, greater production, employment linkages and productivity improvement kupitia technological adaptation; Malengo ya Mwalimu na viwanda ilikuwa to disengage from international capitalism kama milivyojadili awali ili tuweze ku gain economic independence (tofauti na mfumo ulioacha na mkoloni) i.e. mkakati wa ku restructure uchumi wetu ambao ulikuwa based in primary commodity that aimed to serve former colonial powers;
Zakumi, kwa wakati ule, mtazamo huu ulikuwa na tatizo gani?
Juhudi za industrialization zililenga kwenye processing ya mazao ya kilimo na pia import substitution ya basic industries hasa viwanda ambavyo vinge promote our capacity kuwa self reliane in industrial production pamoja na viwanda ambavyo vinge fulfill basic needs za binadamu kwa watanzania walio wengi food, shelter, clothing etc; Viwanda vya namna hii were envisaged not only kuwa the corner stone of our countys industrial structure upon which viwanda vingine vingeweza endelezwa, bali pia kutengeneza linkages muhimu ambazo zinge penetrate katika uchumi kama vile employment n.k;
Mambo hayakuwa mabaya mpaka ilipofikia mid 1970s kama ulivyojadili hapo juu, lakini ni bahati mbaya sana unajadili mapungufu yaliyojitokeza domestically na kupuuza masuala yaliyokuwa yanaendelea in the international scene;
Unaweza kuja na hiyo model waliyopendekeza kwenye sekta ya elimu kisha ufanye analysis ingetusaidiaje relative to mafanikio chini ya sera ya mwalimu?
Vinginevyo katika suala la maendeleo ya uchumi, mwalimu alichukua ushauri wa hao unaowaitia utalaam: Moja ya makubaliano baina ya mkoloni (Britain) na Nyerere ilikuwa ni sisi kuendelea na sera zile zile za mkoloni; Na utambue pia kwamba 5 years development plan adopted in 1962 ilikuwa imeandaliwa na wataalam unaowazungumzia, lakini matokeo yake kiuchumi yakawa disastrous; Nitarudi kujadili hili kwa kina na kwa takwimu, vinginevyo kufeli kwa utaalam huu wan je pamoja na maugomvi makubwa ya cold war yakapelekea external assistance kwa nchi nyingi duniani (including Tanzania) kuanza kukauka; Hapo ndipo Mwalimu akaamua kuja na Azimio la Arusha ambalo liliamsha interest za donors kuliko kipindi cha awalil Nikipata nafasi, nitarudi kujadili haya kwa kina;