Uchumi wa Tanzania: Je, Ni Kitendawili au Ni Mazingaombwe Kwa Maskini?

gfsonwin

Nitakujibu lile uliloniuliza;

Tatizo la Kariakoo sasa hivi ni matokeo ya mchanganyiko wa rushwa na kukosekana kwa utawala wa sheria. Kwa muda mrefu kodi zilikuwa zinalipwa kwa kukadiriwa na afisa kodi ambaye anamuomba mfanya biashara amkatie 25% ya kodi halisi, halafu ailipe serikali 25% na yeye mfanyabiashara kusevu 50%. Kwa hiyo wafanyabisahara wengi hawakuzowea kulipa kodi; rushwa ilishawaharibu. Vile vile ni tatizo la kukosekana kwa utawala wa sheria kwa vile wamezowea kuwa wanaweza kukaidi sheria bila madhara yoyote yale. Tatizo ni pale serikali inataka kuwekza udhibiti sehemu moja na kuacha mapengo sehemu nyingine. Inatakiwa utawala wa sheria unform kwa wote katika skta zote.
 
Last edited by a moderator:

Neo-Nyerere AKA Mchambuzi;

Ni wewe unayesema kuwa naangalia industrialization kwa kutumia darubini ya Liberalization, Marketization and Privatization. Hayo ni maneno yako. Sikuzaliwa nikiwa nimeshikilia hiyo darubini. Nilianza kwa kuamini nguvu ya viwanda. Na kushindwa kwetu kulinifanya nijiulize kwanini? Kwanini wengine wanafanikiwa na sisi tunashindwa. Majibu niliyopata yanaonyeshwa kuwa kuna external and internal factors. Hatuwezi control external factors. Lakini tunaweza kuangalia internal factors. Hivyo darubini yangu imejengwa kwa kuangalia internal factors zetu na kuzilinganisha na internal factors za nchi kama USA, Japan, na China. Ukweli wa mambo hatukuwa na mazingira ya kufanya industrialization.

Mchumi anaweza kusema kuwa South Korea na China ziliendelea kwa sababu walijenga viwanda. Hivyo tukijenga viwanda Tanzania, Tanzania nayo itaendelea kama South Korea au China. Mwanasiasa anaweza kusema kuwa Marshall Plan ilisaidia ujenzi wa Ulaya baada ya vita vya pili vya dunia. Hivyo tuki-apply Marshall Plan katika nchi za kiafrika, nazo zitaendelea.

Ideas kama hizi zinatengeneza sauti kusikiliza lakini the devil is in detail. Uchumi ni eco-system. Ni wajibu wa kiserikali, iwe ya kijamaa au kipebari, kuna nurture hiyo eco-system. Ni lazima serikali iwe na capability na vilevile utamaduni wa kuwajibika.

Kwa maoni yangu katika miaka ya 60, 70 na 80 hatukuwa na capability na utamaduni wa kuwajibika. Yoyote anayesema kuwa tulikuwa tayari anaongopa. Katika kipindi cha sasa capability hipo lakini hakuna utamaduni wa kuwajibika.
 
Mimi ningependa kuchangia kidogo katika uchumi wa Tanzania.

Nisingependa kurejea nyumba kwenye makosa makubwa yaliyofanywa kiuchumi na viongozi waliopita. lakin kubwa kwa sasa na kuwaandaa watu kwa kuwapa ilmu ya uchumi, Utii wa sharia ni muhimu sana na hili litaondoa ile dhana ya kulindana na kuoneana aibu, Kuweka mipango madhubuti ya kukuza uchumi na wa Tz kuwa na uzalendo na mapenzi ya dhati kwa nchi yenu. Kisha kuweka sera nzuri ambao wengi mumezichambua katika mada hii.

Kwani bila hiyo foundation. hamtaweza kuendelea hata kidogo.


Nitapita baadae baada ya kusoma zaidi michango ya wanaukumbi
 
Mkuu gfsonwin,

Bandiko #115 umeleta suala muhimu sana ndani ya mjadala; Ningependa kulijadili briefly, na kwa mtazamo tofauti kidogo:

Kwa mtazamo wangu ambao pengine ni finyu, kinachoendelea ni ishara kwamba kuna existence of injustice tax system in Tanzania; Pengine tuangalie, je nini umuhimu wa taxation kwa taifa?

Taxation inatakiwa kutusaidia kama taifa - to link solidarity from local level (jamii) all the way to the national level (serikali); Kupitia uhusiano huu, kunakuwa na majadiliano na mashauriano (negotiations) kupitia "social contract" ambayo inaweka wazi haki na wajibu wa serikali (state) kwa raia, na raia kwa serikali; katika muktadha huu, unagundua kwamba kumbe "Tax is supposed to be Distributed Wealth, not just Government Money; Hali hii isipokuwepo, matokeo yake ni resistance, non – compliance on part of tax payers; Kwa Tanzania, KODI is government money, not distributed wealth;

Mkuu gfsonwin, fiscal-social contract niliyojadili hapo juu ni litmus test kubaini iwapo there is representative government kwani taxes connects rights to reality; Bila ya mapato ya kutosha, haki za raia kama vile usalama, afya, elimu, maji, n.k vitabakia kuwa ndoto; Lakini tunapozungumzia mapato – a just tax system lazima ikusanye mapato kutoka vyanzo vyote – income taxes, capital gains, property, royalties from extractive industries, financial transactions n.k; A just tax system must treat walipa kodi wote equally and fairly – locals, multinationals according to similar rates na kutoza all sources of income ili kutengeneza a level playing field; Kwa Tanzania, kuna matatizo katika fiscal-social contract, na pia tax payers are not treated equally and fairly;

Solution ni kwa serikali kuhakikisha kwamba perception ya wananchi inageuka kutoka imani kwamba "KODI NI FEDHA ZA SERIKALI, na kwenda kuwa KODI IS ALL ABOUT WEALTH DISTRIBUTION; Kuna njia nyingi za kufanikisha such a redistribution lakini kuu ni pamoja na hizi zifuatazo:

1. Uwepo wa progressive tax rates ambapo wealthier individuals should pay more and vice versa…
2. Kodi itumike kutoa universal access to public goods ambazo Zakumi amezijadili hapo awali, hasa elimu, afya, maji ili kuondoa matabaka yaliyopo sasa ambapo wenye nacho na wasicho nacho wanatumia huduma zisizofanana;
3. Pia serikali ije na scheme itakayosaidia mikopo ya wanafunzi kwa wale wanaostahili, soft loans za ujasiriamali kwa wale wanaostahili, and income grants kwa wale wanaostahili, sio kwa mtindo wa sasa ambapo mikopo kwa wanafunzi na mabilioni ya Kikwete yanaenda kwa wajanja wachache; Hali hii inaumiza sana wananchi kwani kimsingi, hiyo ni kodi yao;

Yakifanyika haya na mengine muhimu, tutafanikiwa kuja na a just tax system na kutatua matatizo ya resistance and non-compliance;
 
Mkuu ondoa hilo la Mkandata kukubishia maana binafsi yangu namuunga na namuelewa sana Nyerere alichotaka kufanya miaka ya 70 japo watu wengi wameshindwa kuelewa outside forces zilivyokuwa vikitupiga vita WAJAMAA..

Ni nguv hizi hizi zilizomweka Mandela na viongozi wote wa ANC ktk list ya ma - Terrorist, hawa hawa hawa waliomwita Magret Thatcher Iron lady kwa sababu ya siasa zake dhidi ya nchi maskini na pengine niseme Reagan apewe sifa zaidi kwa kueneza sera za BUY AMERICAN brand nyumbani wakati wao wanauza mali nje. UKikataa kuitamvua Israel unawekwa ktk kundi la black list hata kama!..yaani miaka ya 70 SIASA ilichafua nchi zote za KIJAMAA kama unavyoona leo ktk nchi za KIARABU.. Huwezi kusema Mfalme wa Saudia ni mzuri ama ana sera nzuri kuliko AhmadinaJad wa Iran pasipo kuzingatia jinsi siasa zinavyotumika kudhoofisha uchumi wa nchi moja na nyingine kukua japo hawana sera nzuri wala Utawala bora.

Will always stand with Mwalimu Nyerere, sema tu nakubali kwamba alifanya makosa makubwa sana kukabidhi nchi kwa wahuni, Nyerere alikuwa na mapungufu makubwa ktk kuwasoma WANAFIKI na malimbukeni hasa baada ya kuingia UBEPARI maana hatukuuzsoma kaa tulivyouzoma UJAMAA..Na ssidhani kaa hadi leo kuna mwanasiasa yeyote nyumbani amewahi kuandika kitabu kuhusu UBEPARI na ukafundishwa mashuleni kama tulivyosoma UJAMAA..Sasa nambieni nyie wasomi uytaweza vipi ku apply elimu zenu ktk somo ambalo hamkulisoma na kujua jinsi mazuri ya UBEPARI na jinsi utakavyo fanya kazi zaidi ya kujua UBAYA wake tu kulingana na mafundisho ya UJAMAA?
 
Last edited by a moderator:
gfsonwin , kuna mambo nimeacha hata kuhoji kwasababu kila nikiuliza sipewi majibu yanayolingana na maswali.

Kuhusu hoja zako, nimeahi kuuliza hivi hawa wasomi tulio nao wamefanya nini ambacho tukiweka katika mizani tunaweza kuona tofauti kati ya sasa na zamani. Hakuna jibu.
Nimehoji kama sera za mwal kuhusu viwanda zilikuwa mbovu, zipi za sasa ambazo ni mbadala mzuri. Hakuna jibu

Nimehoji unawezaje kuuza pamba ikiwa na magugu ili hali huna hata 'jineri' za kusafisha hiyo pamba? Nikajibiwa tuuze malighafi tu. Nikahoji hivi mchanga unaosafirishwa nje ndio uuzaji wa mali ghafi, hakuna jibu.

Nimehoji kama mwalimu alikosea kuanzisha viwanda na waliofuata wakaamu kuuza, nini matokeo ya uuzwaji wa viwanda hivyo? Je, kuvigawa viwe maghala ya chumvi ndio njia bora kuliko kile kilichofanyika, hakuna jibu.

Tunapoangalia viwanda tunaangalia katika monetary value na kusahau faida nyingine zitokanazo.
Hata kama pato lilikuwa dogo kuliko misaada, sasa hivi ni miaka 30 tangu amendoka Mwl na miaka 50 ya uhuru ,kuna tofauti gani ya misaada ? Na je ile 10% ya viwanda vya mwl inapatikana wapi kwa sasa?
Au ndio kuweka kodi kwa vocha za simu kukifanwya na maprofesa ndio uchumi endelevu baada ya mwalimu!

Hapa pia pana underline hoja ya skilled labor inayohitajika na ni sehemu ya uchumi. Je, tunahitaji skilled labor kama ya kuchaji kodi katika vocha ya simu. Hivi miaka 30 tangu mwl aondoke hakuna anayefikiria chanzo kingine cha kodi zaidi ya sigara, bia na vocha za watoto wa sekondari! ndio skilled labor tofauti na ya mwl hiyo.

Nikirudi katika viwanda, maendeleo ya jamii yalitegemea sana viwanda vya mwl. Mji wa Mang'ula kama mfano ni matokeo ya viwanda.

Mwanza ilijengwa sana na Mwatex kwa 'trickle down effect' kuanzia kiwandani hadi kwa mkulima.
Mji kama wa Moshi ulikuwa 'live' 24 hr kwa treni kufanya kazi za kuchukua na kupeleka bidhaa.

Morogoro imekuwa kwa viwanda kama Maturubai, Polyster n.k. Arusha ilikuwa vivyo hivyo.
Dar watu walikuwa na shift work siku hizi baada ya 11 jioni ni viti virefu. Nani utamsikia amekwenda shift.

Enzi hizo wanafunzi walikwenda katika viwanda kufanya tempo.
Lakini kubwa zaidi ni wanafunzi kupata uzoefu wa kuingia katika labor force wakiwa na nidhamu za kazi.

Siku hizi mwanafunzi wa chemical engineering au mechanical sijui anafanya internship au field work wapi.
Hata wale wa utawala na uongozi, wahasibu n.k wamebaki kukimbizana katika serikali na kujifunza bureacracy na si skilled labor kama wanavyodai.

Tumeua general tyre na sasa tunaagiza matairi ya mitumba kutoka Uarabuni. Kama ni mapya ni kutoka China, wakati zao la mpira linakufa Tanga. Huo ndio tunaita usomi wa kileo na kuuza malighafi nje. Ipi hiyo?

Niseme impact ya viwanda ukiiweka katika pesa tu huwezi kuiona. Ukiiweka katika uchumi na kijamii ni kubwa kuliko tunavyodhani. Hatuwezi kuona faida hizo kwasababu tume ji tune kumtuhumu na kumhukumu mwl tukisoma karatasi kwa makengeza tena tukiruka kurasa. mwisho tunasema 'verdict- mwalimu is guilty of all 400 counts'

Tukiuliza wapi mbadala ili tuweze kupata hukumu ya haki kwa mwalimu, tunajibiwa ' hiyo si kazi yetu' kazi yetu ni kuonyesha makosa ya 'mhaini' Nyerere.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi napitia hoja za bandiko lako #124 kuhusu kodi kidogo.
Kwamba kuna injustice tax system in Tanzania, hilo halina mjadala. Anayelipa kodi Tanzania ni yule asiyeweza kukwepa kama wafanyakazi wa serikali, wafanyabiashara wenye shughuli za uzalishaji n.k.

Injustice inatokana na tax evasion ambayo ni zao la corruption na irresponsible government.
Wanaofaidika ni wafanyabiashara ambao hutegemewa kupeleka kodi tofauti na anayechinjwa katika pay slip.
Mfanyakazi anabeba mzigo wote wa tax evasion na tax exemptions ambazo zote hazijaleta tija kwa nchi.

Namtetea Mtanzania anayeona kodi ni pesa za serikali. Hivyo ndivyo ilivyo kwasababu mtanzania wa kawaida haoni kodi yake inafanya nini.

Hakuna mahali anapoweza ku justify matokeo ya kodi yake. Ukienda vijijini watu wanasema tutafute mfadhili wa kufanya ABC. Wanaamini anayesaidia japo kuziba mashimo ya bara bara ni mfadhili na si serikali yao.

Namtetea Mtanzania kwasababu inapotokea bilioni 27 zikatoka hazina na serikali haijui zimetokaje na nani ametoa, kuna sababu gani za kudhani kodi anayolipa mtu inahifadhiwa na kutumika kama ilivyo kusudiwa?

Ili kundilisha mtazamo wa wananchi kuhusu kodi ni lazima waone zinafanya kazi gani katika 'public goods'
Sidhani kuwa kuna sababu za progressive tax rate.

Tatizo lipo katika corruption na irresponsible government.
Kwanini tuwe na progressive tax rates tukisahau embezzlement and mismanagement inayotaokana na serikali.

Kuna sababu gani za kuweka kodi zaidi kwa wealthier wakati kodi hizo zinatoka hazina hadi Uingereza bila mtu kujua na hata zinaporudi hakuna anayejua zimerudishwa vipi.

Kuna sababu gani ya kuweka progressive tax rate itakayotupatia billion 500 wakati kuna tax evasion bandarini inayokadiriwa kuwa 1.8 trillion.

Hoja hapa ni kuwa kwanini tukazane kujaza ndoo maji wakati tunajua inavuja.
Je si vema kuanza kuziba kwanza!

Kuhusu serikali kuja na mikopo laini kusaidia wanafunzi, hili nasema ni 50/50.
Linaweza kuwa kama la mabilioni ya JK ambayo sijui kama yametoa matokeo yoyote ya kiuchumi.

Nadhani serikali ingeshirikiana na taasisi ku identify potential area ambazo zikipewa mikopo zinaweza kuwa exemplary and sustainable

Kwa mfano, kwanini serikali isiachie taasisi zijiendeshe zenyewe huku ikitoa mikopo laini.
Nakumbuka Kibaha education centre ilikuwa mfano mzuri sana wa shughuli za ujasiria mali.
Kwa bahati mbaya ilikuwa ni sehemu ya serikali na hivyo kuwa katika bureaucracy ndio maana haifanyi vizuri.

Kwanini,Mlingano Tanga, Ukiliguru, Uyole, Naliendele zisiwe taasisi nje ya serikali na zikapewa kazi ya kuendeleza kilimo kwanza kwa mifano huku serikali ikijenga mazingira ya kufanikisha miradi hiyo bila kujiingiza katika uendeshaji wake.

Katika nchi za wenzetu research and development zinafanywa na taasisi .
Hata kama kutatoke individuals bado wanatakiwa wategemee taasisi katika kujiendeleza.

Kilichotakiwa kufanywa ni serikali kuwatumia wataalamu na taasisi zao kuja na policy ambazo zinafanya kazi zikiwa na planning, orientations, pilot studies na verifications.

Waambie SUA kuwa tunahitaji kilimo kwanza. Nini kifanyike, kwa njia zipi, changamoto ni zipi na wapi serikali isaidie kwa maana inapobidi. Halafu wape jukumu ukisubiri matokeo 'big results'
Anayeshindwa anawekwa pembeni.

Sidhani kama kilimo kwanza ni suala la mtu kusimama bungeni na kusema tu.
Matokeo ya mipango hiyo hovyo ni kuingiza matrekta substandard, kuwapa watu bila elimu au uwajibikaji kwasababu ni mali ya umma n.k.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu nimepata kipande hiki kutoka gazeti la the Citizen.
Mkapa, Mogae na Obasanjo wakizungumza.

Haya ni baadhi ya maneno ya Mogae ambayo tumeyajadili huko mwanzo kama mada ya Mchambuzi inavyoeleza.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…