SoC04 Uchumi wa vyombo vya habari katika wakati huu wa maendeleo ya Teknologia ya habari na mawasiliano

SoC04 Uchumi wa vyombo vya habari katika wakati huu wa maendeleo ya Teknologia ya habari na mawasiliano

Tanzania Tuitakayo competition threads

HARUNI IDDI

Member
Joined
May 31, 2024
Posts
8
Reaction score
3
Uchumi wa vyombo vya habari katika wakati huu wa maendeleo ya Teknologia ya habari na mawasiliano. Vyombo vya habari, kama vile vituo vya redio, magazeti, vituo vya runinga, vimekuwa vikipitia wakati mgumu katika wakati huu wa mapinduzi ya kidigitali hasa kuibuka kwa mitandao ya kijamii, kama Facebook, YouTube, Instagram na X kwa namna fulani vimepunguza mapata ya vyombo vya habari kupitia matangazo ya biashara ambapo watu wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara na matukio mbalimbali ambayo yalikuwa yanatolewa na vyombo vya habari.

ZIFUATAZO NI NJIA AMBAZO VYOMBO VINAWEZA KUJIPATIA KIPATO WAKATI HUU WA MAPINDUZI YA KIDITALI

1. Kujikita katika habari za uchunguzi.
Ili vyombo vya habari viweze kupendana na mabadiliko ya tehama vinapaswa kujikita katika habari za uchunguzi na kuibua mambo mbali yanayi ikumba jamii iliwatu waweze kufuatilia vyombo vya habari nakuachana namitandao ya kijamii.

2. Kushawishi serikali kufanya kazi na vyombo vya habari kujulisha umma maovu na mafanikio ya serikali kwa wananchi.
Ili vyombo vya habari viweze kupata mapato wakati huu wa mapinduzi ya kidigitali ambao kuna mitandao ya kijamii vinapaswa kuwa karibu na Serikali ili kupata matangazo ya kutosha ili kuweza kukuza uchumi wa vyombo husika.

3. Mamlaka kupunguza gharama za leseni undeshaji wa vyombo vya habari.
Ili vyombo vya habari viweze kujiendesha kwa faida na kuweza kuwa na uchumi ambao utaviwezesha kulipa wafanyakazi, mamlaka kama mamlaka ya Kodi (TRA) na mamlaka ya mawasiliano Tanzania ( TCRA).

4. Vyombo vya habari viajiri watu wenye fani & ubunifu na ujuzi kwenye maswala ya habari na utangazaji.
Kutokana na vyombo vya habari hapa nchini kujikita katika kugombania wandishi wenye majina makubwa na watu maarufu badala ya kutafuta watu wenye ubunifu na ujuzi kwenye maswala ya habari ilikuleta mawazo mapya hasa katika kupata vyanzo vipya vya mapato.

5. Vyombo vya habari vinapaswa kupendana na mabadiliko na mahitaji ya jamii.
Ili vyombo vya habari viweze kujenga uchumi ulivo Bora vinapaswa kwenda na mabadiliko ya tehama ili kupata mapato ikiwemo kuanzisha kurasa katika mitandao ya kijamii kama youtube whatup na n.k nakuacha kutegemea matangazo kama chanzo kikuu Cha mapato pekee.

Katika miaka mitano ijayo na kuendelea mbele vyombo vya habari vinapaswa kutafuta vyanzo mbadala vya mapato ili kuendena na gharama za undeshaji na mabadiliko ya tehama.
 
Upvote 2
Kushawishi serikali kufanya kazi na vyombo vya habari kujulisha umma maovu na mafanikio ya serikali kwa wananchi.
Ili vyombo vya habari viweze kupata mapato wakati huu wa mapinduzi ya kidigitali ambao kuna mitandao ya kijamii vinapaswa kuwa karibu na Serikali ili kupata matangazo ya kutosha ili kuweza kukuza uchumi wa vyombo husika.
serikali ukitaka kushirikiana nayo inakununua
 
1. Kujikita katika habari za uchunguzi.
Ili vyombo vya habari viweze kupendana na mabadiliko ya tehama vinapaswa kujikita katika habari za uchunguzi na kuibua mambo mbali yanayi ikumba jamii iliwatu waweze kufuatilia vyombo vya habari nakuachana namitandao ya kijamii.
hili ndio muhimu
 
Kujikita katika habari za uchunguzi.
Ili vyombo vya habari viweze kupendana na mabadiliko ya tehama vinapaswa kujikita katika habari za uchunguzi na kuibua mambo mbali yanayi ikumba jamii iliwatu waweze kufuatilia vyombo vya habari nakuachana namitandao ya kijamii.
Hizi habari ninazipenda sana, si ndio wanaita documentary eeeeh, au unamaanisha makala.

Sasa hapo inabidi pia uwe na jamii inayotaka kuelewa, inayopenda kujifunza.

Vyombo vya habari vinapaswa kupendana na mabadiliko na mahitaji ya jamii.
Ili vyombo vya habari viweze kujenga uchumi ulivo Bora vinapaswa kwenda na mabadiliko ya tehama ili kupata mapato ikiwemo kuanzisha kurasa katika mitandao ya kijamii kama youtube whatup na n.k nakuacha kutegemea matangazo kama chanzo kikuu Cha mapato pekee.
Vijitathmini na viongeze ubunifu kona zote
 
Back
Top Bottom