Uchungu wa Polepole kuhusu Haki, Demokrasia na Utawala bora unatoka wapi?

Ni kweli hao ndo walikuwa core architects wa kuasisi mambo ya hovyo. Tunawezaje kumwamini kwa sasa?????
ni ngumu sana kumuamini vinginevyo kama ameamua kujitenga na serikali, Basi hata chama chake anatakiwa ajitenge nacho atafute chama kisichokuwa na doa akikosa aanzishe chama chake akishindwa ni vyema achane na siasa kabisa kabisa.
 
Mjinga Mmoja wee, Mnataka kutumia Jina la JPM kuhalalisha Udhalimu wa Serikali hii ya Samia??
 
Nimekuelewa japo kidogo. Kwa nini usifikiri katika angle nyingine kuwa anataka amsikilize bi mkubwa ataongea nini ili naye arushe missile sahihi na inayoweza kupiga target.
 
Hakuna atakachokiongea kesho cha maana yaan issue yake ishapoteza mvuto bora angekaa kimya tu aendelee na issue zingine maana ishaeleweka anaenda kuongea nini, guts za kumchana rais on public km alivyomchana kwenye barua hana anaenda kutubu
Ulioteshwa ndoto kuwa Polepole Anaenda kutubu. ???

Kapoteza mvuto kwako au kwa nani??
 
KAMA POLEPOLE ANATAKA KUTUBU WATANZANIA WOTE WATAMUELEWA,LKN KAMA SIO HILO NI UPUUZI TU WA AINA NYINGINE,KAMA NI MFUMO wa utekaji Polepole ni muasisi,kama ni kupoteza watu Polepole ni muasisi,kama ni kunyima watu haki zao Polepole ni mm muasisi,kama ni wizi wa kura Polepole ni muasisi,na hawa waliopo CCM wanaendeleza kilichoandaliwa na Hamphrey Polepole sasa anataka kutubu,Ngoja tumsubiri tuone anataka kusema nini.
 
ni ngumu sana kumuamini vinginevyo kama ameamua kujitenga na serikali, Basi hata chama chake anatakiwa ajitenge nacho atafute chama kisichokuwa na doa akikosa aanzishe chama chake akishindwa ni vyema achane na siasa kabisa kabisa.
Mtu mwenye dhamira ya kweli ni yule anayejiondoa kwenye mfumo ule na kuingia kwenye mfumo rasmi wa kupinga maovu ya chama na serikali yake.

Unawezaje wewe kujitenga na maovu ili hali ukiwa unaendelea kuishi na waovu walewale ndani ya nyumba moja???
 
Mjinga Mmoja wee, Mnataka kutumia Jina la JPM kuhalalisha Udhalimu wa Serikali hii ya Samia??
Wewe ndo mjinga hata usiyejua unachokiongea.

Unawezaje kumtofautisha mwendazake na Hangaya ili hali wote ni waasisi wa matendo ya hovyo ndani ya serikali yao?

Muasisi wa uchafu wote huu unaoendelea ni huyo mwendazake na Hangaya akiwa makamu.
 
Mtu mwenye dhamira ya kweli ni yule anayejiondoa kwenye mfumo ule na kuingia kwenye mfumo rasmi wa kupinga maovu ya chama na serikali yake.

Unawezaje wewe kujitenga na maovu ili hali ukiwa unaendelea kuishi na waovu walewale ndani ya nyumba moja???
sawa sawa
 
Aliyekuwa sehemu ya tatizo na muasisi wa tatizo eti anataka kutatua tatizo alilolitengeneza mwenyewe. Ni maajabu zaidi ya yale ya Musa.
 
Sasa hivi upinzani dhidi ya Samia ni mkubwa kuliko upinzani dhidi ya CCM. Kuna dalili kuwa hata chamani CCM ana upinzani mkubwa.

Chadema wanakoleza moto huo kwa kuonesha kuwaunga mkono akina Gwajima, Polepole, Majaliwa na wengine wanaodhaniwa kuwa ni miongoni mwa wasioridhishwa na mambo ndani ya CCM.

Sauti za kutaka Samia asigombee zinasikika. Tujaalie hatagombea tena. Hii inatosha kuwafanya wapinzani warming CCM imebadilika na siasa zitaendeshwa kwa misingi ya haki?
 
Hata wewe mleta mada siku ukichoka kumuabudu shetani na matendo yake ukaamua kumrudia Mungu na ukatubu kabisa, na ukaanza kuzichukia dhambi ulizowahi kushiriki na kuwachukia wanaoziendeleza... mbona utasamehewa kwa haraka sana.

Tatizo mnataka kwa vile mtu aliwahi kuwa upande wa shetani, basi aendelee kuwa kwa shetani tu milele.
 
Wanasiasa wanajua kucheza na akili zetu wananchi.
Katika zile kete mbili zilizokuwa zimebakia moja ndo imebaki kusukumwa.

Upinzani kushika dola ardhi hii bado ni ngumu sana.
Watu wanapotezea upepo sisi tunaona ndo wanatukomboa.
 
Na sisi tunataka tujue kama kweli katubu dhambi zake ili tumsamehe na tuone kuwa ana dhamira ya kweli.

Tatizo hatujaona kutubu kwake mbele ya Askofu au Padre au hata kukiri na kuomba radhi kwa umma kushiriki matendo ya hovyo na kuyatetea huko nyuma.

Tukiona hayo tutaamini ana dhamira ya kweli tutamuunga mkono.
 
Polepole uzalendo wake uliishia kwenye kukusanya maoni ya wananchi juu ya katiba mpya.Baada ya hapo amekuwa akifurahi demokrasia kuvunjwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…