Uchungu wa Polepole kuhusu Haki, Demokrasia na Utawala bora unatoka wapi?

Polepole uzalendo wake uliishia kwenye kukusanya maoni ya wananchi juu ya katiba mpya.Baada ya hapo amekuwa akifurahi demokrasia kuvunjwa
Hilo hatuna ubishi nalo kabisa.
 
.

Tukiona hayo tutaamini ana dhamira ya kweli tutamuunga mkono.
Kitendo tu cha yeye kuonesha ujasiri wa kuukataa utawala wa kizandiki wa Bi chura kwa sababu ya mambo mengi ya ovyo yanayofanywa na uongozi tena akiweka wazi kabisa kinaonesha ana dhamira ya dhati na anatamani siku moja tuwe na taifa bora.

Humphrey kafanya kitu ambacho nyie machawa na baadhi ya wapinzani mnaogopa kufanya, najua kuna baadhi yenu hata nyie machawa hamfurahishwi na mienendo ya serikali hii kandamizi iliyojaa unyanyasaji wa akila aina, ila hamna ujasiri wa kusema wala kujiweka kando na uozo wake.
 
Na sisi tunataka tujue kama kweli katubu dhambi zake ili tumsamehe na tuone kuwa ana dhamira ya kweli.

Tatizo hatujaona kutubu kwake mbele ya Askofu au Padre au hata kukiri na kuomba radhi kwa umma kushiriki matendo ya hovyo na kuyatetea huko nyuma.

Tukiona hayo tutaamini ana dhamira ya kweli tutamuunga mkono.
tena kwa kuongezea hapo aondokane na kikundi hcho..
 
CCM ivyo vitu kwenu ni mwiko KABISA.
KAZI ni kipimo cha utu
 
Nimekuelewa japo kidogo. Kwa nini usifikiri katika angle nyingine kuwa anataka amsikilize bi mkubwa ataongea nini ili naye arushe missile sahihi na inayoweza kupiga target.
Hakuna kufikiri kwa angle nyingine kilichopo ndio hicho kwamba kesho anakuja kutubu sio kuongea chochote kwa hio subiri umuone slow slow akitubu kwenye public hatokuja kusema km alivyoandika, kumbuka aliejiuzuru spika wa bunge baada ya kubutua alirudi kutubu sio kusimamia kile alichokisema kwamba tunakopa sana badala yake alitubu mbele ya camera, km kweli alitaka leo iwe leo na alilenga leo angesema leo ukiona imepigwa u-turn ooh nitasema kesho jua tayari mkia ushafyata kesho ni sala ya toba
 
Wewe ni mganga wa kienyeji au mtabiri wa nyota?. Kwamba unajua hadi atakachoongea na mnatulazimisha tukuamini. Serious!!!!!
 
Kitendo tu cha yeye kuonesha ujasiri wa kuukataa utawala wa kizandiki wa Bi chura kwa sababu ya mambo mengi ya ovyo yanayofanywa na uongozi tena akiweka wazi kabisa kinaonesha ana dhamira ya dhati na anatamani siku moja tuwe na taifa bora.

Humphrey kafanya kitu ambacho nyie machawa na baadhi ya wapinzani mnaogopa kufanya, najua kuna baadhi yenu hata nyie machawa hamfurahishwi na mienendo ya serikali hii kandamizi iliyojaa unyanyasaji wa akila aina, ila hamna ujasiri wa kusema wala kujiweka kando na uozo wake.
Binafsi sijaona cha ajabu ambacho Polepole alisema ambacho watanzania walio wengi hawakijui.

Watu wengi wamelalamikia haya mambo hadharani ndo maana wanapotezwa, wanateswa na kuuawa kwa sababu ya kupinga maovu yanayotendwa na serikali.

Sasa unataka tumwamini Polepole kirahisi vile bila kujua dhamira yake. Sarakasi zake za kisiasa ndo tuziamini????.

Mtu kama Lissu na wenzake tunawaamini kwa sababu wamepitia magumu sana wakipigania haki, usawa, demokrasia na utawala Bora. Wamemwaga damu zao na wanaendelea kulipa gharama za kutetea haki za watu.
 
Ulitaka afanye nini hili tuamini kuwa dhamira yake ni ya dhati?
 
😀😀😀😀 Asante sana tena sana kwa Clip hii. Maana tumepata picha halisi ya Polepole akiwa kwenye inner core ya watawala.

Nasema asante kwa sababu umeweka kwenye uzi sahihi na umejibu baadhi ya hoja zangu. Umetusaidia kumjua zaidi huyu mtu.

Kiufupi Polepole kwa maneno yake amekula matapishi yake mwenyewe. Sasa mtu kama huyu tumwamini kirahisi tu kuwa ana dhamira safi?????
 
Ulitaka afanye nini hili tuamini kuwa dhamira yake ni ya dhati?
swali zuri kabisa.

1. Ajitokeze mbele ya umma akiri ushiriki wake na awaombe radhi watanzania juu ya makosa na matendo ya hovyo aliyoshiriki na kuyatetea kwenye utawala wa mwendazake

2. Akatubu mbele ya Askofu au Padre juu ya matendo yake ya hovyo aliyoyafanya gizani na hadharani akishirikiana na watawala akiwa mwenezi wa CCM

3. Kama ana dhamira ya kweli na ameona utawala wa sasa wa CCM na serikali yake unaenda kinyume na principle za haki, usawa, demokrasia na utawala Bora ajiondoke CCM kabisa. Akaunganishe nguvu na wapinzani kupinga utawala huu wa kifalme/Kiimla na kidikteta,
 
Hilo hata wewe huna hakika nalo, kwani kavunja sheria gani kwa kuongea?
Hoja yangu ni kwamba usifanye conclusion ya jambo fulani bila kujiridhisha.

Polepole bado hatujamjua kama ana dhamira ya kweli au kuna kitu nyuma yake au ni mambo ya political mileage??

Muda utaongea. Na subira yavuta heri.
 
Hivi karibuni ndugu Polepole baada ya kujiuzuru ubalozi ame-trend sana na kujipatia maujiko (umaarufu) kuwa ni mpigania haki, demokrasia na utawala Bora.

Swali la kujiuliza ni kweli Polepole ana uchungu na mpigania haki, demokrasia na utawala Bora???.

Hebu tujiulize maswali mengine haya tena.
1. Tundu Lissu alipopigwa risasi akipigania haki, Demokrasia na utawala Bora, ndugu Polepole aliwahi kumpa pole Lissu au hata kwenda kumsalimia akiwa hospitali kama ishara ya kumuunga mkono ??

2. Polepole akiwa kama mwenezi wa CCM mwaka 2017 wakati Tundu Lissu alipopigwa risasi, aliwahi kulaani kitendo hicho cha kinyama??? kuonyesha kuwa anakerwa na uvunjifu wa wazi wa haki, demokrasia na utawala Bora.

3. Wakati wa utawala wa kikatiri wa mwendazake, ambao haukuzingatia haki, demokrasia na utawala Bora, huku yeye Polepole akiwa mwenezi wa CCM, mbona hakuwahi kupinga au kulaani utawala ule wa kidikteta na mabavu uliokuwa unavunja haki, demokrasia na utawala Bora ????

4. Wakati wa utawala wa mwendazake mambo ya utekaji, kutesa na kuwaua watu ulishamiri, huku Polepole akiwa Mwenezi, mbona hatujasikia anayakemea kwa nguvu matendo hayo maovu ya kikatiri na kishenzi????. Na hata yalipoendelezwa na utawala wa sasa hadi yakazidi vipimo mbona alikuwa kimya siku zote hatukusikia kuyakemea???

5. Baadhi ya Mbuga za wanyama wamepewa waarabu, bandari kubwa wakapewa waarabu, mapori wakapewa waarabu, viwanja vya ndege wakapewa waarabu. Mbona hatujasikia polepole anapinga mambo haya ya hovyo na ya kuiangamiza taifa.???

6. N.k

Tuendelee kujiuliza maswali ni kweli Polepole ni mzalendo na mwenye uchungu wa nchi yake kama anavyojaribu kujinasibu????

Wakati tunaendelea kujiuliza maswali mengi haya haina maana kwamba mtawala wa sasa anafuata misingi ya haki, demokrasia na utawala Bora, bali yeye kamzidi hata mtangulizi wake kwa mambo ya hovyo tunayoyahoji. Pengine ni kwa sababu alikuwa ni sehemu ya uasisi wa matendo hayo maovu labda ndo sasa anaya-practice vizuri zaidi.
ivi hayo umeandika, kwa akili yako unaona ni ya kumlaumu polepole? tumia akili basi.
 
Mrudishe dada ake mkuu
 
ivi hayo umeandika, kwa akili yako unaona ni ya kumlaumu polepole? tumia akili basi.
Nimetumia akili ndo maana ukasoma na ukaelewa na ikakuingia sawasawa.
 
Back
Top Bottom