Uchunguzi: Jinsi watu wanavyoporwa mali zao baada ya mechi kumalizika Uwanja wa Taifa, huku Vyombo vya Ulinzi na Usalama vikitumbua macho

Ni vijana wa Msimbazi hao, vituko haviishi, kucheza mpira hawawezi wamekimbilia haya, sisi Yanga tunawavumilia kwa mengi sana...
Ila tutafanyaje, ni mtani wetu na hakuna jinsi zaidi aendelee kuwepo tuzidi kumnyanyasa..
 
Muhimbili wamefafanua ya Mlonganzila , mbona Polisi mmenyamazia ya uwanja wa Taifa ?
 
Nilikuwa najaribu kupitia kwa makini hii thread nione huenda ni ya enzi za jk,kumbe lah!Ni ya leo..leo kipindi cha utawala kama huu wanaweza kuibuka wababe wengine keko tu?

Mheshimiwa Kangi Lugora,IGP Simon Sirro,na mkuu wa mkoa wa Dar wapo.Ninachelea kuamini hizi habari.

Ninachojua,kulea makundi ya jinsi hii,ni sawa na kulea ugaidi.Na magaidi huwa hawachakugui.Kuwaacha hawa ni kukubali mtaani kuwe na jeshi la magaidi.

Wakamatwe wote wakalime mpunga,la hawataki,ile kanuni ya asiyefanya kazi asile itumike


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ufupi ni kwamba,

Kwa asilimia kubwa, wilaya ya Temeke sio salama kijamii na kiusalama. Hapo bondeni Puma, punde tu ukitoka mjini ni pa hatari hakuna mfano, katikati hapo ukiwa unaenda Mivinjeni ni pa hatari hakuna mfano.

Hicho kipande chote ukimaliza tu kambi ya Twalipo ukiianza Sabasaba si salama, na huku ukiwa Oryx ni hatari tupu. Hapo njia ya Keko nenda mpaka Kigogo, wanapokezana tu kule, zinaporwa simu kweli kweli na jamaa wanaopakizana kwenye boda boda. Sijui maaskari hawayajui haya!?
 
Karibu sana mkuu
 
Keko yote si salama, kuna vibaka wanajiamini sijawahi kuona. Siku moja tupo kwenye daladala pale Mivinjeni jioni kunakuwa na foleni sana kama unakuja mjini maana barabara huwa inafungwa yanaruhusiwa magari yanayotoka mjini tu. Basi bwana kama kawaida makondo wakifika pale huwa wanafungua mlango na kukaa nje ya gari, siku hiyo walikuja vijana wawili wakiwa na bodaboda wakasimamisha pale na kuingia ndani ya daladala na kuchukuwa simu za abiria waliokuwa wamekaa mlangoni na kusepa fasta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada Leo umeandika vizuri baada ya kuachana na ukibaka keko
Asante kwa taarifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…