Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Cha kushangaza polisi wanapita humo humo kukamata gongoKuna maeneo vibaka wana nguvu kuliko vyombo vya usalama
Cha kushangaza polisi wanapita humo humo kukamata gongo
Ni vijana wa Msimbazi hao, vituko haviishi, kucheza mpira hawawezi wamekimbilia haya, sisi Yanga tunawavumilia kwa mengi sana..." Nitasema Kweli daima fitna kwangu mwiko "
Zikiwa zimesalia dk 30 mpira kumalizika vijana wezi , vibaka na majambazi kutoka Keko Magurumbasi , Keko Mwanga , Keko torori , keko machungwa na baadhi kutoka Chang'ombe husogea karibu na uwanja wa Taifa , wengi hujikusanya kwenye njia panda ya Taifa kwenye maghorofa ya jeshi karibu kabisa na ofisi za Takukuru Wilaya ya Temeke , wakiwa na visu , bisibisi na mapanga , hii haijalishi kama itakuwa jioni ama usiku ( japo kwa usiku hali huwa mbaya zaidi )
Eneo hili limezungukwa na maghorofa ya Jwtz pande zote , na kwa kiasi kuna maghorofa ya NHC , hatua chache kutoka hapo ni Shule ya msingi Mgulani na kambi kubwa ya Jeshi la polisi inayoanzia Kilwa road , eneo hili pia linapakana na chuo kikuu cha DUCE na kambi kubwa sana ya JKT ambako ndio kuna shule ya Sekondari ya Jitegemee , hili si eneo la vibaka wajinga wa kutoka keko kutamba , lakini kwa sasa hali ni kinyume chake , vibaka wanatamba bila wasiwasi wowote ule .
Baada ya mechi kumalizika mtu yeyote mwenye kitu chochote cha thamani iwe pochi , simu , saa au hata cheni akifika eneo hili huporwa , mara kadhaa magari huvunjwa vioo na watu huporwa mali zao huku waporaji wakikimbia kuelekea Keko machungwa kwa kupita katikati ya maghorofa ya jeshi huku wanajeshi na familia zao wakiangalia kwa macho bila kutoa msaada wowote , waporaji na vibaka hawa wakishapora na kujeruhi hupita pia katikati ya Bar ya Inferno na kukimbilia bondeni kupitia Gesti ya Lyimo na kwenda kujificha uwanja wa mpira wa Keko Juu ambao ni mali ya ccm na ambao uko karibu na kota za polisi za Mchomba line , haya yanatendwa huku vyombo vyote vya dola vikiangalia kwa macho bila kuchukua hatua zozote , tena kwa miaka mingi , njia zote wanazopita vibaka hawa polisi wanazifahamu vizuri lakini hawachukui hatua zozote , Askari au mwanajeshi anayeweza kupinga hoja yangu hii ajitokeze hadharani , yanayotendwa na vibaka hawa mbele ya maeneo ya jeshi ni aibu kwa Polisi Mkoa wa Temeke ambao wengi wanajazana Uwanjani wa Taifa ili kutafuta rushwa ya kujikimu na kuwaacha raia wakiumia bila sababu mitaani .
Natoa wito kwa wote wanaoenda Uwanja wa Taifa kwenye mechi ya Simba na Yanga na kufikiria kurudi kwa kupitia njia hii basi WAJILINDE WENYEWE , tena wajihami kwa silaha nzito wakiweza , lakini kama wakitegemea ulinzi wa jeshi la polisi wasije wakalia na kusaga meno.
Uchunguzi wetu huu ni endelevu na utaendelea tena kwa kuangalia usalama wa washabiki wa soka wanaopitia Mandela road , wanaoelekea Mtoni kupitia Uhasibu na wale wanaoelekea Temeke kupitia Wailes .
Naomba kuwasilisha
Karibu sana mkuuNilikuwa najaribu kupitia kwa makini hii thread nione huenda ni ya enzi za jk,kumbe lah!Ni ya leo..leo kipindi cha utawala kama huu wanaweza kuibuka wababe wengine keko tu?
Mheshimiwa Kangi Lugora,IGP Simon Sirro,na mkuu wa mkoa wa Dar wapo.Ninachelea kuamini hizi habari.
Ninachojua,kulea makundi ya jinsi hii,ni sawa na kulea ugaidi.Na magaidi huwa hawachakugui.Kuwaacha hawa ni kukubali mtaani kuwe na jeshi la magaidi.
Wakamatwe wote wakalime mpunga,la hawataki,ile kanuni ya asiyefanya kazi asile itumike
Sent using Jamii Forums mobile app
ni vema uwe na msimamo huo , hakuna usalama hata ndani ya uwanjaHujanipeleka Uwanjani na mpira umaonyeshwa live kwenye TV
Vibaka hawashirikiani na mabeberuKwa tz vibaka wanadekezwa sana kuliko wanasiasa na waandishi wa habari sijui kwa nini bwana
Sijawahi kudokoa hata sukari .Mleta mada Leo umeandika vizuri baada ya kuachana na ukibaka keko
Asante kwa taarifa
Kwahiyo ndio maana wanaachwa waendelee kujimwambafai
yawezekana .Kwahiyo ndio maana wanaachwa waendelee kujimwambafai
kuna ukweli fulaniPolisi wa Tanzania wanapewa mafunzo ya kukabiliana na Chadema tu.