Kamanda Wambura ametoa taarifa yake kuhusiana na uchunguzi wa kadhia ya Hamza kuwa alikuwa ni gaidi.
Halipo jipya kwenye taarifa hiyo kwani ni wazi kuwa kilichofanyika ni kuhalalisha tu ambacho polisi kama sehemu ya kadhia wangekitaka.
Ikumbukwe pia kamanda Sirro alishahoji hata uhalali wa wazazi wa Hamza kumzaa tu kama binadamu!
Kwanini walioshambuliwa na Hamza walikuwa ni polisi peke yao? Kwanini Hamza hakuonekana kujaribu kujificha ili kuendelea na mapambano kwa siku au hata masaa zaidi?
Kama Hamza alikuwa ni gaidi hakuwa na washirika wowote hapa nchini? Hakuwa na mawasiliano yoyote na washirika hao?
Kama Hamza alikuwa na washirika nje tu, ushahidi uko wapi?
Waliomfahamu Hamza hawakubaliani na ripoti hii ya polisi. Bila shaka CCM alikokuwa kiongozi na kada mtiifu hawakubaliani na ripoti kuwa Hamza alikuwa msiri au mtu wa kujitenga, achilia mbali kuwa gaidi.
Vipi bastola aliyokuwa nayo, ilimilikiwa kihalali? Hivi Hamza alipigwa risasi ngapi? Naye alifyatua risasi ngapi? Ziko wapi taarifa hizi?
Kulisikika pesa kiasi cha 400,000,000/= kuhusiana na kadhia ya Hamza kupotea. Kumesikika kupotea kwa madini ya Hamza na polisi wakihusishwa moja kwa moja kwenye kadhia hiyo.
Kumesikika uwepo wa kikaratasi (suicide note) chenye maelezo yote ya kwanini Hamza alichukua hatua hii.
Polisi ambaye ni mtuhumiwa anakuwa na uhalali upi kutojipendelea kwenye kadhia hii?
My take:
Ilikuwa ni kwa maslahi ya polisi na serikali kwa ujumla kuhakikisha uchunguzi huru, wa haki na unaoaminika unafanyika kwenye kadhia hii.