Uchunguzi usiokuwa rasmi;Ndoa za waliowahi kuwa madada wa kazi( ma house girl) zinadumu kuliko za hawa wengine.......

Uchunguzi usiokuwa rasmi;Ndoa za waliowahi kuwa madada wa kazi( ma house girl) zinadumu kuliko za hawa wengine.......

KikulachoChako

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2013
Posts
19,185
Reaction score
37,239
Habari za asubuhi waungwana......

Wakati mwingine kukaa bila kazi ya kufanya inafanya kichwa kizurure kifikra na kupitia mawazo mbali mbali.......

Katika kuzurura huko kimawazo nikajikuta nimewakumbuka baadhi ndugu, jamaa na marafiki ambao imetokea wameangukia kwenye pendo la hawa wadada wa kazi na wengi wao baada ya kunogewa na utamu wakajikuta wameoa kabisa..........

Tangia hapo sijapatapo kushuhudia au kusikia mgogoro yoyote ya kindoa kwa wanandoa hao....nikiangalia hawa wengine wenzangu na mimi........

Changamoto za kibinadamu za hapa na pale najua hazikosekaniki lakini maisha yanakwenda......

Inawezekana ikawa sample ni ndogo ya kuweza kutoa hitimisho lakini kwenye kuchagiza maongezi na kujazia nyama kupitia shuhuda na maoni ya wengine waliooa wanawake wa hivi nimependa kuliweka hapa ili kukosolewa na ikibidi kuwekwa Sawa......

Nawakaribisha waungwana.......
 
Hao mara nyingi wanajua jinsi ya kukaa na watu, kuishi na watu. Hawa wengine ni hamna kitu
 
Ni makosa makubwa, tunapoelekea kwenye harakati za uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivi karibuni, na uchaguzi mkuu mwakani, kuwaita hivyo hao watu muhimu wa kundi hilo.

Jina lao rasmi ni maafisa malezi. Halafu ukitaka kusema mamalishe usiseseme mamalishe, sema maafisa lishe. Hapo upo?

^Hii ndiyo Tanzania ninayoitaka mimi,^ alisema Anko Joni.
 
Ni makosa makubwa, tunapoelekea kwenye harakati za uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivi karibuni, na uchaguzi mkuu mwakani, kuwaita hivyo watu wa kundi hilo.

Jina lao rasmi ni maafisa huduma za nyumbani. Halafu ukitaka kusema mamalishe usiseseme mamalishe, sema maafisa lishe. Hapo upo?

^Hii ndiyo Tanzania ninayoitaka mimi,^ alisema Anko Joni.
Asante muungwana kwa kunisahihisha....turudi kwenye mada
 
Wanajua vit ving,, Wamekutana na mambo meng,, Weng wavumiliv,, Wanajitambua na Kujielewa ni fursa ya Utafutaji ktk maisha tunawa ona n wat waliofel,,masikin,, hawana akil ,, WANAJUA KUPIKA HAWA,, mkuu ka mtego umenasa weka ndan hawa ni viumbe wachache sanaaa wenye kutambua mahitaji ya NDOA
 
Ukiona hivo ujue wamekutana kopo na mfuniko (match) Kila mtu awe anang'oa wa size yake.
 
Back
Top Bottom