Uchunguzi wabainisha Kombora lililoishambulia Poland lilitokea Ukraine

Uchunguzi wabainisha Kombora lililoishambulia Poland lilitokea Ukraine

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Kombora hilo limesababisha vifo vya watu wawili katika Kijiji kimoja Nchini Poland lilirushwa na vikosi vya Ukraine wakati vikizuia mashambulizi kutoka kwa Urusi

Maofisa wa Marekani ambao hawakutaka kutaja majina yao wamebainisha kuwa tukio hilo lilitokea wakati Urusi ikishambulia miundombinu ya Ukraine.

Taarifa ya awali kutoka Poland ilieleza kuwa kombora lililotengenezwa Urusi limetua katika eneo la Przewodow, Lublin lililopo kilometa 6 kutoka mpaka wa Ukraine.

Ukraine bado inamiliki baadhi ya silaha ambazo zilitengenezwa na Urusi ikiwemo mfumo wa S-300 unaotumika kuzuia makombora.


=============

Poland missile was fired by Ukrainian forces at incoming Russian projectile, US officials say

A missile that hit Poland on Tuesday evening was fired by Ukrainian forces in their attempts to shoot down an incoming Russian projectile, US officials have been quoted as saying.

Three US officials, who spoke to the Associated Press on the condition of anonymity, said preliminary assessments suggested the missile was fired by Ukrainian forces during the Russian bombardment on energy infrastructure across Ukraine.

Polish officials said earlier that a “Russian-made missile” landed in a grain store in Przewodow, Lublin, about 6 km from the border with Ukraine.


Ukraine continues to maintain stocks of former Soviet and Russian-made weaponry, including the S-300 air-defense missile system.

The explosion within the borders of Nato-member state Poland killed two people, sparking an investigation and emergency meeting of the Group of Seven (G7) members who were in Indonesia.

Source: Independent
 
Baada ya Vikosi vya Urusi kufurushwa Kherson mjii mkuu pekee waliouteka toka vita vianze mwezi wa February. Baada ya kupokea kichapo cha mbwakoko huko Kyiv ,toka vikosi shupavu vya Ukraine,na msafara wao wa vifaru wa kilometa 64 kusambaratishwa.Sasa hivi Urusi haina ujanja kwenye vita vya infantry;ana kwa ana,badala yake vikosi vya Urusi vimekuja na mbinu zinazotumiwa na vikundi vya kigaidi vya kipalestina(Hamas,Islamic jihadi) na Hezbollah dhidi ya Israeli vya kufurumusha makombora toka mbali bila kujali wanapiga wapi😡
Sasa hivi ndio uwanja wa mifumo ya ulinzi wa Anga ya NASAMS kufanya kazi ili kuilinda Ukraine dhidi ya Jeshi lililoshindwa na kurudi nyuma la Urusi.🤔
 
Ndio mana putini anajikukuta yeye siye anamuogopa NATO kama ukoma, maamae
 
NATO wanazunguuka sana mbuyu

Mbona ndio walikuwa wamepata sababu ya kumpiga vizuri Mrusi,wananivunja moyo hawa

Imekuwa tena mambo ya uchunguzi mbona mrusi alipotaka wachunguze kuhusu ile maabara iliyokuwepo ukraine walikataa uchunguzi

Sasa hivi wangepigia tu mstari kama vile walivyopigia Iraq,Syria n.k ili tujue nani mbabe na nani msema hovyo

Maana ninachoamini mrusi kaficha silaha za hatari na hata mmarekani na washirika wake nao wameficha silaha zao za hatari

Kwahyo watumie sababu ya kumpiga wanaeamini ndio tatizo la migogoro pale ulaya.
 
Back
Top Bottom