Uchunguzi wangu unaonesha wanaume tunaongoza kuwafanyia ukatili, kuwaumiza na kuwasaliti wanawake


Sahihi
 
Huwezi ukawa na akili alafu usimtaje Mungu
Kiranga ni kilaza wa mwisho jf kwa mujibu wa mtibeli 😂😂😂.

Mtibeli imani yako inaminya uhuru wa wengine, hebu jirekebishe na ufikiri sawasawa.
Hata mimi naamini Mungu yupo ila sio sahihi kubeza na kutweza kile wengine wanaamini.
Mengine hapo upo sahihi.
 
Uko sahihi kabisa. Kama suala la kuchepuka wanaume ndiyo tunaongoza halafu mke akisimama na mwanamme barabarani tunachukuwa hatua kali.
 

Haki ipi Unazungumzia?
Kutambua uwepo wa Watu wasio na akili kwani sio Haki?
Kutambua watu wasio na akili ni kuminya Haki zao?

Labda sijui Unazungumzia Uhuru upi?
Mimi sijakataa wala sijazuia Watu wengine kumkubali au kumkataa aliyewaumba.

Ikiwa wapo wanaowakataa wazazi wao waliowazaa wanaowaona sijashangaa sembuse wanaomkataa aliyewaumba ambaye hawamuoni.
Wana haki kwa sababu hawana ile akili ya kuona uwepo wa Mungu.

Zingatia, kinachoona ni akili(Ubongo) na sio macho.
 
Uko sahihi kabisa. Kama suala la kuchepuka wanaume ndiyo tunaongoza halafu mke akisimama na mwanamme barabarani tunachukuwa hatua kali.

Sisi ndio tunawatoa Bikra hawa wanawake na kuwazalisha na kuwatelekeza ili tuje kuwabeza.

Ingawaje pia yapo makosa ya wanawake lakini mzizi mkuu ni mwanaume kwa sababu sisi wanaume ndio chanzo cha wanawake
 
Me nadhani mwonevu wa kwanza ni yule aliewanyima hulka hio muhimu ya kiutawala...Na kama itabidi kuumia rohoni bac tambua kuwa MEN ARE GOD'S REPRESENTATIVES ON EARTH, WE ARE SACRED.

Kinyume cha God ni Satan sijui kama unajua hivyo.
Mwanaume akiwa mwema huwa ni Mungu akiwa Mwovu hugeuka Shetani.

Mada hii Unazungumzia ushetani wetu.
Umekubali kuwa sisi ndio watawala na katika utawala kuna utawala wa Mema na utawala wa maovu. Na kote huko mwanaume ndiye namba moja
 
Akili inaonaje na wewe mtibeli mbona unazidi kupuyanga, wewe unatumia hisia unasema unatumia macho, tangu lini akili ikaacha kufikiri ikaona??

Kumuita binadamu mwenzio hana akili ilhali hujathibitisha ni sawa??
Yaani kisa mna mawazo tofauti basi umuite hana akili?

Ccm amuite chadema hana akili, chadema amuite ccm hana akili, alieoa amuite aiseoa hana akili nk.
Hapo kutakua na kuheshimu mawazo ya wengine kweli??

Mtibeli, mtu mzima akivuliwa nguo huchutama.
 

Unaweza ukawa na macho usione.
Ila huwezi ukawa na akili alafu usione.
Akili/ubongo ndio huona. Macho hayaoni.

Akili unakuwa huna kama utashindwa kutambua jambo fulani ambalo mwingine analitambua na lipo.
 
Unaweza ukawa na macho usione.
Ila huwezi ukawa na akili alafu usione.
Akili/ubongo ndio huona. Macho hayaoni.

Akili unakuwa huna kama utashindwa kutambua jambo fulani ambalo mwingine analitambua na lipo.
Jamaa yangu kuona ni kufanyaje, au kuna maana zaidi ya moja ya neno kuona bila kuhusisha macho?

Utambuzi hufanywa na ubongo, kuona kunaafanywa na macho.
Baada ya kuona akili ndio hufanya utambuzi kujua kile kilichoonwa na macho.

Kipofu huwezi sema kaona, ila anahisi kwa njia mbalimbali, nae pia akihisi akili hufanya utambuzi.

Mambo ya Mungu yanakupotezea ufikiri ndgu mtibeli, wakati mwingine tumia akili yako na sio hisia zitokanazo imani yako mpya/uliyoificha kwa kipindi kirefu.
 
Hivi ukatili ni nini.?!maana siku iz mwanaume ukiwa na misimamo thabiti juu ya mwanamke tayari unaitwa mkatili,sasa neno ukatili kwa sasa mara nying linafujwa!!wanaume wenzangu tusimame imara,vita ni vikali lakini tutavishinda, full stop
 
cjui kama nakupata vizur ....Me nafkir hulka ya kimungu huwa haina makosa ndo mana mungu akikuumba na macho mawil tnasema yupo sawa lakn akikufanya kipofu pia tnasema mungu hakosei ..Kwa mantiki hii mwanaume kama mwakilish wa mungu hawez kuw n ushetani vinginevyo kanuni yako ianze kushughulika na mungu aliewapa mikono hawa na kuwanyima chakula wale.
 

😃
Mkuu nafikiri haya mambo yanahitaji uwe mzuri wa falsafa.
Kuona ni kutambua. Na macho hayawezi kutambua taswira ambayo macho yametazama.

Ubongo/akili ndio hutoa tafsiri, hutambua, husikia, huonja, hunusa.

Akili au ubongo wako ukigeuzwa iwe kwa madawa au kufanywa ndondocha unaweza ukawa na macho lakini usione.
Ubongo ndio unataswira
 
Leo mtibeli kaingia cha kike
 
Hivi ukatili ni nini.?!maana siku iz mwanaume ukiwa na misimamo thabiti juu ya mwanamke tayari unaitwa mkatili,sasa neno ukatili kwa sasa mara nying linafujwa!!wanaume wenzangu tusimame imara,vita ni vikali lakini tutavishinda, full stop

Msimamo sio kitu kibaya.
Hasa msimamo katika mambo Mema.
Lakini sio mambo ya kipuuzi na akili za kijinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…