Uchunguzi wangu wa awali kuhusu mgodi wa siri uliopo ndani ya pori la hifadhi Singida-Tabora

Uchunguzi wangu wa awali kuhusu mgodi wa siri uliopo ndani ya pori la hifadhi Singida-Tabora

Sioni shida ya mgodi kuwa na ndege
Sio lazima kuwepo barabara
Kujenga barabara yaweza kuwa gjatama kubwa kulliko faida ya mgodi wenyewe
Nadhani hapa Key Word na Tatizo ni Usiri....; Kama hii ni Mali ya Mpaka vizazi vijavyo kwa wachache kuifisadi kwa faida ya wachache ni tatizo na shida kubwa sana...
 
huu uchunguzi hautoshi
nafikiri ukae kama tetesi na wahusika waje na majibu

kwa Tanzania hili linawezekana maana hii nchi watu huiendesha wanavyo taka na sisi tupo kama makondoo tu

utashangaa badala wafanye uchunguzi waje na majibu, watamchukia mtoa bandiko na kuanza kumuwinda
Si unaona hata chawa wao wameshaanza kumshambulia mleta hoja.
 
Umekosea ungetaja huo mgodi unamilikiwa na Waarabu ungepata comments nyingi sana. Lakini hao Wazungu wafuasi wao wataweka ulimi puani.
 
Kizimkazi hajui na hana muda w kujua.yy ni kutengua na kuteua tu. Ndio anacho weza.
 
Mpaka muda huu navyosema watakuwa wameshaamrisha maaskari wakasake maeneo yote ndani na jirani ya hifadhi zilizotajwa ili kuwapata walioweka kambi ili kutoa taarifa za mgodi huo kisha kumsaka bwana mdude apewe kesi. 😁 af kwenye tv utasikia solidarity forever 🤪
 
Watanzania wenzangu mtakumbuka kwamba 4 March 2024 niliripoti kuhusu uwepo wa mgodi wa siri huko Singida - Tabora baada ya kupewa taarifa na mmoja wa wachimbaji wadogo.

Timu yangu ilifanikiwa kufika eneo hilo kwa lengo la kujiridhisha. Baada ya kufika eneo la tukio ikawa ngumu timu yetu kuingia kwenye huo mgodi baada ya kugundua kwamba mgodi huo uko ndani ya pori la Kizigo Game Reserve lililoko mkoani Singida na hakuna njia wala barabara inayoweza kukupeleka ndani ya mgodi huo. Na pori hilo hilo linalindwa na askari wanaohusika kulinda mapori na hifadhi za taifa.

Kutokana na mazingira hayo timu yetu ililazimika kutumia technology ambayo ilisaidia kujua mambo yafuatayo.

1. Ni kweli mgodi huo uko ndani ya hifadhi au pori la Kizigo Game Reserve lililopo Singida na linaingia mpaka Tabora.

2. Ni kweli kwamba karibu na mgodi huo kuna uwanja wa ndege (airstrip) kilomita 1.3 kama ambavyo technology imetuonyesha pamoja na picha za uwanja huo.

3. Kwa muda ambao timu yetu iliweka kambi ya wiki moja ndege ilitua na kuondoa mara 2. Kwa hiyo kwa wiki ndege hutua na kuondoka mara mbili kwa ajili ya kushusha na kubeba mizigo.

4. Tumejiridhisha kwamba Kizigo Game Reserve pia inapakana na hifadhi zingine mbili Muhesi Game Reserve na Rungwa Game Reserve.

5. Kuna njia zinatoka kwenye huu uwanja wa ndege kwenda kwenye hayo hizo hifadhi za jirani nilizozitaja hapo juu. Hii inaashiria kuwa kuna biashara nyingine haramu ya kusafirisha wanyama Wildlife trafficking katika eneo hilo. Ndio maana kuna njia za kuingia kwenye mapori mengine ya hifadhi katika eneo hilo.

6. Kuna nyumba zimejengwa umbali wa mita 800 kutoka katika uwanja huo wa ndege.

7. Hakuna barabara yoyote inayoingia katika mgodi huo isipokuwa huo uwanja wa ndege ambao sijui kama unatambulika rasmi.

Katika mazingira tuna mashaka kwamba serikali au viongozi wa serikali binafsi wanaweza kuwa wanahusika na biashara haramu zinazoendelea katika eneo hilo. Kwa sababu hizo Game Reserve zina askari wanaozilinda muda wote hivyo ni ngumu serikali kutokujua uwepo wa mgodi huo.

Bado timu yangu inaendelea na uchunguzi ili kupata picha clear lakini na wamiliki wa biashara haramu ndani ya msitu huo pamoja na washirika wake. Tutajua tu kama biashara hiyo wameuziwa wazungu au waarabu na wahusika wenye mamlaka ya kuuza au kukodisha eneo ndani ya nchi.

Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
View attachment 2946548View attachment 2946549
Hivi hii nchi itaendelea kutafunwa hivi na wachache hadi lini. Jamani wananchi amkeni nchi imebaki mifupa tupu hii.
 
Back
Top Bottom