“Uchuuzi” Biashara zinazowalemaza Watanzania

Sirudii tena kaka, nilijifunza sana hilo tukio
 
Mimi now, nataka nijikusanyie hata milion 5 tu isio na presha wala haraka wala si mkopo. Nafungua kiwanda kidogo cha bidhaa flani ambazo mpaka masikini hohehahe anatumia kila siku.
Kipindi cha almost mwaka sasa nimekua nikijifunza ujuzi flan wankawaida kabisaaa na Nimeshafanya pilot phase kwenye production na sales na matokea nimeyaona 80% working.
Katika kujifunza na kufanya trial nili inject kama 800,000/= na nikairudisha na faida juu.
 
Vipi wazee wa kuchapisha copy za bidhaa za watu mkuu. Hawa unaweza ukapambana nao vipi. Kuna comments uko juu nimeona wanaotengeneza pombe kali wanalalamika mtaani kuna vinywaji feki vyenye stika zao.
Na TBS, TFDA, NEMC wapo na wanalijua hili lakini hawafatilii, mtu unaweka mtaji unadhalisha bidhaa kwa ubora then mtu anakuja tu anatoa copy za bidhaa zako na anauza kwa bei ya madafu.... imagine juzi juzi mpaka Rwanda wamepiga marufuku baadhi ya liquor kuingia kwao inamaana wameshaona bidhaa feki zipo!
 
Uzi mzuri. Mleta uzi wazo lako liko sahihi ila ni ngumu kutekelezeka. Kuna vikwazo vikubwa kuwa mzalishaji. Kikwazo kikubwa sana nilichowahi kukutana nacho ni upatikanaji wa mali ghafi pamoja na skilled labour. Kwa mfano ukitaka kushona hata Tshirts tu utakumbana na changamoto kubwa ya fabrics na ukija kupata ni ghali. Hadi umalize kushona tshirt moja tayari gharama inakuwa kubwa kuliko anayetoa China. Pia mafundi wetu hawana skills za kutoa products zenye mvuto. Kuanzia ushonaji, mechanics hadi carpentry mafundi wanatoa products zenye finishing zisizovutia. Changamoto nyingine ni umeme bado haujawa stable.
 
Hapo zamani za juzi nilikuwa muumini wa kusingizia vikwazo vya serikali na mamlaka zake, sababu vilinipata. Ikabidi niingie kujifunza kwa waliotakatisha fedha zao mpaka zimekuwa safi. Nikagundua jambo moja, inataka dhamira ya dhati kufikia ndoto na unahitaji consistency ya kufa mtu ili utoboe. Kuanzia chini ni muhimu ili kupitia learning curve yako uweze kupata picha la mchezo linavyoenda.
 
Uko kwenye vilevi ndio pameoza kabisa. Hizi pombe kali na bia brand zakutoka nje kama savanah, heinkein, wondoek sio za kugusa kabisa. Watu wanapiga copy wanainhiza sokoni. Kwa usalama wa afya bora kunywa hizi local beer za tbl
 
Bila shaka ni unga wa sembe
 
Sio sababu kubwa ya kufanya watu wasifungue viwanda vidogo vidogo wakati Africa nzima swala la umeme ni janga, niko kwenye sekta ya vinywaji, na umeme na maji vinasumbua lakini sio sababu kubwa kuacha wakati kuna soko kubwa sana mtaani na wengi tuu hawaangalii brand bali nguvu yako ya kupeleka bidhaa sokoni.

Ukiachana na theory ukaingia kazini utakubaliana na mimi hizi changamoto zipo ukiwa na mtaji wa 50m huna haja ya kuangaika na uchuuzi labda uwe huna exposure na sasa majenereta yapo hadi ya lipa mdogo mdogo.
 
Vijana itabidi tubadilike
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…