“Uchuuzi” Biashara zinazowalemaza Watanzania

tatizo KUU la Taifa hili ni ccm
 
Unamaanisha bei ya umeme imeshuka?Unit moja tunauziwa kwa 300 unasema imeshuka?
Mkuu tafuta wanaozalisha products Tanzania kisha linganisha na bei za kutoka nje kama zinafanana mbona vitu viko wazi kabisa.

Sijasemea Bei kushuka.
Ila nimesemea umeme kidogo uko stable. Hukatiki sana kama zamani.

Ukiacha bidhaa za Electronic,
Ila nyingi za Bidhaa hizi za plastic na vifungashio, Nguo , viatu na bidhaa za Ngozi , vifaa vya Ujenzi na mapambo, mashine ndogo ndogo.
Hivi kuna Viwanda hapa hapa TZ.
Ila malighafi ndio zinakuwa import.

Sasa tofauti iko hapa.
mfano Kiatu cha Kike kutoka China ni bei rahisi kuliko kilichotengenezwa TZ.
ILA pia kuna kiatu China kina gharama zaidi ya Cha TZ.

Sasa tuangalie Kiatu cha Bei Rahisi China (muonekano mzuri, hakina Ubora) vs Bei Kubwa cha TZ (Muonekano sio mzuri , Kina Ubora).

Kwanini wananunua hiko Cha Bei Rahisi?. Jibu ni kuwa Wanaonunua ndio bei wanaiweza.
Lakini unahisi vya TZ havinunuliwi?.
Vinanunuliwa.

Kwahiyo kama nilivyokuambia.
Tusiogope kuanzisha viwanda vyetu na kuzalisha producta zetu. Kwa kuwaogopa wachina. Maana mwisho wa siku Kila mtu ana mteja wake.

Cha kuzingatia kwa bidhaa zetu,
Zitengenezwe zivutie na ziwe bora.
Ili hata Mtu ukimwambia hiki ni China elfu 20 na hiki ni TZ elfu 30. Achague Kununua cha TZ.
Hapa ndio haswaa tupambane nako. Na sio kushuka bei tufanane nao.
 
Mkuu hatutakiwi kuogopa ila hizi hela ambazo ni mtaji mmoja kuingiza kwenye kiwanda ambacho ni kama unaenda kucheza kamari ni hatari sana mpaka kwa afya yako ni ngumu kuingia kwenye soko ambalo watu wanatupa bidhaa kwa bei ndogo kabisa muda mwingine wanawakopesha wauzaji ili wapate chochote harafu wewe ndio ushndane nao ni ngumu sana.
 
Cha kuzingatia kwa bidhaa zetu,
Zitengenezwe zivutie na ziwe bora.
Ili hata Mtu ukimwambia hiki ni China elfu 20 na hiki ni TZ elfu 30. Achague Kununua cha TZ.
Hapa ndio haswaa tupambane nako. Na sio kushuka bei tufanane nao.
Zitengenezwe zivutie na ziwe bora.
Hapo ndio tunakuja kwenye factor ya lack of skilled manpower vyote vilishatajwa kwenye comments za wadau.
Halafu umesema siku hizi umeme uko stable kidogo haukatiki kama zamani-unatakiwa usikatike kabisa sio ukatike kidogo hivi unajua muwekezaji akisimamisha uzalishaji kwa masaa 12 anapata hasara kiasi gani?
Mimi nimeishi Dubai kwa miaka 5 sijawahi kuona umeme umekatika hata siku 1 hivi ndivyo inavyotakiwa na sio kuleta excuse.
 
Mm nakuelewa.
Na nadhan mfano wa Kiatu hapo juu umeusoma.

Soko ni huru. Ww tengeneza bidhaa zako ziwe na ubora na ziwe nzuri.
Mchina muache auze Hata nusu bei.
Ila kama umemzidi ubora , basi bidhaa yako itauzika tu.

Mm nilishawah fanya kama kiongozi wa sales na Marketing. Miaka miwili.
Bidhaa tuliyokuwa tunaipush , ina ushindan sokoni, maana viko viwanda vingne vinatengeneza.
Ila tulikuwa tunauza.
Na wala haikuwa bora zaid ya washindani.
Ila kuna sehemu products ilikuwa ina advantages zaid ya Competitors wengne, na ndio ilikuwa sales pitch yetu. Na ikatubeba na tukauza.

Sio Kila mteja ni Mteja wako, ila Kuna wateja wako, na hao ndio watengeneze bidhaa. Baada ya kufanya Research yako.
 
Mzee wangu alitafuta eneo la kiwanda
Alifunga transformer Kwa million 50 baada ya wiki hao hao tanesco wakaja kumuimbia na hakuipata mpaka leo
Na saiv Hilo eneo hamna kinachoendelea
Maendeleo ya viwanda yanataka mutual factors sio hobby tu
 
Nimeelewa sana Maoni yako.
Pia watu wengi hapa tunapozungumzia kiwanda anawaza kuanza kushindana nchi nzima.

Idea yangu kichwa ni watu kuanza kutengeneza viwanda anavyoweza shindana kwenye eneo lake dogo tu akapata wateja wake watiifu katika bidhaa hao ndio watakuza kiwanda.

Waswahili wanasema hakuna pombe isiyo na mlevi utapata tu walio loyal kwenye bidhaa zako.

Nitoe Mfano. Tanzania hii ukiacha pombe za kienyeji basi ni Giants ndio wanauza beer Nchi nzima. Vijana wamemaliza SUA pale wana ujuzi wa kutengeneza Hizi Pombe

Je kuna aliewahi on sehemu kuna local craft beer? Yani hio ni pombe ya kisasa imetengenezwa kwa radha pekee lakini inauzwa pengine ipo brewed kwenye glosary moja tu Maarufu Sinza watu wanaenda kunywa hapo? Vipi hii haina nafasi ya kukuwa na kukubarika miaka kadhaa mbele ikawa kiwanda kikubwa?

Huko Nje nchi za wenzetu kuna pombe unaenda kunywa sehemu flani tu (eneo) kama vile kwa mama muuza pombe za kienyeji au umaarufu wa visinia vya mihogo vya mtu X mahali flani Tz watu wanaenda kula na wanaipata hapo tu.
 
Daaah watu wana akili aiseee
 
Ni wazo zuri ila utekelezaji wake kibongo bongo ni mgumu mmno

Kwanza kutana na ukiritimba wa kukatisha tamaa serikalini kuomba vibali

Pili inahitaji uwe na mtaji wa kutosha maana hapo kuna kuajiri wataalamu na running cost yake sio ya kitoto

Ushindani haupo fair kabisa, yaani ukitaka kufungua kiwanda cha rangi utakuta wahindi wa Carol paint tayari wemeweka miundombinu toka kwa mamlaka kukupa ugumu usipate vibali
Bado ukiingiza bidhaa sokoni zitaundiwa zengwe unaweza ukajitundika ukafa

Hizi biashara zinataka mitaji mikubwa sana na ndio maana wawekezaji wengi ni ama Wahindi ambao wamekwisha jikita huko na kwenye system pamoja na wawekezaji kutoka nje ambao wamebobea

Vinginevyo labda viwanda vidogo kama vya kukamua alizeti, kutengeneza spirit nk
 
Umeme si uzalishe mwenyewe mkuu
 
Kwani solar za backup hazipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…