Asante sana; unajua sijawahi kukaa na kulifikiria hili la UDA kwani nami kama wengine nilikubali maelezo ya kuwa UDA ilishindwa kuwahudumia watu wa Dar kwa kiwango cha kuridhisha. Niliposikia kuwaa shirika bado lipo na lina assets na linataka kuingizwa kwenye DART swali moja tu lilikuwepo - kwanini UDA haikugeuzwa DART? Ni maneno manne tu lakini bado sijapewa jibu la uhakika na la akili. Nimeamua na mimi kuridhisha udadisi wangu thanks. Mwenye document yoyote kuhusiana na UDA hadi ilipofika hapa naomba mnipatie.
Mkuu UDA kulikuwa hakuna tatizo. UDA, kama mashirika mengine ya umma, ilishindwa kufanya kazi tuu kutokana na ukiritimba uliokuwepo serikalini. UDA ilikuwa na planing nzuri ya usafiri. Makonda walikuwa well trained tofauti kabisa na wale wa Chai Maharage. Routes za UDA zilikuwa well planned (walikuwa hawakatishi safari hata kama basi ni tupu). Tatizo kubwa la UDA ni kwamba nauli zake zilikuwa zinapitishwa na baraza la mawaziri. Badala ya kupitisha nauli in a commercial way, serikali ilikuwa inaangalia tuu kama abiria wata afford hizo nauli. Maamuzi juu ya nauli yalikuwa yanatolewa na serikali bila kuangalia gharama za undeshaji.
Kwa mfano, zilipoanza daladala nauli zao zilikuwa shilingi tano, wakati UDA iliendelea ku charge shilingi moja mpaka moja unusu. Na daladala zilikuwa zinajaa japokuwa zilikuwa illegal wakati huo. Financial deficity ambayo ilitokana na maamuzi ya serikali, ndio yamefanya UDA iwe hapo ilipo. Unajua neno daladala limetokana na nini? Kwa sababu wakati hii biashara inaanza, exchange rate ya dola moja ya Kimarekani ilikuwa shilingi tano (dala).
Wakati huo daladala zilikuwa zina operate illegally mpaka mwaka 1983 ziliporuhusiwa rasmi ili ku comply na Economic Reform Programme (ERP). Tatizo kubwa lililofanywa ni ku legalise daladala bila kuziwekea regulations jinsi zitakavyofanya kazi, kuzitafutia route, n.k. Matokeo yake hata serikali ilipoanza kuziwekea regualations na routes, it was too late.
Utafiti uliyofanywa ndani ya Dar-es-Salaam Region Transport Licensing Authority (DRTLA), ambayo ina regulate daladala, unaonyesha kuna matatizo makubwa sana. Ukilinganisa na UDA, haina professional staff, qualified traffic inspectors or traffic planners. Pamoja na kwamba kuna regulations zinazodhibiti daladala, asilimia 30 tuu ya hizo daladala ni roadworthy. Hapo unajiuliza DRTLA inafanya nini? Future yake itakuwaje baada ya DART kuanza kazi?
Kuna watu toka Dar City Council walitembelea jiji la Bogota nchini Colombia mwaka mwaka 2002 na inasemekana kuwa DART itafuata plan ya Bogota (BRT). Baada ya DART ku take off, kuna senior officers wawili wa DART walitembelea jiji la Miami Marekani sasa sijui kama wameamua kutofuata plan ya Bogota. The Institute for Transportation and Development Policy (ITDP) ilitengeneza plan ya kuboresha usafiri Dar Es Salaam. Plan yao ina incorporate streests, shared streets and pedestrian streets ili kuwe na nafasi ya kutosha kwa magari na pedestrians. Sijui kama hii itakuwa implemented.