UDA imebinafsishwa ili iingie Biashara na DART - Siri ya kuuzwa Bei Chee


Asante sana; unajua sijawahi kukaa na kulifikiria hili la UDA kwani nami kama wengine nilikubali maelezo ya kuwa UDA ilishindwa kuwahudumia watu wa Dar kwa kiwango cha kuridhisha. Niliposikia kuwaa shirika bado lipo na lina assets na linataka kuingizwa kwenye DART swali moja tu lilikuwepo - kwanini UDA haikugeuzwa DART? Ni maneno manne tu lakini bado sijapewa jibu la uhakika na la akili. Nimeamua na mimi kuridhisha udadisi wangu thanks. Mwenye document yoyote kuhusiana na UDA hadi ilipofika hapa naomba mnipatie.
 

Mkuu UDA kulikuwa hakuna tatizo. UDA, kama mashirika mengine ya umma, ilishindwa kufanya kazi tuu kutokana na ukiritimba uliokuwepo serikalini. UDA ilikuwa na planing nzuri ya usafiri. Makonda walikuwa well trained tofauti kabisa na wale wa Chai Maharage. Routes za UDA zilikuwa well planned (walikuwa hawakatishi safari hata kama basi ni tupu). Tatizo kubwa la UDA ni kwamba nauli zake zilikuwa zinapitishwa na baraza la mawaziri. Badala ya kupitisha nauli in a commercial way, serikali ilikuwa inaangalia tuu kama abiria wata afford hizo nauli. Maamuzi juu ya nauli yalikuwa yanatolewa na serikali bila kuangalia gharama za undeshaji.

Kwa mfano, zilipoanza daladala nauli zao zilikuwa shilingi tano, wakati UDA iliendelea ku charge shilingi moja mpaka moja unusu. Na daladala zilikuwa zinajaa japokuwa zilikuwa illegal wakati huo. Financial deficity ambayo ilitokana na maamuzi ya serikali, ndio yamefanya UDA iwe hapo ilipo. Unajua neno daladala limetokana na nini? Kwa sababu wakati hii biashara inaanza, exchange rate ya dola moja ya Kimarekani ilikuwa shilingi tano (dala).

Wakati huo daladala zilikuwa zina operate illegally mpaka mwaka 1983 ziliporuhusiwa rasmi ili ku comply na Economic Reform Programme (ERP). Tatizo kubwa lililofanywa ni ku legalise daladala bila kuziwekea regulations jinsi zitakavyofanya kazi, kuzitafutia route, n.k. Matokeo yake hata serikali ilipoanza kuziwekea regualations na routes, it was too late.

Utafiti uliyofanywa ndani ya Dar-es-Salaam Region Transport Licensing Authority (DRTLA), ambayo ina regulate daladala, unaonyesha kuna matatizo makubwa sana. Ukilinganisa na UDA, haina professional staff, qualified traffic inspectors or traffic planners. Pamoja na kwamba kuna regulations zinazodhibiti daladala, asilimia 30 tuu ya hizo daladala ni roadworthy. Hapo unajiuliza DRTLA inafanya nini? Future yake itakuwaje baada ya DART kuanza kazi?

Kuna watu toka Dar City Council walitembelea jiji la Bogota nchini Colombia mwaka mwaka 2002 na inasemekana kuwa DART itafuata plan ya Bogota (BRT). Baada ya DART ku take off, kuna senior officers wawili wa DART walitembelea jiji la Miami Marekani sasa sijui kama wameamua kutofuata plan ya Bogota. The Institute for Transportation and Development Policy (ITDP) ilitengeneza plan ya kuboresha usafiri Dar Es Salaam. Plan yao ina incorporate streests, shared streets and pedestrian streets ili kuwe na nafasi ya kutosha kwa magari na pedestrians. Sijui kama hii itakuwa implemented.
 
EMT.. nimeuliza hivyo kwa sababu inaonekana public transportation tunaingalia kwa kutumia prism ya faida. Hivi ni lazima UDA iwe kampuni ya kutengeneza faida badala ya huduma tu na faida isiwe katika fedha za nauli bali katika huduma inayotoa? Kwa mfano, kama UDA linaweza kusafirisha watu milioni 2 kwa mwaka, hawa watu wanachangia uchumi vipi katika shughuli zao mbalimbali?

Ukifikiria utaona kuwa hata bei kupangwa na cabinet kwangu haikuwa tatizo kabisa - hapa Detroit na maeneo mengine ya US yenye public (owned and operated) transit system bei haipangwi na soko bali na city councils au bodi na huwa imebakia hivyo kwa muda mrefu sana. Wanaangalia faida nje ya kuuza tiketi na miji hutenga fedha za kuhudumia hizo public transit. Nadhani kosa kubwa ni kwamba hatukutaka kutoa ruzuku kwenye vyombo hivi vya umma lakini tunatoa ruzuku ya mabilioni ya fedha kila mwezi kwa vyama vya siasa ili vitutawale!

Wenyewe tunafikiria ndio ubepari kumbe siyo ubepari ni ujinga tu. I really mean it.
 
Wenyewe tunafikiria ndio ubepari kumbe siyo ubepari ni ujinga tu. I really mean it.
Finally umesema point ambayo wengi wetu huwa tunatafsiri vibaya!...Sijawahi kuona mji wowote marekani ambao hauna public transportation ukiondoa vimiji vidogo.Hivi kwanini sisi tunajiona ni wajamaa?....we are not!
Back to the topic,sorry.
 


Ebu jibu swali moja muhimu hapa nani atakuwa operator wa mabasi ya DART
 

Mzee wa taaluma ebu twambie nani anakuja kuendesha mabasi ya DART?
 

Mzee Avatar yako inapereka mbali
 

Nafikiri hilo ndilo tatizo la daladala Dar Es Es Salaam. They are run on profit. Inaonekana pia waliokimbilia kuwekeza UDA wanaangalia profit zaidi. Hata they DART inaonekana kama itakuwa ni profit based kwa sababu private companies will be invited to place their bids. Matokeao yake matatizo yatakuwa yale yale kwa sababu makampuni yatakayoshinda tenda aims yake itakuwa ni kumiximize faida. Kwa kawaida public transport inakuwa funded na nauli za abiria. Pia transit operators au transit authority zinaweza kupata subsidies kwenye kodi na subsidies nyingine toka serikalini. Matangazo pia ni sehemu ya income. Pia nafikiri UDA inamiliki ardhi kibao ambayo inaweza kutumika kama miradi kupata fedha za kuendesha hayo mabasi. Kituo cha mabasi cha Ubungo na stendi ya Zamani ya Kisutu zinamilikiwa na nani? Tatizo kubwa tulilo nalo ni ubaridhifu ndani ya vyombo kama hivi.
 
Soma kuhusu assets na uwezo wa UDA humo ndani kulinganisha na makampuni binafsi! Kumbe hata leo hii UDA ina mabasi mengi kuliko wamiliki wengine wote wa daladala Dar!

Lakini hayo mabasi yao wapo kwenye hali gani ??
 
Kumbe kuna watu wengi wenye uchungu na UDA - nyaraka zinatiririka kwenye mail box yangu hadi nasikia kizunguzungu. Nilisema baada ya PPF sikutaka kuingia kwenye haya mambo tena lakini it is almost impossible to resist the temptation. Nashangaa haya mambo walitakiwa wabunge ndio wapatiwe!!! grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr halafu wamebakia kulilia posho!! screw 'em!

Nimeongeza hiyo brochure hapo juu kuhusu UDA kumbe kulikuwa na mpango wa kupata Soft Loan ya kununua mabasi 150? Kweli watu wa Dar wana matatizo.
 
Mwalimu alishindwa kuizuia NBC isibinafsishwe mbele ya chaguo lake mwenyewe Mkapa, sidhani kuna shirika la UMMA litabaki wakubwa hawa wakishaamua kuliuza au kuuziana.
 
Hivi Kiroromo amekwenda watu yeye alionekana kujuwa usahihi wa kuuzwa kwa UDA lakini soon akatoweka nao?
 

Tuwekee basi hizo info. Kumbe UDA ina karakana nzuri inayoweza kutengeneza hata bodi za mabasi. Ina vitega uchumi vizuri tuu vinavyofanya UDA iweze kutoa huduma ya usafiri kwenye project ya DART. Lakini kuuza nusu ya shirika kwa kampuni binafisi ina maana kuwa, UDA itakuwa inaendeshwa kibiashara. Huu mkopo nafuuu kutoka Korea ulichukuliwa lini? B'se kuna taarifa kuwa UDA ilishawahi kuomba mkopo CRDB wakatoswa.
 

ndio hivyo; unajua mafisadi huwa wanaona mbali sana; wanapanga move zao kama maili 100 kabla. Wako kama tai wawindaji. Panya anaweza hata asijue kuna tai angani wakati tai ameshampiga jicho. UDA ilihitaji kubadilishwa tu kuwa chombo cha usafiri Dar - lengo ambalo ndilo liliunda. DART wala haikuwa na ulazima wowote! Sasa ili ujue move yenyewe ni kuwa badala ya kuifanya DART iwe kweli Transit system -- na mabaasi yake, karakana, na muundo wake wameamua kuifanya DART iwe ni kutengeneza hizo barabara na kuzisimamia kampuni nyingine "binafsi".

Unfortunately, wasingeweza kufanya hivyo UDA ikiwa ni taasisi huru yenye uwezo. So wakaamua kuiuza UDA badala ya kuiwezesha halafu hiyo UDA itakuja na kuingia mkataba na DART na itaanza kutengeneza hela kama ina akili mbovu. Halafu upande mwingine wanasema wenye kampuni ya daladala wajiunge na kuunda kampuni moja - guess ni kina nani watanufaika siyo wale wenye vijidaladala vidogo? Ooh nooo makampuni makubwa ya usafiri.
 
Jamani.. naona nimemiss swali kuhus UDA na DART; nimeona sehemu ya mwisho waziri akijibu na inaonekana ni Mnyika aliuliza.. any details?
 
Wenyewe kina nani?



Kwanini?



Kwanini?




Sasa wewe sema ukweli. Kwanini UDA imebinafsishwa na kwanini UDA haikuchukua majukumu ya DART au DART nayo itakuja kubinafsishwa?

MKJJ nadhani watunga sera na wanaozisimamia nchi hii wangekuwa wanaanza na maswali haya rahisi na ya msingi kabisa tusingekuwa na huu ubinafsishaji usiokuwa na kichwa wala miguu.
  • Hivi kwa nini watu hawataki kujiuliza sababu za msingi zinazopelekea haya mashirika ya umma yote yawe "yanakufa" na mara tu "yanapokufa" watu wanakimbilia kununua hisa kwa ajili ya kuendesha mashirika mfu/marehemu?. Why?
  • Ni nini hicho ambacho mtanzania huyu akiwa serikalini hawezi kukifanya kuendeleza mashirika lakini mara anapokuwa "mbinafsi" akakabidhiwa shirika lililokufa anakuwa mahiri wa kulifufua na kuliendesha kwa faida?
  • Kwa nini idara za serikali zinashindwa kulipa bili za umeme wakati kila mwaka kuna fungu la bajeti ya umeme linapitishwa na bunge?
  • Kwa nini nyumba za serikali ziliachwa mpaka zikaharibika na kujengewa hoja kuwa ni mzigo ziuzwe wakati miaka yote mafungu ya kuzikarabati yalikuwa yakipitishwa na kutumika?
  • Kama tunakubaliana kuwa mashirika ya serikali hayawezi kufikia malengo yake ya kuanzishwa ni nini kinatufanya tuamini kuwa serikali ile ile iliyoshindwa kusimamia mashirika haya ili yafikie malengo yake inaweza kusimamia mambo mengine ya kitaifa kama kuinua uchumi wa nchi, kuondoa janga la umeme, kuondoa njaa na kudhibiti mfumko wa bei?
  • Hivi kwa kufuata mantiki hiyo hiyo potofu ya ubinafsishaji kwa nini hawa viongozi wa serikali hawajengi hoja kuwa serikali kuu (kwa maana ya Ikulu, Wizara na Idara za serikali) imeshindwa kujiendesha na kufikia malengo yake na hivyo tuibinafsishe kwa wawekezaji wa kigeni toka ulaya, marekani au asia tutakuwa tumekosea?
Just thinking aloud!
 

maswali yako haya nimeyapenda; ningefurahi kusikia waziri mmoja anaulizwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…