Udadisi uliomuua paka: Namna sahihi kiafya ya kuulaza mwili wako

Udadisi uliomuua paka: Namna sahihi kiafya ya kuulaza mwili wako

404 Pages

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,703
Reaction score
2,963
Habari wakuu.

Nisiwapotezee muda ngoja niende moja kwa moja kwenye mada.

Awali ya yote niseme tu wazi Mimi sio mtu wa Afya nikimaanisha Mimi sio daktari wala sio nesi. Namaanisha Mimi si mtu mwenye taaluma ya Afya Ila napenda masuala ya Afya.

Screenshot_20230624-192502.png


.......

Nitagusia kitu kidogo tu kinachohusu namna ya kuulaza Mwili wako. Nitaelezea kidogo na wengine wajuvi zaidi yangu watajazia nyama hapo chini kwa pale nilipoeleza tofauti.

Nitaelezea kwa kile nnachokielewa, ninachokifahamu na nilichokifanyia majaribio binafsi (curiosity killed the cat).

1. Ulalaji wa Bila Mto (Pillow) kichwani

Huu ulalaji nilipata kuambiwa una faida maana huufanya uti wa mgongo usipatwe na msigishano wowote kwenye zile pingili na mimi kuna kipindi nilikua nina shida/tatizo pingili za uti wa mgongo zilikua zinakaza sana hadi nijinyoshe kwa kufanya mazoezi ndio zinaacha kukaza na hivyo nikaambiwa ulalaji huu una faida nyingi zaidi kuliko ulalaji wa kutumia pillow.

Kwa hio nikaacha kulala na pillow nikatumia ulalaji huu na issue yangu ya uti wa mgongo ikaacha pingili zikawa hazikazi tena.

Unahisi nilipotumia huu ulalaji nimegundua nini?

Nilichogundua ni kwamba ndio ni ulalaji mzuri unafanya uti wa mgongo unakua haupati msigishano kwenye zile pingili Ila tatizo linakuja kwenye upande wa tumbo na mapafu hapa nazungumzia mfumo wa chakula na mfumo wa upumuaji.

Hapa nikaja kugundua ndio maana ukiwa hospital unapokua mgonjwa unapopewa kitanda chako madaktari wakakinyanyua kitanda kidogo eneo la kichwa na unawekewa na ka-pillow kichwani haulazwi tu km flat screen kuna slope fulani unawekwa kwenye engo fulani wastani wa nyuzi 25 au 30 au 35 hivi, ile sio bahati mbaya wale jamaa wanajua sana.

Kingine ni upande wa mmeng'enyo wa chakula hapa kwa mujibu wa majaribio yangu nikagundua itachukua mda sana mmeng'enyo wa chakula kufanyika kwa yule anaelala bila pillow kuliko yule anaelala na pillow.

2. Kulala na Mto (Pillow) kichwani

Hii ni njia nyingine ya namna ya kuulaza Mwili.

Hapa nitaelezea kidogo kilichonisibu katika majaribio yangu mpaka nikaandika haya niliyoyaandika leo maana ndio kusudi la uzi huu.

Mimi ninapenda kulala bila pillow niseme nilijizoesha hivyo baada ya kuona inanisaidia kutuliza uti wa mgongo Ila sasa hapa katikati nilishikwa na mafua makali sana na homa hivyo basi ikawa nikilala bila pillow kichwani km kawaida yangu nimezoea naona naanza kukosa hewa nashindwa kupumua kabisa pua zangu zote zinaziba hakuna hewa inatoka puani ni mdomoni tu yaani ni km vile ninazamishwa ndani ya maji, nikawa najiuliza tatizo nini mboni nikiinuka tu kitandani pua zangu zinaacha kuziba naanza kupumua vizuri ?

Kumbe ilibidi nichukue pillow niweke kichwani tu na nikafanya hivyo nikajilaza na ile hali ikaacha ndipo nikaanza kupumua vizuri bila shida yoyote huku pillow ikiwa kichwani.

Ila tatizo ni kwamba nikilala na pillow kichwani mda mrefu uti wa mgongo unaanza kuniuma pingili zinakaza mpaka nifanye mazoezi. Kwa hio hio ndio hasara ya kutumia pillow.

Ukiweka pillow kichwani unakua na uwezo wa kupumua vizuri zaidi bila shida kuliko kulala bila pillow kichwani.

Mwenye la kuongezea ataongezea hapo chini.

Uzi tayari.
 
Back
Top Bottom