benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umebaini kuwapo udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wanachama na viongozi wa dini kwa kufungisha ndoa batili ndugu wa familia moja ili wakidhi vigezo vya kuwamwanachama wa Mfuko huo kama mke na mume. Hayo yalibainishwa jana katika mkutano wa wadau wa mfuko huo kwa Mkoa wa Mtwara, wakati Meneja wa Mkoa wa Mfuko huo, Dk. Adolph Kahamba, akiwasilisha tarifa mbele ya mkutano huo.
"Kuna tukio lilitokea nadhani vombo vya habari vilitoa hapa Mtwara kwamba mtu amefunga ndoa na dada yake ili apate bima ya afya, kwa hiyo kumekuwa na udanganyifu na bahati nzuri viongozi wa dini mpo mtusaidie ili kuweka maadili."
"Ofisi yetu ina kesi shekhe ana 'confess' (kiri) bwana mimi kwa kweli nilidanganya nikafungisha ndoa ya uongo mtu na dada yake ili apate bima ya afya," alisema Dk. Kahamba.