Udanganyifu NHIF, Ndugu Waoana Wapate Kadi ya Bima

Ni kweli kabisa utaratibu wa watu wa bima kupanga lazima umuweke mzazi wako ni wa kipuuzi kwa sababu kuna watumishi wengi hawajawahi kuwaona hao wazazi bali wamelewa na kusomeshwa na watu baki .Mfano wajomba shangazi au mama wakubwa au wadogo.Mara nafasi za wategemezi lazima awe mke wa ndoa mpaka uweke cheti hivi hawa mbwa hawajui kuna ndoa za kimila nazo ni halali ?Na watoto lazima uwe umewazaa mtumishi mwenyewe kama huna kizazi nafasi zinabaki huku unaendelea kukatwa mshahara wako.Ifike mahali sheria ibadilishwe Mwenye mshahara aweke watu anaotaka wanufaike kisheria pasipo kupangiwa na hao watu wa bima lasivyo kujiunga na bima ya afya kwa mtumishi iwe ni hiari.
Kwa kweli wanaopitisha sheria sijui huwa wanawaza nini hawangalii uhalisia wa maisha. Hawaweki sheria za kumsaidia mwananchi bali kumkomoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyoo namba ya nida inakuwa imesajiliwaa UONGOO PIA..???
Huyo jamaa wa NHIF bado hajaeleweka vizuri.

Usajili wa bima ya mke unahitaji cheti cha ndoa, cheti cha kuzaliwa na namba ya NIDA. Sasa kama ni dada wa baba mmoja itagoma kwa sababu majina yatafanana, labda kama ni dada ndugu si wa damu.

Kile cheti cha kuzaliwa kinakuwa na majina ya baba na mama!
 
Pesa zao mnakata kwny mishahara yao halafu mnajipa jukumu la kuwachagulia nani awe Mnufaika wa makato ya Mshahara wake

nyie mlipaswa mumuambie una nafasi kadhaa halafu muachieni yeye aamue nani afaidi hiyo fursa kama Jirani, Malaya wake au hata House girl wake

wana ndoa wote waajiriwa na wana kadi za Bima za Afya na hawana wazazi wameshatangulia mbele za haki na wana Mtoto mmoja hizo nafasi tisa zikizobaki mnatka kuzifanyia nini?
 
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umebaini kuwapo udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wanachama na viongozi wa dini kwa kufungisha ndoa batili ndugu wa familia moja ili wakidhi vigezo vya kuwamwanachama wa Mfuko huo kama mke na mume. Hayo yalibainishwa jana katika mkutano wa wadau wa mfuko huo kwa Mkoa wa Mtwara, wakati Meneja wa Mkoa wa Mfuko huo, Dk. Adolph Kahamba, akiwasilisha tarifa mbele ya mkutano huo.

"Kuna tukio lilitokea nadhani vombo vya habari vilitoa hapa Mtwara kwamba mtu amefunga ndoa na dada yake ili apate bima ya afya, kwa hiyo kumekuwa na udanganyifu na bahati nzuri viongozi wa dini mpo mtusaidie ili kuweka maadili."

"Ofisi yetu ina kesi shekhe ana 'confess' (kiri) bwana mimi kwa kweli nilidanganya nikafungisha ndoa ya uongo mtu na dada yake ili apate bima ya afya," alisema Dk. Kahamba.
Zamani ilikuwa mwanachama anaweza kuunganisha watu WOWOTE watano na yeye wa sita baadae wakaongeza mashart ya vyeti ndio kinachofuata
 
Huyo jamaa wa NHIF bado hajaeleweka vizuri.

Usajili wa bima ya mke unahitaji cheti cha ndoa, cheti cha kuzaliwa na namba ya NIDA. Sasa kama ni dada wa baba mmoja itagoma kwa sababu majina yatafanana, labda kama ni dada ndugu si wa damu.

Kile cheti cha kuzaliwa kinakuwa na majina ya baba na mama!
Ndo nasema labda awe ndugu wa pembenii ambae hata ukoo hamuendanii...!
 
Mtu na dada kivipi! Kwenye Uislam dada yako ni yule wa baba mmoja na mama mmoja au wa mama mmoja au wa baba mmoja lakini mtoto wa mjomba,wa shangazi, wa baba mkubwa au wa baba mdogo,wa mama mkubwa au mama mdogo hao wote ni vyakula kama vyakula vingine japo upande wa mila na tamaduni kuna mitazamo tofauti
Mfano jamii nyingi za ukanda wa pwani ndoa hizi ufungwa sana lakini upande wa bara ndoa hizi ni nadra kutokea.
Wewe hayo maelezo mengine umeyatoa wapi?
 
Kwani kuna shida gani hapo ikiwa mwanachama mchangiaji anakatwa pesa yake kihalali jamani sioni tatizo, sometime waacheni watu, mmekataa mtu asimfungie bima mdogo wake shangazi au ndugu mwingine sasa mnatakaje yaani lengo lao mtu abaki peke yake akatwe pesa ya bure tu!
 
Kama waliweka nafasi kadhaa na hazijazidi kutokana na udanganyifu huo basi hakuna hasara.
 
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umebaini kuwapo udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wanachama na viongozi wa dini kwa kufungisha ndoa batili ndugu wa familia moja ili wakidhi vigezo vya kuwamwanachama wa Mfuko huo kama mke na mume. Hayo yalibainishwa jana katika mkutano wa wadau wa mfuko huo kwa Mkoa wa Mtwara, wakati Meneja wa Mkoa wa Mfuko huo, Dk. Adolph Kahamba, akiwasilisha tarifa mbele ya mkutano huo.

"Kuna tukio lilitokea nadhani vombo vya habari vilitoa hapa Mtwara kwamba mtu amefunga ndoa na dada yake ili apate bima ya afya, kwa hiyo kumekuwa na udanganyifu na bahati nzuri viongozi wa dini mpo mtusaidie ili kuweka maadili."

"Ofisi yetu ina kesi shekhe ana 'confess' (kiri) bwana mimi kwa kweli nilidanganya nikafungisha ndoa ya uongo mtu na dada yake ili apate bima ya afya," alisema Dk. Kahamba.
Tatizo wanalazimisha Watu wa kuweka wewe ruhusu tu mtu akijaza nafasi zake basi hutaona ndoa yake. Gharama za afya zipo juu sana
 
Kama mchango wa mwanachama unaweza kuhudumia watu wa5 Kwanini walazimishe uhusiano na wanufaika
 
NHIF isiwapangie wanachama tegemezi wa kuingizwa kwenye orodha ya mwanachama.

Kama ni nafasi 5 aachwe mwanachama achaguwe anamuingiza nani anaweza kutowa sadaka kumuingiza hata mtoto yatima.
Kweli kabisa
 
Ipo njia ya kumuingiza mtoto yatima, haijawahi kuondolewa. Ulizia tu utaratibu kwawahusika utapewa.
 
Mbona wao NHIF wanatudanganya huduma itakuwa bora lkn tukifika huko tunakutana na miseto?
Ubora huduma unaboreshwa na kituo cha afya husika ikisimamiwa na wizara ya afya kwakuwa vituo vya afya na NHIF wote wapo chini ya wizara ya afya, kinachotofautiana ni mmoja anatoa huduma na mwingine analipia hiyo huduma iliyotolewa ila msimamizi wa kuboresha huduma ni serikari chini ya wizara ya afya. NHIF haiwezi ingilia majukumu ya wizara!
 
Ni kweli kabisa utaratibu wa watu wa bima kupanga lazima umuweke mzazi wako ni wa kipuuzi kwa sababu kuna watumishi wengi hawajawahi kuwaona hao wazazi bali wamelewa na kusomeshwa na watu baki .Mfano wajomba shangazi au mama wakubwa au wadogo.Mara nafasi za wategemezi lazima awe mke wa ndoa mpaka uweke cheti hivi hawa mbwa hawajui kuna ndoa za kimila nazo ni halali ?Na watoto lazima uwe umewazaa mtumishi mwenyewe kama huna kizazi nafasi zinabaki huku unaendelea kukatwa mshahara wako.Ifike mahali sheria ibadilishwe Mwenye mshahara aweke watu anaotaka wanufaike kisheria pasipo kupangiwa na hao watu wa bima lasivyo kujiunga na bima ya afya kwa mtumishi iwe ni hiari.
Utaratibu wa kuwaweka walezi na watoto ambao siyo watumbo lako upo sema kama kawa TZ tunapenda kulalamika[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Pia ndoa iwayo yeyote cheti cha ndoa hutoka serikarini hivyo mtambuzi kuwa hii ni ndoa ni halali au sio ni msajili wa ndoa serikarini nasi NHIF. Ndio maana ukiwasilisha tu cheti cha ndoa kutoka serikarini hakuna wakukuzuia ila sio cheti cha kanisani au msikitini.
 
Wabongo watu wa kujiongeza slopu bin kuteleza.
 
Back
Top Bottom