Udhaifu katika katazo la kuuza vyakula mchana wa ramadhani Zanzibar

Udhaifu katika katazo la kuuza vyakula mchana wa ramadhani Zanzibar

[emoji172][emoji169]
Nimeenda kanisa la kinabii, ile naingia tu, kwa nabii, nabii akasema, wewe baba uliyevaa jezi ya mbeya city na skuna nyekundu, njoo hapa mbele.

Nikaenda, fasta nikazingirwa na Makerubi na Maserufi, wameshika maiki mikononi mwao, wengine wamevaa miwani myeusi kama maafisa kipenyo.

Nabii kwa sauti yake nzito akasema, kwa mamlaka ya kikuhani niliyonayo, kuanzia sasa wewe utakuwa mume wa Jeni, (inaonekana huyo jeni ndiyo tajiri wa kanisa ila hadi sasa na 46years hana ndoa wala mtoto)
Nikauliza kivipi aiseee..... nikaambiwa nisibishane na sauti ya bwana, nijiandae tu na ndoa, posa, mahari na vinginevyo kanisa litalipa.

Mama yangu weeeeee na ulevi wangu huu wa Konyagi, huyo malaika hajawaonyesha kabisa?
[emoji23][emoji23][emoji23] acha ufala[emoji16][emoji16]
 
Mbali na kuzuwiwa kwa vyakula kuuzwa mchana wa ramadhani katika baadhi ya maeneo,lakini bado zuio hili halijatendewa haki.

Waislamu tunaamini kwamba ukifunga basi hata ukila ile punje ya karanga tu na ukameza kwa makusudi basi umefungua sio mpaka ule biriani au urojo bakuli zima.

Sasa ni jambo la ajabu sana kuona kuna baadhi ya vyakula eti ruhusa kuuza kama vile..

Ndizi
Karanga
Mapapai
Korosho
Machungwa
Matikiti ambayo mengine yameshakatwa tayari kwa kuliwa.
Maji pia yanauzwa.
Juisi aina zote zinauzwa madukani.
Biskuti zinauzwa madukani.

Na vitu vingine vingi achilia mbali vitu hivyo.

Lakini vyakula vya kupikwa vimezuiwa kabisa na migahawa imefungwa kabisa.

Mimi naona hii haiko sawa kwa sababu orodha ya vyakula nilivyotaja pia mtu akila anafungua kwa hiyo navyo ilikuwa vizuiliwe kuuzwa ama maduka yafungwe kama ambavyo migawaha imefungwa.

Siku za kawaida tunawaona watu wanakunywa maji hadharani hivyo na maji ilikuwa yapigwe marufuku yasiuzwe ama maduka yanayouza maji yafungwe.

Siku za kawwida watu hula hadharani karanga,hivyo na karanga ilikuwa zizuiwe zisiuzwe.

Siku za kawaida watu hula ndizi hadharani hivyo ilikuwa na vibanda vya matunda vipigwe marufuku lakini hawa wauza matunda ndio utawakuta wanalalamika endapo migahawa haifungwi kana kwamba wao hawauzi vyakula.

Na vinywaji vingine vyote vinavyouzwa madukani tunaona kabisa vinywaji hivyo hunywewa katika siku za kawaida.

Hivyo ilikuwa maduka yanayouza vinywaji yafungwe kama ambavyo migahawa imefungwa.

HOJA WANAYOTUMIA.

HOJA:.eti migahawa inauza vyakula vya kula hapohapo yaani wanaandaa ili kiliwe kwa nyakati hizo.

JAWABU : ndizi,embe,korosho,mapapai,na machungwa maji,juisi,biskuti n.k haya yote yapo tayari kuliwa muda wote na wala hayajapigwa marufuku ama kufungwa maduka,hivyo sio sawa na maduka yafungwe pia.

Kama itasemwa kwamba migahawa watu wanakula hapo hapo nddio maana wamezuia basi wangekataza tu kwamba watu wasile migahawani lakini migahawa ipike vyakula,kidoogo ingemake sense japokuwa tungehoji zaidi.

Imagine familia yote imefunga alafu kuna mgonjwa ana vidonda vya tumbo,sasa badala ya mama kusumbuka kupika huku amefunga si angetoa pesa tu kwendakununjua chakula akarahisisha ?

Huu utaratibu uangaliwe upya na kufanyiwa maboresho katika hayo maeneo ambayo taratibu hizo zipo.
Hayo unataka yafanyike katika nchi isiyo na dini?

Yaani wasio waislam wanyanyasike kwa sababu kuna watu wamefunga?

Halafu maana ya kufunga ni ipi kama wewe kwa vyakula tu unashindwa kudhibiti nafsi yako?
 
Una ushahidi gani
Huwezi kuta waromani wasabato, wana andika upumbavu upumbavu huu kila siku juu ya imani nyingine.

Hawa ni Wanaojiita walokole, ushahidi mimi naishi kwenye jamii najua walokole wanajiona wako sahihi sana.
Lakini dhiki za Dunia ni zilezile tena hawa jamaa ndiyo wanaongoza kuishi kwa kuomba omba.
 
Umeongea vitu vingi sana ambavyo sijavizungumzia kabisa

Umechukia kuitwa kafiri?,Je,Unafahamu maana ya kafiri?
Najua zaidi ya ujuavyo. Mwislam Safi na Mwenye maadili ya dini hawezi kumwita binadamu mwenzako kafiri au mshenzi.
Umefail na huna sifa ya kuitwa mwislam. Jina likufaalo ni unafki.
 
Bila waislamu mngepata uhuru nyie acheni zarau wakristo kipindi chakupigania uhuru mlikuwa choka mbaya kama sio yule jamaa kutugeuka waislam tungekuwa mbali sasa hivi halafu mnakuja hapa mnatuka dini iliyowaletea uhuru.
Mbona Zanzibar hawako mbali?
 
Kwanza kabisa naamini wana jamvi mko salama kabisa.
Ninaamini swala la kuabudu ni la kila mmoja kulingana na imani aliyonayo kuhusu dhehebu au dini anayohusiana nayo.

Kwanza kabisa naomba kuanza kwa kusema wenzetu wakristo dhehebu la wakatoriki, walipoanza kufunga wala hawakuweka masharti watakapokuwa wamefunga wafanyiwe nini!!!

Lakini ndugu zangu waislam wanataka wakiwa wamefunga watu wasifanye shughuli zao za kila siku zinazowaingizia kipato kwa mfano wamama wanaopika chakula kwa ajili ya kujipatia kipato ati waache kisa waislam wamefunga.

Ninaomba kujua, kwani mfungo wenu ili uwe kamili ni lazima nyie waislam msiwe karibu na watu wanaokula au kupika vyakula vyao?! Kwa mtazamo wangu siyo sawa.

Mchungaji mmoja jina kapuni aliwahi kuhoji mbona Airport kuna msikiti lakini hakuwahi hata kujibiwa, na mchungaji huyo anadai kwamba alipotaka aingie msikitini akasali kwa kuwa ni nyumba ya ibada alikataliwa kwa sababu ya kwamba ni mkiristo, je wakristo wanaosafiri kwa usafiri wa ndege je wao wakaabudu wapi?? Au wenye nia ya kusali au kuabudu wakiwa kabla hawajasafiri ni waislam tu??

SIJAJUA KAMA NI UDINI LAKINI KAMA NDIYO BASI ONDOA UDINI TUISHI KAMA NDUGU.

Jambo lingine ambalo leo nimeshangaa, hapa tanga sehemu moja panaitwa forodhani, kwa chini yake kuna sehemu panaitwa DEEP SEA, huku bana kuna maisha
Ya raha sana, lakini kitu ambacho kimenishangaza kuna msikiti ambako pia ni eneo la serikali, lakini hakuna kanisa, hiii ikoje jamani. Au wakristo wenyewe ndo hawajaomba ridhaa ya kujenga kanisa hapa bandarini na kule Airport??

Naomba kuwasilisha kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ferry Dar es Salaam ni mali ya serikali na msikiti unajengwa hapo, na ni hatua chache sana kutoka ikulu ya Magogoni na ofisi ya Waziri Mkuu.
 
Bila waislamu mngepata uhuru nyie acheni zarau wakristo kipindi chakupigania uhuru mlikuwa choka mbaya kama sio yule jamaa kutugeuka waislam tungekuwa mbali sasa hivi halafu mnakuja hapa mnatuka dini iliyowaletea uhuru.
Mkuu wbu acha mawqzo mgando kwamba eti kuna mtu alikwamisha uislamu huu ni uongo wa wazi kabisa.

Uislamu hauwezi kwenda mbele kwa mindset zetu waislamu wengi zilivyo na wala tatizo sio yule mtu.

Kwa sababu shida inaanza kwa nini alichaguliwa huyo msijichague nyinyi waislamu ?

Kwa hiyo kama kosa ni la hao waliomchagua huyo asiyekuwa muislamu.

Tusimtupie lawama mzee nyerere wakati kuna mengi ya kwetu kwenye uislamu yanahitaji marekebisho.
 
Mtaumia sana watu wanaendelea na maisha yao, hizi mada kila siku inashushwa, mada ileile inatofautiana vichwa vya habari tu.

Wakristu wamekua watu wa kunung'unika juu ya uislamu, Kama ilivyo yanga, Wanavyonukia Simba.

Makanisa ya kilokole waingiapo makanisani wakimaliza kulia, kinachofuata kucheza mziki na baada ya hapo ni shuhuda na kuzituhumu imani zingine.
Hawa wanaoandiki hizi habari kila Siku ni wale wanajiita walokole.
Kwa hiyo mimi kwa kutoa bandiko hili nishakuwa mkristo sio ?

Waislamu tuna shida sana.

Juzi shekhe wa mkoa kasema ukweli kwamba wakristo wametuzidi katika elimu na afya basi waislamu wamwlaani vibaya na kusema yule shekhe ni kafiri tupu.

Sasa kwa akili za waislamu kama hizi huo uislamu wataufikisha wapi zaidi ya kulaumu tu.
 
Hayo unataka yafanyike katika nchi isiyo na dini?
Swali lako limekosa maana kwangu kwa sababu sistahiki kuulizwa mimi kutokana na mada yangu.

Labda uliweke vizuri.
Yaani wasio waislam wanyanyasike kwa sababu kuna watu wamefunga?

Halafu maana ya kufunga ni ipi kama wewe kwa vyakula tu unashindwa kudhibiti nafsi yako?
Soma mada vizuri alafu ndio uje uulize.

Au quote kipengele unachoona kimekupa shida kisha unauliza.

Sasa hayo maswali yako sijayaelewa mkuu
 
Hayo unataka yafanyike katika nchi isiyo na dini?
Swali lako limekosa maana kwangu kwa sababu sistahiki kuulizwa mimi kutokana na mada yangu.

Labda uliweke vizuri.
Yaani wasio waislam wanyanyasike kwa sababu kuna watu wamefunga?

Halafu maana ya kufunga ni ipi kama wewe kwa vyakula tu unashindwa kudhibiti nafsi yako?
Soma mada vizuri alafu ndio uje uulize.

Au quote kipengele unachoona kimekupa shida kisha unauliza.

Sasa hayo maswali yako sijayaelewa mkuu
 
Kwanza kabisa naamini wana jamvi mko salama kabisa.
Ninaamini swala la kuabudu ni la kila mmoja kulingana na imani aliyonayo kuhusu dhehebu au dini anayohusiana nayo.

Kwanza kabisa naomba kuanza kwa kusema wenzetu wakristo dhehebu la wakatoriki, walipoanza kufunga wala hawakuweka masharti watakapokuwa wamefunga wafanyiwe nini!!!

Lakini ndugu zangu waislam wanataka wakiwa wamefunga watu wasifanye shughuli zao za kila siku zinazowaingizia kipato kwa mfano wamama wanaopika chakula kwa ajili ya kujipatia kipato ati waache kisa waislam wamefunga.

Ninaomba kujua, kwani mfungo wenu ili uwe kamili ni lazima nyie waislam msiwe karibu na watu wanaokula au kupika vyakula vyao?! Kwa mtazamo wangu siyo sawa.

Mchungaji mmoja jina kapuni aliwahi kuhoji mbona Airport kuna msikiti lakini hakuwahi hata kujibiwa, na mchungaji huyo anadai kwamba alipotaka aingie msikitini akasali kwa kuwa ni nyumba ya ibada alikataliwa kwa sababu ya kwamba ni mkiristo, je wakristo wanaosafiri kwa usafiri wa ndege je wao wakaabudu wapi?? Au wenye nia ya kusali au kuabudu wakiwa kabla hawajasafiri ni waislam tu??

SIJAJUA KAMA NI UDINI LAKINI KAMA NDIYO BASI ONDOA UDINI TUISHI KAMA NDUGU.

Jambo lingine ambalo leo nimeshangaa, hapa tanga sehemu moja panaitwa forodhani, kwa chini yake kuna sehemu panaitwa DEEP SEA, huku bana kuna maisha
Ya raha sana, lakini kitu ambacho kimenishangaza kuna msikiti ambako pia ni eneo la serikali, lakini hakuna kanisa, hiii ikoje jamani. Au wakristo wenyewe ndo hawajaomba ridhaa ya kujenga kanisa hapa bandarini na kule Airport??

Naomba kuwasilisha kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
(Nadhani) Sina uhakika sana, lakini kwa ninavyofahamu waislamu wanaswala zao za faradhi (lazima) ambazo zina muda maalum wa kuziswali.
Na kwenye kuswali lazima mwili uwe safi, nguo safi na sehemu ya kuswalia iwe safi yaani (twaahir-aka tohara), ndio maana penye jumuia kubwa Waislamu wanapigania sana wawe na sehemu kama hiyo iliyo karibu na walipo.
Tofauti na upande wa pili kule hata uwe na mavi na mikojo na najisi nyengine mwili nzima au kwenye nguo au sehemu panapofanyiwa ibada haina dhara unaweza tu kuendelea na ibada yako unayo jiamulia muda wa kuifanya.
Utofauti ndio huo lakini sio kwamba Waislamu wao wanajiona special saana kuliko wa dini nyengine.
 
Mbona Zanzibar hawako mbali?
Ushawahi kwenda zanzibar au unasikiliza story za vijiweni sasa zanzibar unafananisha na huku kule mtu wa kawaida kuwa na gari washazoea kiufupi vitu bei chee na wangekuwa mbali zaidi kama wangejitenga wakabaki wenyewe kula hakuna mambo yenu ya vitu kupanda bei wala hakuna mafisadi yanayokula hela za wananchi huku yanachekelea.
 
Mkuu wbu acha mawqzo mgando kwamba eti kuna mtu alikwamisha uislamu huu ni uongo wa wazi kabisa.

Uislamu hauwezi kwenda mbele kwa mindset zetu waislamu wengi zilivyo na wala tatizo sio yule mtu.

Kwa sababu shida inaanza kwa nini alichaguliwa huyo msijichague nyinyi waislamu ?

Kwa hiyo kama kosa ni la hao waliomchagua huyo asiyekuwa muislamu.

Tusimtupie lawama mzee nyerere wakati kuna mengi ya kwetu kwenye uislamu yanahitaji marekebisho.
Alichaguliwa kwasababu alikidhi vigezo vilivyokuwa vinatakiwa kwa wakati ule sasa mzungu wa kipindi hicho ampe uongozi muislamu atamuendesha vipi waislam walikuwa matajiri toka zamani na mpaka leo matajiri wakubwa nchini ni waislamu hao waendelee kuhudhuria ndoa za jinsia moja kanisani na kuoa mke mmoja mpaka unakufa maana ndo ujanja waliobaki nao kiufupi wakristo waliigeuza nchi ya kwao ngoja siku waingie anga zetu kwenye mitihani walikuwa wanakata jina la mwamedi wanaweka Johnson na Jacob sema waislam tumetoka mbali pongezi kwa kigoma malima kwa kutupigania vijana wake sasa kuna waislam wasomi.
 
Najua zaidi ya ujuavyo. Mwislam Safi na Mwenye maadili ya dini hawezi kumwita binadamu mwenzako kafiri au mshenzi.
Umefail na huna sifa ya kuitwa mwislam. Jina likufaalo ni unafki.
Daah! Hii nchi katiba mpya inahitajika haraka sana
 
Back
Top Bottom