Udhaifu wa hoja kwamba Hamza alitekeleza mauaji kwa sababu alidhulumiwa na polisi

Udhaifu wa hoja kwamba Hamza alitekeleza mauaji kwa sababu alidhulumiwa na polisi

Kuna watu mitandaoni wanadai ya kwamba Hamza alifanya alicho kifanya kwa sababu ya kulipa kisasi baada ya kudhulumiwa madini yenye thamani kubwa siku Chache kabla ya tukio...


Kwa wafanya biashara ya madini wanajua kwamba mfanya biashara ya madini anapo enda kuuza madini yenye thamani kubwa iwe ni kwenye soko halali au kwenye black market huwa anakuwaga heaveily armed au at least anakuwa armed..

So kwa vyovyote vile Kama Hamza alienda kuuza hayo madini kweli maana yake na yeye alikuwa na silaha .

Sasa basi hivi kwa ukakamavu na ujasiri alio uonyesha Hamza siku ya tukio unadhani angeweza kukubali kudhulumiwa madini yake kiboya kweli?

Mtu mwenye ujasiri wa kuwafuata Askari POLISI kwenye kibanda Chao na kuwaua kwa risasi Kisha kuchukua silaha zao na kuendelea kutamba nazo huku akitafuta Askari wengine , unadhani anaweza kupeleka madini yake mahali kuuza akadhulumiwa halafu eti aondoke bila kufanya Jambo lolote wakati ana silaha ya Moto?

Nope isinge wezekana hata kidogo. Angekufa na watu wengi siku hiyo hiyo na kila kitu kingekuwa wazi.

Nilicho gundua kuhusu watanzania wengi ni kwamba you people are a poor judges of character.

Kusema kwamba eti Hamza ALIDHULUMIWA madini yake siku kadhaa kabla ya tukio ni kumkosea heshima Hamza.

Kwa ujasiri alio uonyesha siku ya tukio isingewezekana hata kidogo kudhulumiwa bila yeye kufa na watu saa hiyo hiyo wakati ana dhulumiwa.

Kusema Hamza ALIDHULUMIWA madini siku Chache kabla ya tukio ni kumdhalilisha Hamza.

Nadharia ya Kamanda Siro na jeshi la POLISI kwamba Hamza alifanya alicho kifanya kwa sababu za kigaidi Ina make a lot of sense.


Oooh alikuwa mtu mzuri alikuwa anatoa misaada.. kwani nani alikwambia gaidi huwa anajionyesha mtaani ?

Hawa magaidi huwa wanaishi double life. Hata Osama Bin Laden alikuwa mtu mzuri Sana katika jamii inayo mzunguka tena alikuwa shabiki mzuri Sana wa Arsenal.

Ugaidi ni ideology sio personality.

Mtu anaweza kuwa mwema kabisa katika mambo mengine lakini ndani yake ana agenda ya ugaidi.

Oooh alikuwa mfanya biashara wa madini anamiliki mgodi ...

Hivi Alie kwambia magaidi wanakuwaga masikini wasio na shughuli za kufanya nani?

Ma expert wa anti terrorism duniani kote wanajua kwamba magaidi huwa na mitandao mikubwa na huwa na watu wanao wafadhili kipesa nk.

Hivi unadhani Osama na Al Qaeda walikuwa wanapata wapi pesa za kufanya operations zao?

Acheni kuwaza Kama watoto wadogo.
Umesema kweli

Hamza alikua gaidi ama aliyerukwa na akili basi.
 
Kwa jinsi linajadiliwa suala hili naona kabisa Tanzania inajitengenezea uwanja kwa hao jamaa

Mpk sasa kuna wanaomtetea hamza na kuna waliohitimisha ni gaidi .ila naona tunatengeneza bomu
 
Kwa jinsi linajadiliwa suala hili naona kabisa Tanzania inajitengenezea uwanja kwa hao jamaa

Mpk sasa kuna wanaomtetea hamza na kuna waliohitimisha ni gaidi .ila naona tunatengeneza bomu
Waache waendelee kutetea ujinga
 
Kwanini kaua Askari sio wale raia waliokua kwenye eachier?
Swali la kitoto kweli. Wale hazikuwa siku zao zimefika. God just protected them and in addition to that at that time hawakuwa threat kwake ... Nakuombea next time tukio kama.hilo lilitokea apigwe risasi ndugu yako wa damu ambae sio Askari halafu uje ku uuliza swali la kihanithi hapa. ..
 
Huyu jamaa inaonekana aliamini polisi(Sirro) ana bifu Na waislam.
So kajitoa muhanga kulipiza kisasi...Huo Ni ugaidi nonetheless
 
Hujajibu swali langu mkuu !!

Majibizano ya risasi kila mtu ameona... Je, Wewe una ushahidi unaoonesha dhahiri Hamza akiongea hayo maneno ?

Kama unayo tuma hapa tuichambue.
Basi hata ushahidi wa hamza kuongea maneno ya kigaidi na kuonyesha yeye ni gaidi kila mtu ameona labda wewe ndio hujaona, fanya jitihada zako uone ndio uje hapa tujadiliane.
 
Lile gaidi limeua askari ikitakiwa litolewe lichapwe risasi tena
 
Huyu jamaa inaonekana aliamini polisi(Sirro) ana bifu Na waislam.
So kajitoa muhanga kulipiza kisasi...Huo Ni ugaidi nonetheless
Ukiita kisasi inakubalika vzr, ila sio ugaidi..

Haiwezi kuwa ugaidi kama raia hawakuuliwa na walionekana wakiranda mbele yake !!

Hichi kitu ndo mnashindwa kuelewa !!
 
Gaidi ni nani? Nini maana ya ugaidi? Ni vitendo vipi vikifanywa vinakuwa ni kitendo cha kigaidi? ( Ugaidi wa kujitoa mhanga )

Kisasi ni nini? Nini maana ya kisasi?


Ushawahi kuona ama kusikia raia wa kimarekani amevamia uwanja wa mpira, sinema ama popote kwenye halaiki na akaanza kuwamiminia risasi watu woote walio mbele yake? Huwa anaitwaje mtu wa kariba hivyo? Tuchukulie ni mzungu wa kuzaliwa eneo husika, husema mtu aliyejihami kwa silaha ameuwa watu kadhaa naye auawa, hutafutwa sababu ya kufanya hivyo na baadae ripoti ya uchunguzi hutolewa kabla ya kisema ni tukio la kigaidi. Bali ni tukio la mauaji dhidi ya raia ama polisi.

Uislam wa Hamza haumfanyi kuwa Gaidi, lakini inawezekana tukio alilolifanya likawa ni la kigaidi, anaweza kuwa ni muuaji wa kujihami pia. ( Uchunguzi ni pamoja na kujua yale mafunzo aliyapata wapi, sio mtandaoni, silaha aliipata wapi, sio kwa kudownload, maana mpaka upate kibali cha umiliki wa silaha, process huanzia ngazi ya serikali za mitaa mpaka Central Police huyu jamaa ilikuwaje akaipata hiyo bastola? Ina maana tangu huku ngazi za chini walishindwa hata kugundua ana viashiria vyovyote vya ugaidi mpaka akafikia kupewa kibali cha kumiliki silaha?

Ni kweli ukiangalia video kwa ushabik utaona kabisa huyu jamaa alikuwa na kisasi zaidi na polisi ( chuki dhidi ya polisi ) kwanini polisi zaidi? Na sio raia? Wamemfanya nini jawa walinzi wa raia na mali zao? Kwanini achagie eneo lile la ubalozini? Balozi zaidi ya nne? Alikiwa anataka kufikisha ujumbe gani? Je kwenye balozi hisika? Ujumne kwa nchi ama ujumbe kwa jeshi la polisi? Je tukio lile limetokea kwa bahati mbaya ama lipo organized? Mtiu asiyepitia mafunzo hawezi funga barabara kwa zidi ya dakika tano hasa kwenue eneo muhimu kama lile,

Kama hamza ni Gaidi kama report ilivyotoka basi kuna haja ya kuwatafita na wengine wenye mawazo sijui niite ama nini maana bado suala hili ni tata kuliko majibu tuliyopewa, maamini hili bado lipo katika uchunguzi wa kina na si busara pia kutolewa maelezo meengi sababu ni kazi ya vyombo vya ulinzi na usalama, sisi raia tukubaliane na reports zote.
 
Wengi wanaomsingizia Hamza kuwa ni gaidi wanashindwa kujibu hili swali na kujikuta wamenasa kwenye mtego !!

Tangu lini gaidi aone raia kisha asiue hata mmoja ? Na kama wapo mtupe ushahidi wa kimataifa.

Hapa chini nimeweka maana ya Terrorism :

" the unlawful use of violence and intimidation, especially against CIVILIANS , in the pursuit of political aims."
A good lawyer must not be the one who looks at the law as it is written in the statutes but the one who look at the law as it is supposed to be
 
Mmeona Hamza akitamka kutoka kinywa chake ? Una hakika gani kama ni kweli na sio uzushi ?
Swali zuri, ndio maana kabla ya kujibu swali lako la kwanza nikakuuliza ushahidi wa hamza kurushiana risasi umeutoa wapi, ukasema uko wazi kila mtu ameona, vizuri.

Sasa swali langu la msingi ambalo linaendana na swali lako pia, una ushahidi gani kama yule ni hamza ama una ushahidi gani kwamba zile video clips zote ulizoona ni real na hazikua staged? Pia kama ni hamza, unaweza kusema zile bunduki alizitoa wapi? Je una ushahidi kwamba hamza aliua wale askari na sio mtu mwingine na akasingiziwa hamza? Huo ushahidi umeutoa wapi?

Najua majibu ya hayo maswali huna, kama huna maana yake unajifanya kua dogma, unachagua ushahidi, kwamba huu ni real na huu sio real ku fit your narratives and definition of the events.

Hata mimi naweza kukataa kwamba yule hakua hamza na wala hamza hajauwawa na ile event ilikua staged, ama nikasema hamza hakuua polisi, walimsingizia ili kupata sababu ya kumuua ama ile event yote ilikua fake, huwezi kunilazimisha tofauti na hivyo.
 
Then tell me the criterias for an act to be considered as a terrorist act,,
Support your answer with a formal proof..
Ur not in a lecture room . Use ur common sense HOJA yAngu ipo kwenye thread yangu
 
Ndo maana nikakwambia nioneshe huo ushahidi /video inayoonesha Hamza akitamka hayo maneno kutoka kinywani chake,and not otherwise.... mpka sasa hujatuma...

Niulize mm ushahidi kuonesha Hamza na polisi kama walirushiana risasi nikutumie chap !!

The event would have been referred to as terrorism, if at least one innocent civilian was killed..
Tuachane na hayo mambo ya ushahidi, I am now interested na hii definition yako ya terrorism.

Kwamba terrorism ni pale tu raia akiuwawa, right?😂😂.

Kwa mfano mimi nikiua mtu tayari ni ugaidi huo, mimi ni gaidi, sio?.

Aisee.
 
Mbona kama wewe ndio kilaza wa kufikiri na kuchambua?
 
Huu uzi wa kijinga Sana ..mods ilibidi muwe mnafuta nyuzi Kama hizi.
 
Back
Top Bottom