Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Aliyeandaa ile taarifa kama hakukurupuka basi ana agenda ya siri ama hakuwa timamu kiakili, tangu kuiandaa mpaka kuisoma na pengine sasa anajutia makosa ya wazi yanayoacha shaka kubwa!
Jamii, wazazi na ndugu wa marehemu wana hamu ya kujua ni nini hasa kilimaliza uhai wake! Baadhi wanatuhumu kwamba aliuawa akiwa mahabusu na wengine wanahoji daktari polisi imekuwaje awe sehemu ya watuhumiwa?
Pengine jeshi la polisi litakuja na ufafanuzi utakaoondoa ukakasi na lawama kwenye tukio zima lililoondoka na uhai wa mmoja wa watuhumiwa. Kuna maswali 10 common itabidi yapate majibu
1. PGO ya polisi inasemaje inapokutana na tukio la mtu kujinyonga?
2. Je, kuna picha zozote za ushahidi zilichukuliwa? Ili kuja kuondoa shaka baadae?
3. Je, selo ya mtumiwa ilikuwa salama kiasi gani kuweza kumhifadhi mtuhumiwa muhimu kama yeye?
4. Je, ni nani aliweka tambara la deki ndani ya selo? Na kwanini halikuondolewa?
5. Je, tambara la deki lililotumika kama kitanzi lilifungwa eneo gani la selo? Darini? Dirishani? Kuna ushahidi wowote wa picha?
6. Report ya PM haijawekwa wazi lakini ni wazi kwamba shingo itakuwa na michubuko ama alama ya kitanzi
7. Je, kama picha zilisahaulika kupigwa ni nani mashuhuda wa tukio? Wa kwanza kuona na waliohusika kuushusha mwili?
8. Kwa kawaida mtu akijinyonga lazima ama atoke haja ndogo au kubwa. Je, nguo za marehemu alizovaa wakati anajinyonga zimehifadhiwa kwa ushahidi?
9. Je, tambara la dekio alilotumia kujinyongea limetunzwa vema kama kielelezo?
10. Je, ni nani alithibitisha kuwa marehemu kajinyonga na hakunyongwa?
Mpaka sasa taarifa rasmi ya ufafanuzi iliyotoka ni namna ya kuzikwa kwa askari aliyekufa ambayo hata hivyo imezua mjadala na kuzidisha utata kuwa kwanini itoke kipindi hiki.
Maswali 10 husika hayajatolewa taarifa wala ufafanuzi wowote mpaka sasa.
Pengine hili litafanyika kabla tetesi hazijawa habari kamili na kuzidi kulichafua jeshi letu la polisi