“Mheshimiwa Waziri (Hammad Masauni- Waziri wa Mambo ya Ndani) umezungumzia mauaji Mwanza, yapo yaliyofanyika Mtwara na Jeshi lako ndio lililofanya mauajia, taarifa nilizonazo ni kuwa jeshi limetengeneza kamati ya kuchunguza, haiwezekani jeshi lifanye mauaji, alafu lijichunguze lenyewe, ndugu zangu wananchi na watanzania, nimemuelekeza Waziri Mkuu aunde kamati huru nyingine ikafanye uchunguzi wa mauji yaliyofanywa na jeshi la Polisi tulinganishe taarifa tuchukue hatua.
"Wakati huo huo nataka jeshi lako lijitafakari kinachotokea ndio misingi ya jeshi au vinginevyo.
Nawaombeni wananchi kulinda amani kutokufanya mauaji kwa sababu yoyote ile, tusaidie kuleta amani kwenye nchi ili kuleta maendeleo, kusipokuwa na amani, tutashughulika kutafuta amani na maendeleo yatasimama,” Rais Samia Suluhu, ziara Mwanza
#dailynewsdigitalupdates #habarileoupdates