Udhalilishaji: Video ya PNC akimuomba msamaha Ostaz Juma na Musoma

Udhalilishaji: Video ya PNC akimuomba msamaha Ostaz Juma na Musoma

Wabongo saa nyingine mi hata siwaelewi, yaani mtu kuona video tu mtu anaomba msamaha mshaanza kuhukumu!!! Wengine hata hawajui kisa ni nini lakini mishipa imewashupaa hiyoooo!!! Mleta hebu tupe habari kamili, kosa la huyu dogo ni lipi hasa hadi kufikia hatua hiyo?
 
Mkuu hapo kweli mi nawewe tuna View za kitofauti, kama kwako kudharirisha mpaka iwe picha za uchi duh???Je Waweza kushare nasi mtu mzima yeyote mwenye umaarufu aliyewahi omba msamaha kwa kumpiga mwenzie magoti na kuchukuliwa kwa video kisha kutupwa mitandaoni??One thing hapo kwa blue, U missed my point, SIJASEMA KUOMBA MSAMAHA NI KUJIDHARIRISHA/KUDHARIRISHWA maana hakuna ambaye hajawahi Omba msamaha kijana!!ila swala hapo ni kuchukuliwa video unaomba msamaha ukipiga magoti kisha isambazwe kwenye social N/W.

Bado nasimamia pointi yangu ndugu......tuifute hii dhana ya kuwa kuomba msamaha ni kujidhalilisha....

kwani bila hiyo video jamii mngejua vipi labda kuna vitendo vingi vya (udhalilishaji kama mnavyoita) vinaendelea kwa mitindo kama hiyo.......

kwa hiyo mnaridhika kudhani mambo ni sawa kwa kuwa tu huwa hamjui/hamtaki kujua yanayoendelea nyuma ya pazia kwa wasanii au wafanyakazi wa kada nyingine kama hseboys na hsegirls ?

Hamuoni kwa kupitia video hii mmegundua kitu ?

Ndio maana nimehoji kujua ni lipi haswa lilikuwa lengo la kutoa hiyo video...coz sifahamu....je ni stunt ama ?......ila kama lengo la ustaadhi Juma ilikuwa ni kumdhalilisha pnc, basi kwa matazamo wangu amebugi...

Nadhani ndio kwanza amempa dogo chati a.k.a boost, kwani sympath iliyojengeka ndani ya jamii juu ya pnc kwa video hii. , pnc aitumia kama FURSA kurudi kwenye game.
 
Ostadhi Juma na Musoma: "Watanzania wanaona kama tunawazurumu wasanii ama tunawanyanyasa. Ndio PNC kunipigia magoti na kuniomba radhi, lakini sasa mimi nikaamua kuwaonesha watanzania kwamba PNC amerudi kweli kuniomba msamaha. Je, kama kweli PNC alikuwa analalamika ‘Ostaz anafanya kazi zake hanijali hanisaidii…' Alisema Ostaz Juma.
"Mimi kitu ambacho kinachoniumiza zaidi ni kile ambacho wasanii ukishawasaidia wakasimama wanaonekana, wanaanza kuwa wanafanya vitu vibaya wanasnitch yaani wanadharau na tabia mbovu wanamdharau boss wao na ndio maana nikawa nimekataa baadhi ya wasanii wote." Aliongeza.

"Lakini kweli PNC karudi kuja kuomba msamaha na mimi nikampa option, kama akitaka nimsamehe lazima arudi kwenye vyombo vya habari kama alivyoenda mwanzo, akawaombe msamaha watanzania na aniombe mimi msamaha kupitia vyombo vya habari ndio mimi ntamsamehe." Ananukuliwa Ostaz Juma.


PNC: "Mimi naweza nikasema ni kawaida tu, kwa sababu kuomba msamaha pia ni kitu cha kawaida sio tatizo. Mimi nimefanya hivyo kwa maana yangu tu najua mwenyewe nimefanya hivyo kwa sababu bado nahitaji kufanya kazi zangu ziende. Kwa hiyo sasa nikisema niwe kiburi nini…japokuwa sijakosa mimi ila mkubwa anapoona kuna makosa akawajumlisha wote inabidi mjishushe saa nyingine, ujichukulie kama mdogo sio na wewe unaanza kuwa una viburi na jeuri. Nimeshakaa kwenye game…muziki nimeuanza muda najua madhara yake ni yapi. Kwa hiyo nimefanya tu kawaida kumwambia bwana mambo haya yaishe na nini tufanye mambo yetu.

"Kwa sababu yeye mwenyewe kitu kilichokuwa kinaongeleka kwake ni lawama zake kwamba mimi nilimletea watu, mwisho wa siku wamekuja kuharibu mambo yake mpaka wanafikia hatua ya kufanya mambo mengine wanamkana na nini. Sasa mimi ukiangalia ukweli mimi ndiye niliyewakaribisha wasanii wote waliokuwa Mtanashati. Lakini sio kwamba mimi ndio niliyekosea kwamba nilikosea…mimi sikugombana na Ostaz ila niliona kimya nikaanza kuona hapa kazi hazieleweki nikaamua kusema kama vipi siko Mtanashati. Ila mwisho wa siku nikaa kuongea nae nikajua tatizo liko wapi. Kwa hiyo ikabidi nimweleze bana kama vipi basi tusameheane mambo hayo yaishe tufanye kazi.
"Ukiangalia kwenye hizi picha, nimeziona hizi picha na kuna watu wanaandika mambo yao ya ajabu ajabu wanadiss, lakini mimi naona sawa tu kwa sababu kupiga goti na kumuomba mtu msamaha sio kwamba umemsujudia yeye ndio Mungu hakuna. Ni kama umeonesha heshima tu kwamba wewe ni brother. Ukiangalia mimi silingani nae umri hata kidogo na huyo mtu ndio mtu ambaye hata kwa ndugu zangu anaongea nao.
"Kwa hiyo fresh tu nimeomba samahani kama brother angu. Potelea mbali maneno yataongeleka yataenda yatapita, mimi kazi zangu ntaendelea kufanya."


SOURCE:Audio: PNC Afunguka Baada Ostaz Juma Kuweka Picha Ikionesha Anampigia Magoti, Ostaz Nae Aleleza Sababu Ya Kupost Picha Hiyo - Times FM 100.5
 
hawa wasanii hata kama wananyonywa wajitahidi kuishi kutokana na kipato chao na si u-maarufu wao hawatafikia hatua hii.
 
huyu PNC na huyo pimbi juma musoma nna uhakika asili yao si dar es salaam wala mji wowote mkubwa afrika....watakuwa watu wa mkoani tu!............watu tuliozaliwa miji mikubwa na tukakulia miji mikubwa tabia zetu zinajulikana,hatuwezi kufanya huo upimbi uliofanywa na hao watu wawili wa mkoani
 
huyo ustadh kakosea sana kumdharilisha PNC, haya ni maisha haijui kesho ya PNC au yake itakuweje hakuna anayejua kesho
 
huyu PNC na huyo pimbi juma musoma nna uhakika asili yao si dar es salaam wala mji wowote mkubwa afrika....watakuwa watu wa mkoani tu!............watu tuliozaliwa miji mikubwa na tukakulia miji mikubwa tabia zetu zinajulikana,hatuwezi kufanya huo upimbi uliofanywa na hao watu wawili wa mkoani
Jumana Musoma ni tapeli kutoka Mwanza aliyetapeli sana watu kwa kujifanya mganga wa kienyeji na huyo pimbi mwingine naye ni wa Mwanza pia. Hawa wote ni wakuja tu.
 
Kuna mikoa mingine huku Tanganyika hiyo ni sehemu ya salaam kwa kijana ambae hajaoa!
 
huyo ustadhii hata nguruwe ni mzuri kuliko yeyee mtu gani hana utuu
ashajifanya mungu mtuuu:israel:
 
huyo ustadhii hata nguruwe ni mzuri kuliko yeyee mtu gani hana utuu
ashajifanya mungu mtuuu:israel:

Sura kama spanner ya canter, kumbe ndo ostadh juma alivyo? Bora elimu ingekuwepo sasa , elimu hana mmh full masnura
 
Haramu ni kuabudu sanamu la mzungu! Na picha yake!

Muziki ni ktk matendo yaliyokatazwa ktk uislamu na mwenye kutafanya hastahili kuitwa Ustadh!

Lkn all in all HAKUNA HARAMU KUBWA KAMA KUABUDU SANAMU NA PICHA YA MZUNGU!

Hivi jiwe sio sanamu ? kuna watu kutwa mara tano wanasujudia jiwe fulani liko Mecca linaitwa ka'aba.
 
Hivi jiwe sio sanamu ? kuna watu kutwa mara tano wanasujudia jiwe fulani liko Mecca linaitwa ka'aba.

Andiko please! Sio kuniandikia utumbo mkavu.
Nipa andiko wapi watu waliambiwa wakasijudie mawe huko mecca

Anae sujudia jiwe au sanamu ya mzungu aliovaa nepi wote hao ni watu wa jahanamu ya moto!
 
Andiko please! Sio kuniandikia utumbo mkavu.
Nipa andiko wapi watu waliambiwa wakasijudie mawe huko mecca

Anae sujudia jiwe au sanamu ya mzungu aliovaa nepi wote hao ni watu wa jahanamu ya moto!

Tena nepi yenyewe Ina miba miba pembeni...yaani hawa jamaa uwezo wao wa kufikiri ni F
 

PNC AKIMWOMBA MSAMAHA USTAZ JUMA - YouTube

Mimi kama mdau wa muziki wa kizazi kipya napinga na kulaani huu udhalilishaji wanaofanyiwa wasanii wetu.

Nimestushwa kuona hii video inayosambaa kwenye social network ambayo member wa zamani wa kundi la Watanashati PNC akiwa amempigia magoti don wa kundi hilo Ostaz Juma Namusoma huku akimwomba msamaha.

Hakika hii video inaondoa thamani ya wasanii wetu na kuonesha kuwa bila hao wanyonyaji wanaojiita mameneja wa wasanii basi muziki sio kitu.

Na nyie wasanii muwe na msimamo thabiti na sio kuhama hama makundi kama malaya na ndiyo maana mnaishia kudhalilishwa kwa ujinga wenu.

Na ninyi madon wa muziki acheni kudhalilisha wasanii,kwa kuwanyonya inatosha tu na sio kuanza kuwaanika kwenye mitandao mambo wanayofanya.Mimi sijafurahishwa kabisa na hii video.

Narudia tena; Nalaani vikali huu udhalilishaji kwa wasanii.

attachment.php

Wasanii wanaojiita wasanii hawajitambui na hao wauza unga wanaojiita mabosi hawajitambui,yaani ni kama Pipa na mfuniko,huyo Juma zuzu tu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom