Udhalilishaji wa Kijinsia Arabuni wavuka Mipaka - Achezea vibao Hadharani

Udhalilishaji wa Kijinsia Arabuni wavuka Mipaka - Achezea vibao Hadharani

Hawa jamaa ndio wametuletea Hizi dini huku Afrika ila sasa wao hawaheshimu kabisa Wanawake.
Wabillah Taufiq
Halafu hata ikiwa kweli kwani waarabu wote ni waislamu?

Waliokuwa wanapinga uislamu na mtume ( saw) hawakuwa waarabu tena kabila la mtume?

Halafu hata akiwa muislamu, muislamu hakosei? na akikosea inakuwa kakosea yeye au dini?
 
Mimi sio 'I'm proud to be' lakini huyo mama ndo kaanza kumpiga poti, hapo tuseme tu wamegombana na poti ameshinda
 
Imagine unaambiwa na afande Kombo au Mwita kuwa usipite hapa then ukamchapa na Kofi, Nina uhakika mwili wako kama hautakuwa pale MOI unafanyiwa ukarabati na nyuzi zaidi ya mia Tano mwilini mwako au ukazikwe pale kisutu...unamchapa askari Kofi tena umemuanza?
 
🤣🤣🤣🤣 huyo mama atakuwa si jamii ya kina mudi, sema ameforce tu kuvaa hizo hijab ili aheshimu tamaduni zao. Alivyoona jamaa anamletea zengwe kawasha kofi 🤣🤣🤣 hiyo siyo kwa kina mudi tu, hata bongo umpige kofi police, watakuua tena naona hao wamefanya ustaarabu kurudisha kofi moja
 
Udhalilishaji huu haukubaliki. Wafia dini wa Kisiju tunalaani kwa nguvu zote.
Achaaa ushabiki mandazi,mama ndo kaaza kumpiga kibao afande,alafu mama anajiona jeuri,wamezuiliwa anapita kwa kiburi,ana bahati angekulaa mitama kabisa.tusi shabikie upumbavu kwa kujificha kwenye haki za binadamu.nyau nyieee
 
Uwache chuki na uislamu.
kulingana na kipande hiki cha video, hii inaonekana dhahir kwa aliyekosa adabu ni mwanamke aliyeanza kumzaba kibao askari. Askari amechukua hatua kwa kurejesha kibao kwa raia ambae ni mwanamke.

Hivyo ulitamani askari akubali udhalilishaji aliofanyiwa kisa aliyeanza kidhalilisha ni mwanamke?

Wanawake wanahaki na wajibu wao katika jamii kulingana na mila na desturi za jamii husika. Hivyo ni wajibu wao kuheshimu haki za wengine na mipaka ya kisheria na kikanuni katika maeneo husika.

Uislamu umemtukuza mwanamke kwa kumstiri na kumuekea heshma yake mbele ya jamii. Hivyo hata wao wenyewe wanapaswa kujiheshimu kwa kuheshimu sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa kuwalinda na kulinda jamii na uovu hasa unaotokana na wao wanawake.

Nakushauri ukitaka kujenga hoja za kulaumu imani ama dini fulani, usichukue matendo na tabia za wenye dini husika, kwa kiwa wao bado ni binaadamu na wanatabia zile zile za kibinaadamu kabla ya kufungamana na dini, wakiwa wenye kufuata vyema maamrisho ya dini hawawezi kifanya nje ya sheria na taratibu za dini husika ila wakikengeuka watafanya kinyume chake.

Usilamu kama dini, una ukamilifu wake, karibu kuusoma na kuufahamu na anza kuukosoa kwa hoja kutokana na unachokifahamu kuuhusu.

ACHA MIHEMKO, JENGA IMANI YAKO KWA DINI YAKO, ENDELEA KITAFUTA PESA NA UHESHIMU DINI YAKO NA DINI YA MWENZAKO.
 
Jaribu kumpiga Kofi mwanajeshi pale getini lugalo.ndio utajua haujui.unaipiga Kofi jamuhuri
,ndugu zako watakukuta moi unachomelewa
 
Magalatia extremists kutoka vikanisa uchwara ambao wamejaa hapa Jf ni watu wa hovyo sana na wengi wao hawaka akili .

Mtu akishiba makande anawaza chuki tu bila sababu za msingi.
 
Nachukua nafasi hii kulaani kitendo hiki cha kinyama na kudhalilisha utu wa mtu

Kwa niaba ya Waisilamu wote wa Yombo kituka, nakemea vikali jambo hili

Kama vipi tuwaachie dini yao
😎
 
Back
Top Bottom