Matatizo ya waislamu yameanza siku nyingi,lakini mimi kwa umri wangu mkubwa nilio nao sijawahi kusikia au kuona muislamu akionewa,akinyanyaswa na mkristo kuanzia shule ya msingi hadi chuo nilichosoma eti kwa kuwa tu ni muislamu,kwa maoni yangu ni kwamba waislamu hawajiamini na dini yao kwamba ni ya kweli.kama dini ya uislamu imetoka kwa Mungu wao wana wasiwasi gani juu ya wengine? wafuate dini yao inavyosema,wawapeleke watoto shule na sio kubaki kusema tu Wakristo wanapendelewa.Siku zilizopita waislamu walichoma makanisa Zanzibar kisa muungano,lakini wakristo hawakusema lolote kwa sababu wanamtegemea Mungu atawapigania,jiulize ingekuwa msikiti umechomwa moto sijui ingekuwaje.
Bwana Erick kwa kuwa umesema una umri mkubwa ni wazi mie nawe tutakuwa tunalingana umri.
Kwa jili hii hata mijadala baina yetu itakuwa ya kiungwana zaidi.
Bahati mbaya inaelekea hujui nchi yetu inatawaliwa vipi na nani kashika madaraka na hayo madaraka yamepatikanaje.
Lakini nina hakika ulishuhudia harakati za kudai uhuru kama ulikuwa Dar es Salaam itakuwa umewaona wazee wangu walivyokuwa bega kwa bega na Nyerere kupambana na Gavana Edward Twining.
Nimeandika kitabu "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes..." ni kitabu maarufu unaweza kukipata Tanzania Publishing House, Samora Avenue.
Kitabu hicho kimeeleza mambo mengi kuanzia jinsi TANU ilivoundwa, harakati za uhuru, wafadhili wa harakati, nini kilitokea baada ya uhuru, ugomvi katika ya Nyerere na Waislam kuanzia 1963, kuwekwa kwa masheikh kizuizini mwaka 1964, Kuhujumiwa ujenzi wa chuo kikuu cha Waislam mwaka 1968 na Nyerere na mwishowe kuivunja East African Muslim Society (EAMWS) taasisi iliyokuwa ikitaka kujenga chuo hicho Bakwata ilvyoundwa nk. nk. harakati za Waislam chini kwa chini kudai haki zaokuanzia miaka ya 1970 hadi kufika hapa tulipo leo.
Yaliyomo humo yamebadilisha historia yote ya Tanzania.
Ndiyo unaona humu JF tunajadili mambo ambayo miaka labda kumi iliyopita hakuna aliyekuwa anayajua.
Binafsi nimezunguka kwingi, Afrika, Ulaya, Marekani nikifanya mihadhara katika vyuo na kuhudhuria makongamano.
Somo hili la matatizo ya nchi yetu yanafahamika na baada ya yaliyotokea Rwanda wapenzi na marafiki zetu wanaiomba serikali yetu isipuuze malalamiko ya Waislam.
Wanashauri yazungumzwe matatizo yote bayana na kasoro zirekebishwe.
Nadhani hadi hapa umepata picha kidogo.
Kilichobaki ni wewe kufanya bidii kujua zaidi.
Kulikoni?
Ninakuhakikishia ndugu yangu hakuna Muislam anaeweza kuthubutu kunyanyua mkono wake kuchoma kanisa. Allah (SW) ametukutaza hayo. Makanisa yamechomwa na maadui wasioitakia Zanzibar kheri. Kanisa la Mkunazini lipo Zanzibar zaidi ya miaka 100 mbona Waislam hawajalitia kibiriti?
Tafakari ndugu yangu tusichonganishwe tukajagombana bila sababu na mwisho sote tukajuta tukajiuliza.
Ilikuwaje?
Majuto siku zote ni mjukuu.
Huo ndiyo ukweli.