Udhalilishwaji wa waislam na vyombo vya dola

Udhalilishwaji wa waislam na vyombo vya dola

Bwana Chama,

Ikiwa kwa hakika uanpenda kujua historia ya Bakwata kwa undani wake nakuomba tafadhali soma kitabu changu. Kisa kizima nimekieleza humo.

Hapa nafasi itakuwa ndogo na nitawachosha wanaukumbi.

Bwana Mohamed Saidi
Nimekuuliza maswali rahisi sana ambayo hata mwanafunzi wa shule za kata anaweza kuyajibu kwa ufasaha naomba unijibu kwani kwa kufanya hivyo itarahisha uelewa wangu kuhusu BAKWATA; tupo hapa kujifunza sikutaka maelezo mengi nilichokuomnba ni kitu rahisi sana TAMKA BAYANA KWAMBA BAKWATA SI CHOMBO CHA WAISLAMU; kitabu nitakisoma bila shaka yoyote ile.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Gwalihenzi;
Barubaru asikuumize kichwa ni mmoja kati ya wanafiki wakubwa hao ndio wanaodai mfumo kristo cha ajabu yeye watoto wake wanaishi na kusoma Marekani kwenye mamilioni ya wakristo; Barubaru huyu huyu amesoma chuo kikuu cha Dar es Salaam kwa sera za Mwalimu Nyerere; Barubaru amesoma Canada kwa pesa za walipa kodi wakristo wa Canada; hana jipya; kama si sera za Mwalimu Nyerere Barubaru angekuwa mvuvi Pemba au anauza Ice Cream kwa Bakhresa

Chama
Gongo la mboto DSM
Asante sana kwa uchambuzi wako makini. Barubaru amekosa kabisa uungwana, anatumia uislam kama mwamvuli kueneza chuki zake dhidi ya Nyerere! Ama kweli dunia haitaisha maajabu.
 
Hoja nzuri na zinahitaji majibu ambayo yatamfahamisha msomaji ukweli wa mambo.

Waislam wamegundua mengi katika mfumo wa serikali yetu na wameitahadharisha kuwa kuna upendeleo kwa Wakristo na hujuma dhidi ya Waislam.

Ushahidi upo.

Rejea tu matatizo ya hivi karibuni yaliyogunduliwa NECTA achilia mbali utafiti wa Warsha wa mwaka 1991 na aliyoyagundua marehemu Prof. Malima ndani ya Wizara ya Elimu.

Ingependeza kama serikali yenyewe ikatoa majibu.
Serikali iko kimya majibu yanatolewa na watu wengine kabisa kama hivi humu JF.

Somo hili mimi nimeliandikia kitabu kizima.
Itakuwa vigumu kukupa jibu humu JF.

Hata hivyo ukiwa una wasaa soma kitabu changu "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...." sehemu ya tatu ya kitabu inaitwa, "Njama Dhidi ya Uislam."

Hapo utasoma nilichosema kinachofanyika kwa miaka mingi dhidi ya Waislam kuanzia ukoloni wa Wajerumani hadi hivi sasa.

Kitabu hiki ndicho kilichonifanya nikajulikana kwingi.
Maudhui yaliyo ndani ya kitabu hiki yamegusa fikra za wasomi wengi duniani.

Haijafanyika utafiti wowote kuhusu siasa za Tanzania sharti mtafiti apitie kitabu hiki.
Hapa jamvini kitabu hiki ni mashuhuri.

Mimi niko tayari kusimama na yeyote na mahali popote kuhusu mada hii.
Mkuu jaribu kumjibu nguruvi kwa hoja...kuna hoja hapo zinahitaji majibu siyo kuishia kusema ushahidi upo...
 
Adui yako ni ujinga wako.
Bigirita, 2012.

Quote hiyo, ifanye kuwa signature yako, itaweza kukusaidia maishani.
 
Pole sana kwa yaliyo kukuta...walikushuku umebeba madawa na si kwa sababu za kidini la hasha...hii inatokana na nchi unazotembelea mara kwa mara hivyo walikuwa na haki ya kukukagua..hata polisi wakimshuku mtu wana haki ya kumpekua kwa mujibu wa sheria.Wangeamua kukumaliza wangekuwekea dawa za kulevya.hivyo walikushuku tu na si vinginevyo..
 
Siku zote Mzee wetu Mohamed Said anajitambulisha kwa UISLAM wake. Hana utambulisho mwingine. Uislamu anaoutaka sio huu wa akina Jakaya Mrisho Kikwete. Sio Uislam kama ule wa akina Salim Ahmed Salim.

Sio ule wa akina Rashid Kawawa au Mzee Ali Hassan Mwinyi. Kwake yeye hawa walikuwa Waislam ambao hawakuutendea haki Uislamu. Bila shaka Waislamu halisi katika Uongozi wa Nchi hawajapata kuwepo tangu Disemba 9, 1961!

Kwa wale mliopata kuzisoma makala zake nyingine humu mtagundua hana jipya. Ni muendelezo tu wa agenda yake hatari ya udini. Dini zingekuwa nzuri kiasi hicho yanayotokea Mashariki ya Kati wala yasingekuwepo.

Tunisia, Libya, Misri na sasa Syria wote kule ni Waislamu wanauana. Rwanda, Congo DRC, Burundi ni nchi za Wakatoliki wengi. Wameuana kwelikweli.

Mzee Mohamed, baki na DINI yako ikusaidie kutambika.
 
Kinondoni Muslim School sio shule ya waislamu??? Nimewahi kufundisha kwa muda mfupi kabla waalimu "wagalatia" kufukuzwa kwa kuwa tu ni "wagalatia" leo hii imekuwa si shule ya waislamu!! Makubwa haya!
Kwa Mzee Mohamed, chochote kinachomilikiwa, kuongozwa au kuhusishwa na BAKWATA, hicho si cha WAISLAMU ikiwemo BAKWATA yenyewe!
 
Majisifu si uungwana.
Ikiwa umeona hapo nimejisifu ukweli ni kuwa sijafanya hivyo.

Aliyetoa sifa za usomi si mie mimi nimejibu tu kuwa sijasimama katika mada ya usomi.
Kasifiwa mtu kwa "nondo" na "usomi" kuwa nimeshindwa kumjibu huyo msomi.

Ndipo nakasema sijasimama katika usomi.

Hayo unayoita "majisifu" ni maelezo yangu nifahamike kwa wasionijua.
Mkuu wangu Mohamed Said, tatizo lako ni kuwa unapenda sana kujisifu halafu unasahau ulichokwisha kisema. Kule kwetu kunausemi kuwa ukiwa muongo usiwe msahaulifu, kwakuwa umesahau bora nikukumbushe maneno yako wewe mwenyewe ya kujisifu kuhusu usomi wako;

Bwana Gwalihenzi,

Ingekuwa mie nataka kushindana humu kwa usomi nadhani ni wachache sana wangekuwa na ujasiri wa kusimama na mimi uso kwa uso.

Mimi sishindani na usomi wa Nguruvi3 na nadhani yeye binafsi hilo alishalitambua kwangu siku nyingi sana.
 
Wanajamvi,
Nimefuatilia mjadala huu nikidhani kuwa tunaijadili mada kama ilivyoletwa. Tofauti, naona takwimu za elimu na mengine yasiyo na uhusiano na mada. Ukifutailia utagundua kuwa MS anakwepa kujibu hoja na kutumbukiza mengine au zile mada zake zimewaingia vema baadhi yetu na kila mara wanazifikiri bila tafakuri.

Wanakosa tafakuri kwasababu makala za MS zinachanganya na zinahitaji utulivu na fikra kuzielewa na kuzinyumbulisha ili upate hitimisho alilokusudia. MS anauwezo sana wa kufanya majumuisho yanayoeleweka kiurahisi sana kwa wale aliokusudia (Conclusion) hata kama hawaielewi mada...
Duuh! we mzee kiboko....hii inaitwa counter attack a.k.a za uso.
Jibu la babu yangu MS hapa utasikia nimekuelewa tuendelee na mnakasha. Yaani usanii mtupu
 
Mkuu jaribu kumjibu nguruvi kwa hoja...kuna hoja hapo zinahitaji majibu siyo kuishia kusema ushahidi upo...
Hana hoja za kupambana na Nguruvi3 wala Chama eti anadai akifunguka kwa mahoja ataijaza JF yote na wanaukumbiw
atachoka kwa kusoma....hii ndiyo inaitwa za mbayuwayu changanya na zako
 
Matatizo ya waislamu yameanza siku nyingi,lakini mimi kwa umri wangu mkubwa nilio nao sijawahi kusikia au kuona muislamu akionewa,akinyanyaswa na mkristo kuanzia shule ya msingi hadi chuo nilichosoma eti kwa kuwa tu ni muislamu,kwa maoni yangu ni kwamba waislamu hawajiamini na dini yao kwamba ni ya kweli.kama dini ya uislamu imetoka kwa Mungu wao wana wasiwasi gani juu ya wengine? wafuate dini yao inavyosema,wawapeleke watoto shule na sio kubaki kusema tu Wakristo wanapendelewa.Siku zilizopita waislamu walichoma makanisa Zanzibar kisa muungano,lakini wakristo hawakusema lolote kwa sababu wanamtegemea Mungu atawapigania,jiulize ingekuwa msikiti umechomwa moto sijui ingekuwaje.
 
Pole sana kwa yaliyo kukuta...walikushuku umebeba madawa na si kwa sababu za kidini la hasha...hii inatokana na nchi unazotembelea mara kwa mara hivyo walikuwa na haki ya kukukagua..hata polisi wakimshuku mtu wana haki ya kumpekua kwa mujibu wa sheria.Wangeamua kukumaliza wangekuwekea dawa za kulevya.hivyo walikushuku tu na si vinginevyo..

Mwakijila,
Baada ya mkasa ule nikajaelezwa kisa cha kukamatwa kwangu.

Nimeeleza katika makala.
Kile ambacho sikupenda kueleza ni kuwa wakati naandika pp ile nilikuwa naingia katika web ambazo nilionywa nisifanye hivyo.

Mimi nilikaidi.

Ahsante kwa mchango wako.
 
mzee said,
awali ya yote nieleze neno linalotumika katika medani ya vita. Neno hilo ni 'shoot any moving object'.
Kauli hii inatumika majeshi yanapokuwa katika wakati mgumu, ya kwamba mbinu zote zimeisha na hakuna mkakati. Nitafafanua wakati nahitimisha maelezo yangu.

Kwa mtu asiyeielewa tanzania na utangamano wa wananchi wake wenye imani, makabila na itikadi mbali mbali za kisiasa,pindi anaposikia mihadhara yako ima anatishika sana au anajawa na hasira kama ulivyowajaza wanigeria.

........"!

nguruvi3: This is one of the best articles nafikiri bwana muhamed said atakuwa amekuelewa aache kuleta propaganda za kijinga hapa.
 
Matatizo ya waislamu yameanza siku nyingi,lakini mimi kwa umri wangu mkubwa nilio nao sijawahi kusikia au kuona muislamu akionewa,akinyanyaswa na mkristo kuanzia shule ya msingi hadi chuo nilichosoma eti kwa kuwa tu ni muislamu,kwa maoni yangu ni kwamba waislamu hawajiamini na dini yao kwamba ni ya kweli.kama dini ya uislamu imetoka kwa Mungu wao wana wasiwasi gani juu ya wengine? wafuate dini yao inavyosema,wawapeleke watoto shule na sio kubaki kusema tu Wakristo wanapendelewa.Siku zilizopita waislamu walichoma makanisa Zanzibar kisa muungano,lakini wakristo hawakusema lolote kwa sababu wanamtegemea Mungu atawapigania,jiulize ingekuwa msikiti umechomwa moto sijui ingekuwaje.

Bwana Erick kwa kuwa umesema una umri mkubwa ni wazi mie nawe tutakuwa tunalingana umri.

Kwa jili hii hata mijadala baina yetu itakuwa ya kiungwana zaidi.

Bahati mbaya inaelekea hujui nchi yetu inatawaliwa vipi na nani kashika madaraka na hayo madaraka yamepatikanaje.

Lakini nina hakika ulishuhudia harakati za kudai uhuru kama ulikuwa Dar es Salaam itakuwa umewaona wazee wangu walivyokuwa bega kwa bega na Nyerere kupambana na Gavana Edward Twining.

Nimeandika kitabu "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes..." ni kitabu maarufu unaweza kukipata Tanzania Publishing House, Samora Avenue.

Kitabu hicho kimeeleza mambo mengi kuanzia jinsi TANU ilivoundwa, harakati za uhuru, wafadhili wa harakati, nini kilitokea baada ya uhuru, ugomvi katika ya Nyerere na Waislam kuanzia 1963, kuwekwa kwa masheikh kizuizini mwaka 1964, Kuhujumiwa ujenzi wa chuo kikuu cha Waislam mwaka 1968 na Nyerere na mwishowe kuivunja East African Muslim Society (EAMWS) taasisi iliyokuwa ikitaka kujenga chuo hicho Bakwata ilvyoundwa nk. nk. harakati za Waislam chini kwa chini kudai haki zaokuanzia miaka ya 1970 hadi kufika hapa tulipo leo.

Yaliyomo humo yamebadilisha historia yote ya Tanzania.

Ndiyo unaona humu JF tunajadili mambo ambayo miaka labda kumi iliyopita hakuna aliyekuwa anayajua.

Binafsi nimezunguka kwingi, Afrika, Ulaya, Marekani nikifanya mihadhara katika vyuo na kuhudhuria makongamano.

Somo hili la matatizo ya nchi yetu yanafahamika na baada ya yaliyotokea Rwanda wapenzi na marafiki zetu wanaiomba serikali yetu isipuuze malalamiko ya Waislam.

Wanashauri yazungumzwe matatizo yote bayana na kasoro zirekebishwe.

Nadhani hadi hapa umepata picha kidogo.
Kilichobaki ni wewe kufanya bidii kujua zaidi.

Kulikoni?

Ninakuhakikishia ndugu yangu hakuna Muislam anaeweza kuthubutu kunyanyua mkono wake kuchoma kanisa. Allah (SW) ametukutaza hayo. Makanisa yamechomwa na maadui wasioitakia Zanzibar kheri. Kanisa la Mkunazini lipo Zanzibar zaidi ya miaka 100 mbona Waislam hawajalitia kibiriti?

Tafakari ndugu yangu tusichonganishwe tukajagombana bila sababu na mwisho sote tukajuta tukajiuliza.
Ilikuwaje?

Majuto siku zote ni mjukuu.

Huo ndiyo ukweli.
 
Sijaelewa, huyu Mohamed alikatamwa kwa sababu ya dini yake? Na kwenye ndege ni yeye pekee alikuwa muislam?

Mimi nafikili matatizo yalichangiwa na hotuba zako ilizotoa huko Ibadan ukishutumu Merikani na Tanzania kuhusu sheria za Ugaidi, vile vile kuhojiwa kwako na Redio ya Teheran wahasimu wakubwa wa Merikani nacho kilichangia katika kufuatiliwa kwako kwa karibu na Wamerikani. Mimi siamini kama dini yako ya kislaam ndio tatizo - mbona Merikani na Ulaya kuna waslaam wengi tu.

Tukumbuke kwamba nchi za magharibu wako paranoid na mambo ya ugaidi, wanaweza kabisa ku-misinterprate hotuba zako ukijikuta unakuwa black listed bila ya sababu za msingi, si hilo tu Wamerikani vile vile wataeleza Serikali ya TANZANIA na nchi rafiki wasi wasi wao kuhusu mwenendo wako unaotiliwa SHAKA na wao.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Men lie, women lie numbers don't lie
Ndio nini tena!! wamissionary walipokuja Africa pamoja na dini walitoa elimu kwa watu wao kwa sharti la kubadilisha dini ili uwe mkristo,lakini,waarabu wao wakaleta quoran tu na matokeo yake waislam wengi hawajasoma.Sasa unalalamika nini
 
Bwana Erick kwa kuwa umesema una umri mkubwa ni wazi mie nawe tutakuwa tunalingana umri.

Kwa jili hii hata mijadala baina yetu itakuwa ya kiungwana zaidi.

Bahati mbaya inaelekea hujui nchi yetu inatawaliwa vipi na nani kashika madaraka na hayo madaraka yamepatikanaje.

Lakini nina hakika ulishuhudia harakati za kudai uhuru kama ulikuwa Dar es Salaam itakuwa umewaona wazee wangu walivyokuwa bega kwa bega na Nyerere kupambana na Gavana Edward Twining.

Nimeandika kitabu "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes..." ni kitabu maarufu unaweza kukipata Tanzania Publishing House, Samora Avenue.

Kitabu hicho kimeeleza mambo mengi kuanzia jinsi TANU ilivoundwa, harakati za uhuru, wafadhili wa harakati, nini kilitokea baada ya uhuru, ugomvi katika ya Nyerere na Waislam kuanzia 1963, kuwekwa kwa masheikh kizuizini mwaka 1964, Kuhujumiwa ujenzi wa chuo kikuu cha Waislam mwaka 1968 na Nyerere na mwishowe kuivunja East African Muslim Society (EAMWS) taasisi iliyokuwa ikitaka kujenga chuo hicho Bakwata ilvyoundwa nk. nk. harakati za Waislam chini kwa chini kudai haki zaokuanzia miaka ya 1970 hadi kufika hapa tulipo leo.

Yaliyomo humo yamebadilisha historia yote ya Tanzania.

Ndiyo unaona humu JF tunajadili mambo ambayo miaka labda kumi iliyopita hakuna aliyekuwa anayajua.

Binafsi nimezunguka kwingi, Afrika, Ulaya, Marekani nikifanya mihadhara katika vyuo na kuhudhuria makongamano.

Somo hili la matatizo ya nchi yetu yanafahamika na baada ya yaliyotokea Rwanda wapenzi na marafiki zetu wanaiomba serikali yetu isipuuze malalamiko ya Waislam.

Wanashauri yazungumzwe matatizo yote bayana na kasoro zirekebishwe.

Nadhani hadi hapa umepata picha kidogo.
Kilichobaki ni wewe kufanya bidii kujua zaidi.

Kulikoni?

Ninakuhakikishia ndugu yangu hakuna Muislam anaeweza kuthubutu kunyanyua mkono wake kuchoma kanisa. Allah (SW) ametukutaza hayo. Makanisa yamechomwa na maadui wasioitakia Zanzibar kheri. Kanisa la Mkunazini lipo Zanzibar zaidi ya miaka 100 mbona Waislam hawajalitia kibiriti?

Tafakari ndugu yangu tusichonganishwe tukajagombana bila sababu na mwisho sote tukajuta tukajiuliza.
Ilikuwaje?

Majuto siku zote ni mjukuu.

Huo ndiyo ukweli.
Mzee Mohamed,
Sio wewe tu unayeifahamu historia ya NCHI hii. Tuliowaona huku bara wakihutubia mikutano ya hadhara na kutafuta wanachama wapya wa TANU enzi hizo za mkoloni, Wamanyema wako wa Kariakoo hawamo mbali na Bibi Titi mzawa na mzalendo wa kweli wa nchi hii ambaye kwa kiasi fulani aliweka kando mila na tamaduni nyingi za mwanamke wa Pwani na Uislam wake. Wao walimpa hela kula Mwalimu na kumwandalia chai na kisha kumpeleka kwenye matambiko tu. Kitabu chako kile kina hadithi nyingi sana ulizoona hazikinzani na agenda yako kuu ya WAISLAM kunyanyaswa nchi hii.
Hakuna aliyedai uhuru wa nchi hii kwa kutumwa au kusukumwa na DINI yake na Nchi hii itabaki bila DINI.
 
Mwakijila,
Baada ya mkasa ule nikajaelezwa kisa cha kukamatwa kwangu.

Nimeeleza katika makala.
Kile ambacho sikupenda kueleza ni kuwa wakati naandika pp ile nilikuwa naingia katika web ambazo nilionywa nisifanye hivyo.

Mimi nilikaidi.

Ahsante kwa mchango wako.
Bw.mohamed said,usicheze na mwisrael yeye ni hatari,kwani hao marekani wanafanya mambo ambayo israel inayataka.
Ni ukweli usiopingika kuwa ugaidi mara nyingi unaunganishwa na uislam,ninakupa ushauri wa bure jitenge na waisrel kwani
wale kwa sasa hakuna taifa linaloweza kupingana nao.Hao marekani wanajikomba kwa waisrael na siku watakaoisaliti israel ndio utakuwa mwisho wa taifa la marekani.
 
Julius Nyerere katajwa mara 2 kwenye hii stori, akihusishwa na manyanyaso ya waislamu wakati yeye akiwa rais.

Manyanyaso mengine kwa waislamu ya mwaka 1993 yanatajwa lakini raisi aliyekuwepo wakati huo (Ali Hassan Mwinyi), hajatajwa kabisa, badala ya imetajwa 'serikali'!!!

Manyanyaso mengine kwa Bw M. Said ya mwaka 2006 yanapewa msisitizo wa hali ya juu, lakini raisi hahusishwi (Jakaya Kikwete) badala yake inahusishwa 'serikali' na Marekani na Ukristu!!!

Ingetajwa unyanyasaji mwingine wowote kati ya 1995-2005, naamini isingelaumiwa serikali, angelaumiwa raisi!!!

Siamini kama mtu wa 'chuo kikuu' anaweza kutumia mbinu dhaifu namna hii kuficha hisia zake za kisiasa akitumia mwamvuli wa dini. Hata mtoto wa std IV angeishtukia hii...
 
Back
Top Bottom