Udhalilishwaji wa waislam na vyombo vya dola

Udhalilishwaji wa waislam na vyombo vya dola

Mara kadhaa huwa najiuliza kama wanaojiita waislamu humu JF ni waislamu kweli!!!
Sina uhakika kama kuna mtu amejihoji kuwa ni kwa nini walioambatana na M. Said kutoka Tanzania kwenda Iran, ni waandishi kutoka Daily News na Channel ten?!!!

Tuunganishe dots watanzania (Channel ten...Iran...2006... ???Mhazini CCM???)

Wagawe, uwatawale...
 
Julius Nyerere katajwa mara 2 kwenye hii stori, akihusishwa na manyanyaso ya waislamu wakati yeye akiwa rais.

Manyanyaso mengine kwa waislamu ya mwaka 1993 yanatajwa lakini raisi aliyekuwepo wakati huo (Ali Hassan Mwinyi), hajatajwa kabisa, badala ya imetajwa 'serikali'!!!

Manyanyaso mengine kwa Bw M. Said ya mwaka 2006 yanapewa msisitizo wa hali ya juu, lakini raisi hahusishwi (Jakaya Kikwete) badala yake inahusishwa 'serikali' na Marekani na Ukristu!!!

Ingetajwa unyanyasaji mwingine wowote kati ya 1995-2005, naamini isingelaumiwa serikali, angelaumiwa raisi!!!

Siamini kama mtu wa 'chuo kikuu' anaweza kutumia mbinu dhaifu namna hii kuficha hisia zake za kisiasa akitumia mwamvuli wa dini. Hata mtoto wa std IV angeishtukia hii...
Tuko,
Mzimu wa Mwalimu kwa Mzee Mohamed utazidi kumtafuna tu. Kamsingizia mambo mengi mno tena kwa maandishi na mahubiri kwenye nyumba za Ibada. Niliwahi kumuuliza maswali yafuatayo kwenye makala zake nyingine hakunijibu:
-Kama kweli Mwalimu aliwachukia Waislam na Uislam ilikuwaje alipostaaafu akamwachia NCHI Mwislam safi kabisa AHM?
-Alikubali vipi kuunganisha Tanganyika na Zanzibar ya Waislam 99%?
-Watu wake wa karibu kabisa wakati wa utawala wake ni akina Salim, Rashid, Hashim,...?
-Alimwombaje Gaddafi fedha za kujenga msikiti Butiama alikozaliwa?
-Mfumo KRISTO unawachaguaje marais Waislam? Hili linawezekana kwa nchi kama Kenya?
-Hivi kweli watu walidai uhuru wa nchi hii kwa msukumo wa DINI zao?
-Mwalimu alitaifisha shule za madhehebu ya DINI kwa sababu gani?
Mzee Mohamed mwepesi kuyakwepa haya kwa hoja dhaifu kwelikweli. Ajue tu jambo moja kwa uhakika. NCHI hii itabaki bila DINI. DINI itabaki kwa mtu na Mungu wake.
 
Pole sana ndugu yangu lakini kumbuka Quran inavyosema, "Hawatokubali wayahudi na manaswara mpaka mfuate mila zao".
 
Tuko,
Mzimu wa Mwalimu kwa Mzee Mohamed utazidi kumtafuna tu. Kamsingizia mambo mengi mno tena kwa maandishi na mahubiri kwenye nyumba za Ibada. Niliwahi kumuuliza maswali yafuatayo kwenye makala zake nyingine hakunijibu:
-Kama kweli Mwalimu aliwachukia Waislam na Uislam ilikuwaje alipostaaafu akamwachia NCHI Mwislam safi kabisa AHM?
-Alikubali vipi kuunganisha Tanganyika na Zanzibar ya Waislam 99%?
-Watu wake wa karibu kabisa wakati wa utawala wake ni akina Salim, Rashid, Hashim,...?
-Alimwombaje Gaddafi fedha za kujenga msikiti Butiama alikozaliwa?
-Mfumo KRISTO unawachaguaje marais Waislam? Hili linawezekana kwa nchi kama Kenya?
-Hivi kweli watu walidai uhuru wa nchi hii kwa msukumo wa DINI zao?
-Mwalimu alitaifisha shule za madhehebu ya DINI kwa sababu gani?
Mzee Mohamed mwepesi kuyakwepa haya kwa hoja dhaifu kwelikweli. Ajue tu jambo moja kwa uhakika. NCHI hii itabaki bila DINI. DINI itabaki kwa mtu na Mungu wake.

Asante Mkuu... Huwa wanakimbia sana ukianza kujadili nao kwa hoja hizi. maana kuna mwingine anajiita Malumbano, juzi juzi alikuwa analalamika kuwa NECTA inawaonea!!! Nikamuuliza maswali machache tu akakimbia.

Waislamu wengi tulio nao huku maofisini na mtaani hawana malalamiko ya hivi...
 
Jamani mimi si mtaalam wa hoja ila naomba mnitajie dini za watu wafuatao na walitutoka duniani kipindi cha mtawala gani:

1. Horace Kolimba
2. Moringe Sokoine
3. Joan Mwaikusa
4. Amina Chifupa
5. Salome Mbatia
6. Wachimbaji wa almas bulyankulu.
 
Mzee Mohamed,
Sio wewe tu unayeifahamu historia ya NCHI hii. Tuliowaona huku bara wakihutubia mikutano ya hadhara na kutafuta wanachama wapya wa TANU enzi hizo za mkoloni, Wamanyema wako wa Kariakoo hawamo mbali na Bibi Titi mzawa na mzalendo wa kweli wa nchi hii ambaye kwa kiasi fulani aliweka kando mila na tamaduni nyingi za mwanamke wa Pwani na Uislam wake. Wao walimpa hela kula Mwalimu na kumwandalia chai na kisha kumpeleka kwenye matambiko tu. Kitabu chako kile kina hadithi nyingi sana ulizoona hazikinzani na agenda yako kuu ya WAISLAM kunyanyaswa nchi hii.
Hakuna aliyedai uhuru wa nchi hii kwa kutumwa au kusukumwa na DINI yake na Nchi hii itabaki bila DINI.

Mkuu, tujaribu kutafakali mambo bila ya kuwa na trait ya U-ISLAAMPHOBIA - mimi nimesoma historia ya Tanganyika wakati niko primary, tuwe wakweli tulicho kuwa tunafundishwa ni ujio wa wajerumani, vita vya majimaji, vita vya kwanza vya DUNIA, ujio wa Waigereza na magavana wake, vita vya pili vya DUNIA - historia yote hiyo was too brief. Kusoma historia kwangu kulisitishwa nilipo ingia kidato cha tatu na kuchukua mkondo wa sayansi, lakini nakumbuka vizuri historia niliyosoma form one na two ilihusu tawala za kirumi, mambo ya kale, ujamaa TANU na Nyerere; walio endelea na somo la historia walijifunza zaidi historia ya West Africa kama nakumbuka vizuri.

Back to the point, hivi juzi juzi wakati JK anatoa nishani kwa wanaharakati waliosaurika (wengine wao walikwisha tangulia mbele ya haki masikini) ambao walihusika kupinga ukoloni wa waingereza bila woga, je ni Watanzania wangapi waliwahi kusikia kwamba kuna watu (Wafrica) wengine zaidi walio wahi wanapingana na ukoloni wakati Nyerere akiwa bado mwanafunzi hata alipomaliza masomo yake na kuwa Mwalimu, kundi ili lilikuwa linaendeleza harakati zao za kupinga ukoloni - si hilo tu, kundi ili ili ndilo lilimkaribisha Kambarage aungane nalo bila ya kujali DINI - oh yes, karibu 99.5% ya members wa kundi hilo walikuwa Waislaam - tuwe wakweli hapa. Nimesikitishwa sana ku-underrate mchango wa Bibi TITI Mohammed, mama huyu alikuwa jasiri sana, mtu kusema eti "alikuwa mpishi wa chai" tutakuwa hamtuntedehi HAKI hata kidogo.

Hivi tukiwa wakweli tunaweza kusema list ya majina yaliyo tajwa na JK tuliwahi kuyasoma kwenye historia ya Tanganyika kweli? Jibu ni HAPANA! Kwa nini walikuwa hawasemwi? - kulikuwa na agenda gani ya siri ya kuficha majina yao, na kwa manufaa ya kina NANI!

Mimi ni mkristo lakini sipendi kabisa kuona historia ya nchi hii inapindishwa kimaksudi hili kukidhi EGOS za watu wenye chuki binafsi kuhusu kundi fulani au kutaka kutukuza binadamu mwenzao kama demi-GOD! Ukweli wa historia unapashwa kujulikana ili vizazi vijavyo viwaenzi mashujaa hao kama alivyo fanya JAKAYA, si hilo tu hata vitabu vya historia vya nchi hii vinapashwa kuchapishwa UPYA.

Mwisho labda nisema tusiwe tunamu-dismiss Ndugu Moh off hand just like that, cha muhimu hapa ni kutafakali anacho kisema na sisi tulinganishe na yale tulio wahi kusimuliwa na watu wengine weledi kama yeye; tujaribu kujilidhisha kwamba mambo ambayo anayasema/kulalamikia yana UKWELI ndani yake, alafu kama kuna ukweli basi Serikali yetu ina wajibu wa kulekebisha kasoro hizo kwa manufaa ya mastakabali wa TAIFA letu - ni vizuri ku-address tatizo hili now not later, otherwise we gonna regret our own FOLLY kwa kupuuzia jambo hilo.
 
Binafsi ningependa kumhoji kwa kina bw. M Said. Tatizo najua mjadala mzima utakavyokwenda -hatojibu maswali ya yale anayodai.
 
NI maaskofu wangapi waliorudishwa makwao au kuwekwa kizuizini wakati wa Nyerere?

warudishwe wamefanya nini kwa mfano, alafu acha kulinganisha kina ponda na mtu kama ponda
 
Nawapenda waislamu sawa na wakristo. Kitu kimoja sikielewi ni kuwa na tabia ya ulalamishi na kujiona wameonewa kwenye kila kitu! Sipendi tuwe inferior kiasi chakujidhalilisha, sipendi tuwe inferior kiasi cha kuzuia hata wanaotaka kujiunga na dini hii wenye utashi mzuri waogope. Au ndiyo strategy? Hebu jaribuni kufanya vitu positive watu watapenda dini yenu.
Nawasilisha
 
Kinachonisumbua ni kuwa wengi wanaoandika kuhusu uislamu wamekaa kiuchochezichochezi wa kidini vile! Hii tabia italipelekea taifa letu lifike pabaya tusipopataka. Vinginevyo tuambiwe kuwa uislamu maana yake vita, damu, mauaji na mambo ya jinsi hiyo. Mbona kuna mambo mazuri tu tunayoweza kushirikisha watu kuliko kuchocea vurugu hapa nchini kwa kisingizio cha dini? Najua tofauti za kidini zipo na nivizuri kupata watu wapya kwenye dini zetu, lakini kwa nini tusiseme sera za dini zetu watu wakavutwa nazo? Kwani tusieleze faida za uislamu na ukristo watu wakapima na kuamua kujiunga kwa hiari? nitakuwa wa mwisho kujiunga na kundi lolote la kidini kwa kauli za ucochezi zisizokuwa na tija!
 
waislam tunaelewa fika kuwa tunafanywa daraja la pili katika nchi yetu wenyewe. waislam wote wanaelewa,huwezi amini kuanzia primary level to university level,makazini,mitaani mpka majumbani waislam wanaelewa kuwa kuna ubaguzi mkubwa wa kini. tumeongea na tunaongea sana lakini hayapatiwi ufumbuzi, na siku zote binadam haonewi mda wote! kama hakuna ufumbuzi naiona Biafra ya tanzania.
 
Binafsi ningependa kumhoji kwa kina bw. M Said. Tatizo najua mjadala mzima utakavyokwenda -hatojibu maswali ya yale anayodai.

Mzee Mwanakijiji

Ahaa haaa Unaweza kuuliza ukuta maswali ukakujibu ila si huyu Bwana Mohamed Saidi mwandishi wa viroja nyenye uchochezi wa kidini.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mzee Mwanakijiji

Ahaa haaa Unaweza kuuliza ukuta maswali ukakujibu ila si huyu Bwana Mohamed Saidi mwandishi wa viroja nyenye uchochezi wa kidini.

Chama
Gongo la mboto DSM

Aisee mwandishi wa viroja..unatamani uwe kama yeye lakini ndiyo hivyo..umeishia na kujaaliwa kaundika vi-mistari miwili hapa JF period..

Mohammed ni kiwango kingine kwako.
 
Mjadala mzuri huu toka kwa MS, Mwanakijiji, Chama, Nguruvi3 na wengineo........Wakati mwingine najiuliza ndugu zangu waislam tulicheza nao, tukaishi nao, tukala nao, tukashereheka nao (Chritmas & Idd n.k) na tukasoma nao na uwezo kielimu tulijuana Waislam kwa Wakristo.....na ufaulu ulikuwapo kwa Waislam kwa Wakristo....LAKINI leo eti kuna Waislam wachache wanalalamika wanaonewa?

Kweli nchi hii amabayo imekuwa na Ma-Rais wakristo kwa Waislam bado tunaona kuna kuonewa?

Wanakamatwa na kusekwa lupango Wakristo kwa Waislamu bado tunaona uonevu ni kwa dini moja tu?

Njaa inawapiga Waislamu kwa Wakristo bado tunahisi kuna dini fulani inaonewa?

Angalau nimetembelea nchi jirani sijaona utangamano wa kidini kama ulioko tz.........haiwezekani huku mtaani tuishi bila kubaguana halafu wakubwa fulani watuambie tunabaguana kwa misingi ya kidini.

Hitimisho langu ni kuwa hapa kuna ajenda ya kisiasa inayovishwa joho la udini period............na watakaoingia kwenye mtego ni mateka au washirika wa kundi "dogo".
 
Aisee mwandishi wa viroja..unatamani uwe kama yeye lakini ndiyo hivyo..umeishia na kujaaliwa kaundika vi-mistari miwili hapa JF period..

Mohammed ni kiwango kingine kwako.

Topical;
Usitake kunitusi mimi nitamani kuwa kama Mohamed Saidi kwa kipi? Nashukuru kwa Mola alichonijalia nacho na hekima nyingi alizonipa; haya ya kukaa na kutunga uzushi Mungu aniepusha nayo . Tuelezeni nyie washabiki na wanafunzi wake kinamshinda kuja na majibu mujarab ukimuuliza tende akakimbilia kujibu halua vyote vitamu lakini tofauti kaka kaeni mchanganue mambo msikimbilie kushabikia msivyojua.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Bwana Gwalihenzi,
Ingekuwa mie nataka kushindana humu kwa usomi nadhani ni wachache sana wangekuwa na ujasiri wa kusimama na mimi uso kwa uso.Mimi sishindani na usomi wa Nguruvi3 na nadhani yeye binafsi hilo alishalitambua kwangu siku nyingi sana.
Mimi niko tayari kusimama na yeyote na mahali popote kuhusu mada hii.
Mohamed, uliopleta hoja hii tulitegemea ichambuliwe na ijadiliwe kama ilivyowasilishwa.

Jambo la kusikitisha sana ni kuwa umeiondoa hadhira katika mada yako na kuchomeka mambo yasiyohusiana na mada.
Kwa mtu anayejinasibu kuandika paper nyingi hili linatia doa kama kweli unaweza kuzitetea kwa wenye ufahamu na Tanzania.

Ukisoma hoja nyingi za wanajamvi utaona wamejikita katika mada, kwa mshangao wewe hujibu hoja na uanjieleza kuandika vitabu vingi na paper za kutosha. Unawaondoa watu katika mada yako na kujibu hoja za 'spelling' lugha, Bakwata na kusafiri duniani n.k.

Ni kwasababu ya kukosa hoja zenye mashiko umetumbukia katika mtego wa 'personal attack' kama nilivyokunukuu.
Hakuna swali hata moja uliloweza kujibu miongoni mwa maswali lukuki ya wanajamvi.
Ninashangaa unaposema unaweza kusimama na mtu yoyote wakati umeshindwa kusimama hapa jamvini kujibu hoja za wanajamvi.

Hebu turudi kwenye mjadala bila kwenda kulia au kushoto.
Tafadhali simama na kujibu hoja hizi kwa kuangalia kila nukta maana hujazijibu zaidi ya 'personal attack' kwangu na wala sihitaji samahani, wewe jikite katika hoja tu!

1. Umeeleza kisa cha Sheikh Amir kufukuzwa akiwa na khanga kana kwamba huyo alikuwa malaika.
Umesahau kuwa ukombozi unaosema ulifanywa na Waislam ulikuwa si bahati mbaya bali mikakati.
Sijui utawezaje kumsafisha Sheikh Amir kwa hilo ili serikali ya Nyerere ionekane imemuonea. Hata hivyo, hivi Mohamed, Sheikh huyo angefanya alichokusudia leo ungeandika kama kaonewa au shujaa?

2. Katika kueleza kisa cha Sheikh Amir,umemtaja Nyerere na Siyo serikali ya Nyerere 'iliyomdhalilisha'.
Ilijuzu uwe 'consistently' katika kuelezea visa vilivyofuata.
Sijui kwanini mabucha ya Nguruwe yalipovunjwa husemi serikali ya Mwinyi unasema 'mapambano ya waislam na vyombo vya dola'? Sijui kwanini unapoeleza masheikh waliogaragazwa Bagamoyo usiseme Kikwete unasema vyombo vya dola? Je hii siyo double standard na kwamba inaharibu mtirirko mzima wa maoni, mada au tuhuma zako!

3. Viongozi wa dini hasa wageni wanatakiwa watoe taarifa ili kuwalinda na kulinda hadhi zao. Mara nyingi kiongozi wa Ismailia au Shia anapokuja nchini hupewa waongozi tena wakiwa na vimuli muli. Je, huyo Mufti wa Yameni alijulikana yupo nchini na alitolewa taarifa za uwepo wake? Hivi askari watawezaje kuwatambua wageni maarufu kwa mavazi tu bila taarifa?

4. Mohamed, unaweza kuuthibitishia umma kuwa ni viongozi wa kiislam tu ndio 'wanaodhalilishwa' na hakuna wa imani, au wapagani wanaofanyiwa hivyo? Je, wazee wa iliyokuwa EAC nao walipobebwa na Landrover walichaguliwa kwa misingi ya dini au majina yao? Je, yule Padri aliyeondolewa miaka 70 kwa amri ya 24hrs naye alikuwa Mwislamu?

5. Tunapoongelea bunge kukubali sheria ya kigaidi umesema ni shinikizo la Wakristo na wala si shinikizo la Bunge.
Sasa, kwanini masheikh wakidhalilishwa isiwe ni shinikizo la Said Mwema liwe la vyombo vya dola?
Je, mzee Said, mumewahi kumona IGP kuhusiana na sakata hili? Je IGP angekuwa John William Joseph hadithi hii ingebeba kichwa cha hapo juu au ingegeuka kuwa hadithi ya kanisa? Je, ilikuwaje Rais Kikwete anayejua hadhi ya Mufti aachilie vitendo vya namna hiyo, achilia mbali Urais wake?
 
waislam tunaelewa fika kuwa tunafanywa daraja la pili katika nchi yetu wenyewe. waislam wote wanaelewa,huwezi amini kuanzia primary level to university level,makazini,mitaani mpka majumbani waislam wanaelewa kuwa kuna ubaguzi mkubwa wa kini. tumeongea na tunaongea sana lakini hayapatiwi ufumbuzi, na siku zote binadam haonewi mda wote! kama hakuna ufumbuzi naiona Biafra ya tanzania.

Una mfano wowote unaothibitisha mwanafunzi kunyimwa nafasi ya shule - iwe msingi, sekondari au chuo kikuu kutokana na yeye kuwa muislamu?
 
huko Nigeria kila siku makanisa yanachomwa hiyo imekaaje mkuu
 
Mwisho labda nisema tusiwe tunamu-dismiss Ndugu Moh off hand just like that, cha muhimu hapa ni kutafakali anacho kisema na sisi tulinganishe na yale tulio wahi kusimuliwa na watu wengine weledi kama yeye; tujaribu kujilidhisha kwamba mambo ambayo anayasema/kulalamikia yana UKWELI ndani yake, alafu kama kuna ukweli basi Serikali yetu ina wajibu wa kulekebisha kasoro hizo kwa manufaa ya mastakabali wa TAIFA letu - ni vizuri ku-address tatizo hili now not later, otherwise we gonna regret our own FOLLY kwa kupuuzia jambo hilo.

Sioni euledi wowote kwa huyu mzee zaidi ya kujenga chuki za kidini. Anaongelea "manyanyaso" ya watu kwa sababu ni waislamu, na wananyanyaswa na watawala. Kinachonifanya nimuone sio mweledi, anajadili kwa kuwahusisha watawala wanaonyanyasa waislamu na ukristo, simply because Nyerere alikuwa mkristo. Anashindwa kabisa kusema ni kwa nini "manyanyaso" haya yamekuwepo hata wakati ambao mtawala mkuu ni muislamu!!! Hivi wewe huoni katika hali kama hii kunakuwa na maswali mengi zaidi ya majibu. Mweledi yeyote anayeongelea suala la watu kunyanyaswa (na sometimes kuuawa) na watawala anatakiwa azingatie yafuatayo
- Sio wahanga wote ni wa dini moja
- Sio watawala wote walioamuru hayo ni wa dini moja
- Siasa na itikadi vimehusikaje
- Kufungamana na mataifa fulani ya nje kumehusikaje
- Mhanga wa manyanyaso alikuwaje tishio kwa watawala na/au taifa

Sio mtu anakuja na hoja dhaifu saaaana kuwa waliotendewa vibaya na watawala ni kwa sababu walikuwa waisalmu!!! wakati tunajua akina Oscar Kambona hawakuwa waislamu!!!
 
Jamani samahani' natoka nje ya mada kidogo....hivi sisi waafrica hizi dini tulizaliwanazo au tumeletewa?
i mean uislaam na ukristu. majibu pls!
 
Back
Top Bottom