Bwana Gwalihenzi,
Ingekuwa mie nataka kushindana humu kwa usomi nadhani ni wachache sana wangekuwa na ujasiri wa kusimama na mimi uso kwa uso.Mimi sishindani na usomi wa Nguruvi3 na nadhani yeye binafsi hilo alishalitambua kwangu siku nyingi sana.
Mimi niko tayari kusimama na yeyote na mahali popote kuhusu mada hii.
Mohamed, uliopleta hoja hii tulitegemea ichambuliwe na ijadiliwe kama ilivyowasilishwa.
Jambo la kusikitisha sana ni kuwa umeiondoa hadhira katika mada yako na kuchomeka mambo yasiyohusiana na mada.
Kwa mtu anayejinasibu kuandika paper nyingi hili linatia doa kama kweli unaweza kuzitetea kwa wenye ufahamu na Tanzania.
Ukisoma hoja nyingi za wanajamvi utaona wamejikita katika mada, kwa mshangao wewe hujibu hoja na uanjieleza kuandika vitabu vingi na paper za kutosha. Unawaondoa watu katika mada yako na kujibu hoja za 'spelling' lugha, Bakwata na kusafiri duniani n.k.
Ni kwasababu ya kukosa hoja zenye mashiko umetumbukia katika mtego wa 'personal attack' kama nilivyokunukuu.
Hakuna swali hata moja uliloweza kujibu miongoni mwa maswali lukuki ya wanajamvi.
Ninashangaa unaposema unaweza kusimama na mtu yoyote wakati umeshindwa kusimama hapa jamvini kujibu hoja za wanajamvi.
Hebu turudi kwenye mjadala bila kwenda kulia au kushoto.
Tafadhali simama na kujibu hoja hizi kwa kuangalia kila nukta maana hujazijibu zaidi ya 'personal attack' kwangu na wala sihitaji samahani, wewe jikite katika hoja tu!
1. Umeeleza kisa cha Sheikh Amir kufukuzwa akiwa na khanga kana kwamba huyo alikuwa malaika.
Umesahau kuwa ukombozi unaosema ulifanywa na Waislam ulikuwa si bahati mbaya bali mikakati.
Sijui utawezaje kumsafisha Sheikh Amir kwa hilo ili serikali ya Nyerere ionekane imemuonea. Hata hivyo, hivi Mohamed, Sheikh huyo angefanya alichokusudia leo ungeandika kama kaonewa au shujaa?
2. Katika kueleza kisa cha Sheikh Amir,umemtaja Nyerere na Siyo serikali ya Nyerere 'iliyomdhalilisha'.
Ilijuzu uwe 'consistently' katika kuelezea visa vilivyofuata.
Sijui kwanini mabucha ya Nguruwe yalipovunjwa husemi serikali ya Mwinyi unasema 'mapambano ya waislam na vyombo vya dola'? Sijui kwanini unapoeleza masheikh waliogaragazwa Bagamoyo usiseme Kikwete unasema vyombo vya dola? Je hii siyo double standard na kwamba inaharibu mtirirko mzima wa maoni, mada au tuhuma zako!
3. Viongozi wa dini hasa wageni wanatakiwa watoe taarifa ili kuwalinda na kulinda hadhi zao. Mara nyingi kiongozi wa Ismailia au Shia anapokuja nchini hupewa waongozi tena wakiwa na vimuli muli. Je, huyo Mufti wa Yameni alijulikana yupo nchini na alitolewa taarifa za uwepo wake? Hivi askari watawezaje kuwatambua wageni maarufu kwa mavazi tu bila taarifa?
4. Mohamed, unaweza kuuthibitishia umma kuwa ni viongozi wa kiislam tu ndio 'wanaodhalilishwa' na hakuna wa imani, au wapagani wanaofanyiwa hivyo? Je, wazee wa iliyokuwa EAC nao walipobebwa na Landrover walichaguliwa kwa misingi ya dini au majina yao? Je, yule Padri aliyeondolewa miaka 70 kwa amri ya 24hrs naye alikuwa Mwislamu?
5. Tunapoongelea bunge kukubali sheria ya kigaidi umesema ni shinikizo la Wakristo na wala si shinikizo la Bunge.
Sasa, kwanini masheikh wakidhalilishwa isiwe ni shinikizo la Said Mwema liwe la vyombo vya dola?
Je, mzee Said, mumewahi kumona IGP kuhusiana na sakata hili? Je IGP angekuwa John William Joseph hadithi hii ingebeba kichwa cha hapo juu au ingegeuka kuwa hadithi ya kanisa? Je, ilikuwaje Rais Kikwete anayejua hadhi ya Mufti aachilie vitendo vya namna hiyo, achilia mbali Urais wake?