Udhalilishwaji wa waislam na vyombo vya dola

Udhalilishwaji wa waislam na vyombo vya dola

attachment.php


attachment.php


attachment.php
Inauma!......mpaka lini? mpaka lini?
 
Hata maovu yanazidi kuongezeka duniani, so what does that tell you?

Ndio maana makundi kwa makundi ya watu wanaingia na kufata mfumo wa Maisha wa Mwenyeezi Mungu nao ni Uislaam.
 
Kwa wasiojua watakejeri na kukashifu kua waislamu ni watu wa kulalamila....Lakini ndugu zetu upande wa pili wanapaswa wajue ajenda za Mataifa makubwa hasa MAREKANI historia ni ndefu lakini kiufupi US kwao maadui wa kubwa kwao walikua ni wawili according to their interest

1. USSR 2. UISLAMU...Wamefanya juu chini na kuweza kuusambaratisha iliyokua nchi tishio kwao USSR na ilimeguka na sasa baadhi ya nchi iliyokua USSR ndo zimejiunga na UE then NATO na wana mpinga RUSSIA iliyokua ni USSR na hivyo ni ahueni kwa US kwani they keep on divide and rule...

Then another enemy kwa US is ISLAM na hiyoipo declared kwao kwani they say Islam faith doesnot change hence it is dangerous to our interest so what they do is to steer misunderstanding between them na kufanya nchi zao zisitawalike na ikibidi kuzivamia kivita na kuuchafua uislam ili ionekane ni DINI ya fujo na machafuko...

Angalia uvamizi wa IRAK je ni waislamu wangapi wamekufa kwa upuuzi tu wa kuzushiwa ili ipatikane sababu ya kutimiza matakwa yao,,SOMALIA ni mwaka wa 17 sasa haina serikali ni chanzo cha serikali ya awali kuondoshwa wote tunajua lengo lao litimie,,LIBYA sasa imevamiwa lengo ni kuitawala na kuuondoa utamaduni wa kiislam...AFGHANISTAN ilivamiwa kwa uzushi tu kua eti OSAMA ndie aliedungua world trade centre or twin tower japo ata wamarekani wenyewe wamekuja kuujua ukweli kua that was the plan of invading AFGHANISTAN iliyokua na utawala wa kiislamu..fatilia chanzo za WTO kuangushwa na wakinanani walihusika utasikitika sana...YEMEN hakuna amani tena kila siku utasikia US DRONE HAS KILLED watu kadhaa, Mara utasikia PAKISTANI ndege zisizo na rubani zimeua watu kadhaa PAKISTAN anyway yakuelezewa ni mengi WAISLAMU NI ADUI WA MAREKANI na LENGO NI KUTOUNGANA NA KUA KITU KIMOJA....

Turidi TANZANIA watu wengi hasa upande wa pili hua wanakejeri sana bila kufanya tafiti..Ebu tujiulize hivi ni kwanini NYERERE na serikali ya CCM walikataa kupeleka maendeleo na hasa ya ELIMU mikoa yenye idadi kubwa ya waislam mf. TANGA, KIGOMA, RUKWA, LINDI, MTWARA nk nini ilikua ajenda? jibu ni raisi sana wajinga ndo wanatawalika so wanyime ELIMU lakini MUNGU mkubwa hiyo mikoa ambayo ilisuswa ndo imekuja gundulika kua na rasilimali nyeti sana mf MAFUTA,GAS nk.....

Nakumbuka kuna mwakan fulani IRAN ilijitolea kujenga vyuo vikuu kwa ajiri ya waislam na mahospital km vile BUGANDO,KCMC kwa wenzetu na alikuja waziri wao wa mambo ya nje na kuahidi wakati huo MKAPA alikua rais within 3 days alitumwa waziri wa mambo ya nje wa UK kipndi kile alikua mwanamke somebody clearshort if am not mistaken na kutua nchini na kusisitiza kua serikali ifute mkataba wa kigaidi sasa unaweza ukaona haya ni madogo lakini lengo nadhani umeshalijua...kuna mashirika mf DHINUREYN ISLAMIC FAUNDATION kuna wakati lilipigwa marufuku kutoa misaada ya kujenga mashule,hospital kwa waaislam eti lina link na ugaidi ili tu waislamu wasiwe na vyao sidhan km tutafika...mbona misaada ya wenzetu haichunguzwi wapi inatoka? Hivi kukamatwa kwa viongozi wa kiislamu tena bila stara inaleta picha gani what if PENGO afanyiwe kitu km hicho tena akiwa na wageni wake toka nje ya nchi? Jamani mkiona wenzenu wanalalamika mjue kuna sababu ya kuwafanya walalamike.

Hatupendi TZ iwe km Nigeria ila hizi kero za mfumo kristu ziachwe mara moja...mfano mdogo kipindi cha nyuma tulikua tukiwashuhudia maaskofu wakitoa maagizo yao kwa serikali hasa kipindi hiki cha JK mpaka masheik wakavunja ukimya wakasema no no mbona wakati wa MKAPA hatukuwaona mkitoa maagizo kwake kwanini sasa? so kuna consipiracy nyingi sana na ata ktk serikali na mpaka mdau leo kaposti eti viongozi wa kiislamu yani MWINYI na JK eti uongozi wao maisha ni magumu sana kulinganisha na wengine hizo zote ni ISLAMICPHOBIA watu walizojengewa na nchi za magaribi...ISLAM IS THE BEST RELIGION NO MATTER WHAT!
 
Wee jamaa unaonekana ni mtu mzima na msomi lakini hoja zako ni za kitoto ile mbaya! Hivi wakati wa kipindi cha Nyerere ni watu wangapi waliokuwa detained kutokana na sababu mbalimbali? Au walioondoshwa na kurudishwa kwao; wazungu kwa waafrica? Tukianza kuwa na akili na mawazo mgando kama haya, basi hata wakinga watakuja na kichwa cha habari kinachosema udhalilishaji dhidi ya wakinga kwa kuwa tu Tuntemeke Sanga alinyanyaswa na Nyerere. Au wale watu wa Ukerewe watakuja na hoja kama hizo hizo kwa kuwa wengi wa walioko kule walipelekwa kama adhabu. Ni ufinyu wa fikra, kutolea mfano wa shehe aliyerudishwa Zanzibar kama mfano wa unyanyasaji dhidi ya uislamu.

Ninapata shida sana kukuelewa wewe binafsi na pia uwezo wako wa kuchambua mambo. Ni watu wangapi wamekatwa, achilia mbali uwanja wa ndege na kusingiziwa hizo kesi za madawa ya kulevya na hata mauaji? Ni kwa vipi kukamatwa kwako ukuhusishe na Uislamu? Nyie waislamu kama mtaendelea kuwa na akili finyu hivi hivi, mtaipeleka nchi vitani hii. Yaani wasomi wa elimu dunia kama wewe ambaye tulidhani muwe mmestaarabika, na nyie mnaendekeza ujinga uleule wa mafundisho ya madrasa. Kama na wakristo wangekuja na mafundisho ya kanisani na kutaka yaongoze nchi mnadhani kungekalika? Acheni fikra mbovu na finyu ya kuwazia udini kila wakati!
 
Edit basi tuweze kukusoma. Tukisema upeo wenu mdogo mnalalama. Kuandika tu shida.
 
Yeah naUlimboka alitekwa na kuteswa kwa sababu ni mkristu!!!
Mwanakijiji! mzee wetu Mohamed Said ameianza nakala yake kwa kuturudisha nyuma kidogo na habari ya yule Sheikh aliyerudishwa "kwao" Zanzibar halafu akaendelea kutupeleka mwaka 1964 wakati masheikh wengi waliwekwa kizuizini, hakutuacha hapo bali alitukumbusha mwaka 1993 ambapo kulizuka tafrani kati ya askari na Waislamu akamalizia tukio la Sheikh Kishki juzijuzi na Mufti wa Yemen halafu akaunganisha na lilomkuta yeye.
Huu ni mlolongo wa matukio baada ya matukio haiwezekani ulifananishe na tukio moja la Ulimboka au na jingine kama la Ulimboka pale na hapa......mwisho kauli yako imenishangaza sana kwani inaonekana kuihukumu Serikali kuwa na hatia ya utekwaji wa Ulimboka!
Mohamed said ametuletea udhalilishwaji wa Waislamu unaofanywa na vyombo vya dola, wakati ya Ulimboka ndio kwanza uchunguzi unaendelea!
 
Wee jamaa unaonekana ni mtu mzima na msomi lakini hoja zako ni za kitoto ile mbaya! Hivi wakati wa kipindi cha Nyerere ni watu wangapi waliokuwa detained kutokana na sababu mbalimbali? Au walioondoshwa na kurudishwa kwao; wazungu kwa waafrica? Tukianza kuwa na akili na mawazo mgando kama haya, basi hata wakinga watakuja na kichwa cha habari kinachosema udhalilishaji dhidi ya wakinga kwa kuwa tu Tuntemeke Sanga alinyanyaswa na Nyerere. Au wale watu wa Ukerewe watakuja na hoja kama hizo hizo kwa kuwa wengi wa walioko kule walipelekwa kama adhabu. Ni ufinyu wa fikra, kutolea mfano wa shehe aliyerudishwa Zanzibar kama mfano wa unyanyasaji dhidi ya uislamu.
NI maaskofu wangapi waliorudishwa makwao au kuwekwa kizuizini wakati wa Nyerere?
 
Kama kweli ulinyanyaswa kwa sababu ya imani yako pole. Lakini kama ni kweli ulikuwa na kosa, basi hii na iwe fundisho kwako wewe na kwa wengine wote wa aina yako. Hata hivyo, katika kuusoma uzi wako nimegundua kwamba una udini wa hali ya juu, maana chuki uliyonayo dhidi ya watu wa imani nyingine na hasa wakristo inajidhihirisha wazi kabisa katika maneno yako hilo huwezi kukana. Ina maana wewe uliona ni halali kabisa waislamu kwenda kubomoa mabucha ya nguruwe kwenye nchi kama hii ya watu wa imani zote? Hii maana yake nini hasa? Halafu umetuambia waislamu walipigania uhuru dhidi ya wajerumani na waingereza, mbona hukusema kama wapigania kuondolewa kwa utumwa ulioletwa na Waarabu ambao ni waislamu wenzako? Au kwa kuwa unyama huo uliofanywa dhidi ya waafrika wenzetu ulifanywa na mwarabu mwislamu basi unakuwa ni halali? Kwahiyo ubaya ukitendwa na mtu wa imani nyingine ni dhambi lakini ubaya ule ule ukitendwa na mwisilamu unakuwa ni safi na halali. Umeona jinsi ulivyo na chuki za kidini?. Ni kweli waingereza na wajerumani waliwatendea babu zetu vibaya sana na hili ni la kulaaniwa na kila mpenda haki.Kibinafsi ninalaani uovu wa wakoloni hawa wa ulaya kama jinsi ninavyolaani ukandamizaji uliofanywa na waarabu. Usitake kuubariki uovu wa waarabu kwasababu tu ni waislamu. walichokitenda pia ni cha kulaaniwa vilevile. Halafu, msipende kuwa watu wa kulia lia kila wakati, Hivi kama serikali ya TZ ingekuwa rais na makamu wake wote wakristo mngesema nini? Si mngeandamana kila siku na nchi isingekalika? Ikiwa leo Waislamu mmeshika nafasi zote za juu na bado mnalia mmeonewa na kupunjwa ingekuwaje kama mambo yangekuwa kinyume cha hapo? Ninaamini kabisa kwamba kwa hali hii, hata mkipewa nafasi zote kuanzia uongozi wa mashina nchi nzima bado mtasema kanisa limehodhi serikali au Bunge. Tafadhali jitahidi kubadilisha fikra zako za kidini, hazijengi zaidi ya kubomoa tu.
 
Hadithi yake nimeipenda ingawa inaonekana baadhi ya mawazo kakopi kwenye hadithi ya kusadikika.
 
Pole kwa usumbufu uliokupata Mzee Mohamed.Katika Dini Njia bora ni kusamehe ila ktk siasa ni kusema ukwel.Usichanganye Dini na Siasa na muhimu zaidi tambueni adui yenu hasa ni nani na ni vema sana uache kuchochea chuki miongon mwa jamii ya Wanadamu maana hakika hukumu iko mbele yako.
 
S.Liondo said:
katika kuusoma uzi wako nimegundua kwamba una udini wa hali ya juu, maana chuki uliyonayo dhidi ya watu wa imani nyingine na hasa wakristo inajidhihirisha wazi kabisa katika maneno yako hilo huwezi kukana. Ina maana wewe uliona ni halali kabisa waislamu kwenda kubomoa mabucha ya nguruwe kwenye nchi kama hii ya watu wa imani zote? Hii maana yake nini hasa?
Anazungumzia kilichotokea BAADA ya uchomwaji wa mabucha ikimaanisha waliingizwa hata wasiohusika!
Mimi binafsi siwaoni na hatia waliochoma mabucha (lakini hilo ni suala jingine unaweza kulifungulia thread ukitaka, nitakuja huko)
S.Liondo said:
Halafu umetuambia waislamu walipigania uhuru dhidi ya wajerumani na waingereza, mbona hukusema kama wapigania kuondolewa kwa utumwa ulioletwa na Waarabu ambao ni waislamu wenzako? Au kwa kuwa unyama huo uliofanywa dhidi ya waafrika wenzetu ulifanywa na mwarabu mwislamu basi unakuwa ni halali? Kwahiyo ubaya ukitendwa na mtu wa imani nyingine ni dhambi lakini ubaya ule ule ukitendwa na mwisilamu unakuwa ni safi na halali. Umeona jinsi ulivyo na chuki za kidini?.
Hapa inabidi ututhibitishie kwanza kuwa ni Waarabu Waislamu ndio walioleta utumwa Tanganyika.
S.Liondo said:
Halafu, msipende kuwa watu wa kulia lia kila wakati
Hawa "wanaolialia" na kupanda majukwaani na kuelezea hisia zao au wanaoandamana ni watu wazuri Mkuu, ogopa wale wasio lialia!
 
Why encouraging the enlargement of the circle of concerns instead of enlarging the circle of influence? Kila siku ni kulia lia tu na kutafuta mtu wa kuwaonea huruma watu wachache wasio na agenda nyingine yoyote zaidi ya Nyerere. Nyerere is gone and we cant change that fact. Kizazi hiki kianze kushughulika na mambo yasiyotuhusu ili iweje? Tukumbuke wa mbili havai moja! Tupigane kutoka hapa tulipokwamba.

Hapana kilio hapo.
Inaandikwa historia ambayo si wengi wamebahatika kuifahamu.

Kwani wewe unakijua kisa cha Sheikh Hassan bin Amir? Au urafiki wa Nyerere na Sheikh Hassan bin Amir kuanzia 1953 hadi 1961 wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika?

Haya ni katika "theme" muhimu katika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Ndiyo maana nikamtaja kabla hya kueleza yangu.
 
Hans Roger Dibagula, utafiti wako ni dhaifu, kwa sababu umeangalia maeneo machache tu na wala haujaainisha hizo nyadhifa. naomba uainishe, na ulete tafiti kamili, sababu hapo sijaona idara nyingine muhimu. ainisha pia ugawaji wa madaraka kwa ngazi tofauti. otherwise siwezi kuiamini tafiti yako, huenda ulikaa tu, kwa vile una MS Word kwenye desktop yako, basi ukawashwa washa mpaka kuja na pumba hizi.
"
Inawezekana hujui chanzo cha data hizo. Data hizo hazina shaka na kwa ajili ya kutaka "amani na mshikamano" iliamuliwa zisitolewe.

Ukipenda unaweza ukazipuuza lakini waliokuwa Wizara ya Elimu miaka hiyo na wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wanafahamu nani alileta data hizo na kwa kisa gani.
 
Hapa inabidi ututhibitishie kwanza kuwa ni Waarabu Waislamu ndio walioleta utumwa Tanganyika.
Hili nalo linahitaji uthibitisho? Ina maana wewe historia ya darasa la tano hukusoma? Mbona liko wazi kwamba walioendesha biashara ya utumwa Tanganyika ni waarabu, na kama ni waarabu, definitely ni Waislamu, sasa unataka ushahidi gani tena?
 
Ndugu mbona wewe mtata sana? Hulengi chochote zaidi yakupandikiza udini!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Anazungumzia kilichotokea BAADA ya uchomwaji wa mabucha ikimaanisha waliingizwa hata wasiohusika!
Mimi binafsi siwaoni na hatia waliochoma mabucha (lakini hilo ni suala jingine unaweza kulifungulia thread ukitaka, nitakuja huko)Hapa inabidi ututhibitishie kwanza kuwa ni Waarabu Waislamu ndio walioleta utumwa Tanganyika.Hawa "wanaolialia" na kupanda majukwaani na kuelezea hisia zao au wanaoandamana ni watu wazuri Mkuu, ogopa wale wasio lialia!

Hili la Utumwa zuri sana lakini kwanza itabidi tuanze na Transatlantic Slave Trade. Una ubavu tuanze kazi? Unajua kulikuwa na meli inayobeba watumwa kupeleka Marekani ikiitwa Jesus?
 
Back
Top Bottom