Mzee Said,
Awali ya yote nieleze neno linalotumika katika medani ya vita. Neno hilo ni 'shoot any moving object'.
Kauli hii inatumika majeshi yanapokuwa katika wakati mgumu, ya kwamba mbinu zote zimeisha na hakuna mkakati. Nitafafanua wakati nahitimisha maelezo yangu.
Kwa mtu asiyeielewa Tanzania na utangamano wa wananchi wake wenye imani, makabila na itikadi mbali mbali za kisiasa,pindi anaposikia mihadhara yako ima anatishika sana au anajawa na hasira kama ulivyowajaza WaNigeria.
Kwa mantiki hiyo utaangaliwa kwa jicho toafauti na lile la Kapuku Nguruvi3.
Umaarufu unagharama zake na katika dunia ya sasa gharama yake ni hiyo ya wewe kuangaliwa kwa jicho mujarabu si kwasababu ya jina lako au imani yako, bali kwa facts na spinning zako katika habari.
Kwa kuanzia hili la vyombo vya dola, mtu anayesoma vizuri 'between the lines' atagundua mambo kadha.
1. Umeeleza kisa cha Sheikh Amir kufukuzwa akiwa na khanga kana kwamba huyo alikuwa malaika.
Umesahau kuwa ukombozi unaosema ulifanywa na Waislam ulikuwa si bahati mbaya bali mikakati.
Sijui utawezaje kumsafisha Sheikh Amir kwa hilo ili serikali ya Nyerere ionekane imemuonea. Hata hivyo, hivi Mohamed, Sheikh huyo angefanya alichokusudia leo ungeandika kama kaonewa au shujaa?
2. Katika kueleza kisa cha Sheikh Amir,umemtaja Nyerere na Siyo serikali ya Nyerere 'iliyomdhalilisha'.
Ilijuzu uwe 'consistently' katika kuelezea visa vilivyofuata.
Sijui kwanini mabucha ya Nguruwe yalipovunjwa husemi serikali ya Mwinyi unasema 'mapambano ya waislam na vyombo vya dola'? Sijui kwanini unapoeleza masheikh waliogaragazwa Bagamoyo usiseme Kikwete unasema vyombo vya dola? Je hii siyo double standard na kwamba inaharibu mtirirko mzima wa maoni, mada au tuhuma zako!
3. Viongozi wa dini hasa wageni wanatakiwa watoe taarifa ili kuwalinda na kulinda hadhi zao. Mara nyingi kiongozi wa Ismailia au Shia anapokuja nchini hupewa waongozi tena wakiwa na vimuli muli. Je, huyo Mufti wa Yameni alijulikana yupo nchini na alitolewa taarifa za uwepo wake? Hivi askari watawezaje kuwatambua wageni maarufu kwa mavazi tu bila taarifa?
4. Mohamed, unaweza kuuthibitishia umma kuwa ni viongozi wa kiislam tu ndio 'wanaodhalilishwa' na hakuna wa imani, au wapagani wanaofanyiwa hivyo? Je, wazee wa iliyokuwa EAC nao walipobebwa na Landrover walichaguliwa kwa misingi ya dini au majina yao? Je, yule Padri aliyeondolewa miaka 70 kwa amri ya 24hrs naye alikuwa Mwislamu?
5. Tunapoongelea bunge kukubali sheria ya kigaidi umesema ni shinikizo la Wakristo na wala si shinikizo la Bunge.
Sasa, kwanini masheikh wakidhalilishwa isiwe ni shinikizo la Said Mwema liwe la vyombo vya dola?
Je, mzee Said, mumewahi kumona IGP kuhusiana na sakata hili? Je IGP angekuwa John William Joseph hadithi hii ingebeba kichwa cha hapo juu au ingegeuka kuwa hadithi ya kanisa? Je, ilikuwaje Rais Kikwete anayejua hadhi ya Mufti aachilie vitendo vya namna hiyo, achilia mbali Urais wake?
Mohamed, wengi tunasafiri duniani na tunakutana na vituko vya ubaguzi. Siku moja nilikuwa Dubai nikaona Raia wenye rangi nyeusi wakiwekwa pembeni na passport zao kuingizwa kwa uchunguzi zaidi. Raia wengine hasa wa kihindi wenye passport za nchi hiyo hiyo waliachiwa kuingia ndani ya ndege bila kikwazo. Sasa hapa tusemeje, waliobaguliwa kwa rangi na Waarabu wale wale unaodhani ni wema sana kuliko Wamarekani ilikuwa ni halali yao au iliuma kama inavyokuuma leo hii
Lakini pia lazima ujiulize, iweje London, New York, Sidney, Bon n.k. kuna miskiti na lisiwepo kanisa Saudia au Bahrain kama yalivyo kwa wenzetu. Hapa kuna nini kama si ubaguzi.
Lazima ujiulize,kwanini mtu aombe ukimbizi Australia na siyo Malysia, Uingereza na siyo Saudia, New York na siyo Qatar?
Je, hapo hakuna ubaguzi? Huko wanakofikia Ulaya na Marekani kwanini wasibaguliwe katika 'social security' ambazo wao ni wafaidika wakubwa kwa takwimu za Uingereza, Australia, Canada na Marekani.
Kwanini majina yao yasiwahukumu kama linavyokuhukumu lako.
Na mwisho, kuhusu kubaguliwa kwa tuhuma za Ugaidi ni makosa kuwalaumu wanaojilinda. Imefika mahali mtu kama Abdumutwalab alivaa chupi ya bomu kwenda kuua watu wasio na hatia ili tu amtie chuki mmarekani.
Majuzi wapo waliokuwa wanataka kulipua majengo tu hata kama majengo hayo wamo watoto. Mohamed Ghailan kutoka ZNZ amelipua ubalozi wetu na kuua watu wasioweza hata kutamka Marekani. Wote hawa wanafanya uharamia na uhuni na ujahilia huo kwa jina la Uislam. Ni nani anayeweza kutenganisha Muislam Gaidi na Muislam Muumini.
Yale ya Nigeria ndiyo ya UAMSHO. Kupinga muungano kwa kuua watu.
Ninachotaka kusema hapa ni kuwa hao wanaojinasibu kuupigania usilam hawafanyi hivyo kwa misingi ya dini.
Hapo ndipo jeshi la wajahidini linapokuwa na kauli yangu ya awali 'shoot any moving object', kwamba hawana mkakati na hawajui wanapigania nini.
Kama unaushahidi kuwa ukiuaa wanadamu 300 wasio na hatia kwasababu tu unataka kuua Mmarekani mmoja utakwenda peponi, basi weka ushahidi huo kwa aya, hadithi na suna na kama huna basi jitenge na utetezi wa kisichodhahiri na kilicho na shaka! Hivyo ndivyo vinakutia matatani. Msome Mkuu Chama hapo juu.
Watu wanaokusikiliza usidhani ni wajinga! wanafanya tafiti na huenda wanakubaliana nawe au la.
Kitu kiomja nachopenda kukuasa ni kuwa una maneno ya uchochezi sana tena ukipindisha hadithi ili zilete kile ulichokusudia. Una ajenda ya kisiasa nyuma ya mgongo wa dini. Kwa vile unazunguka duniani nitaishangaa serikali yoyote itakayokuangalia kama inavyomwangalia Kibwengo na kapuku Nguruvi3. You deserve thorough scrutiny the least to say.
When there are no rules of engagement, anything is fair!