Mtoboasiri
JF-Expert Member
- Aug 6, 2009
- 5,101
- 1,952
Majibu na kejeli zako zinaonyesha unakijua kilichomkuta huyo Shekh. Hakuna marefu yasiyo na ncha.
Nguruvi3,Mzee Said,
Awali ya yote nieleze neno linalotumika katika medani ya vita. Neno hilo ni 'shoot any moving object'.
Kauli hii inatumika majeshi yanapokuwa katika wakati mgumu, ya kwamba mbinu zote zimeisha na hakuna mkakati. Nitafafanua wakati nahitimisha maelezo yangu.
......"
When there are no rules of engagement, anything is fair!
Karibu tena ... Kaka yetu .. mwalimu wetu.. Mohammed said.. darasa lako huru sikuzote linaeleweka pamoja na mashambulizi uyapatayo
Hivi kuonyeshwa inconsistencies zilizopo kwenye hadithi yako ni matusi na/au kejeli?
Ahsante sana mdogo wangu,
Katika ukumbi huu tungelifanikiwa kuwa na adabu za mijadala yaani kushindanisha hoja kwa hoja bila kejeli, matusi nk. hapa lingelipatikana darsa zuri sana na miaka mingi baadae sisi hatupo wataokuja kutusoma wangesema, "Palipita watu JF hebu angalia usomi huu wa hali ya juu."
Mbona mashehe wengi tu wanapita hapo airport bila kusumbuliwa? Kwanini iwe ni wewe tu? Hili halihusiani na uislamu bana. Wewe bora utueleze ukweli.
Hapa ni JF mkuu, sio kila kitu ni NDIO. Lazima ubishiwe na uombwe maelezo.
Na katika hizo safari zako ulikuwa unaondokea airport gani? Kama ni Dar mbona hukusumbuliwa kwenye hizo safari?Ukwerli gani Majebere, kuwa nauza unga na siku yangu ilikuwa imewadia?
Nimesafiri sana dunia hii nimgekuwa mtu a unga weshanikamata siku nyingi.
Kuonyesha inconsistencies ndiyo usomi wenyewe na unatoa changamoto kwa mwenzako arejee katika maandiko yake ajieleza upya.
Hebu soma tena ulichoandika.
Si umeona umeniuliza swali na mimi nimekupa jibu.
Sasa futa kejeli onyesha migongano katika nisemayo tuendelee na mjadala.
Mohamed Said,
..mimi nadhani haya mauza-uza yanayokupata yamesababishwa na sept 11.
..kama ugaidi ungeishia na mashambulizi ya dsm na nairobi tu, basi mpaka leo hii tusingekuwa na sheria ya ugaidi Tanzania.
..tangu sept 11 usafiri wa anga umekuwa wa usumbufu sana, na wapo wengi wanasumbuliwa wakati hata siyo Waislamu.
..pia how do u explain your situation, pamoja na ya mufti wa Yemen, wakati wakuu wa vyombo vya usalama vya Tanzania ni Waislamu??
Umesema kweli lakini juu ya hayo wapo watu wanabughudhiwa pasi na sababu.
Ziko prejudice nyingi na nina uzoefu mkubwa.
Nilipata kuzuiwa Heathrow mwaka 1991 kwa karibu saa mbili.
Kisa?
Pasi yangu ilikuwa imeingia na kutoka Mozambique, Swaziland, Sudan, Egypt, Kenya kwa vipindi vifupi vifupi. Walitaka niwaeleze kwa nini nasafiri sana.
Ilikuwa kazi sana kuwaeleza.
Zama hizi hazikuwa za ugaidi lakini huyu Mswahili mbona anasafiri hivi kuna nini hapa?
Pole kwa maswaibu yaliyokukuta sheikh. wengi naona wanachangia kwa kebehi tuu. lakini haya mambo mpaka yakukute wewe ndio utaielewa vizuri hii hadithi.
Kama wote tutakuwa na mtazamo kama wako, basi na sisi tutasema: Hatuwaoni na hatia waliochoma Koran kule Mbeya. Je unaionaje hiyo? Imekaa vizuri ee? Ni kweli kwamba hawana hatia kwa kuchoma Koran kwa vile tu mtu fulani anaamini hivyo kwasababu ya udini wake? Achaneni na udini, ni sumu mbaya, hauna tofauti na ukabila na ubaguzi wa rangi. Kuweni na dini lakini udini uepukeni kwa gharama zozote zile.Anazungumzia kilichotokea BAADA ya uchomwaji wa mabucha ikimaanisha waliingizwa hata wasiohusika!
Mimi binafsi siwaoni na hatia waliochoma mabucha (lakini hilo ni suala jingine unaweza kulifungulia thread ukitaka, nitakuja huko)Hapa inabidi ututhibitishie kwanza kuwa ni Waarabu Waislamu ndio walioleta utumwa Tanganyika.Hawa "wanaolialia" na kupanda majukwaani na kuelezea hisia zao au wanaoandamana ni watu wazuri Mkuu, ogopa wale wasio lialia!