Thank you for the useful information.Hii topic tu hapo juu ni enough kukuondoa katika watu waliokua na akili timam.
Wacha waarabu kuuliwa hadhani kama paka, mwisho Karume alianza kuwauwa wasomi wote.
Kina Abdul Aziz Twala, Othman Sharif, Mohamed Hamoud, Saleh Sadala, Abdallah Kassim Hanga, Mdungi Ussi, na wengine wengi.
Uliza historia, hao hapo juu wamefanya nini na wamekufa vipi? Maana hata makaburi yao hayapo.
Mkuu naomba nikurekebishe kwenye modern slavery wahabeshi,wasomali na sudan wenye light skini hawakupelekwa utumwani naomba kutoa hojaNarejea ktk maelezo yangu ya awali.
Na ningependa Unijibu km nilivyokuuliza. Historia ilioandikwa na Mzungu huyo huyo inasema KABLA YA 1807 legislation Ndani ya Miaka 300. wazungu walifanikiwa KUBEBA WATUMWA WA KIAFRIKA ZAIDI YA 12,000,000 kutoka Pwani ya East africa na Savannah area of Africa (which includes countries such as Mali, Niger, Chad and Sudan) and the Horn of Africa (which covers Djibouti, Somalia and Ethiopia).
Sasa Swali ni kwamba! Je MZUNGU Hapa HAKUHUSIKA HATTA KIDOGO ktk BIASHARA HII ya WATUMWA WA Huko EAST AFRICA Including ZANZIBAR?
Nadhani wewe ni Mswahili km mimi ktk matumizi ya Lugha. Na neno "KUHUSIKA" nina imani maana yake unaijua.
Ntakupa mfano hai hapa.
During the second half of the 18th century, France opened up larger sugar plantations on the islands of Reunion, Mauritius and in the Indian Ocean. na Hapa WAFANYAKAZI WOTE Walikuwa WATUMWA WA KIAFRIKA.
Mfano wa Pili.
Je! Umeshawahi Kumsoma Napoleon 1 of France ktk Mswada wa Sheria alioupitisha Mwaka 1802 kuhusu UHALALI WA WATUMWA?
Baada ya Hapo NINI KILIWATOKEA WAZEE WETU wa EAST AFRICA?
Sasa Naomba Jibu lenye USHAHIDI na udadavuzi ulio wazi. Sio Jibu la Mitaani.
PASCOWee Baragashi, ulikuwepo kuyashuhudia hayo au umehadithiwa?!. Mimi nakiri sikuwepo ila sijahadithiwa bali nimesikiliza mimi mwenyewe shududa wa Mapinduzi yale Matukufu, yalivyorudisha hishma kwa visiwa vile, yena ili kuondoa ubaguzi, wamatumbi wakawao Waarabu kinguvu!.Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa, Walikimbia Wenyewe!.
Nimemsikia aliyepindua akisema hakuna Mwarabu alyefukuzwa Zanzibar, walioomdoka, waliondoka wenyewe bila yoyote kutimuliwa!. Kwa taarifa tuu, hata ASP wapo waliopote maisha!.
Pasco
Sielewi kuhusu Sudan na Somalia, lakini ninachokijua kuwa wahabeshi hawajawahi kutawaliwaMkuu naomba nikurekebishe kwenye modern slavery wahabeshi,wasomali na sudan wenye light skini hawakupelekwa utumwani naomba kutoa hoja
Mkuu Crabat ukisikia ilmu ndio hii, uzi wako huu umenifundisha mengi ambayo sikuyajua na miongoni mwa haya ni kuwa kumbe Sultan Said Sayyid alipohamisha makao makuu ya sultanate yake toka Oman na kuyahamishia Zanzibar ile mwaka 1832, hakuivamia Zanzibar bali alikaibishwa na mtawala wa Zanzibar aliyeitwa Mwinyi Mkuu!. Wajerumani na Waingereza, Wabelgiji, Wareno, Wataliano, Wahispania, etc kila wakishika maeneo, waliingia mikata na wenyeji, hivyo lazima kuna mkataba Mwinyi Mkuu aliingia na Waarabu kuitawala Zanzibar, hata kama sio mkataba wa maandishi, lakini there must be something, haiwezekani Mwenyeji ampishe tuu mgeni!, kwa mujibu wa bandiko lako, sababu kuu ya Wenyeji wa Zanzibar chini ya Mwinyi Mkuu, kuwakaribisha Waarabu Zanzibar, ni ulinzi wa visiwa hivyo visivamiwe tena na Wareno!.Wengi wetu hatufahamu uhusiano kati ya Oman na Zanzibar/Mombasa/Kilwa Na Pwani hii ya Mashariki..wengi tunafundishwa kuwa Wa Oman walikuja kutawala Znz Na pwani yake....Tukumbuke Wa Oman walifika Znz kitambo kwa biashara na Makaazi ya kawaida.
Tuwashukuru wa Oman kwa kuwatoa Wareno..
View attachment 341277
Du!. Mkuu Baraghash, heshma mbele!. Nitakuheshimu kama ninavyomheshimu Mkuu, Maalim Mohamed Said, ila nawe lugha yako, michango yako na kauli zako zifanane na umri wako na zireflect heshima hiyo!.PASCO
Nadhani kuanzia leo unite kaka na uniheshimu.
Mapinduzi na unyama wake nimeushuhudia kwa macho yangu, sikuhadithiwa. Nakumbuka waziwazi alipouliwa Inspector Sketi(?) na mkewe kwa mapanga mapolisi wazalendo kuwekewa vigogo vya mnazi kifuani, na wamakonde wakiwa na mishale wakiranda mitaani kuwaambia watu wawafichue mahizbu waliowaficha wapelekwe ( rahaleo) kituo cha madhila kilichowakusanya (mateka) wa hizbu na chachandu(ZPPP)
ASP waliopoteza maisha kwa ajili ya Mapinduzi ni wachache sana, hata kumi hawafiki! Uliza yalipo makaburi ya waasisi wa Mapinduzi. Yalikuwa ni mauaji ya upande mmoja. Ninachojua kuwa ASP wa Zanzibar waliwahifadhi wanachama wa hizbu wasiuawe na " wakombozi" kutoka bara na nchi jirani.
Ule uwanja wa Kibanda maiti uliobatizwa jina la uwanja wa demokrasia ndio una " mass graves" za wazanzibari waliouwawa Mapinduzi kwa kosa moja tu la kuwa wanachama wa ZNP/ZPPP. Tuombe mungu tu atusmehe madhambi yetu.
Mimi nimeshudia uhuru na hata kushiriki kumuaga Gavana Sir. George Mooring pale Forodhani ikishushwa bendera ya Union Jack na kupandishwa Bendera rasmi ya watu wa Zanzibar na Gavana akaingia kwenye meli ya Uingereza, huku mkewe akilia kama mtoto kuondoka Zanzibar ( yenye neema). Mimi sasa ni mzee( lakini si kikongwe)
1) Waraabu hawakuwatesa babu zetu.
2) Waraabu na Wazanzibari weusi (Waislamu) ndio walioteswa na John Okello (kutoka Uganda) na wafuasi wake walipo ipindua Serekali ya halali ya Zanzibar (John Okello na wafuasi wake walifanya mauwaji ya kinyama kabisa, waliuwa maelfu ya Waislamu bila ya hatia yeyote ile).
3) Kwenye uzi huu wa bieshara ya watumwa, kwanini huyu Pasco hakuwataja Wazungu waliowatesa sana Waafrika? na kuwauza Waafrika huko South American na Europe? na wanaendelea kuwatesa Waafrika mpaka hivi leo kwa siasa zao za ubaguzi.
4) Pasco Acha chuki dhidi ya Waislamu
Mkuu Mandago, ukinionyesha sentesi moja tuu niliotukana Waislamu, nitakushukuru!, huu uzi sio kuhusu Waislamu ni kuwahusu Waarabu dhalimu waliofanya biashaa ya utumwa!. Unless kama unamaanisha nikisema Mwarabu ndio kumaanisha Uislamu!, hapo nitakuelewa kidogo, na bado kwenye bandiko zima sijatukana popote!, ila nakiri katika majibishano, kuna vichaa humu tunakutana nao, sasa kwa vile na mimi ni kichaa fulani, tukikutana na vichaa tunazungumza nao lugha moja, na tukikutana na Wataarabu kama Waarabu kina MaalimWee Pasco, unatukana watu (Waislamu) kisha unatarajia kukumbatiwa?
Sometimes, inabidi tutumia dawa ya moto ni moto, kukujibu uongo wako huu unaoandika hapa.
Ukitaka heshima, anza wewe kuheshimu watu na wewe utaheshimiwa, In Sha Allah.
Heshima kamwe hailetwi na matusi.
(kama wewe unavyo fanya, eti unatafuta heshima kwa kutukana watu, kamwe hauzi kupata heshima mpaka ujirekebishe na uwaheshimu watu wote).
Sielewi kuhusu Sudan na Somalia, lakini ninachokijua kuwa wahabeshi hawajawahi kutawaliwa
Mkuu Maalim Mohamed Said, wewe ni hazina kubwa sana humu jf na kwa taifa letu kwa ujumla, tatizo lako ni dogo tuu!, yale mambo yetu yale....ukiliondoa hilo, unastahili kuwa among the few members wa jf ambao wao ni ma great thinkers wa ukweli na ma walking Encyclopedia Tanzannica!.Pasco,
Mimi ni mtoto wa Mama Daisy.
Kushoto: Mama Daisy, mbele ni Bi. Titi Mohamed
na kushoto yake ni Bi. Zainab mkewe Tewa Said Tewa
katika maandamano siku za mwanzo za uhuru
Ingekuwa si huu uhusiano wa kindugu Mama Daisy asingenieleza
chochote katika historia ya mumewe marehemu Abdulwahid Sykes.
Wakati ule watu walikuwa wakiogopa sana kusema lolote lililo kinyume
na historia ambayo watu walikuwa wameaminishwa.
Jina la Abdul Sykes na mdogo wake Ally na wazalendo wengine kama
Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Bi, Tatu bint
Mzee, Iddi Faizi Mafongo, Oscar Kambona kuwataja wachache yote
yalikuwa yamefutwa kabisa.
Siku ile Mwalimu Nyerere ambayo aliwahutubia Wazee wa Mzizima
yaani Dar es Salaam kuwaaga ambayo kwa bahati mbaya sana ndiyo
siku aliyosema hakumbuki Abdul Sykes alikuwa na cheo gani katika
TAA yeye alipoingia TAA Mama Maria Nyerere alikuwa na kikao kifupi
na akina Mama wa Dar es Salaam hapo hapo Diamond Jubilee Hall.
Mmojawapo katika hao akina mama alikuwa Mama Daisy.
Mama Maria aliwaeleza akina mama wale kuwa yeye na mumewe
walipokelewa Dar es Salaam na Abdul Sykes.
Wanamajlis,
Mtakumbuka siku niliposema kuwa Mwalimu Nyerere alisema kuwa
hakumbuki cheo cha Abdul Sykes katika TAA palizuka ubishi mkubwa
sana hadi Yericko Nyerere kusema yeye ataiweka hapa hotuba hiyo
tusikize kama kweli Mwalimu Nyerere alitamka kweli maneno yale.
Mama Daisy hakuwa na wasiwasi na mimi akinieleza kila kitu na kubwa
ambalo lilinishtua sana ni siku aliponiambia kuwa Allah ndiye atoae
ufalme, ''Baba yako yeye akimtaka sana Chief David Kidaha Makwaia
ndiyo aingie TAA wamchague president kisha waunde TANU.
Lakini Chief hakutaka.
Kila Chief akija Dar es Salaam kuhudhuria vikao vya Legico tukimualika
nyumbani kwa chakula cha jioni na mimi nilikuwa pale nikiwaandalia na
nikisika mazungumzo yao yote.
''Bwana Abdul akimwabia Chief Kidaha, ''David hebu achana na hao
Waingereza bwana njoo huku tudai nchi yetu.''
Mama Daisy alikuwa na mengi na akizungumza alikuwa hana uchungu
kwa yale yaliyopita akizungumza huku ametulia kabisa.
Hali ya siasa katika TAA ilikuwa hivi katika miaka ya mwanzoni ya 1950.
Yako mengi lakini kwa leo haya yanatosha.
Anaetaka zaidi kuhusu Chief Kidaha Makwaia aingie hapa:
Mohamed Said: Chief David Kidaha Makwaia 1922 - 2007
Pasco,
Naona nikuage na picha ya maalim wako Chama Omari Matata:
Kushoto: Ali Saleh, Mwandishi, Chama Omari Matata na aliyesimama nyuma ni
Balozi Mohamed Maharage BBC Club, Bush House London 1991
Pasco,Mkuu Maalim Mohamed Said, wewe ni hazina kubwa sana humu jf na kwa taifa letu kwa ujumla, tatizo lako ni dogo tuu!, yale mambo yetu yale....ukiliondoa hilo, unastahili kuwa among the few members wa jf ambao wao ni ma great thinkers wa ukweli na ma waliking Encyclopedia Tanzannica!.
Pasco
Wakamata watumwa, walikamata watu ambao ni makabila ya majembe kazi!, watu wa makabila ya nyanya hawakushughulika nao kabisa, ndio maana hata huko Zenj, hawakukamata watumwa!.Ni kweli pia watu wenye ngozi angavu na nywele laini hawakuchukuliwa utumwani,wafugaji kama wamasai,Bedouin,wafulani,wanubi pia hawakufanywa watu wengi walitakiwa wabantu wenye miili mikubwa iliyojijenga wanaofanya kazi hasa za kilimo
Maalim,Pasco,
Tatizo unalo wewe na mfano wa wewe.
Mimi naalikwa kote kwa kuwa nina ilm ambayo haikufahamika kabla.
Ilm ambayo wewe inakutaabisha.
Kote nakwenda nahadhiri kuhusu ''Islam and Politics in Tanzania.''
Hiki ni kitu ambacho hawakukijua kuwa kulikuwa na ''strong Muslim
movement'' katika kupambana na ukoloni kuanzia Vita Vya Maji Maji
hadi katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Wanamajlis,Wakamata watumwa, walikamata watu ambao ni makabila ya majembe kazi!, watu wa makabila ya nyanya hawakushughulika nao kabisa, ndio maana hata huko Zenj, hawakukamata watumwa!.
Pasco
Pasco,Maalim,
Mohamed Said
hakuna ubishi kwenye the role of Muslim katika ukombozi wa taifa hili, tatizo ni it was not the only ones, bat kulikuwa na wengine wengi tuu nao walichangia pakubwa na kuna wengine wengi tuu pia walikwamisha, tatizo ni pale recognition inapokuwa attached kwa kikundi kimoja as if there were the only one, ndio huu mimi nauita urongo!. Mfano Baghdellah alifungwa jela moja na Robert Makange na kosa lili lile, kisha mtu ajitokeze amtaje Baghdellah pekee na kacha kumtaja Makange!.
Kwenye maendeleo ya elimu, kuna tatizo mahali linalochangiwa na imani ya dini za kukaririshwa, kuna wengi wenu, immetoka kielimu kwa msaada wa seminari na sio madrassa, lakini hili ni nadra sana kulisikia mkiwasifu!, huo huo mfumo Kristu japo uliumiza baadhi ya watu, uliwakomboa wengi!, hivyo sometimes we have to swallow the bitter with the sweeter!, kwenye hili, ukilisoma bandiko, HILI ...ukanigundua ni kitu gani ambacho sikukisema, ujue kwa huyu jamaa aliyepo sasa, Juliasi ni afadhali!. Alianza na wa TRA, akaja na NSSF ataendelea mpaka awamalize wote!.
Pasco
Uzi wa mauaji upo na tumeichangia kule, huu ni uzi wa madhila ya Utumwa na mababu zetu walichofanyiwa na Waarabu!.Wanamajlis,
Naona kuna hofu kuu ya kuzungumza mateso na mauaji yaliyofanyika
Zanzibar katika na baada ya mapinduzi.
Wenzetu wanakimbilia historia ya miaka zaidi ya 170 iliyopita.
Wnataka wawahukumu watu kwa historia ya mababu na babu
zao.
Kisa cha mbwa mwitu na mwanakondoo.
Pasco,
Nimekuwekea ushahidi wa Aman Thani umekuwa kimya.
Huna lolote la kusema kuhusu mauaji ya akina Twala, Hanga
Saleh Saadala na wengineo?
Hawa si kizazi cha wakamata watumwa wa mika 200 iliyopita.
Huna chochote?
Hakukuwa na mashindano ya kuchangia, lakini kama ni fedha taslim, hakuna aliyeichangia TANU kama Mzee John Rupia!. Kunawezekana shilingi elfu moja ya tajiri Mzee John Rupia, inaweza isiwe na thamani kama thumuni ya masikini muokota makumbi!.Pasco,
Hakuna aliyetoa mchango kuwashinda Waislam kuanzia watu
hadi fedha.
Au mengine Mama Daisy hakukuambia?
Nimekuwekea picha yake umeiona?
Pasco,Hakukuwa na mashindano ya kuchangia, lakini kama ni fedha taslim, hakuna aliyeichangia TANU kama Mzee John Rupia!. Kunawezekana shilingi elfu moja ya tajiri Mzee John Rupia, inaweza isiwe na thamani kama thumuni ya masikini muokota makumbi!.
Mama Daisy hakunihadithia mambo ya michango, bali the role ya wanawake kwenye harakati za uhuru na jinsi alivyomfunza Mama Maria ujasiliamali, kukanda chapati, kuokota makumbi, kuuza mauta ya taa, na walitembea peku!, ndala ni siku ya Jumapili!.
Ni kweli ni Sykes walimlea Nyerere na kumpokea kuishi nae kwao baada ya kutokea Pugu, kabla hatahamia Magomeni!.
Pasco
Pasco
Kwa mujibu wa nilivyohadithiwa, ilikuwa ni zaidi ya hivyo, lakini kwa vile umenishauri nifute nimefuta ila mambo ya jf, hata vitu visivyo na maana huwa tunaacha tuu. Hicho kisa kizuri kifungulie uzi wake!.Pasco,
Ondoa hiyo sentensi yako ya mwisho,
Haina maana yoyote.
Muhimu katika yale niliyoandika kuhusu Mama Daisy
ni ule mkakati wa kuunda TANU na nafasi ya viongozi
waliokuwapo wakati ule.
Ndipo nilipomleta Chief David Kidaha Makwaia.
Hapa ndipo ungeuliza maswali.
Kuna kisa kizuri sana hapo.
Katika Dar es Salaam ya wakati ule hakuna kiongozi
ambae alikuwa hafiki nyumbani kwa Abdul Sykes
anza na Chief Abdallah Fundukira na malizia na
Chief Thomas Marealle.
Nyerere alifika kwa Abdul Sykes kama walivyofika
hawa watu mashuhuri wengine.
Du!. Mkuu Baraghash, heshma mbele!. Nitakuheshimu kama ninavyomheshimu Mkuu, Maalim Mohamed Said, ila nawe lugha yako, michango yako na kauli zako zifanane na umri wako na zireflect heshima hiyo!.
Nakiri Mapinduzi Matukufu ya 1964, yameacha majeraha na makovu makubwa ndani ya mioyo ya watu!, namna pekee ya kutibu majereha haya na makovu haya ni kuundwa kwa tume ya peace and reconciliation, watenda wajitokeze kukiri kutenda, na sababu zilizowafanya watende hayo waliyoyatenda, na kujutia na kuomba msamaha, na watendwa wajitokeze na kusema walishuhudia nini kikitendwa, kisha wawasamehe walio watenda na kuwahakikishia hawana kitu machoni wala moyoni!.
Hii itasaidia yule jamaa yenu akishinda, atakabidhiwa nchi!, kwa hali ilivyo, kuna watu ukiwaona machoni, unaviona visasi viko wazi dhahri shahir, hivyo ukiwapa nchi, kazi ya kwanza itakuwa kuwalipizia kwa yale waliowatenda!.
Pasco